Thursday 22 August 2013

Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA

EM

Nikweli kabisa hakuna mttu anaeishi kama.kisiwa, lakini kama wenzio hawakupendi unafanyaje? Unaweza kuja na njia mbadalla haapa mzee, yaani tukae tu tuangalie au tunung'unike au tuwabembeleze warudi tena kwetu au tufanyeeje?

Sent from Yahoo! Mail on Android

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA
Sent: Thu, Aug 22, 2013 3:37:59 PM

flein47,
'Rwanda na Uganda ni watu wazuri tu. No man is an island.
em

2013/8/22 <flein47@yahoo.com>
Na mimi naunga mkono JK aitoe nchi yetu kwa EAC naona tunaungana kinafiki sana. Hao wenzetu si watu wema hata kidogo hasa Rwanda na Uganda. Mi naona kama tunaungana na majambazi
Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on www.zantel.com/zantelapps

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Date: Thu, 22 Aug 2013 13:21:42 +0100 (BST)
Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA

Tusiwaangalie hao. Wana mambo yao tofauti na sisi. Walikwishakutafuta namna ya kututenga miaka mingi iliyopita na tunafahamu hilo na kwa taarifa yenu.

Walivunja jumuiya ya afrika mashariki kwa sababu zao na hadi sasa sababu hizo zipo waulize Wakenya wanajua na.walikatalia vitu vingi sisi tukakubali yaishe.sasa wanahaha kuchukua ardhi yetu tumewashtukia wanatapatapa.

Ushauri wanhi kwa JK sasa tuanze maandalizi ya kujitoa EAC halafu tuone nani atalia zaidi kama siyo wao.

Wasitubabaishe tumekuwa na tunaweza kusimama wenyewe bwana ala.....

KEMS.

Sent from Yahoo! Mail on Android

From: Rwambogo Edson <rwambogoedson@yahoo.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA
Sent: Thu, Aug 22, 2013 11:52:52 AM

katika hali ya kawaida.... haishangazi kuona majirani hao wameenda au wanaenda zao... tatizo ni kwamba tanzania ina misimamo yake na kenya ina misimamo yake, tuwaache wataalamu wetu wanaosimamia hiyo idara ya usafirishaji wafanye kazi yao.. nitashangaa kama tutavunja sheria zetu zilizoundwa na wasomi wetu eti kwa kuangalia MUSEVENI, KAGAME NA KENYATA wanafanya nini... jamani RAISI wetu, nchi yetu na hulka za watanzania  hazifanani kwa lolote na hao majirani watatu.

sisi tunafanana na majirani zetu walioko SADC na sio EAC... tusibababishwe na umoja wao, ikiwezekana ata umoja wao wabaki wao na sisi tule hamsini zetu, tuantishwa na nini nadhani ni wakati kwa wasomi wetu kutazama soko jipya na kuboresha zaidi ukusanyaji wa kodi, wamechuma sana SASA INATOSHA lazima kodi zitozwe ili wao wanufaike na sisi tunufaike zaidi

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, August 22, 2013 1:08 PM
Subject: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA

Na Raymond Kaminyoge, 

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

"Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam," alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... "Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo."

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

"Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi," alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

"Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo," alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.

Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment