Saturday, 19 November 2016

Re: [wanabidii] SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Hata za kutoka Serikali ya Uganda, Kenya...? Ila congratulations!  Kuna maendeleo katika usahihi wa kuandika 



Sent from Samsung tablet.


-------- Original message --------
From: 'Mashaka Makana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date: 19/11/2016 12:56 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Dada Happy hiyo takwimu ya fedha haikujumuisha zile zilizotolewa na ubalozi fulani ikatangazwa kukaribia shilingi sita bilioni? Au nimechanganya madawa?



From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, November 19, 2016 10:56 AM
Subject: [wanabidii] SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA



SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Na Happiness Katabazi

ITAKUMBUKWA  Kuwa 10/9/2016 saa 9 Alasiri maeneo ya Kanda ya Ziwa na hasa MKoa wa Kagera yalipatwa na tetemeko la Ardhi linalokadiriwa Kuwa na ukubwa wa 5.9 Katika vipimo Vya Richter. 

Tetemeko Hilo lilisababisha athari  mbalimbali zikiwemo Vifo ,majeruhi,uharibifu  wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi . Jumla ya watu 17 wa lipoteza Maisha na 560 kujeruhiwa kutokana na maafa hayo.


Kwa  siku Kadhaa sasa Kumekuwa na taarifa zikisambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyama Vya siasa Vya upinzani vimetoa  matamko ya kupinga uamuzi wa Serikali kutumia Rasilimali zilizopatikana kwa michango ya  kuwasaidia waathirika na kuendelea kuwarekebishia miundombinu muhimu kwa Maisha na manufaa ya wakazi wa Kagera.

 Wanaopinga uamuzi huo wa serikali wengine wamediriki Kusema " serikali ya Rais John Magufuli imetafuna Fedha za Waathirika wa Tetemeko Kagera', ' serikali ya CCM imekula hela za Ubani' ,wengine wanasema serikali ingie tafuta Fedha zake zenyewe ndiyo ijengee miundombinu na siyo Kujenga miundombinu kwa kutumia Fedha za michango waliochangiwa waathirika wa tetemeko la Kagera.

Lakini Novemba 15 Mwaka huu ,serikali ilitoa tamko lake na kupinga Madai hayo na Kusema huo ni upotoshaji kuhusu Hatua zikizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa Katika kukabiliana na maafa hayo. 

Serikali ikasema ukweli ni kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau  Imechukua Hatua kubwa za kuwasaidia waathirika na inaendelea kufanya Hivyo .

Ili kuleta uhalisia wa takwimu za Fedha ya maafa zilizotolewa kwa walengwa na wahisani mbalimbali,wananchi wangependa kupata data zifuatazo ili kuwaondoa wasiwasi ; 

Jumla ya Majina ya watu 17 waliopokea Maisha pamoja na kutaja familia zao. Majina ya majeruhi 569 kwa kutaja kila kaya na Hospitali zilizotoa matibabu na tarehe waliopatiwa matibabu na aina gani ya matibabu. Gharama za Mazishi kwa Kila kilichochogharamiwa kwa watu 17. 

Majina ya Wahanga waliyopewa Chakula kwa kutaja kiasi cha Chakula kwa kila Mhanga ,Madawa,nguo za aina gani na makazi yapi kwa kutaja kila Muhanga na kaya yake. Huduma za Tiba, Matunda aina gani na mangapi kwa kila mwathirika na vifaa gani na kwa kila shule na thamani.

 Vyote Hivyo viwekwe Kwenye Tovuti  ya serikali ili watu waone na wale wanaosambaza kile serikali inachoita ni upotoshaji waumbuke na hiyo ndiyo sifa Moja ya wapo ya serikali yoyote Duniani inayowajibika kwa uwazi.

Hata hivyo baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu niliyozungumza nao wamenitbitishia Kuwa kweli serikali ilitoa Sh.Milioni 1.8  kwa familia ya marehemu kama mkono wa pole .Ni  jambo  Jema.

Baadhi ya wananchi  wangependa kufahamu tathimini ya maafa yaliyotokea ya
Yalifanywa  Kwa  watu gani ,majengo ya aina gani na kwa watu wa aina gani kama masikini ,wazee,matajiri,majeruhi .

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali inaonyesha jumla ya Fedha taslimu iliyopo kelewa  Katika Akaunti ya Benki ya Maafa ni Sh.5,412,984,934.82 na Sh 17,579,427.00 zilipo kelewa na serikali kwa njia ya mitandao ya simu.

Serikali ilisema imeishapokea misaada mingine yenye thamani ya Sh.bilioni 2.25 kama ifuatavyo : Unga Tani 58.12, Sukari Mifuko 1,150 , Mchele gani 133.96 ,Maharage Tani 19.666,mahindi  Tani  70.1  na majani ya chai Tani 3.

Wananchi wangependa vilevile kupata orodha ya Majina waliyopatiwa vitu hivyo toka kila Wilaya ,Mkoa na Kaya na kiasia gani kwa kila mtu na vilevile wangetaka kujua kama kulikuwa na Tatizo la Maji Katika Mkoa wa Kagera hadi ukatolewa msaada wa Maji kwa walengwa.

Kuhusu miundo mbinu ya barabara Je ni barabara ngapi zimejengwa na Tenda ilifanyakazi lini gharama?gharama ya utengenezaji wa barabara ulifikiwaje na makandarasi  na Wakandarasi wapi walipewa Kazi hiyo ?

Mifuko ya Saruji 2,300 yenye thamani ya Sh.39,000,000 iliyotolewa na Shirika la World Vision iligawiwa kwa akina nani Katika Kaya 460 zilizotajwa na kila mfuko uligharamia kiasia gani?

Wananchi wanataka kujua serikali ilivyokuwa ikiwaamasisha wachangie misaada kwa waathirika  wa tetemeko la ardhi  walioanisha Makundi ya watu Maskini ,wazee,wajane na walemavu?  Au waathirika? Na tathimini ya kipato imefanyika lini?

Kama ndivyo Mbona serikali inapanga Kujenga Taasisi kwa kutumia Fedha za misaada badala ya kutumia Fedha za serikali?

Je serikali inawekwa katika kundi lipi Kati ya walemavu ,wajane na wazee au ni Maskini ?Kama ndivyo kwa nini msaada haukufikishwa kwa kila Muhanga?

Kama watu waathirika mtaji mkubwa ni nyumba zilizoharibika na hatakuwa na taarifa za Njaa kwa Sababu zilizoharibika ni nyumba za makazi na si Mazao 

Kwa hayo machache baadhi ya wanachi tungependa kumjulishwa na kumfafanuliwa vizuri kuhusu jinsi gani misaada iliyotolewa ilivyogawiwa  na Sababu ya kufanya msaada hiyo kugeuzwa Kujenga Taasisi za serikali wakati Taasisi hizo zinapaswa Kujengwa kwa Fedha za serikali.

Ikumbukwe Fedha hizi haziitaji  Uhakiki kama Fedha za mikopo ya wanafunzi wa Elimu yaVyuo Vikuu  ambazo Fedha za Bodi ya Mikopo zinataja  vigezo wa wanufaika wa mikopo  Kigezo Kimoja wapo ni watoto wa masikini  .

 Misaada na Fedha zilitolewa na makundi mbalimbali kwa waathirika wa Kagera zilitolewa kwa waathirika wote bila kubagua kundi lolote.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo:Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
19/11/2016.







Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment