Friday 23 August 2013

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] UCHOKOZI WA KISIASA WA KAGAME DHIDI YA RAIS KIKWETE.

Ndugu Yangu Ben na Wengine

Moja ya propaganda ambayo kagame na Rwanda wamekosea sana ni hii ya kumhusisha salma kikwete na rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeuwawa baada ya ndege yake kushambuliwa kwa kombora .

Mimi sioni ubaya wa salma kikwete kuwa na uhusiano na rais wa zamani wa nchi hiyo kwa maana sisi wote ni ndugu tu ila tatizo langu linakuja pale wanavyoonyesha chuki zao za kikabila zilizosababisha mauaji wa kimbari mwaka 1994 na viongozi wetu wa nchi .

Hii sasa imetupa fursa ya kujua ni kwanini ushauri wa kikwete kwa kagame umemwingia na jinsi gani nchi ya Rwanda ilivyogawanyika na baadhi ya viongozi walivyokuwa na chuki za wazi dhidi ya viongozi wenzao wan chi hiyo hiyo .

Pamoja na haya yote kuna mifano wa viongozi wa nchi wenye ndugu ambao ni viongozi wa nchi nyingine au wamewahi kuwa viongozi wa nchi .

Rais wa zamani wa Ethiopia . meles zenawi na rais wa Eritrea , isias afweki ni ndugu lakini hawakuwahi kutuhumiana , mwa malkia wa sasa wan chi ya uholanzi ana mume mwenye asili ya argentina ingawa kuliwahi kuwa na malalamiko kidogo kwa sababu baba wa huyu mumewe alikuwa ni waziri katika serikali ya kidikteta lakini walishamaliza mzozo huo .

 



2013/8/23 Haidari BENN <benntz@yahoo.co.uk>
 

UCHOKOZI WA KISIASA WA KAGAME DHIDI YA RAIS KIKWETE.

Suala la kuushuku Utanzania wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete,ni uchokozi wa kisiasa muflis
za walio ishiwa na la kusema au ni watu waliopotelewa na akili /ukasoro wa muamko wa kisiasa za 
hivi sasa baina ya Kigali na Dar-es-salaam.

Tukumbuke kwamba hivi karibuni tu Kagema na waziiri wake wa mambo ya njee walitapakaza 
"sumu ya kisiasa" kwamba Salma Kikwete , amehusiana ya Rais wa Rwanda , aliyeuwawa katika
ndege ya Rwanda 1994 - ajali ambayo ilisababisha mauwaji baina ya WanyaRwanda,Wao Kwa Wao.
Wa-Hutu waliamini kabisa kwamba Ndege ya Rais wao ,iliangushwa na akina Kagema,ambae ni wa kabila 
la Wa-Tusti ,wanao itawala Rwanda kwa namna watakavyo wao bila kujali fikira za wengine,si ndani ya
Rwanda seuze watu nchi za njee. Rais Kagema, ameharamisha yeyote,na jambo lolote ambalo litakuwa
ni kinyume ya fikira zake lishambuliwe kuwa ni sawa na ushiriki katika mauwaji ya Tustis ya 1994 ambayo
anataka yajulikane kama ni "Rwanda Holocaust ". 

"Dhambi" la Rais Kikwete ,ni pale alipotowa ushauri wake kwamba"... wakati umefika kwa wananchi wa 
Rwanda, wanaotawala na wale wapinzani ambao bado wapo maporini wakae pamoja kwa mazungumzo ya 
kuleta Usalama na Amani" Adis Abeba OAU meeting 2013.
Rais Kagame ,hakupenda kusikia jambo hilo kutoka kwa Kikwete,ingawaje Museveni ,aliunga mkono fikira hiyo.

Ukakamavu na Ujeuri wa Rais Kagema unafanana na ule wa Israelis ,hasa pale wanapoambiwa waanze 
mazungumzo na Palestanians,utaona kama wametiwa upupu,jinsi wanavyo ruka huku na kule na kuanza zile 
payuka payuka zao za kutoa visababu au masharti haya na yale au hata kuanza uchokozi wa ujenzi wa haramu wa majumba katika occupied territories na kukumbusha ulimwengu wote kuhusu Auschwitz and "Jewish Holocaust"
iliyotokea wakati wa vita vya pili vya Dunia . 

Maisraelis ,wao hata hutowa masharti "nani khasa ndie msemaji takatifu wa Palestanians,ambae watamkubali 
kuzungumza nae ikiwa si hivyo huendfa hata wakagomeya mazungumzo".

Rais Kagame , nae kwa vile hampendi Rais Kikwete ,kwa ule ushauri wake wa mazungumzo ya amani ,amefanya
njama za kutaka kumtiya dosari na kuushuku Utanzania wa Rais Kikwete,si kwa sababu nyingine yeyote ya msingi
bali ni mfilisiko wa hoja za kupinga "Mazungumzo ya Salama na Amani baina ya WaRwanda ".

Mazungumzo ambayo endapo yakifanyika na pakapatikana usalama ,basi jambo hilo litaleta amani na utulivu
kwa nchi zote jirani - Congo,Tanzania,Uganda,Kenya na Burundi.
Njama nyingine za Rais Kagema ,akishirikiana na Rais Musoveni ,hivi karibuni walizuka na chokochoko za kuacha
utumiaji wa Bandari ya DSM na barabara za Tanzania ,wanafanya hivyo sio kwa masilahi ya wananchi wao na
kuitakia kheri Afrika Mashariki na watu wake bali kwa Ubinafsia wao , ambao wantaka kuzifanya nchi zao kama
ni mashamba tu ya "Utawala Wao na Familia Zao"na kuwafanya wananchi wa huko ni Watumwa Wao.

Kwa nini Ushauri wa Kuleta Amani Uzushe Ugomvi na Uchokozi wa Kisiasa ? 

Kwa nini suala la uasiliya wa Rais wa Tanzania,au mahusiano ya kidamu baina ya Salma Kikwete na rais wa kale wa Rwanda ,ambae aliuliwa kikatili na wakina vikundi vya Kagema - liiingizwe katika mada hii ?

Mkala hii ya Ndugu Amissi , lengo lake ni kusambaza "Sumu ya Kigali kwa Watanzania , kwa manufaaa ya Kagema".

Imekhusu nini kuushuku Utanzania wa Rais Kikwete au Kusema uasilia wa watu wa Bagamoyo,ni watumwa ambao
walikuwa ni wadhaifu kimwili kwa bishara za Utumwa ndio maana walibakishwa hapo bagamoyo na kukufanya ni
kwao - porogo lote hili la nini na lina sshabaha gani ?
Hebu tujiulize hii makala iliyoletwa ndugu Amissi ,imeandikwa na nani na katika Gazeti gani ?

Kwa Kumalizia , wakati wowote wa siasa muflis na maaduwi wa Tanzania wanapoishiwa - wao daima hupayuka
payuka na kusambaza "Sumu za Kisiasa kwa Wajinga Wa Siasa na khasa to the "Educated Fools ".

Wapinzani wa Mwalimu Nyerere ,walisema alikuwa na asili ya Nyasaland.Wapinzani wa Maremu Karume ,walisema
asili yake Malawi na Congo , NgombaleMwiru ,nae alitiliwa shaka ya Uraia wake kwa sababu ya siasa yake wakati
ule. Ali Nabwa ,Uzanzibari wake ulikataliwa kwa sababu za Kisiasa , Rais Museveni , aliwahi kutiliwa shaka uraia wake kwa sababu ya siasa zake za ndani , Professor Shivji , aliambiwa "hana uchungu wa Zanzibar kwa sababu eti nimtu
aliyezaliwa huko mara tu pale alipoonekana kuwa msimamo wake ni kinyume na masilahi ya CUF ",Balozi Ali KARUME ,nae ameandamwa na pocho wa siasa kua uasilia wa Baba yake ni Malawi .
Mapocho hawa wa kisiasa hawazungumzii uasilia Mhindi Jussa au Seif Sharif wala Sultan Jamshid, au babu yake
Sayyid Khalifa ,kwamba asili zao ni Oman.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ikiwa ana asili ya Ki-DNA ,ya uasiliya wa Binaadam wa Afrika Kusini,Afrika ya Kati,
Afrika Magharibi au Afrika Mashariki au kutoka visiwani Unguja ,Pemba ,Ngazija, Moheli ,Anjouni au Mayotte au
Burundi,Rwanda,Madagaskar au kutoka kisiwa cha MAFIA ,au ikiwa ni Mmakua , Mmakonde ,Mzaramo ,Mchaga, Mhaya au ni Mruguru - is not the issue - la msingi kuliko lolote ni kwamba ni mzaliwa kidamu na kimwili ni Mwaafrika, ni Mtanzania,kifikra na kivitendo.Kihulka na Kitamaduni. 
Ikiwa maaduwi wa Tanzania wanalalamika kwa sababu ya msimamo wake wa kupenda Usalama na Amani na nchi Jirani - tatizo hilo ni lao. 

Kilicho wapasa maadui hao ni jambo moja tu "Wabaki kwao na Porojo la Sumu Yao,Waimeze Wao,lakini watuwachie na Waikome Tanzania yetu ya Usalama , AMANI NA UTULIVU. 

Kwa wale ndugu zetu wasio na uraia wa Tanzania au haki za ukaazi wa daima kwa vitambulisho rasmi vya kiserikali lao la kufanya ni ama ni kwenda wapendapo au waombe ruhusa ya ukaazi au uraia kwa mujibu wa sheria husiaka. Kwani tatizo lipo wapi ?

Rais Kikwete, ni Mtanzania kama Mbuyu na Mkorosho au kama Ndovu na Simba,jana ,juzi na
milele ni Mtanzania .
 
Benn Haidari
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826

__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)
Recent Activity:
.

__,_._,___



--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment