Tuesday 22 November 2016

Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Masanja. Ubarikiwe kwa hili nitakalisema. Katiba iliyopo ilikuwa shirikishi. Nilishapoteza barua niliyopelekewa na Mfaume Kawawa akinishukuru kwa maoni yangu.kuhusu katiba. Hiyo ilikuwa 1970 au 77 kama sijasahau wakati wa wananchi kushiriki mjadala wa katiba kwa njia mbalimbali.
Rais Magufuli amesema katiiba hakikuwa kipaumbele chake katika uchaguzi 2015. Hadanganyi lakini hakusema kweli. Ngoja niseme kweli akanushe akitaka. Katiba ni kipaumbele chake na tayari mchakato umeanza.
Hatua za kwanza zitakamilika 2010. Ni kusafisha jamii ya kitanzania, kuondoa uovu uliozidi mpaka kuweka misingi bora ya kiuchumi na kuhakikisha watanzania wanajua wanachofanya na wanakoelekea. 2020 ataka[pokamiliasha mpango huo atakuja na agenda ya katiba mpya wakati akiomba ridhaa ya watanzania kwa awamu ya pili. Hapo watanzania wataandika katiba mpya wakiongozwa na Magufuli. Huenda itakuwa katiba bora kuliko ya Warioba ambayo watanzania waliandika kwa hasira kwa sababu ya maovu yaliyokuwepo. Kwa hiyo katiba bora inaweza kupitia barabara hiyo. Ukiondoa wenye chuki binafsi kwa Magufuli kwa sababu aliwashinda; watanzania watakuwa wamoja zaidi wakati huo
Elisa
--------------------------------------------
On Mon, 11/21/16, Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, November 21, 2016, 11:50 AM




Ndg. Elisa, Katiba inafuatwa sasa
kuliko huko nyuma ni mawazo yako kwa vigezo ulivotumia
kupima. La msing ni kwamba Katiba iliyopo haijawahi kuwa
shirikishi kwa Mwananchi wa kawaida katika uaandaaji wake.
Wanodai katiba mpya ni kwamba waliona mwanga fulani katika
huu mchakato na wanataka usiachwe ukazimika na ndiyo maana
wanadai mchakato wa Katiba Mpya urejerewe.
Ni kweli kabisa kuna mambo
yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano ambayo huko nyuma
ilikuwa ni ndoto kufanyika jambo ambulo ni zuri sana kwa
taifa. Mambo haya yakiachwa yaendelee kudumu kuwa maono ya
mtu mmoja bado si afya kwa taifa vile vile, kwa sababu
yanaweza kuporomoka Siku moja Kama ambavyo yamekuja. Katiba
mpya ndiyo suruhu ya hilo. Mambo mazuri yanayoendelea
yatengenezewe mfumo madhubuti ambao si rahisi mtu mwingine
kuyabadirisha au kuyaondoa kirahisi kwa masirahi yake
binafsi au ya kikundi fulani kidogo, hapo ndipo suala la
Katiba Mpya linapokuwa na umuhimu mkubwa.



2016-11-21 10:34 GMT+03:00
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Edgar.

sasa katiba inafuatwa kuliko wakati uliopita. Ndiyo maana
waliozoea kukwepa kodi wanashawishi watu kuwa katiba
inavunjwa. Mafisadi waliofikiri hawawezi kuguswa wanaguswa.
Ukichunguza sana utakuta wanaoshawishi wengine kuwa katiba
haifuatwi ni wale waliozoea kuivunja na watu tukafikiri ndio
utaratibu. Uholela hauwezi kuruhusiwa kuendelea bali
tujiruhusu kuzoea kufuata taratibu

------------------------------ --------------

On Sat, 11/19/16, Edgar Mbegu
<embegu@hotmail.com>
wrote:



 Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya
isubiri nchi inyooshwe

 To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>

 Date: Saturday, November 19, 2016, 3:18 PM





 Tusishabikie na ubabe wa ndani vile vile. Tusikubali

 nchi kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja hata kama ana
akili

 kiasi gani! Katiba iliyopo ifuatwe to the letter hata
kama

 ni mbovu. Utawala wa sharia utamalaki kwa maslahi ya wote
na

 siyo ya mtu au kikundi

  cha watu. 





















 Sent from Samsung

 tablet.















 -------- Original message

 --------

 From: 'Mashaka Makana' via
Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>

 Date: 19/11/2016 12:50 (GMT+03:00)

 To: wanabidii@googlegroups.com

 Subject: Re: [wanabidii] Magufuli
kasema yote: katiba

 mpya isubiri nchi inyooshwe













 Watanzania

 tusishabikie ubabe wa nchi kigeni kuwa ndiyo suluhisho
ya

 matatizo ya ndani ya nchi. Tunasiakia na kuona ya Libya
na

 kule Iraq watu walishabikia wakidhani ingekuwa suluhisho
ya

 tamaa ya mali

  na madaraka na kukubali kutumika na hawajapata
chochote

 zaidi ya kuharibu miundombinu ya nchi yao na vita vya

 wenyewe kwa wenyewe. Hii Demokrasia ya uchaguzi kila
baada

 ya miaka mitano ukilinganisha na gharama za uchaguzi ni

 hasara tupu na matumizi mabaya

  ya pesa za umma, Wakati wa kampeni za uchaguzi raia

 hawafanyi kazi kungojea mikusanyiko ya kampeni. Je. ni
hali

 ya namna hii na kwa nchi zenye utawala wa kifalme?
Msaada

 hapo!





















 From:

 'Lesian' via Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>



 To:

 wanabidii@googlegroups.com



 Sent:

 Saturday, November 19, 2016 11:39
AM



 Subject: Re:

 [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri
nchi

 inyooshwe











 Katiba

 iliopo ni'mbovu reuben.....inawapa watu mamlaka ya
ajabu

 anateua hadi wajumbe wa nyumbakumi...hawa ma dcs wa n
sasa

 kama si upotevu wa pesa......



 Katiba iliopo ni nzr kwa watu kama kina reuben tu

 wqnaofagilia kila jambo ilmradi limesemwa na kusimamiwa
na

 ccm



 Hawanaga mawazo mbadala na hawatak,'na maana yake

 hawataki kuona mbele na trump kaja atawanyooshen
subirin

 mnaokomaa madarakan navyma vyenu kaja komesha..teh teh







 'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:









 Mbegu;

 Sio

 kwamba inji haina Katiba kabisa,itanyooshwa na katiba

 iliyopo.

 Katiba

 iliyopo sio kwamba ni mbaya kabisa kwamba sawa na
haipo,

 mabadiliko ya katiba yana sehemu chache za kuboresha na

 kuongeza.

 Uhuni

 uliokuwepo/uliopo umetokana na kutofuata Katina, shaeria
na

 kanuni zake i.e. lazier free

  



 Reuben

























 On Thursday,

 November 17, 2016 7:42 PM, Edgar Mbegu

 <embegu@hotmail.com>
wrote:





















 Nchi itanyooshwa kwa sheria zipi? Kwa utaratibu upi?

  Kwa utashi wa mtu binafsi?  Ametumwa na nani?





















 Sent from Samsung

 tablet.

















 -------- Original message --------

 From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>

 Date: 17/11/2016 10:36 (GMT+03:00)

 To: ELISA MUHINGO' via Wanabidii

 <wanabidii@googlegroups.com>

 Subject: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya

 isubiri nchi inyooshwe













 Serikali

 za Wanyama na ndege au Wadudu;







 Ndani

 zina taadhima, kama kwamba maabudu;







 Na

 watu wenye hekima, siku hizi hawamudu







 Madaraka

 na heshima, heri mnyama na mdudu







 Vinywa

 vimewaachama, tamu imekuwa ngwandu







 Na

 heshima imehama baki taka na mashudu







 Na

 madhara na dhuluma miungu ya kuabudu









 (Shaaban

 Robert; katika "Kielelezo cha Fasili")







 SHAABAN Robert katika shairi nililonukuu hapo juu,
anaelezea

 madhara ya Uongozi na Viongozi wanapokosa maono, hekima
na

 heshima kwa wananchi akisema, inapokuwa hivyo heri
Serikali

 za Wanyama, Ndege au Wadudu zina taadhima kuliko za
viongozi

 wenye kukithiri

  kwa dhuluma na kujigeuza miungu watu.







 Japo gwiji hilo la ushairi Afrika Mashariki alikuwa

 akiandikia zama zake zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo

 fukuto la ufisadi, rushwa, kutoweka kwa uzalendo,
uadilifu,

 maadili ya uongozi na ubinyaji wa demokrasia ilivyo
sasa

 halikuwa jambo lililopevuka, lakini

  utabiri wake wa kinabii kwa yajayo hayo wakati huo
ulikuwa

 sahihi na ndiyo yaliyoikaba koo nchi yetu hivi leo.







 Ilivyo leo, na kama tunavyoambiwa na wataalamu wa siasa
na

 sayansi ya jamii kwa ujumla, suluhisho la maovu haya ya

 kijamii ni kwa njia ya Katiba ya nchi itakiwayo na
itokanayo

 na wananchi wahanga wa maovu hayo, kwa njia ya maoni na
kura

 ya maoni.







 Pengine ni kwa sababu hii miaka ya karibuni, na hasa

 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwamba suala la Katiba
mpya

 lilikuwa ajenda moto, na zaidi kwa vyama vya upinzani

 vilivyodai kuwa Katiba iliyopo imepitwa na wakati kwa
sababu

 iliandaliwa katika mazingira

  tofauti na ya sasa miaka 40 iliyopita.







 Tangu mwanzo, Serikali, kupitia Mwanasheria wake Mkuu
(AG)

 na mara nyingi pia kupitia waziri mwenye dhamana ya mambo
ya

 Katiba na vigogo wengine wa chama tawala, ilitamka wazi

 kuwa, "Katiba mpya si ajenda ya serikali
madarakani",

 tamko lililochukuliwa na wengi

  kama sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa viganja vya

 mkono.







 Hatimaye mwaka 2012, serikali ilisalimu amri kwa

 "mafuriko" hayo kwa kuteua Tume ya Kupendekeza
"Rasimu

 ya Katiba", chini ya uenyekiti makini wa Jaji Joseph
Sinde

 Warioba kwa matarajio kwamba Katiba hiyo mpya ingetumika
kwa

 mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu

  wa Oktoba 2015.







 Hadi kipindi hicho na mpaka sasa, nchi yetu ilikuwa na
moja

 ya Katiba bora Afrika Mashariki – Katiba ya Jamhuri
ya

 Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ukiondoa

 mapungufu machache kadhaa yaliyomo, likiwamo lile la
harufu

 ya chama kimoja; madaraka makubwa

  ya Rais (Mhimili wa Utawala) dhidi ya mihimili mingine


 Bunge na Mahakama na baadhi kuhusu Muungano, ilitosha na
kwa

 utoshelevu mkubwa katika ujenzi wa demokrasia na
utawala

 bora nchini.







 Ni mwananchi gani mpenda demokrasia ya kweli bila
kificho,

 anaweza kubeza ubora usio na mshindani wa Katiba hii
kwa

 mambo muhimu inayotetea, kama vile, "malengo muhimu
na

 misingi ya shughuli za serikali madarakani" (ibara 6


 11); na "Haki ya Usawa

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment