Monday 21 November 2016

Re: [wanabidii] MAKONDA TULIA UNYWE DAWA

Malosha Zefania,

Leo hii saa 10 nikiwa ndani ya daladala music loud sana tukaomba apunguze wapi!
Pamoja na kukataakupunguza sauti kulikuwa na kipindi East African Radio wakitoa taarifa za ajabu za Rombo. Watoto 4 wa shule walipewa mimba na baba zao wazazi na kesi zikamalizwa kifamilia. Mmoja wa wahojiwa alitoa taarifa ya msichana wa miaka 18 ambaye alipokuwa akirudi nyumbani baba akienda naye bar kunywa au akinywa naye home lakini akimuwekea kitu alewe asijitambue halafu akitembea nae. Mke wa baba alikufa hivyo baba mzazi akitembea na mwanae. Mimba kuja kutokea na mtoto kusema kwa ndugu waliojazana-ikamalizwa kienyeji pamoja na viongozi wa eneo kufahamu shauri hilo. Utaona pale jinsi ambavyo watanzania Nduma Kuwili. Mtoto aliyezaliwa alifariki. Ukweli hapa itakuwa wamemuua kuficha aibu. Hivyo, badala ya kumfunga baba miaka 30+ kulingana na sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya 1998-ndugu wanaficha aibu ya familia. Vitendo hivi vinaendelea na vinakua ila tunafumbia macho. Kwa nini viongozi wa Mtaa wasimkamate Baba na nduguze na wale wa upande wa mama waliozima kesi hii kienyeji. Wamtumie Social Welfare Officer au wa Maendeleo ya Jamii kama hawana wa Ustawi wa Jamii Wilaya. Pamoja na kuogopa visasi na klufanyiziwa na muhusika na ndugu zake, sheria ikichukua mkondo wengi wataogopa kuficha siri.

Hutokea pia mbakaji akahonga hela polisi na wazazi husika na kesi ikaishia ila mtoto kuathirika kisaikolojia, kimwili na kiafya wengine kupata HIV/AIDS.

Viongozi kusutana hadharani si nidhamu nzuri na si maadili. Wakae katika vikao vyao husika. Kumshushua lkiongozi hadharani na kumfukuza hapo hapo ni mbaya sana na ni ujengaji wa uadui mwingi. Pamoja na mapungufu mengine-Makonda ameshirikiana na Kamanda Afande Sirro wa Kanda maalum DSM katika suala ya kuwafichua wamiliki Shisha na la kuwafichua wauza unga wakuu akiongea na vijana 500 walioathirika kwa madawa ya kulevya ambao wapo Souber House Kigamboni DSM lakini magazeti yanaandika mengineyo.

Magazeti yakitumbuliwa wanasema Uhuru wa habari hakuna! Uchonganishi mtupu kinyume na magazeti ya nchi za wenzetu ulaya. Wao ni kutaka kufurahisha watu na kupata pesa sio kuzingatia sheria. Tunapenda sifa lakini kutenda vitu positive na kuzingatia sheria, kujituma kwa uhakika kwa kuzingatia miongozo na ethics za kazi ni ndogo sana. Inasikitisha. Tulimlaumu mkoloni, tukataifisha mali za mapepari, tukaingia ujamaa na kujitegemea, sasa liberalism na elimu zinatolewa na public na private sector lakini tupo palepale sio mbali sana na tutarudi nyumba tubaki na majungu mwisho tuuane ktk civil war kama hatutabalikika kikweli.

Kama Kawa.



--------------------------------------------
On Mon, 21/11/16, 'malosha zephania edward' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] MAKONDA TULIA UNYWE DAWA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 21 November, 2016, 15:33

Hildegarda kiwasila
pamoja na kupita umepita vyema uliyosema ni kweli tupu.
Serikali lazima inyoshe mambo kama ya vibali vya biashara
kama hizo sii manisipaa kuangalia mapato tu. Ndii maana
magufuli kasema nchi inyoke kwanza. Sheria zipi kutumika
hakuna

Sent
from Yahoo Mail on Android
On Mon, Nov 21, 2016 at 11:34,
'Hildegarda Kiwasila' via
Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Ndio yale
tunayosema wengine:
Serikali inapotoa vibali
vya biashara haramu kama bar kuwa na shisha; vifaa vinapitia
wapi ambako havikaguliwi kabla ya kuingizwa nchini?

Haya na haya ya Kubeti. Kila
kona siku hizi kuna majumba/halls za kubeti. Sasa hii
betting/gambling kila kona haikuona kuwa ni mchezo mchafu?
Vinana na watu wazima wapo hapo kutwa wanakunywa na kucheza
kamali hawafanyi kazi. Betting katika nchi ya Vibaka mtaani,
vijana wasio ajira unategemea uchumi wa viwanda
utafanikiwa?


Tunafanya makosa kwa vibali na leseni zisizo
zingatia maadili tunajali pesa tu. Bar kila kona kila baada
ya nyumba  tatu Bar ya pombe, video, music za makelele
majumbani mitaani; pembeni mwa nyumba ya kuishi watu mtaani
mtu kaweka karakana ya nondo kusagwa, kuchunwa na ya mbao
inayopakwa dawa zinazoingia majumbani na kusababisha afya
mbaya watu wanavuta hewa za kemikali na kubwia vumbi la mbao
na chuma. Bado hiyo daladala na bajaji, bodaboda zinapita
mtaani na loud music! Usalama gani ndani ya bus la mtaani
loud music? Dreva atasikia lini warning toka gari
nyingine?Hata upigiwe simu ukipokea hamsikilizani. Watoto
wadogo, watoto matumboni exposed to noise nyumbani, ndani
bus, mtaani. Wanapata buses hizo wanaona wahusika; mtaani
police wanaona na kusikia makelele hayo ya magari na
bodaboda inapita inapiga kona za mapambo!

Itakuwa hiyo ya Shisha-Cha
mtoto hicho! Wanapanda bangi vijijini mashamba makubwa
police kupoteza muda kwenda kuyafyeka. Maiti zinasafirishwa
na unga tumboni na bangi ndani ya gunia juu vitunguu! Kutaka
hela na utajiri rahisi rahisi na kila kiingiacho mijini na
vijijini ni halali!?

Tusiporekebisha sasa kisheria na kimatendo ya
kweli-tutajenga taifa la baadae la vijana zombie, vilema
wengi wa umri mdogo na mkubwa watakaohitaji kutunzwa.
Mmiliki wa Shisha ni mzazi anaona yanayoendelea hajali utu
bali pesa tu.

Ndio hao si
Shisha tu bali magulio ya kuuza watoto wa kike na
wakiume.
Inakokwenda Bongoland ni
kubaya-wazazi kuwajibika kidogo, utaifa umezamishwa topeni
ndani ya kubeti issues zinazoonekana wazi ni kinyume na
sheria na maadili.

Nilikuwa
ninapita tu!!

On Mon,
21/11/16, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] MAKONDA
TULIA UNYWE DAWA
To: "WANABIDII"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 21 November, 2016, 11:15

MAKONDA TULIA UNYWE DAWA

Na Happiness Katabazi

WIKI Iliyopita Mkuu wa MKoa
wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda
Mara Kadhaa
amenukuliwa Katika vyombo Vya Habari akisema
yeye ameiita hidi kadri ya uwezo wake
Kupambana na matumizi
ya dawa za kulevya
ikiwemo Shisha lakini Jeshi la Polisi

limekuwa likisita kuwachukulia Hatua.

Makonda alitoa tuhuma hizo Mbele ya Waziri
Mkuu Kassim
Majaliwa Katika Uzinduzi wa
Mradi wa Uboreshaji wa
upatikanaji wa Umeme
Katika Mkoa wa Dar Es Salaam dhidi ya

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon
Sirro
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Suzan Kaganda .

Kuwa Mara kwa Mara amekuwa akimuuliza Sirro
Kuwa Mbona
wananchi wanampatia taarifa
wauzaji wa Shisha bado wanatamba
na Sirro
Amekuwa akimjibu Kuwa Hali  ni shwari .


Makonda aliwashushia tuhuma Makamanda hao
Wawili
Wamelambishwa ile hongo aliyoikata
kutoka kwa
wafanyabiashara wale wa Shisha
ndiyo maana wanasita
kuwachukulia Hatua
wauzaji wa Shisha.Shisha imepigwa
marufuku
kutumiwa hapa nchini.


Mkuu Huyo wa Mkoa Alidai kuna wafanyabiashara 10 bila ya
kuwataja majina walimfuata  wakitaka
Kumhonga
Sh.Milioni 50 kila mwezi ,lakini
alikataa.


Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa
alimtaka   Makonda aache Kulalamika
badala
yake akatekeleze maagizo
yanayotolewa na viongozi wa juu wa

serikali.

Kauli hiyo
Makonda dhidi ya makamanda hao wa polisi

imeibua  mjadala  katika jamii huku wengine
wakitofautiana na yeye vikali.

Kwa upande wa Jeshi la
polisi Makao Makuu Kamanda Robert
Boaz
mwishoni mwa wiki alizungumza na umma na akasema
taarifa hizo za tuhuma za Rushwa  dhidi ya
makamanda wa
jeshi Lao  wamesikia na jeshi
hilo limefikia uamuzi wa
kuanza kufanyia
uchunguzi tuhuma hizo ( Inquiry).

Kwanza Napongeza Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi
kwa uamuzi
huo wa uweledi wa kuchukua Hatua
za kufanya uchunguzi wa
tuhuma hizo
zilizotolewa barabarani yaani Kwenye vyombo Vya
Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama na Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaam
,Paul Makonda.

Aidha pia
Kifungu  cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa

Makosa ya Jinai 2002 , kinatoa mamlaka kwa Ofisa wa
Polisi  kuhoji mashahidi,watuhumiwa au mtu
yoyote
ambaye Polisi inaitaji  kupata
maelezo yake kutokana na
tuhuma au
uchunguzi wa jambo lolote .
 
Hivyo Jeshi la Polisi wapo sahihi kufanyia
uchunguzi taarifa
hizo zilizotolewa na
Makonda wiki iliyopita.


Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya  Mwenendo wa Makosa ya
Jinai ya Mwaka 2002 ,kina Mtaka mtu yoyote
ambaye anafahamu
taarifa za kutendeka au
kutaka kutendeka kwa tukio ka
Uhalifu
apeleke taarifa hizo Katika mamlaka husika za
kiserikali ili zifanyiwe Kazi na  akishindwa
kufanya
hivyo atashitakiwa kwa kosa lolote
chini ya Sheria ya Kanuni
ya Adhabu sura ya
16  ya Mwaka 2002.


Tumuulize Makonda yeye Kabla ya ile Sherehe ya Uzinduzi
wa
Mradi wa umeme  aliyotoa tuhuma hizo
nzito dhidi ya
Makamanda Hao wa Polisi 
alishazipeleke taarifa hizo za
watu wale
walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha
Katika mamlaka gani za kidola?

Makonda ana anakofia Ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar e Salaam na
kofia ya Pili ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama

ya Mkoa wa Dar es Salaam.


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambaye Mkuu wa Mkoa
husika ndiyo Mwenyekiti , baadhi ya wajumbe wa
Kamati hiyo
ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi
( JWTZ), Jeshi la Polisi,
Usalama wa Taifa
( TISS) ,TAKUKURU ,Uhamiaji ,Magereza na

vyombo vingine.

Namuuliza
Makonda alivyokuwa akiendesha vikao vya Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam
akiwa na kofia ya
Mwenyekiti wa Kamati hiyo
alishawahi kuwasilisha taarifa
zake hizo
za  wafanyabiashara 10 aliyodai eti walifika
ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha  kila
mwezi ili
aachane na mapambano ya
Shisha?

Makonda uliwai
Kuwasilisha  taarifa Katika Kamati ya

Ulinzi na Usalama kuwa  Kamanda  Sirro

anasita   kuchukua Hatua dhidi ya 

wafanyabiashara hao na uenda ile hongo iliyokataa kutoka
kwa
wafanyabiashara wale wa
Shisha   uenda
imewapitia?

Makonda uliwahi kuwasilisha
mezani  taarifa Katika
Kamati hiyo
unayoiongoza  Kuwa Jeshi la Polisi kupitia

RPC- Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu
Biashara
ya Shisha?

Maana kupitia mahojiano yako na Redio Clouds
umesikika
ukisema Mara kadhaa umekuwa
ukipewa taarifa na Jeshi la
Polisi kupitia
Kamanda Sirro Kuwa Shisha Hakuna Dar Es

Salaam na kwamba Jeshi la Polisi lomefanikiwa 
Kudhibiti Shisha  wakati wewe Makonda umekuwa
ukipewa
taarifa na wananchi wanaoichukia 
Shisha Kuwa Shisha
ipo ,na ukaenda kukamata
na vielelezo unavyo .


Kama uliiwasilisha  Taarifa hizo katika Kamati ya
Ulinzi na Usalama Tueleze. Taarifa hizo
zilijadiliwa ?

Na wajumbe
wa Kamati hiyo walijibu nini ulivyosasilisha
taarifa hizo walikujibu nini ?Je wajumbe 
wa 
Kamati Walisema hawatafanyia Kazi ?Au
Walisema watafanyia
kazi?Walikupa tarehe ya
mwisho ya kujifanyia Kazi

'deadline'?


Nafahamu Hilo Swali kwa mwana Usalama aliyefundwa
akafundika
hawezi lijibu hadharani ila
kwakuwa wewe Makonda ni
Mlopokaji na
hufahamu majukumu ya kofia zako zote mbili

unaweza ni jibu hilo swali.

Au Makonda ndiyo ameamua  kuleta Habari
zako   za Kimbea ,majungu ,kujipendekeza
Mbele Waziri Mkuu Majaliwa ?Ili uonekane
wewe   ni mfanyakazi bora kuliko  Jeshi
Polisi kupitia makamanda wao Sirro na Kanda ?
Upuuzi mtupu.

Je tukisema
wale wahongaji hawakurudi tena kukuletea 

ile Rushwa   ndiyo maana umeamua Kusema

taarifa hizo hadharani? Mbona walivyokufuata ofisini
kwako
hukujitokeza hadharani kutuambia kuna
wafanyabiashara 10 wa
Shisha wamekufuata
ofisini kutaka wakuhonge kiasi hicho cha

Fedha na ukakataa?

Kama
uliamua kunyamaza kimya wakati walipokufuata kutaka
kukuhonga Fedha kama unavyodai ,Tukuulize ni
kitu sasa
kimesukuma utoboe Siri hiyo
hadharani hivi sasa?

Hivi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hasa ya Mkoa wa Dar Es Salaam,
Ina uwezekano mkubwa ikawa imefungwa CCTV
kamera.

Hivyo ni vyema
Makonda atoe  ushirikiano
atakapotakiwa 
kufanya hivyo aseme  Hao
wafanyabiashara
wa Shisha walikuja Lini ofisini kwake , ili

watu wanaohusika  na CCTV Kamera waweze kuwabaini kwa
sura ikibidi na mazungumzo Yao  ili
ithibitike ni kweli
walifika ofisini
wake?walitaka Kumhonga kiasi hicho cha

Fedha ?Na Hao watu 10 wasakwe wako jiwe waseme ni kweli
walitaka Kumhonga Makonda kama Makonda
alivyodai Mbele ya
Umma?


Aiingi akilini Mkuu wa Mkoa mzima
anasema 
wafanyabiashara Hao haramu eti
walifika ofisini kwake ,
anawafahamu 
kabisa ni wafanyabiashara haramu ,.

Akakaa na kufanya nao mazungumzo ofisini
kwake   hadi wakamtajia  na kiasi cha
fedha watawachmpa  halafu yeye  Mkuu wa
Mkoa
ambaye lazima Atakuwa  na walinzi
ashindwe 
Kuwaeleza walinzi Hao wawakamate
wafanyabiashara Hao ambao
yeye 
amejinasibu  Kuwa anawajua  ni
wanafanya
Biashara hiyo haramu ya Shisha.

Na katika mtazamo wa yeye  kama Mwenyekiti wa
Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar
Es Salaam, Hilo suala la
yeye  kutaka
kuhongwa kiasi hicho cha Fedha na

wafanyabiashara hao haramu 10  Narudia tena kumuuliza
aliwasilisha   mezani taarifa hiyo ?

  Inaoenekana Makonda
alikuwa  nania ovu ya kutaka
kuzipokea
maana  kama alikuwa  hatamani 
kuzipokea
hizo Fedha kwanini hukuwasilisha taarifa

hizo  za yeye  kutaka kuhongwa Kwenye Kamati ya
Ulinzi Usalama ya Mkoa ambayo yeye ndiyo
Mwenyekiti?

Kwanini
umesubiri Waziri Mkuu aje Kwenye sherehe za Uzinduzi
wa Maboresho  Upatikanaji wa Umeme Dar Es
Salaam ,ndiyo
useme Hilo?


Makonda kijana mwenzangu umeacha  Mashaka
mengi sana
Katika hili kwa sisi wananchi
wako wa Mkoa wa Dar Es Salaam
unaotuongoza
.

Umeonyesha  hujui
wajibu wako  kwasababu wewe
Ndiyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na
wewe ndiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo .Hufahamu
sehemu ya
kutoa taarifa au kushitaki ?

  Unasubiri shughuli za
uzinduzi wa mradi maboresho ya umme
ndiyo
ushitaki hadharani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa? Ni
dhahiri hutufai maana tayari umeishapata
doa.

Nina mashaka na
uwezo wake wa kiutendaji na uwezo wake wa

kuchanganua mambo.Makonda umetuacha na maswali kama
anajua
majukumu yake ya Ya kofia ya Mkuu wa
Mkoa na kofia ya
Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Nashawishika kusema kuwa Makonda kama RC
,Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama
wa Mkoa ,akiwa pia ndiyo
anayesimamia
utendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam hafahamu

majukumu yake  tena hata kwa wale watendaji wake wa
Moja kwa Moja yaani wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama.

Na Pia
Makonda kupitia matamko yake mbalimbali kuhusu sakata
hilo ameonyesha hafahamu Maadili ya Kazi yake
Kwani kama
Angekuwa anajua Maadili ya
kiongozi mwenye hadhi ya
Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa

asingethubutu kupayuka Yale aliyoyatamka hadharani dhidi
ya
Kamanda Sirro na Kaganda pia
asingethubutu kwenda Redio
Clouds kwenda
kuzungumzia ule upuuzi aliouongea kupitia

Redio hiyo.

Nasema ni
upuuzi kwasababu Makonda kama Kweli an ajitambua
yeye ni nani,ana madarakani siku ile ile
aliposikia Waziri
Mkuu Majaliwa
alivyomshushua mbele za watu kwa kumtaka

Makonda aache kulalamika afanyekazi na atekeleze maagizo
toka viongozi wa juu, alivyosikia Kamanda
Sirro
alipozungumza na waandishi wa habari
akisema kuwa operesheni
ya kukamata
waharifu wa makosa ya aina mbalimbali ikiwemo
wauza dawa mbalimbali za kulevya imekuwa
ikifanyika na
inaendelea kufanyika na
kwamba majarada ya uchunguzi wa
watuhumiwa
hao polisi wameyapeleka ofisi ya Mwanasheria Mkuu
kwaajiili ya hatua zaidi za kisheria na tayari
na maana
polisi hawana mamlaka ya
kufungulia washitakiwa kesi za
jinai
mahakamani mwenye jukumu hilo ni Mkurugenzi wa
Mashitaka ( DPP) .

Na ni kweli kifungu cha 9 cha Sheria ya Taifa
ya Huduma ya
Uendeshaji wa mashauri ya
Jinai Na. 27 ya Mwaka 2008 ,
inasema DPP
ndiyo mwenye Mahakama ya Kufungua na kuendesha
Kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya
serikali.

Na aliposikia
Jeshi la Polisi Makao Makuu Kupitia Kamanda

Boaz Kuwa
Jeshi la Polisi  limeanza
kufanyia uchunguzi wa shutuma
za Makonda
dhidi ya Makamanda wake Sirro na Kaganda, RC
-Makonda angefunga  mdomo wake kwa
kunyamaza
kimya  kimya lakini sijui ni
Utoto ,ulimbukeni
akaendelea kuongea tu
Mara kuhojiwa Redio Clouds Mara
kunukuliwa
na Gazeti moja akitamba Kuwa ataendelea

kuwachongea. Aibu gani hii jamani!

Ni wakati mwafaka wa Makonda arudishwe darsani
ili akapewe
mafunzo yatakayomwezeka
kufahamu majukumu yake ya Uenyekiti
wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama na majukumu ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam.

Waswahili wanasema Dalili za Mvua ni Mawingu.
Hivyo kama Leo
hii Mwenyekiti Huyo wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama RC
Makonda
ameshindwa kutumia majukwaa sahihi ( Proper Forum)
yakupeleka malalamiko yake badala yake
anatumia vyombo Vya
Habari na kusubiri
kudandia mkutano wa Waziri Mkuu kulalama

tena mambo mengi ambayo ambayo yanapandikiza Chuki baina
ya
wananchi na Jeshi la Polisi Kuwa Jeshi
la Polisi ndiyo
linalowalea wauza Shisha
kwasababu ha liwachukulii Hatua
basi ipo
siku Makonda Atakuja kuropoka mambo Siri ya vikao
Vya Kamati ya Ulinzi Usalama kupitia Vyombo
Vya Bahari kwa
Lengo la kutaka kujionyesha
yeye ni mchapakazi kuliko
watumishi wengine
wowote .

Na ushahidi ni
Yale mahojiano aliyoyafanya  a Redio

Clouds ambayo Clip yake ninayo ambayo Makonda kwa kinywa
Chake anamtuhumu Sirro ambaye ni mjumbe wake
wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama Kuwa amekuwa
alimpa taarifa za uongo
kuhusu Biashara ya
haramu ya Shisha.

Sasa
kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo analalamikia mjumbe wake
wa Kamati hiyo hadharani tena Kwa zaidi ya
Mara Moja , ni
wazi RC Makonda Hana Imani
na Jeshi la Polisi Kanda Maalum
ya Dar Es
Salaam ambalo ndilo Hilo Hilo Askari wake

wanamlinda nyumbani anakoishi na ofisini.


Lakini hata kama ni kweli Kamanda Sirro
alikuwa akikupa
taarifa za uongo kuhusu
Shisha ,Sirro na wewe Makonda wote
ni
wateule wa Rais John Magufuli .Je Makonda ulishawahi pia
kwenda kumweleza Rais Magufuli,au boss wa
Sirro ambaye ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Kuwa Sirro amekuwa akikupa taarifa
za uongo
na auridhishwi na Utendaji wake?

Makonda umedai Jeshi la Polisi limekuwa
likisita kuchukulia
Hatua wafanyabiashara
haramu ya dawa za kulevya, hivyo Jeshi
la
Polisi Leo Hii likiibuka na takwimu za Kuonyesha Jeshi
Hilo limekuwa likichukua Hatua Kabla hata ya
wewe kufikiri
wa au wewe kufikiria utakuja
Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es
Salaam sura
yako Utaiweka wapi?

Maana
Mimi ni shahidi mahakamani nimekuwa nikishuhudia
Mkurugenzi wa Mashitaka aliwashitaki
watuhumiwa mbalimbali
wa makosa ya dawa
kulevya ambao Chanzo cha washitakiwa Hao

kushitakiwa ni walidaiwa Kutenda makosa hayo na
walikamatwa
na Jeshi la Polisi.

Elewa Uhalifu ulikuwepo toka
enzi na Enzi na serikali ya
awamu ya tano
imeukuta na itauacha na haiwezi kuukomoesha

maana kila kukicha wahalifu wanabuni mbinu mpya za
kufanya
Uhalifu.

Hivyo hata wewe Makonda Biashara ya dawa
kulevya umeikuta
hapa Dar Es Salaam na
Duniani kwa ujumla.Usijidanganye Huna
Nguvu
wala mamlaka ya Kupambana nayo kwasababu Huna Mafunzo
ya kutambua hizi dawa za kulevya, kukamata
wenye hiyo
taaluma wapo ndani ya Jeshi la
Polisi kupitia Kitengo cha
Kuthibiti Dawa
za Kulevya Chenye Ofisi zake Barabara ya

Kilwa Dar es Salaam.


Umejitapa kupitia Redio Clouds  Kuwa umekamata dawa za
kulevya aina ya Shisha . Mina Kuuliza una
Hakika gani hizo
ni dawa za kulevya?

Hivi hizo unazodai ni Shisha
ulizokimata zikichukuliwa
zikapelekwa kwa
wataalamu wakazikagua kitaalamu Kisha wakaja
kutoa ripoti Kuwa hizo siyo Dawa za kulevya
utasema
nini?Acha wenye taaluma za
Kupambana na dawa za kulevya
wafanyakazi
Yao.Wewe taaluma hiyo Huna.

Mkuu wa Mkoa Mzima unaacha kushughulika na
mambo makubwa
makubwa unaamua kujigeuza
'korokoroni 'unaenda kukamata

Shisha na vifaa Vya Kuvutia Shisha wakati Polisi wenye
vyeo
Vya chini wa kufanyakazi ya ukamataji
wapo na wala
hawakueleza  wameshindwa
kukamata hivyo wa naomba
utasaidie.

Hivi Hao wahalifu wa Shisha
unawaowafuta Fuata hadi Kwenye
vijiwe vyao
Vya Kuvuta Shisha na bangi wakikumwagia Kinyesi
usoni utalia na nani?

Fanyakazi yako uliyotumwa na vyombo Vya Ulinzi
na Usalama
ambayo ndiyo wenye taaluma ya
Ulinzi na Usalama wafanyakazi
Yao kwa Uhuru
.Heshimu wakubwa wako ,Chagua matamshi ya

kuzungumza Mbele ya hadhara dhidi ya viongozi wenzako.

We bado ni kijana Mdogo sana
bado unaitaji kulelewa na
wanasiasa
wenzako,wanausalama hivyo haina maana wewe

kujiingiza Katika msuguano na Jeshi la Polisi kupitia
Kamanda Sirro na Kaganda. Kushangaa siku Moja
kitendo hicho
kikaja kukugharimu.

Aidha Makonda kaa chini
ujitathimini na utafakari
hicho 
ulichokifanya ambacho kutokana na matamshi yako
ambacho kimezusha mjadala  na kufanya watu
Tutulie
Mashaka uwezo wa Utendaji wako .

Kisha wewe binafsi ujiulize
Je ulikuwa sahihi wakati
ukifanya hayo
uliyoyafanya  kwa mujibu wa maadili ya

kofia zako mbili za kimadaraka. Kisha ujipime wewe
mwenyewe
mwisho uchukue maamuzi. 

Nimalize makala hii kwa
kukushauri Makonda  Kuwa '
Usiwe na
haraka kuliko Upesi'. Mji huu wa Dar Es Salaam Una
Masharti hadi ufanikiwe ,sio kuvaa Masharti
/Suti ukajiona
wa maana . Acha tabia na
kutaka kujipatia Umaarufu wa chee
kwa mambo
yasiyo na tija .
Naomba kutoa hoja.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy
Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.com
0716 774494
21/11/2016


Sent from
my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com


Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit

https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata
Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment