Thursday, 24 November 2016

Re: [wanabidii] MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU

Katabazi.
Ukiwa msomi, muelewa wa haki za binadamu (kwa taaluma yako ya sheria) na huku ukijua kuwa huyu jamaa ana watu wanaomuona kaqma " mungu" kwa kumwita majina kama katapila na mengine mengi, ukijua kuwa watu hao waliyahama makanisa yao wakidhani sasa wanamfuata Mungu kwa mtu kama huyo (kwa hiyo waumini hao ni victims). Ulikosaje kupiga picha ya video ukaweka humu potelea kote ufungwe lakini uwasaidie watu hao??? Umekosea sana. Majuzi niliandika makala humu watu wakaogopa kuijadili (isheheni vifun gu vya biblia vinavyokataa viongozi wa kihuni wanaojitokeza kwa njia ya ibada na kupotosha watu) pengine kwa kudhani huyu jamaa anamhubiri Mungu. Huoni kuwa hapo umeuzuia upanga wa Bwana usimwage damu (Yeremia 48: 10). Nyoka hupigwa kichwa sio kiwiliwili.

--------------------------------------------
On Thu, 11/24/16, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, November 24, 2016, 10:59 AMMCHUNGAJI
ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI
HUU
Na
Happiness Katabazi
MITHALI
20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo
huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo Hana
Hekima".
Nimelazimika
kutumia nukuu hiyo ya Biblia Kuonyesha matendo ya kishetani
yaliyotendwa Jana hadharani na Kiongozi wa Kanisa la
Maombezi nchini lenye masikani yake Ubungo Kibangu Dar Es
Salaam,Anthony Lusekelo yana baraka  za kitabu cha
Mithali 20:1 Katika Biblia Kwani matendo Yale aliyoyatenda
ambayo nimeyaanisha Katika ndani ya makala hii ya
lithibitishwa mtumishi Huyo wa Mungu Hana
Hekima. 
Jana
23/11/2016   nikitoka nyumbani kwetu saa 11 asubuhi
  Sinza  C nakuelekea  University of Bagamoyo
eneo la Kawe Beach Dar es Salaam  Ambapo chuo hicho
kimepakana na Ofisi ya Redio Times kwaajili ya kukamilisha
mambo yangu ya kitaaluma.
Hatua
chache kabla ya kufika chuoni hapo ni kama nyumba  Tatu
kurudi  nyuma  kuna Ukumbi unaitwa Mtana Multipose
Hall  na katikati kuna barabara ya vumbi
inayotenganisha nyumba zilizopo upande wa kushoto na kulia
.Ni barabara ndogo ambayo Dereva hawezi geuza Gari
 hadi aende Mbele zaidi.
 Upande
wa kulia wa ukumbi huo wa Mtana Multipose Hall kuna nyumba
 ya ghorofa ambayo inalimdwa na walinzi wa makampuni ya
Ulinzi  ambao walinzi Hao  ni Waaafrika na
wanaishi pia raia wa kigeni .
Nyumba
ina namba  KAW / MZN/ 1348  ambayo imebandikwa
katika ukuta wa geti la nyumba hiyo na mabango ambayo
yanayoonyesha nyumba hiyo inalindwa na kampuni ya ulinzi
nyuma ya nyumba hiyo ni  Bahari ya Hindi .
Saa 12: 32 asubuhi nilipita Katika njia
hiyo nikiwa nimepanda usafiri wa aina ya Bajaji kwaajili ya
kwenda Chuoni kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma
 nilipofika  katika eneo la nyumba hiyo yenye
namba KAW /MZN / 1348 inayotenganisha
nyumba zilizojengwa  upande wa kulia na kushoto na
Kabla ya kufika chuoni ambapo ni mwisho kabisa ya barabara
hiyo nyembamba nilikuta Gari limesimama katikati ya barabara
yenye namba za usajili  T126 DFN  huku watu kama
nane  wakiwa wamesimama pembeni ya Gari Hilo huku
wakimtazama mtu mmoja aliyekuwa akiongea kwa sauti ya juu
nje ya geti ya  nyumba hiyo.
Mimi
nilipofika karibu nione kuna nini na kwanini Gari limeziba
njia na nani Kaziba njia Yule anayeongea kama kuna ugomvi
ninani niliposogea Karibu nikabaini aliyekuwa anafoka ni
Mchungaji Anthony Lusekelo  maarufu " Mzee wa
Upako.
Nilishtuka
nikamtaka Dereva anishushe Mara Moja licha safari yangu
ilikuwa haijafika mwisho licha ni Hatua Chache kufika chuoni
Kwangu ili niwahi kwenda kumsihi Mchungaji Lusekelo aondoke
eneo lile Mara Moja Kwani yeye ni kiongozi wa Kiroho na
Mtumishi wa Mungu haifahai , kujibizana na watu tena
hadharani Kwani mwisho wa siku anayedhalilika ni
yeye.
Nilimkaribia
Mchungaji Lusekelo na kumshuhudia kwa macho yangu akiwa
anatoa lugha za matusi na zisizofaa kwa wakazi wa nyumba
Namba KAW / MZN/ 1348 huku akiwa amesimama nje ya geti la
nyumba hiyo ambayo wanaishi pia Raia wa kigeni huku
akisikika akisema wamezidi kumchokoza kwa kumuita yeye ni
Mlevi.Nilihisi  kuchanganyikiwa kabisa maana sikuamini
nilichokuwa nilikushuhudia.
Mzee
wa Upako ni miongoni wa wapenzi wa makala zangu  
 na zaidi ya Mara Tatu alishanipigia simu kunipongeza
kwa ujasiri wangu wa kuandika makala zenye Lengo la Kujenga
nchi na Akawa anasema ananiombea kwa Mungu azidi kunilinda
ili niendelee kuandika.
Namimi
pia nimekuwa nikifuatilia   mahubiri yake kupitia
Televisheni ya Chanel Ten , Mara kwa Mara ila sikuwahi
kubahatika kuonana ana kwa ana na yeye hadi Jana saa 12
asubuhi nilipomuona akiwa Katika Hali ile ambayo siyo ya
binadamu wa kawaida .
Ambapo
nilimsabahi nikamwambia Mimi ni Muhumini wake na ni
mwanafunzi wa Univeristy of Bagamoyo chuo ambacho kipo
nyumba ya pili kutoka nyumbani kwake .
Licha
 ukweli ni kwamba Mimi siyo muumini  wa Kanisa
lake . Nililazimika  kuficha jina langu ili asinijue
kwani ningemtajia jina langu tu lazima angenifahamu kuwa
mimi ni Mwandishi wa habari ' Mkonoko ' ambaye
amekuwa akiwasiliana namimi na kunipongeza kwa makala zangu
kwasababu  angekosa amani kwasababu Angejua waandishi
wamemuona.
Kwa
mujibu wa wale watu Saba  niliyowakuta eneo la tukio
saa 12 asubuhi walinieleza Mzee wa Upako asubuhi hiyo
alikuwa anatoka alikokuwa atatokea ndiyo muda huo alikuwa
akirudi nyumbani kwake ndipo aliposimamisha Gari lake Hilo
Mbele ya geti ya nyumba ya jirani yake yenye Na.KAW/MZA 1348
ambapo ndani ya geti Hilo kuna walinzi alianza kujibizana na
walinzi akidai wamekuwa wakimkebehi yeye hafai Kuwa
Mchungaji kwasababu ni Mlevi kupita kiasi.
Nilimsii
sana hadi saa Moja asubuhi ikanikuta eneo Hilo la tukio huku
Mvua ikitunyeshea nikimwomba anisikilize  aache
kutukana,kufoka Katika eneo la nyumba ya watu kwasababu yeye
ni mtumishi wa Mungu anajidhalilisha ,na anavunja
 Sheria za nchi Kwani kutoa lugha chafu ni kosa la
jinai,na pia kuziba njia ili watu wasipite kwasababu eti
anaugomvi na wale watu siyo ustaarabu na anavunja Haki za
watu wengine za kwenda Kokote watakako .
Sasa
yeye Mzee wa Upako kwa kitendo Chake kile kuegesha Gari
katikati ya barabara ile nyembamba ni kuvunja Haki za watu
wengine wanatumia usafiri wa Magari Katika barabara ile
wasiende wanakotaka kwenda kwaajili yake na kweli
alifanikiwa Kuzuia Magari  yasipite eneo Hilo kwa zaidi
ya muda Kadhaa huku Mvua ikinyesha na wengine wakichelewa
kwenda Katika shughuli zao kwa muda .
Baadae
alinisikia huku akiwa ameloana maana Mvua ilionyeshea
alikuwa akisikika akinuka Pombe  huku akiyumbayumba
akafungua Gari lake akatoa Kikapu kilichokuwa kinachupa za
Maji ya Kunywa ,kavaa viatu Vya wazi  na kashika miwani
huku akiwa amekunja suruali.
Nikamsaidia
Kubeba miwani na funguo wa Gari tukaelekea  
 nyumbani kwake ambapo ni jirani kabisa na eneo la
tukio huku tukinyeshewa na Mvua tutafika nyumbani kwake saa
Moja asubuhi tukafunguliwa  geti na vijana wake
nikamuingiza hadi ndani ya geti la nyumba yake  na
vijana wake wakanihoji nimetoka na baba Yao wapi asubuhi ile
maana ndiyo baba Yao anarudi nyumbani muda ule tangu
alivyoondoka Juzi (Jumanne) .
Nikawajibu
nimetoka aye nyumba za Mbele alikuwa akigombana kwa maneno
ndiyo nikamuondoa eneo la tukio nakumleta nyumbani kwake
hapo kama msamalia Mwema.
Vijana
wake wakatukaribisha  Mimi na baba Yao ( Mchungaji
Lusekelo)  .Mzee wa Upako huku akiendekea kuongea kwa
sauti ya juu akaingia ndani na kile kikapu na Mimi nikampa
ile miwani niliyokuwa nimeishika ,akaingia nayo ndani Kisha
akarudi ndani ya uwa wake   akaanza  Kuwaeleza
vijana wake Kuwa yeye hata siku Moja hataki
kudharauliwa,kuonewa  na atapambana  .
Wakati
huo Mimi ule funguo wa Gari bado nilikuwa nimeishikilia
kwaajili ya kutaka niwape wale vijana wake waende kukichukua
lile Gari lilokuwa eneo la tukio walilete nyumbani wa Mzee
wa Upako ili wananchi wengine waweze kutumia ile
barabara.
Mzee
wa Upako baada ya kumfikisha nyumbani wake aliniambia
anaishukuru sana kwa kumfikisha nyumbani salama  na
akaniambia ananiheshimu sana Mimi ni kama binti yake ila
nimsamehe sana yeye anarudi eneo la tukio kwaajili ya
kuendelea kupambana na wale majirani ambao ni
Wazungu.
Nilimsii
 sana Aiingie ndani akaoge,alale  kwanini yeye
mwenyewe ndiyo ameniambia muda ule wa asubuhi ndiyo alikuwa
akirudi nyumbani kwake akitokea katika matembezi yake ya
jioni lakini akakakata akaanza Kuwaeleza vijana wake
amedhihakiwa kwa kuambiwa yeye hafai Kuwa mtumishi wa Mungu
Kwani ni Mlevi sana wakati mtumishi wa Mungu hapaswi Kuwa
Mlevi na kufanya vurugu.
Vijana
wake wale walivyokosa akili na busara wakaungana na uamuzi
mbovu wa baba ya I wa kurudi eneo la tukio wakati Mvua
ikinyesha kwaajili ya kwenda kuendelea Kujibu
mapigo. 
Kwa
zaidi ya Mara Sita nikawabembeleza  wale vija na wake
waache upumbavu huo Mzee wa Upako ni mtu mashughuli nchini
na kiongozi wa kidini wasiruhusu tena baba Yao kurudi tena
eneo la tukio kwenda tena kufanya Fujo siyo vizuri Kwani
mwisho wa siku Atakayedhalilika ni baba Yao.
Nikawataka
wale vijana wasikilize ushauri wangu wamfungie ndani Baba
yao ( Mchungaji Lusekelo ) a kalale Kwani anaonekana
amechoka sana hajapumzika maana kanieleza alfajiri ile ndiyo
alikuwa akirudi nyumbani kwake.
Ili
Mimi niwapatie ule ufunguo wa Gari la baba Yao ili wao
vijana ndiyo waongozane na Mimi   nikawaonyeshe eneo la
tukio na Gari lilipoegeshwa Katikati ya barabara ,wale
vijana walinijibu ' uwa hawatakagi
Ujinga'.
Haraka
sana wakanitaka niwape funguo nikawapa , huku Mzee wa Upako
 akiiondoka hapo ndani kwake kurudi Katika eneo la
tukio Kujibu mapigo huku Mzee wa Upako akiwa miguu peku
,vile viatu vyake Vya wazi ( Open Shoes ) vyenye rangi
nyeusi Nikiwa nimevishika Mimi wakitembea Mwendo haraka na
vijana wake ambapo njia nzima Mzee wa Upako alikuwa akifoka
na matope miguuni.
Na
alipofika tena eneo la tukio la wale vijana wake huku Mimi
Nikiwa nimebeba Open Shoes zake ambazo nimezipiga picha
.
Tayari
kulikuwa kumeishapambazuka watu wamejaa anaendelea kufoka
Magari hawawezi kupita kwasababu Mchungaji Lusekelo aligoma
kuondoa Gari lake katikati ya barabara huku akisema aondoi
 Hilo Gari hadi Rais John Magufuli na RPC Simon Sirro
waje ndiyo wataliondoa Hilo Gari.
Nilisikitika
sana Kwani jitihada zangu za Kuzuia Mchungaji Lusekelo
asidhalilike  Mbele ya umati wa watu kadri kunavyozidi
 kupambazuka Kwani watu walizidi kujaa na kumshuhudia
Vituko alivyokuwa akivifanya huku akilindwa na vijana wake
ambavyo Mtumishi wa Mungu hapaswi kuvifanya.
Nikahamua
kukaa Mbali kujifanya natuma SMS Katika simu yangu Kumbe
napiga  picha vile viatu vyake alivyoniachia ,na Gari
yake iliyokuwa imageshwa katikati ya barabara Mbele ya geti
la nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo tukio Hilo la aina yake
lilitokea hadi saa mbili asubuhi Jana .
Hata
Hivyo wale wale vijana wake alinishitukia  napiga picha
tukio lile walitaka kunipiga kisa nampiga picha baba Yao
.
Kwa
makusudi  Niliamua kukanusha Kuwa sijapiga picha na
kusingizia Mimi Nina matatizo ya macho hivyo nilikuwa Nasoma
SMS lazima simu niinue juu na nisogeze  karibu na macho
yangu.
Mmoja
wa kijana wake akanitishia kunipiga ikabidi nimbadilikie
 na kumtaka kwanza anikome, cha pili jeuri ya kunipiga
Hana,Tatu sikumtuma baba yake arudi alfajiri aanze kufanya
vituko vile vya kujidhalilisha,nne nikamwambia yule kijana
ni shetani mwenye Mkia  ndiyo maana wameshindwa
Kumfungia ndani  Mzee wao ( Mchungaji Lusekelo ) aache
kufanya Fujo Mbele ya umati wa watu wakati wana nguvu za
kumzuia na baba Yao Huyo ni kiongozi wa kiroho anajishushia
heshima.Akawa mpole.
Akageuka
pembeni nikawaweka mkono wangu nyuma kiaina ,nikairusha
 simu yangu kwa nyuma Kwenye  majani na kulikuwa
na majani yanaunyevu unyevu wa Maji ya Mvua   ili hata
akianza kunipiga na kunilazimisha nimpe simu ,ashindwe
kuipata simu.

Kijana
Yule ambaye alioneka ni mtu wa mazoezi na
misuli alivyoona sijamuogopa Akaamua kuondoka
nilipokuwa nimesimama mimi na akasogea  eneo la
tukio na kumshuhudia Mzee wao  Mchungaji Lusekelo
akizidi kufoka nikageuka nyuma haraka nikaokota simu yangu
nikaenda kusogea Mbali nikampa mwanamke mmoja anayefanyakazi
 chuoni kwetu anishikie tukasogea mbali
na  aneo la tukio ,tukasimama  mbele ya geti
la Redio Times na kuendelea   Kutizima  Sinema
yote ilivyokuwa ikiendelea ambayo Mwongozaji wa Sinema
alikuwa ni Mchungaji Lusekelo.
Kumbe
vile vitendo vilivyokuwa vikifanywa na Mchungaji Lusekelo
Jana Mbele ya Hadhara viliwakera   wakazi wa eneo hilo
na watumiaji wa eneo hilo  licha ni la makazi ya watu
lina Ofisi  pia na chuo wakaamua kupiga simu polisi kwa
siri .
Baada
ya muda mfupi polisi wa Kituo cha Kawe walifika eneo la
tukio na kushuhudia tukio hilo na kuondoka na Mchungaji
Lusekelo na kwenda kumuifadhi ndani ya kituo hicho kwa muda
 kwa saa Kadhaa.
Hata
hivyo taarifa toka ndani ya Kituo hicho zilieleza Kuwa licha
ya Mchungaji Lusekelo kuifadhiwa ndani ya Kituo hicho
 aliendelea kutoa lugha zisizo na staha kwa baadhi ya
Askari Polisi ambao walikuwa wakimshangaa Kuwa imekuwaje
yeye ni mtumishi wa Mungu halafu amekunywa Pombe kiasi kile
na anatoa lugha zisizo na staha .
Hata
hivyo mchana wa jana kuna taarifa ambazo hazikuwa
 zimethibitishwa  Kuwa Mchungaji Lusekelo
alihamishwa pale Kituo cha Polisi Kawe na kupelekwa Katika
Kituo kingine.
Kwa
mujibu maelezo hayo ya tukio Hilo la ' Sinema ya
Bure' nililolishuhudia kwa macho yangu yaliyokuwa
yanafanywa  na Mchungaji Lusekelo huku akiwa Katika
Hali isiyokawaida kwa zaidi ya saa mbili ya kufoka na kutoa
lugha chafu na kuleta Usumbufu Katika eneo la nyumba ya
jirani yake  limenifundisha mambo mengi ikiwemo Mimi
Leo kukubaliana ule usemi usemao ' Mungu adhihakiwi'
Kwani ukimdhihaki atakuumbua hadharani.
 Mchungaji
Lusekelo ni muhubiri maarufu nchini na ana waumini wengi
sana nchini ndani na nje ya nchi na wamekuwa wakimuamini na
hata serikali ya sasa inayoongozwa na Rais John Magufuli
Inamuamimi na hata Rais Magufuli Mwenyewe siyo Siri
anamuamini mtumishi huyu wa Mungu Mchungaji wa Lusekelo na
alishampongeza Lusekelo kwa Kazi nzuri anayoifanya ya kutoa
huduma ya Kiroho kwa Watanzania ambao ni waumini wake
.
Juni
5 mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza
katika kanisa hilo ambapo alienda kwaajili ya kusali katika
kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo na Rais Magufuli
akatumia fursa hiyo kuzungumza kanisani hapo eneo la Ubungo
Kibangu na akamwagiza sifa Lusekelo Kuwa anafanyakazi nzuri
ya Kiroho.
Magufuli
akasema kwa  mamlaka aliyonayo ameishaagiza mamlaka
zake zianze mchakato wa Kujenga barabara Inayopita Katika
Kanisa la Mzee wa Upako ili waumini na wananchi wa eneo
wasiendelee kupata tabu kwasababu barabara ile ni Mbaya
sana.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi  walipinga uamuzi huo wa Rais
Magufuli na walidai uamuzi huo ni wa upendeleo waziwazi na
wakukurupuka.
Licha
ya Lusekelo ya Kuwa na heshima kubwa nchini hadi Rais
Magufuli Akaamua kwenda kusali kanisani kwake lakini Jana
alishindwa kutunza Umaarufu wake,heshima yake aliyokuwa nayo
Katika Jamii kama kiongozi wa Kanisa lenye waumini Wengi
Akaamua kuporomosha matusi hadharani ,kuyumbayumba wakati
amesimama Na kutembea Mithili ya mtu aliyelemewa na kilevi.
 Uzuni.
Vituko
vile alivyovifaya Jana Mchungaji Lusekelo pia vimenifundisha
Mimi binafsi Kuwa kuanzia Jana niache tabia ya Kuwa mgumu
kuamini /kunisha baadhi ya  taarifa za mambo
 machafu yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa
Mungu.
Miezi
mitatu iliyopita kuna watu watatu  toka vyombo Vya
Ulinzi na Usalama walinieleza Huyo Mchungaji Lusekelo ni
Mlevi mzuri tu wa Pombe aina ya Konyagi na wakati mwingine
anavyokuwa madhabauni anavyokuwa na kitaulo anajifuta jasho
mara kwa mara ni zile pombe kali zinakuwa zinachemka mwilini
zinamfanya ajisikie jasho na walishamnasa katika matukio
zaidi ya Mara Tatu  akiwa hoi kwa kilevi ,kwakeli
nilikuwa mgumu kuwakubali maelezo hayo kwasababu kwanza
sikuamini na niliwaona wale maofisa ni wazushi .
Ila
Jana asubuhi nilichokiona kilichokuwa kikifanywa na Mzee wa
Upako Mbele ya umati watu ,na alivyokuwa ananuka pombe ya
kuyumbayumba nilikubaliana na Yale waliyonieleza watu wale
na nikachukua simu nikamupigia mmoja baada ya mwingine na
kuwaambia kweli waliyonieleza Leo Mungu amenileta eneo la
tukio nithibitishe Yale waliyonieleza Kuwa Mzee wa Upako
naye anakunywa Pombe.
Hata
hivyo mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka mitatu  sasa
tukikaa wote sebuleni tukiwa tunaangalia Kipindi cha
Mchungaji Lusekelo kinachorushwa na Channel Ten ,mama
amekuwa akiniambia huyu Mzee wa Upako ana michanganyo yaani
alikuwa anamaanisha  Kuwa licha ni Mchungaji ila bado
anafanya mambo ya kidunia ambayo Mungu hayapendi.
Basi
mama akisema hivyo namwambia aache hiyo tabia ya kumsema
Mzee wa Upako kwasababu Hana ushahidi.Mama anasema haya
anafunga mdomo ila ipo siku Mungu atamuanika hadharani ndipo
nitakapoamini.
Kweli
kupitia tukio la Jana aliyofanya Mchungaji Lusekelo
,Nimelazimika kukubaliana na maneno ya Mama yangu Mzazi
kuhusu Mzee wa Upako Kuwa licha ni mtumishi wa Mungu bado
anafanya matendo ambayo Mungu hayataki  mfano
Fujo, kutoa lugha zisizonastaa,kulipa kisasi wakati Mungu
anatutaka tusamehe ,tusi lipe kisasi kwa watesi wetu lakini
Mchungaji Lusekelo alishindwa kuwasamehe watesi wake na
Akaamua Kupambana na maneno makali huku alipokuwa Kaipamba
nao wakiwa wanamtazama hawamjibu.
Lusekelo
ni binadamu kama Sisi ila tofauti yetu na yeye amejipambanua
kama mtumishi wa Mungu ambaye ni kiongozi wa Kiroho hivyo
Hakupaswa kufanya Yale yote aliyoyatenda Jana ambayo
niliyashuhudia kwa macho yangu ambayo kwa kiasi Fulani
yalinivuruga  akili na akili zangu za kawaida Jana
mchana.
Maana
sikutengemea kumkuta kiongozi wa dini akiwa Katika Hali kama
ile aliyokuwa nayo Mzee wa Upako na kufanya matendo Yale
ambayo uwafanywa  na watu wasiyo na hofu na Mungu
na hawajashiba  neno la Mungu.
Hata
hivyo Fedhea iliyomkuta Jana Mchungaji Lusekelo pia naweza
Kusema licha Mimi nilikuwa anajitahidi kumuokoa Lusekeo as
izidi  Kuaibika Mbele ya watu Wengi Kumbe Mungu
 naye aliamua kuruhusu mtumishi wake Huyo wa Mungu
afedheheke  Mbele ya watu Wengi ili watu wa mjue Kuwa
mtumishi Huyo wa Mungu ambaye Kutwa anahubiri  
neno la Mungu naye Si Msafi  na kwamba anayefanya Mambo
ambayo Mungu ameyakataza.Na kweli Mungu Jana kumdhalilisha
kweupe Lusekelo. Mungu anatisha.
Nilikuwa
najiuliza hivi ndiyo mmoja wa waumini wake angepata fursa ya
kushuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya Mchungaji Lusekelo
Jana au kama Alikuwepo muumini Akawa anashuhudia tukio lile
,wamejisikiaje? 
Hata
hivyo tukio la Jana pia limenifanya nikubaliane na Kauli ya
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani alisema
 hivi : ' Kuna baadhi ya viongozi wa dini Si wa
safi,ni wachafu na wengine wanauza dawa za
kulevya'.
 Nimuulize
Mchungaji Lusekelo hivi kupitia tukio
lile  ,atapata wapi tena ujasiri wa kusimama
madhabau ni kuwataka waumini wake wasitumie vileo,wasilipize
Ubaya kwa Ubaya ,wasiingie Katika vita ya maneno na watesi
wao?
Sikutaka
kuandika makala hii ila ni mejikuta nikijiuliza ni kwanini
Mungu alipenda nikutane na Mchungaji Lusekelo kwa mara ya
kwanza ana kwa ana akiwa katika hali ile na akiwa anafanya
matendo yale ya kishetani?
Kwanini
Mungu asingepanga nikutane na Mchungaji Lusekelo akiwa Mzima
ananukia harufu  ya mafuta mazuri badala ya halufu ya
kileo na akiwa anafokea na kutoa lugha chafu dhidi ya jirani
yake na kuziba njia na kusababisha kuziba njia kwa muda na
hali ya sintofahamu ?
Na
Kwanini Mungu hakuruhusu waandishi wa habari wengine wapige
asubuhi ile jana katika eneo hilo ili washuhudie tukio Lile
isipokuwa mimi Mwandishi wa Habari Mimi Happiness Katabazi
peke yangu?
Nikahitimisha
 kwa Kusema Huyo  ni Mungu ndiyo aliyesababisha
mimi nikutane na Mchungaji Lusekelo ambaye kwa zaidi ya
miaka minne tumekuwa tukiwasiliana kwa simu ila jana
nikakutana naye ana kwa ana na ndiyo  ananisukuma
niandike makala hii ambayo imeanika   matendo hayo ya
kishetani yaliyotendwa na Mchunga Kondoo wa Bwana  (
Lusekelo)  ili watu waumini wake na watu wengine wajue
matendo yanayotendwa na Lusekelo  nje ya
madhabau.
Na
wao wenyewe wapi me Je  Mzee wa Upako ambaye ni kinara
wakulusha ' Madongo' Je anastahili kuendelea
kuaminiwa Kuwa kiongozi wa kidini na Baba wa Kiroho wa
waumini wake ?
Nikajikuta
nachukua Kompyuta na kuacha kwenda GYM kufanya mazoezi ya
viungo  Jana jioni nikaa chini hadi saa Kumi alfajiri
wa usiku wa kuamkia Leo nilipomaliza kuiandika.
 Kwa
 kupitia makala hii ambayo itamfedhehesha Lusekelo kwa
kiasi Fulani  na Imani kwa baadhi ya watumishi wa Mungu
itazidi kutiliwa Shaka lakini neno la Mungu litasimama
.
 Uenda
makala hii  akiisoma anaweza kujirudi na asirudie tena
Kutenda matendo yasiyompendeza  Mungu Kwani yeye
Lusekelo ni mtumishi Mungu anapaswa asitende mat endo ya
kishetani kama Yale  aliyoyafanya  badala yake
abaki na kazi moja ya kumtumikia Mungu tu .Na ni aomba iwe
hivyo.
Kwani
hata EZEKIELI 3:19 Katika
Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala
yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa
Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.
Hivyo
kupitia kitabu maneno hayo yaliyopo Katika kitabu cha
Ezekiel ,Mimi nimeitimiza wajibu wangu kwako wewe Mtumishi
wa Mungu Lusekelo kukuonea ili uache michanganyo ya mambo ya
kidunia badala yake Ubaki na jambo Moja tu la kumtumikia
Mungu.
Mchungaji
Lusekelo Kumbuka  Biblia inasema Mungu wetu ni Mungu
mwenye wivu na hataki michanganyo.
Ukiamua
kumtumaini / kumtumikia basi Ufuate mafundisho yake na
uyatii  maandiko yake Kwani Mungu anauwezo wa kukuinua
na kukushusha  pindi Akiamua.
Lusekelo
Mungu ameinua huduma yako lakini sasa umeanza kurudi nyuma
una michanganyo kama hiyo.Siyo vizuri .Mungu
hapendi. 
Nina
Hakika ungekuwa mzima usingetenda matendo ya kishetani
uliyoyatenda Jana asubuhi Mbele ya kadamnasi .
Au
ulivamiwa na mapepo ndiyo ya kakutuma  utende ushetani
ule ambao ulikufedheesha ?Kwa lugha nyepesi ulikuwa umelewa
.Aibu sana mtu wa Mungu.
Ingia
ndani tubu kwa Mungu wako atakusamehe songa Mbele ila tu
wale watu wote waliokushuhudia Jana ukiwa Katika Hali ile na
kufanya vitendo vile Vya kishetani siyo rahisi tena kuiamini
huduma ya Kimungu unayoitoa.Nisamehe sana.Licha Nitaendelea
kukuheshimu na kukupenda.
Kama
 kweli Mchungaji Lusekelo umeitwa na Mungu umtumikie
,sikutegemea kabisa mimi binafsi au umati ule watu huku
ukiwa umelewa Pombe na huku hujavaa viatu   ukifanya
ushetani ule hadharani tena asubuhi asubuhi.
Inatisha.
Mchungaji
Luseleko kama kweli umeweza Kutenda ushetani huo wa
kuporomosha matusi hadharani ,nakuwa Katika Hali ile
isiyoyakawaida ambayo unafahamu Mungu hataki matendo Yale
,Kesho wewe utashindwa kuingia tamaa ya kufanya mambo
yasiyompendeza Mungu kama kwenda kufanya matendo ya
kishirikina ili uwapumbaze waumini wako waendelee kuamini
Kuwa ni mtumishi safi wa Mungu Kumbe unatenda matendo sirini
yasiyompendeza Mungu?
Hivi
Leo hii watu wakikurushia vijembe Kuwa Sadaka zinazotolewa
na waumini wako pia unazitumia Katika ulevi ,Utakataa au
utasema wanakuonea wivu?
Pombe
inavishawishi Vingi sana na inaweza kumshawishi mtu
aliyekunywa kufanya chochote anachokisia ikiwemo hata
kufanya  zinaa.
Hivi
ule ushetani ulioutonda Jana  wewe Mzee wa Upako
,wakiibuka watu wakisema unywagi Pombe tu pia hata dhambi ya
uzinzi unatenda ,utakuja kukataa useme wakuzushie?

Pole
waumini wa Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo Kwa
makala hii Kwani nafahamu baadhi yenu itawakwaza ila ndiyo
mvumilie ukweli ndiyo huo niliyoohushudia Mimi kwa macho
yangu nanilitahidi kumsitili kiongozi wenu ili asidhalilike
bila mafanikio na mwisho wa siku nilichoambulia nikutaka
kupigwa na vijana wake .
Ila
roho yangu nyeupe na wala makala hii haina Lengo la kuwazuia
muache kumuabudu Mungu kupitia Kanisa linaloongozwa na
Mchungaji Lusekelo.
Namimi
ni madhaifu yangu sikatai ila bado sijafikia Hatua ya kama
alifikia Lusekelo ya Kuwa mtumishi wa Mungu halafu kufanya
matendo hayo ambayo kila Mara amekuwa akisimama madhabauni
Kukataza waumini wake wasiyafanye kwasababu Mungu
ameyakataza Kumbe yeye Anayafanya .
Lengo
la Makala hii ni Kuonyesha Mchungaji Lusekelo ambaye
anasimamaga madhabau ni anakemea dhambi Kumbe na yeye
anatenda baadhi ya dhambi.Mtaamua wenyewe.Ila nawashauri
sote tumuombee maana sote sisi ni binadamu Hakuna Mkamilifu
.
Ila
kuna utofauti wa upokewaji wa Jamii wa baadhi ya matendo ya
dhambi yanayofanywa hadharani na viongozi wa kidini na
matendo hayo hayo ya dhambi yakifanywa Na mtu ambaye siyo
kiongozi wa kidini.
Mtumishi
wa Mungu akitenda  dhambi za aina hizo alizozitenda
Mzee wa Upako Jana za kutukana ,ulevi Jamii zitaipokea kwa
uzito wa aina yake na kwa Mshangao mkubwa sana.
Hakuna
ubishi Mchungaji Lusekelo umefedheheka Jana tena sana Katika
eneo unaloishi Kawe Beach Karibu Univeristy of Bagamoyo na
Redio Times .Kaa utulie,maana Hasira ya Mungu Jana
imekushukia ,tubu Mungu atakusaidia uondokane na shetani wa
Kupenda Konyagi na aina nyingine za Pombe Kali.
Mchungaji
Lusekelo kama utashindwa kuachana na anasa za Dunia basi
achana na Kazi ya Mungu ili uwe huru kufanya mambo ya anasa
kuliko Jumapili na siku za katikati ya wiki Una
Simama  madhabauni unaubiri neno la Mungu Kumbe
ukitoka madhabauni unaenda kufanya mambo yasiyompendeza
Mungu ukiwemo Kunywa Pombe.
Mchungaji
Lusekelo jana kweli ilikuwa ni mara yako ya kwanza kunywa
pombe kwa kiwango kile hadi zikakutuma kufanya matendo yale
hadharani ambayo Mungu hapendi?
Je
Mchungaji Lusekelo jana ni mara yako ya kwanza kurudi
nyumbani kwako saa moja asubuhi ? Maana miminilikufika
nyumbani kwako saa moja asubuhi huku nikiwa nimekubeba
baadhi ya vitu vyako kama funguo wa gari ,miwani  huku
wewe ukiwa umebeba Kikabu chenye chupa za maji ya kunywa
;
 Baada
 ya kufanikiwa kumuondoa Kwenye eneo la tukio la ugomvi
uliotokea na Kisha baada ya kukufikisha ndani ya nyumba yako
wewe na vijana wako wewe ukatoka miguu pekupeku bila kuvaa
viatu maana viatu ulikataa kuvaa nimevishika mkononi mkarudi
tena eneo la tukio huku ukiwa Ujavaa viatu unakanyaga matope
na Mvua inatunyeshea unafoka Katika nyumba ya jirani yako
kuishinikiza walinzi wakifungulie Mlango uwaonyeshe
Kazi?
Nakupenda
kwasababu unapenda kuzungumza ukweli na mimi naupenda ukweli
.
Hivyo
nakushauri jirekebishe ,tubu kwa Mungu wako, na ukipata muda
omba msamaha majirani zako kwa Usumbufu uliowasababishia
Jana asubuhi wakuwazibia njia wenzio wasiende makazini na
Magari Yao kwasababu Lako ulilipaki katikati ya barabara
kumalizima tangu saa 12 asubuhi hadi saa mbili  huku
ukisikia hutaliondoa Hilo Gari Hali RPC Sirro,Rais Magufuli
waje kuliondoa. Nilikushuhudia ukiyasema haya sina Sababu ya
kunisingizia .
Pia
Hao vijana wako unaoishi nao hapo ndani baadhi yao wana
akili mbovu wote watatu waliotufungulia geti kwasababu wao
waliochangia kukurudisha tena   eneo la ugomvi Matokeo
yake  ukaenda kudhalilika zaidi wakati Mimi
nilifanikiwa kukuondoa  mapema eneo la tukio mapema na
watu walikuwa  wachache na Magari yalikuwa hawajaanza
kupita Wingi Katika njia ile .
Vijana
Hao kama wangekubali ana na ushauri wangu niliyotoa wakati
nome kufikisha ndani kwako wa kukuingiza ndani na kukufungia
na Kisha wao vijana ndiyo ni wapeleke eneo la tukio niwape
ufunguo wa Gari la Baba Yao Mchungaji wa Luseko wafike eneo
la tukio wachukue Gari walioleta nyumbani bila kujibizana na
watu kwani lakini walinipuuza Matokeo yake ndiyo hayo umati
ulifurika ukakushuhudia ukibwatuka .
Polisi
wa Kituo cha Kawe Dar es Salaam wakaitwa na wasamalia wema
kwa siri wa kakukuta  eneo la tukio ukibwatuka
 wakakupeleka kituoni ukiwa bado pombe hazijakuisha
ukaifadhiwa  Kituo hapo kwa muda  ukasababisha
hata Polisi ambao walikuwa hawafahamu Kuwa unakunywa Pombe
wakajua,wakakudharau maana matendo yako ya Jana
yalitukanisha pia watumishi wa Mungu .
Mchungaji
Lusekelo na wale vijana wako mngeuzingatia ule ushauri wangu
  Kuwa uende ndani ukaoge kisha ukalale  ile saa
Moja asubuhi maana ulikuwa umechoka ungefanikiwa kukwepa
Kadhia na Fedhea hiyo.
Mchungaji
Lusekelo wewe ni mtumishi wa Mungu ,jiheshimu ,usijaribu
kumgeuza Mungu Kuwa ni Mwanasesele labda aoni mambo
unayoyafanya Gizani.Mungu siyo Mwanasesele anatuona yote
tunayoyafanya hadharani na Gizani Akiamua kukuumbua
anakuumbua na wewe Jana ni Mungu Yule ndiyo aliyekuumbua
 hadharani kwakuonyesha wewe ni mtumishi wa Pombe,
Haukulala nyumbani umerudi nyumbani kwako asubuhi, umeenda
kufanya Fujo nyumbani kwa jirani na matusi ukayamwaga na
ukawakera watumiaji wa barabara hiyo.Pole sana.

Na
kukubaliana  na maneno haya yaliyoandikwa
Katika  MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema :
" Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Na akosaye
 kwa vitu hivyo Hana Hekima".
Kwasababu
maneno hayo yametimia kwa Lusekelo ambaye alikuwa amepata
kileo amefanya ugomvi na alipofanya ugomvi Jana
alithibitisha umati ule wa watu  Hana Hekima Kwani
Angekuwa na Hekima asingekubali kufanya ushetani ule
 ambao umefedheesha Vya kutosha.
Naitimisha
kwa kutoa ushauri wa viongozi wa dini akiwemo Mchungaji
Lusekelo kama mmeamua kumtumikia Mungu basi mmtii Mungu
kweli kweli Kwani sisi waumini wenu tunamuamini Mungu na
Nyie viongozi wa dini sasa mnapokuwa mnafanya mambo ya
kishetani Mnatupa wakati mgumu na kutuvuruga akili na
kusabisha Kondoo mnaowachunga kutawanyika na wengine
wanaamua kurudi kwa shetani. Mungu alishasema ole wake
Mchunga Kondoo anayetawanya Kondoo wake .
Matendo
kama hayo aliyoyafanya Mchungaji Lusekelo ndiyo
yanayowatukanisha viongozi wa dini nakufanya wasiaminike
Kumbe siyo viongozi wote hawana uadilifu wapo waadilifu na
wameitwa kumtumikia Mungu na kuna viongozi ambao wao
hawajaitwa kumtumikia Mungu na makanisa ni Biashara
inayowaingizia picha .Mtalaaniwa lazima.
Mungu
Ibariki TanzaniaChanzo:
Facebook: Happy KatabaziBlogg: www.katabazihappy.blogspot.com0716 774494.24/11/2016.

Sent from my iPad--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment