Wednesday, 28 August 2013

Re: [wanabidii] Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa Umma Kuhusu Uraia Pacha

Mwasaga

Nikwambie jambo, wakati fulani Martin Luther (Jnr) aliwahi kuandika giza haliondolewi na giza bali na mwanga, hivyo chuki huondolewa na upendo siyo chuki kwa chuki.

Hebu niambie katika maelezo ya YFM lipi la unafiki hapa kama hadi umkandie hivi eti anajifanya anajua mambi mengi. Hii siyo sahihi, hata kama unamchukia si kukandia kila jambo kaka mwishowe kiwango ambacho wengine tulikuweka kinaweza kushuka bure kwa kutojali kwako ni wakati gani useme nini na kwa nani.

Ni ushauri tu na mtizamo wa kiungwana bila kutegemea kuungwa mkono au kulaumiwa.
Sent from Yahoo! Mail on Android

From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>;
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa Umma Kuhusu Uraia Pacha
Sent: Wed, Aug 28, 2013 9:27:03 AM

Yona

Yaweke panapofaa hukuwa na haja ya kutuonesha unayajua mengi usiyotaka tuyafahamu kwangu huu ni unafiki. Sema kile unchitaka kusema mengine yaache hata kuyatambulisha.

On Aug 28, 2013 12:16 PM, "Yona Fares Maro" <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Mara ya Kwanza nasikia waziri membe akiongelea suala la uraia pacha ni miaka 3 iliyopita katika mkutano wa TPN Nadhani golden tulip hotel na target yake ilikuwa ni wale watanzania haswa wa marekani na ulaya kupata fursa za kushiriki katika ujenzi wa nchi yao hata kama hapo mwanzo walioukana au la ,kabla ya hapo miaka kadhaa kabla ya hapo kuna vikundi vya watu vilikuwa na kampeni za chini kwa chini kuhusu suala hili la uraia pacha .

Kwa mtazamo wangu turuhusu raia pacha kwa wale ambao ni wazaliwa wa nchi ya nchi lakini wazazi wao ni watanzania ambao hawajawahi kuukana uraia wao , lakini wale waliokana uraia wao tusiwafikie kwa sasa , hawa ni watu waliokulia humu ndani wakasomeshwa kwa kodi zetu na kurubuniwa na mataifa ya nje wakatumika wamechokwa sasa wanataka kurudi nchini kwa njia hii mengi siwezi kuyaweka humu .

Tanzania tutaijenga wenyewe na kuibomoa ni sisi wenyewe kwa kukubali kutumika .

On Wednesday, August 28, 2013 11:11:21 AM UTC+3, Edgar Mbegu wrote:
Je, ni Mambo mangapi ambayo hayakuwemo katika Rasimu ya Katiba yataendelea kuongezwa?
Hili nalo lazima kuliangalia kwa makini!
 
Date: Wed, 28 Aug 2013 00:12:39 -0700
From: hami...@gmail.com
To: wana...@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa Umma Kuhusu Uraia Pacha

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuujulisha Umma kuwa jana tarehe 26 Agosti, 2013, Mheshimiwa Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikutana na Uongozi wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.  Lengo la kukutana na Tume ilikuwa ni kuwasilisha pendekezo la haki ya Uraia wa nchi mbili kutamkwa na kutambuliwa kwenye Katiba mpya.

Mheshimiwa Waziri alikutana na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Augustino Ramadhani, Makamu Mwenyekiti wa  Tume pamoja na Katibu wa Tume 
na Naibu Katibu wa Tume.

Akiwasilisha hoja yake mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Waziri alisema yafuatayo:-

  1. Suala la Uraia wa Nchi mbili haliko kwenye rasimu ya sasa iliyotolewa.  Lengo la kufika Tume ni ni kuomba suala hilo liingizwe kwenye rasimu.
  2. Amependekeza Katiba itamke kwamba, Raia wa Tanzania aliyeko nje hatafutiwa uraia wake na mtu yeyote, chombo chochote sheria au Katiba, eti tu kwa sababu raia huyo amechukua uraia nje ya nchi.
  3. Katiba ikitamka hivyo, itungwe Sheria itakayofafanua haki, wajibu na masharti ya Mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili.
  4. Katika kujenga hoja hizo tatu, Tume ilielezwa faida zitakazopatikana kwa kuitambua na kuishirikisha jamii ya Watanzania waliopo ughaibuni (Diaspora).  Tume pia iliondolewa wasiwasi juu ya madai kuwa uraia wa nchi mbili unahatarisha usalama wa taifa au utawafanya baadhi ya watu kupiga kura wakiwa nje. Tume iliambiwa kuwa Sheria za Uchaguzi hutawala upigaji kura kwa raia walio ndani  na nje na hauwi  holela.  Kuhusu suala la usalama, Waziri alisisitiza kama ni mashaka, basi mashaka hayo yawe kwa wageni wanaoomba uraia  nchini kuliko watanzania walioko nje.

Katika kumalizia, Mheshimiwa Waziri alisisitiza, "bado naamini watanzania walioko nje sio wasaliti, They are just as smart citizen".

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment