Monday, 21 November 2016

Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe

Elisa, wewe unashawishiwa. Mimi nina uwezo wa kuona na sihitaji mtu anishawishi. Sent from Samsung tablet.


-------- Original message --------
From: Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com>
Date: 21/11/2016 11:50 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe
Ndg. Elisa, Katiba inafuatwa sasa kuliko huko nyuma ni mawazo yako kwa vigezo ulivotumia kupima. La msing ni kwamba Katiba iliyopo haijawahi kuwa shirikishi kwa Mwananchi wa kawaida katika uaandaaji wake. Wanodai katiba mpya ni kwamba waliona mwanga fulani katika huu mchakato na wanataka usiachwe ukazimika na ndiyo maana wanadai mchakato wa Katiba Mpya urejerewe.

Ni kweli kabisa kuna mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano ambayo huko nyuma ilikuwa ni ndoto kufanyika jambo ambulo ni zuri sana kwa taifa. Mambo haya yakiachwa yaendelee kudumu kuwa maono ya mtu mmoja bado si afya kwa taifa vile vile, kwa sababu yanaweza kuporomoka Siku moja Kama ambavyo yamekuja. Katiba mpya ndiyo suruhu ya hilo. Mambo mazuri yanayoendelea yatengenezewe mfumo madhubuti ambao si rahisi mtu mwingine kuyabadirisha au kuyaondoa kirahisi kwa masirahi yake binafsi au ya kikundi fulani kidogo, hapo ndipo suala la Katiba Mpya linapokuwa na umuhimu mkubwa.
2016-11-21 10:34 GMT+03:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Edgar.
sasa katiba inafuatwa kuliko wakati uliopita. Ndiyo maana waliozoea kukwepa kodi wanashawishi watu kuwa katiba inavunjwa. Mafisadi waliofikiri hawawezi kuguswa wanaguswa. Ukichunguza sana utakuta wanaoshawishi wengine kuwa katiba haifuatwi ni wale waliozoea kuivunja na watu tukafikiri ndio utaratibu. Uholela hauwezi kuruhusiwa kuendelea bali tujiruhusu kuzoea kufuata taratibu
--------------------------------------------
On Sat, 11/19/16, Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe
 To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Saturday, November 19, 2016, 3:18 PM


 Tusishabikie na ubabe wa ndani vile vile. Tusikubali
 nchi kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja hata kama ana akili
 kiasi gani! Katiba iliyopo ifuatwe to the letter hata kama
 ni mbovu. Utawala wa sharia utamalaki kwa maslahi ya wote na
 siyo ya mtu au kikundi
  cha watu. 


 Sent from Samsung
 tablet. -------- Original message
 --------
 From: 'Mashaka Makana' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: 19/11/2016 12:50 (GMT+03:00)
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba
 mpya isubiri nchi inyooshwe


 Watanzania
 tusishabikie ubabe wa nchi kigeni kuwa ndiyo suluhisho ya
 matatizo ya ndani ya nchi. Tunasiakia na kuona ya Libya na
 kule Iraq watu walishabikia wakidhani ingekuwa suluhisho ya
 tamaa ya mali
  na madaraka na kukubali kutumika na hawajapata chochote
 zaidi ya kuharibu miundombinu ya nchi yao na vita vya
 wenyewe kwa wenyewe. Hii Demokrasia ya uchaguzi kila baada
 ya miaka mitano ukilinganisha na gharama za uchaguzi ni
 hasara tupu na matumizi mabaya
  ya pesa za umma, Wakati wa kampeni za uchaguzi raia
 hawafanyi kazi kungojea mikusanyiko ya kampeni. Je. ni hali
 ya namna hii na kwa nchi zenye utawala wa kifalme? Msaada
 hapo!


 From:
 'Lesian' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com>

 To:
 wanabidii@googlegroups.com

 Sent:
 Saturday, November 19, 2016 11:39 AM

 Subject: Re:
 [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi
 inyooshwe

 Katiba
 iliopo ni'mbovu reuben.....inawapa watu mamlaka ya ajabu
 anateua hadi wajumbe wa nyumbakumi...hawa ma dcs wa n sasa
 kama si upotevu wa pesa......

 Katiba iliopo ni nzr kwa watu kama kina reuben tu
 wqnaofagilia kila jambo ilmradi limesemwa na kusimamiwa na
 ccm

 Hawanaga mawazo mbadala na hawatak,'na maana yake
 hawataki kuona mbele na trump kaja atawanyooshen subirin
 mnaokomaa madarakan navyma vyenu kaja komesha..teh teh 'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
 Mbegu;
 Sio
 kwamba inji haina Katiba kabisa,itanyooshwa na katiba
 iliyopo.
 Katiba
 iliyopo sio kwamba ni mbaya kabisa kwamba sawa na haipo,
 mabadiliko ya katiba yana sehemu chache za kuboresha na
 kuongeza.
 Uhuni
 uliokuwepo/uliopo umetokana na kutofuata Katina, shaeria na
 kanuni zake i.e. lazier free
  

 Reuben
 On Thursday,
 November 17, 2016 7:42 PM, Edgar Mbegu
 <embegu@hotmail.com> wrote:


 Nchi itanyooshwa kwa sheria zipi? Kwa utaratibu upi?
  Kwa utashi wa mtu binafsi?  Ametumwa na nani?


 Sent from Samsung
 tablet.
 -------- Original message --------
 From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: 17/11/2016 10:36 (GMT+03:00)
 To: ELISA MUHINGO' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com>
 Subject: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya
 isubiri nchi inyooshwe


 Serikali
 za Wanyama na ndege au Wadudu; Ndani
 zina taadhima, kama kwamba maabudu; Na
 watu wenye hekima, siku hizi hawamudu Madaraka
 na heshima, heri mnyama na mdudu Vinywa
 vimewaachama, tamu imekuwa ngwandu Na
 heshima imehama baki taka na mashudu Na
 madhara na dhuluma miungu ya kuabudu
 (Shaaban
 Robert; katika "Kielelezo cha Fasili") SHAABAN Robert katika shairi nililonukuu hapo juu, anaelezea
 madhara ya Uongozi na Viongozi wanapokosa maono, hekima na
 heshima kwa wananchi akisema, inapokuwa hivyo heri Serikali
 za Wanyama, Ndege au Wadudu zina taadhima kuliko za viongozi
 wenye kukithiri
  kwa dhuluma na kujigeuza miungu watu. Japo gwiji hilo la ushairi Afrika Mashariki alikuwa
 akiandikia zama zake zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo
 fukuto la ufisadi, rushwa, kutoweka kwa uzalendo, uadilifu,
 maadili ya uongozi na ubinyaji wa demokrasia ilivyo sasa
 halikuwa jambo lililopevuka, lakini
  utabiri wake wa kinabii kwa yajayo hayo wakati huo ulikuwa
 sahihi na ndiyo yaliyoikaba koo nchi yetu hivi leo. Ilivyo leo, na kama tunavyoambiwa na wataalamu wa siasa na
 sayansi ya jamii kwa ujumla, suluhisho la maovu haya ya
 kijamii ni kwa njia ya Katiba ya nchi itakiwayo na itokanayo
 na wananchi wahanga wa maovu hayo, kwa njia ya maoni na kura
 ya maoni. Pengine ni kwa sababu hii miaka ya karibuni, na hasa
 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwamba suala la Katiba mpya
 lilikuwa ajenda moto, na zaidi kwa vyama vya upinzani
 vilivyodai kuwa Katiba iliyopo imepitwa na wakati kwa sababu
 iliandaliwa katika mazingira
  tofauti na ya sasa miaka 40 iliyopita. Tangu mwanzo, Serikali, kupitia Mwanasheria wake Mkuu (AG)
 na mara nyingi pia kupitia waziri mwenye dhamana ya mambo ya
 Katiba na vigogo wengine wa chama tawala, ilitamka wazi
 kuwa, "Katiba mpya si ajenda ya serikali madarakani",
 tamko lililochukuliwa na wengi
  kama sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa viganja vya
 mkono. Hatimaye mwaka 2012, serikali ilisalimu amri kwa
 "mafuriko" hayo kwa kuteua Tume ya Kupendekeza "Rasimu
 ya Katiba", chini ya uenyekiti makini wa Jaji Joseph Sinde
 Warioba kwa matarajio kwamba Katiba hiyo mpya ingetumika kwa
 mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu
  wa Oktoba 2015. Hadi kipindi hicho na mpaka sasa, nchi yetu ilikuwa na moja
 ya Katiba bora Afrika Mashariki – Katiba ya Jamhuri ya
 Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ukiondoa
 mapungufu machache kadhaa yaliyomo, likiwamo lile la harufu
 ya chama kimoja; madaraka makubwa
  ya Rais (Mhimili wa Utawala) dhidi ya mihimili mingine –
 Bunge na Mahakama na baadhi kuhusu Muungano, ilitosha na kwa
 utoshelevu mkubwa katika ujenzi wa demokrasia na utawala
 bora nchini. Ni mwananchi gani mpenda demokrasia ya kweli bila kificho,
 anaweza kubeza ubora usio na mshindani wa Katiba hii kwa
 mambo muhimu inayotetea, kama vile, "malengo muhimu na
 misingi ya shughuli za serikali madarakani" (ibara 6 –
 11); na "Haki ya Usawa na Wajibu
  wa Serikali kwa Raia" (ibara 12 – 30) ambayo Katiba za
 nchi nyingi hazina?. Ibara hizi za Katiba zina umahiri wa pekee kutokana na
 ukweli kwamba zilitungwa na kupewa nguvu na msukumo enzi za
 utawala ulioweka mbele mambo kama vile uwajibikaji na
 maadili kwa viongozi; usawa wa binadamu na wa kijamii, utu
 na dhana nzima ya uchumi/utajiri
  wa nchi kuwa mikononi mwa wananchi kwa ajili ya na kwa
 manufaa ya wananchi wenyewe. Kwa kuzingatia haya, nchi haikuhitaji, na bado haihitaji
 Katiba mpya kwa wakati huu, ila ipo haja isiyohojika ya
 kuifanyia marekebisho ya hapa na pale Katiba iliyopo kwa
 kuondoa ibara zinazopwaya au zinazokinzana (repugnant
 provisions) na mnyumbuliko wa demokrasia
  kwa mazingira ya sasa. Serikali ya Awamu ya Nne ilitishika na kusalimu amri kwa
 "mungurumo" wa mbali wa kudai Katiba mpya bila sababu
 wakati ikijua ubora wa Katiba iliyopo, ila kwa sababu ya
 "uzembe" wake wa kuruhusu maovu ya kijamii tuliyoyataja
 kutamalaki. Uzembe huo ulisababisha kujipaka matope na uchafu wa kila
 aina ama kwa kushiriki au kwa kunyamazia maovu hayo kufikia
 kile anachosema kila mara Rais wa awamu ya tano, John Pombe
 Joseph Magufuli (JPM), kwamba, "nchi iliendeshwa kihovyo
 hovyo tu kana kwamba hapakuwa
  na (viongozi) serikali". Kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Tume ya Warioba kwa njia
 ya Rasimu ya Katiba ni kuboresha na kufafanua kwa fikra na
 "mantiki" pana zaidi ya yaliyo bora yaliyomo katika
 Katiba ya 1977 pamoja na namna ya utekelezaji kwa uthabiti,
 na kwa kuziba au kuondoa mapungufu
  tuliyokwishaelezea hapo mwanzo. Ni Rasimu iliyohusisha "akili" bora za ainaaina
 zinazofahamika hapa nchini, zenye fikra za kimapinduzi, utu
 na usawa wa binadamu na wa kijamii na ambayo kama ingepita
 ilivyo, bila ya shaka yoyote ingetoa Katiba bora na ya aina
 yake kumfanya Mtanzania aishi
  bustani ya Edeni bila hofu wala mawaa, badala ya kuendelea
 kuishi kwenye "shamba la bibi" ilivyo sasa, kwa kila mtu
 kuishi kadri ya ukali wa meno yake kuweza kurarua na kupora
 kiharamia awezavyo, bila kujali wanyonge na mafukara wa nchi
 wa kufukarishwa na
  mfumo. Rasimu hii ilikuwa tishio kwa maslahi ya mfumo wa kifisadi
 uliotaka kubakia na uliofanya nchi "kuendeshwa kihovyo
 hovyo tu kana kwamba hapakuwa na serikali". Waingereza wana msemo, kwamba, "give a dog a bad name and
 it will be killed", yaani, "mpe mbwa jina baya na
 atauawa". Haraka haraka mafisadi wa nchini na wa kimataifa
 walivuta pumzi kukusanya nguvu kuiangamiza rasimu hii kwa
 kuipa tume na baadhi ya wajumbe
  wake majina mabaya mabaya ionekane ya "majahili" na
 rasimu hiyo kuwa haifai. Kanuni na taratibu za kutunga Katiba zikapindwa bungeni
 kuhakikisha kwamba inanyumbulishwa na kusukwasukwa mithili
 ya meli ndani ya tufani na kupoteza mwelekeo wa Katiba
 iliyokusudiwa. Kisha, kwa matumizi ya hoja za nguvu; ubaguzi wa kiitikadi
 wa kubumba; ushawishi wa kilaghai na matumizi ya pesa chafu
 kwa kushirikisha ubepari wa ndani na wa kimataifa, tabaka
 hili la kifisadi lililewesha bangi sehemu kubwa ya Bunge
 Maalum la Katiba kiasi
  cha kupanua midomo na kulishwa kila aina ya "mvinyo",
 vinywa vimewaachama mithili ya makinda ya ndege, huku
 likijipa bila uhalali wa kisheria, mamlaka ya kuandika
 lenyewe "Katiba Inayopendekezwa" kwa kutupilia mbali
 sehemu kubwa ya maoni ya wananchi. Matokeo ya ubabe huu yalikuwa ni pamoja na kunyofolewa kwa
 sehemu kubwa, misingi ya usawa wa kijamii, tunu za taifa,
 maadili ya taifa, usimamizi wa rasilimali za taifa kwa
 manufaa ya wananchi wote na uwajibikaji wa viongozi ili
 kusimika kile kinachoweza kuitwa
  "jamii ya kitabaka". Baada ya kunyofolewa kwa sehemu kubwa mengi mema kwenye
 Rasimu ya Tume ya Warioba, "Katiba Inayopendekezwa" ya
 wababe wa ufisadi na mawakala wa ukoloni mamboleo, si tu
 kwamba iliweka rehani demokrasia na uhuru wa nchi na raia
 kwa ubeberu mpya, bali pia inasaliti
  yaliyo mema katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 kuturejesha
 "utumwani" kwa Farao, Misri. Pengine, na huenda JPM aliyaona mapema haya kiasi cha kupata
 ujasiri wa kuhoji kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo
 vya habari nchini hivi karibuni akisema, "Je, mliwahi
 kunisikia wakati wa kampeni zangu nikitaja lolote juu ya
 Katiba?". Maadam wababe wa ufisadi bado wana ushawishi mkubwa wa
 kilaghai juu ya mkondo wa Katiba nchini kwa kushirikiana na
 vigogo wengi ambao bado wapo ndani ya mfumo wa serikali,
 mwendelezo wowote wa "Katiba Inayopendekezwa" hauna
 maana tena kwa sababu utaipeleka
  nchi pabaya kwa matakwa ya wababe hao. Acha muda upite kwa jambo hili, hadi umma utakapofunguka
 macho kuona uchafu uliokuwa ukilishwa ili kuchangamkia
 mchezo huo wa kifo. Na maadam sehemu kubwa ya Katiba iliyopo
 ina mengi mazuri ila kwa sababu tu ilibezwa kwa maslahi ya
 kitabaka; JPM hana sababu
  ya kukosa usingizi juu ya "mwongozo" wa kufanyia kazi
 ila kwa kuzingatia na kuheshimu mema yaliyomo. Wananchi (mimi nikiwa mmoja wao) baada ya kuona kuwa maovu
 ya kijamii yanavuma na kunyamaziwa wakati Katiba iliyopo
 ikivunjwa bila hofu kwa wavunjaji kuwajibishwa, walifikia
 kutamani kuwa na kiongozi "kichaa" kidogo, dikteta mwema
 (benevolent dictator) ainyooshe
  kwanza nchi japo kwa awamu moja tu kwa kuwashikisha adabu
 wote wenye kuchezea demokrasia, uhuru na haki za raia, hata
 kama ni kwa "kuweka pembeni" kidogo baadhi ya vifungu
 vya Katiba nzuri iliyopo. Tangu mwanzo, serikali haikuwa na nia njema na suala la
 Katiba mpya ila kuziba ombwe la uongozi kwa njia hiyo
 kufuatia kutamalaki kwa ufisadi, rushwa na demokrasia duni
 na hivyo kuelekea kuipa nguvu kambi ya upinzani dhidi ya
 serikali iliyokwenda likizo kuchapa
  usingizi. Ni wazi pasingekuwa na hoja ya upinzani juu ya maovu haya
 kama uongozi ungetekeleza wajibu wake vyema kwa kuongozwa na
 Katiba iliyopo, na hivyo pia pasingezuka hoja ya Katiba
 mpya. Ndiyo maana, baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia
 madarakani na kujitoa mhanga kupambana na maovu haya, kambi
 ya upinzani imeishiwa hoja na madai ya Katiba mpya kukosa
 mantiki. Hebu angalia mifano hii kuona ilivyokuwa. Ukiona serikali madarakani inaatamia kwa mbawa zake maovu
 yenye kuhujumu nchi, kupora au kuibia serikali mapato na
 kuwakingia kifua wafanyabiashara wahujumu wa uchumi,
 wakishirikiana na wanasiasa ili wasiguswe; hapo elewa
 kwamba, serikali hiyo imejiweka rehani
  kwa wenye fedha, mafisadi na maharamia wa uchumi wa
 nchi. Ukiona kuibuka kwa tabaka la wafanyabiashara kuchangamkia
 nafasi za uongozi wa chama na serikali kwa udi na uvumba na
 kwa kupenyeza nguvu ya fedha kupata uongozi, fahamu kwamba
 demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria unayoyoma na
 kukaribisha utajiri (fedha)
  kununua madaraka na uongozi, na uongozi kuwa sehemu ya
 kundi la kimafia la kupora utajiri wa nchi, hata kama nchi
 itakuwa na katiba bora kupita zote duniani. Chini ya awamu hii, yaonesha kama vile JPM anawaambia
 viongozi wa aina hii, wauze kwanza vyote walivyo navyo na
 kisha wamfuate katika kuutafuta ufalme wa kisiasa, kwa maana
 hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa pamoja, yaani watu na
 mali. Nakwambia, subiri uchaguzi mkuu ujao (2020) uone; zaidi ya
 nusu kati yao hawatachukua fomu, maana walizoea vya kunyonga
 na sasa vya kuchinja hawaviwezi. Hapo, iko wapi hoja ya
 Katiba mpya?. Ukiona uchumi wa nchi unahama mikononi mwa wananchi kwenda
 mikononi mwa wajanja wachache; rasilimali za taifa kuporwa
 na "wawekezaji" wa kigeni bila hofu kwa kushirikiana na
 mawakala wao wa ndani; elewa kwamba nchi iko hatarini
 kugeuzwa "shamba la bibi", kwa
  kila mtu kurarua na kupora kadri ya ukali wa meno yake. Ukiona viongozi wa kitaifa wakiutangazia umma kwa ulaghai
 kwamba uchumi wa taifa unapaa wakati wananchi wakizidi
 kufukarika kuliko mwanzo, na eti kwamba wasiokubaliana na
 uongo huo ni "wavivu wa kufikiri" au wapinzani wa chama
 na serikali; fahamu kwamba hizo
  ni dalili za serikali kujiweka mbali na wananchi wake na
 kuwa "mwenye shibe (viongozi) hamjui mwenye njaa". Ukiona serikali inapuuza maoni ya wananchi na kusikiliza ya
 wenye pesa na wenye madaraka; elewa kwamba serikali hiyo
 imelewa madaraka; itanyanyasa vyombo vya habari na
 wanahabari kwa changamoto zao za "kuuamsha umma". Lakini ilivyo leo, mambo yanaonekana kugeuka, kwamba
 kiongozi wa awamu ya tano (JPM), anaonekana kuongozwa na
 kauli mbiu na hekima ya Rais, mwanademokrasia wa zamani wa
 Marekani, Abraham Lincoln, kwamba "Kwa kuungwa mkono na
 umma (si na mafisadi na majambazi
  ya kisiasa) naweza kufanya jambo lolote; lakini bila hivyo
 na mbele ya upinzani wa umma, siwezi kufanya lolote". Kauli mbiu hii inakidhi ule msemo wa Kilatini "Vox Populi,
 Vox Dei", yaani, "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu".
 Pengine ni kwa sababu hii, kwamba JPM mara nyingi hachoki
 kuwaomba wananchi wamwombee kwa Mungu amlinde katika
 harakati hizi. Kwa nini?. Hapa tena, Shabaan Robert anaonekana kumpa sala JPM kwa
 shairi "NILINDE", linapokuja suala la kutetea na kulinda
 maslahi ya taifa katikati ya ufisadi uliotamalaki. Kwenye
 shairi hilo, Shaaban Robert anasema: "Ni
 weledi wa kusema, watu wa leo Na
 elimu na hekima, si haba kwao Bali
 hawana huruma, katika moyo Na
 fahari (kwa taifa) na heshima ni
 chache kwao tamthili ya wanyama,
 mfano
 wao kisha waweza kuuma, sumu wanayo E
 Mungu mwenye uzima, nilinde nao". Na tumuombee sote kwa Mungu afanikishe vita hii bila hoja ya
 Katiba mpya. Raia mwema


 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to
  abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to
  abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to
  abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to
  abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment