Masanja. Ubarikiwe kwa hili nitakalisema. Katiba iliyopo ilikuwa shirikishi. Nilishapoteza barua niliyopelekewa na Mfaume Kawawa akinishukuru kwa maoni yangu.kuhusu katiba. Hiyo ilikuwa 1970 au 77 kama sijasahau wakati wa wananchi kushiriki mjadala wa katiba kwa njia mbalimbali.
Rais Magufuli amesema katiiba hakikuwa kipaumbele chake katika uchaguzi 2015. Hadanganyi lakini hakusema kweli. Ngoja niseme kweli akanushe akitaka. Katiba ni kipaumbele chake na tayari mchakato umeanza.
Hatua za kwanza zitakamilika 2010. Ni kusafisha jamii ya kitanzania, kuondoa uovu uliozidi mpaka kuweka misingi bora ya kiuchumi na kuhakikisha watanzania wanajua wanachofanya na wanakoelekea. 2020 ataka[pokamiliasha mpango huo atakuja na agenda ya katiba mpya wakati akiomba ridhaa ya watanzania kwa awamu ya pili. Hapo watanzania wataandika katiba mpya wakiongozwa na Magufuli. Huenda itakuwa katiba bora kuliko ya Warioba ambayo watanzania waliandika kwa hasira kwa sababu ya maovu yaliyokuwepo. Kwa hiyo katiba bora inaweza kupitia barabara hiyo. Ukiondoa wenye chuki binafsi kwa Magufuli kwa sababu aliwashinda; watanzania watakuwa wamoja zaidi wakati huo
Elisa
--------------------------------------------
--------------------------------------------
On Mon, 11/21/16, Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, November 21, 2016, 11:50 AM
Ndg. Elisa, Katiba inafuatwa sasa
kuliko huko nyuma ni mawazo yako kwa vigezo ulivotumia
kupima. La msing ni kwamba Katiba iliyopo haijawahi kuwa
shirikishi kwa Mwananchi wa kawaida katika uaandaaji wake.
Wanodai katiba mpya ni kwamba waliona mwanga fulani katika
huu mchakato na wanataka usiachwe ukazimika na ndiyo maana
wanadai mchakato wa Katiba Mpya urejerewe.
Ni kweli kabisa kuna mambo
yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano ambayo huko nyuma
ilikuwa ni ndoto kufanyika jambo ambulo ni zuri sana kwa
taifa. Mambo haya yakiachwa yaendelee kudumu kuwa maono ya
mtu mmoja bado si afya kwa taifa vile vile, kwa sababu
yanaweza kuporomoka Siku moja Kama ambavyo yamekuja. Katiba
mpya ndiyo suruhu ya hilo. Mambo mazuri yanayoendelea
yatengenezewe mfumo madhubuti ambao si rahisi mtu mwingine
kuyabadirisha au kuyaondoa kirahisi kwa masirahi yake
binafsi au ya kikundi fulani kidogo, hapo ndipo suala la
Katiba Mpya linapokuwa na umuhimu mkubwa.
2016-11-21 10:34 GMT+03:00
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Edgar.
sasa katiba inafuatwa kuliko wakati uliopita. Ndiyo maana
waliozoea kukwepa kodi wanashawishi watu kuwa katiba
inavunjwa. Mafisadi waliofikiri hawawezi kuguswa wanaguswa.
Ukichunguza sana utakuta wanaoshawishi wengine kuwa katiba
haifuatwi ni wale waliozoea kuivunja na watu tukafikiri ndio
utaratibu. Uholela hauwezi kuruhusiwa kuendelea bali
tujiruhusu kuzoea kufuata taratibu
------------------------------ --------------
On Sat, 11/19/16, Edgar Mbegu
<embegu@hotmail.com>
wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya
isubiri nchi inyooshwe
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, November 19, 2016, 3:18 PM
Tusishabikie na ubabe wa ndani vile vile. Tusikubali
nchi kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja hata kama ana
akili
kiasi gani! Katiba iliyopo ifuatwe to the letter hata
kama
ni mbovu. Utawala wa sharia utamalaki kwa maslahi ya wote
na
siyo ya mtu au kikundi
cha watu.
Sent from Samsung
tablet.
-------- Original message
--------
From: 'Mashaka Makana' via
Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: 19/11/2016 12:50 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli
kasema yote: katiba
mpya isubiri nchi inyooshwe
Watanzania
tusishabikie ubabe wa nchi kigeni kuwa ndiyo suluhisho
ya
matatizo ya ndani ya nchi. Tunasiakia na kuona ya Libya
na
kule Iraq watu walishabikia wakidhani ingekuwa suluhisho
ya
tamaa ya mali
na madaraka na kukubali kutumika na hawajapata
chochote
zaidi ya kuharibu miundombinu ya nchi yao na vita vya
wenyewe kwa wenyewe. Hii Demokrasia ya uchaguzi kila
baada
ya miaka mitano ukilinganisha na gharama za uchaguzi ni
hasara tupu na matumizi mabaya
ya pesa za umma, Wakati wa kampeni za uchaguzi raia
hawafanyi kazi kungojea mikusanyiko ya kampeni. Je. ni
hali
ya namna hii na kwa nchi zenye utawala wa kifalme?
Msaada
hapo!
From:
'Lesian' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To:
wanabidii@googlegroups.com
Sent:
Saturday, November 19, 2016 11:39
AM
Subject: Re:
[wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri
nchi
inyooshwe
Katiba
iliopo ni'mbovu reuben.....inawapa watu mamlaka ya
ajabu
anateua hadi wajumbe wa nyumbakumi...hawa ma dcs wa n
sasa
kama si upotevu wa pesa......
Katiba iliopo ni nzr kwa watu kama kina reuben tu
wqnaofagilia kila jambo ilmradi limesemwa na kusimamiwa
na
ccm
Hawanaga mawazo mbadala na hawatak,'na maana yake
hawataki kuona mbele na trump kaja atawanyooshen
subirin
mnaokomaa madarakan navyma vyenu kaja komesha..teh teh
'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Mbegu;
Sio
kwamba inji haina Katiba kabisa,itanyooshwa na katiba
iliyopo.
Katiba
iliyopo sio kwamba ni mbaya kabisa kwamba sawa na
haipo,
mabadiliko ya katiba yana sehemu chache za kuboresha na
kuongeza.
Uhuni
uliokuwepo/uliopo umetokana na kutofuata Katina, shaeria
na
kanuni zake i.e. lazier free
Reuben
On Thursday,
November 17, 2016 7:42 PM, Edgar Mbegu
<embegu@hotmail.com>
wrote:
Nchi itanyooshwa kwa sheria zipi? Kwa utaratibu upi?
Kwa utashi wa mtu binafsi? Ametumwa na nani?
Sent from Samsung
tablet.
-------- Original message --------
From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: 17/11/2016 10:36 (GMT+03:00)
To: ELISA MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya
isubiri nchi inyooshwe
Serikali
za Wanyama na ndege au Wadudu;
Ndani
zina taadhima, kama kwamba maabudu;
Na
watu wenye hekima, siku hizi hawamudu
Madaraka
na heshima, heri mnyama na mdudu
Vinywa
vimewaachama, tamu imekuwa ngwandu
Na
heshima imehama baki taka na mashudu
Na
madhara na dhuluma miungu ya kuabudu
(Shaaban
Robert; katika "Kielelezo cha Fasili")
SHAABAN Robert katika shairi nililonukuu hapo juu,
anaelezea
madhara ya Uongozi na Viongozi wanapokosa maono, hekima
na
heshima kwa wananchi akisema, inapokuwa hivyo heri
Serikali
za Wanyama, Ndege au Wadudu zina taadhima kuliko za
viongozi
wenye kukithiri
kwa dhuluma na kujigeuza miungu watu.
Japo gwiji hilo la ushairi Afrika Mashariki alikuwa
akiandikia zama zake zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo
fukuto la ufisadi, rushwa, kutoweka kwa uzalendo,
uadilifu,
maadili ya uongozi na ubinyaji wa demokrasia ilivyo
sasa
halikuwa jambo lililopevuka, lakini
utabiri wake wa kinabii kwa yajayo hayo wakati huo
ulikuwa
sahihi na ndiyo yaliyoikaba koo nchi yetu hivi leo.
Ilivyo leo, na kama tunavyoambiwa na wataalamu wa siasa
na
sayansi ya jamii kwa ujumla, suluhisho la maovu haya ya
kijamii ni kwa njia ya Katiba ya nchi itakiwayo na
itokanayo
na wananchi wahanga wa maovu hayo, kwa njia ya maoni na
kura
ya maoni.
Pengine ni kwa sababu hii miaka ya karibuni, na hasa
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwamba suala la Katiba
mpya
lilikuwa ajenda moto, na zaidi kwa vyama vya upinzani
vilivyodai kuwa Katiba iliyopo imepitwa na wakati kwa
sababu
iliandaliwa katika mazingira
tofauti na ya sasa miaka 40 iliyopita.
Tangu mwanzo, Serikali, kupitia Mwanasheria wake Mkuu
(AG)
na mara nyingi pia kupitia waziri mwenye dhamana ya mambo
ya
Katiba na vigogo wengine wa chama tawala, ilitamka wazi
kuwa, "Katiba mpya si ajenda ya serikali
madarakani",
tamko lililochukuliwa na wengi
kama sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa viganja vya
mkono.
Hatimaye mwaka 2012, serikali ilisalimu amri kwa
"mafuriko" hayo kwa kuteua Tume ya Kupendekeza
"Rasimu
ya Katiba", chini ya uenyekiti makini wa Jaji Joseph
Sinde
Warioba kwa matarajio kwamba Katiba hiyo mpya ingetumika
kwa
mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba 2015.
Hadi kipindi hicho na mpaka sasa, nchi yetu ilikuwa na
moja
ya Katiba bora Afrika Mashariki – Katiba ya Jamhuri
ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ukiondoa
mapungufu machache kadhaa yaliyomo, likiwamo lile la
harufu
ya chama kimoja; madaraka makubwa
ya Rais (Mhimili wa Utawala) dhidi ya mihimili mingine
–
Bunge na Mahakama na baadhi kuhusu Muungano, ilitosha na
kwa
utoshelevu mkubwa katika ujenzi wa demokrasia na
utawala
bora nchini.
Ni mwananchi gani mpenda demokrasia ya kweli bila
kificho,
anaweza kubeza ubora usio na mshindani wa Katiba hii
kwa
mambo muhimu inayotetea, kama vile, "malengo muhimu
na
misingi ya shughuli za serikali madarakani" (ibara 6
–
11); na "Haki ya Usawa na Wajibu
wa Serikali kwa Raia" (ibara 12 – 30) ambayo Katiba
za
nchi nyingi hazina?.
Ibara hizi za Katiba zina umahiri wa pekee kutokana na
ukweli kwamba zilitungwa na kupewa nguvu na msukumo enzi
za
utawala ulioweka mbele mambo kama vile uwajibikaji na
maadili kwa viongozi; usawa wa binadamu na wa kijamii,
utu
na dhana nzima ya uchumi/utajiri
wa nchi kuwa mikononi mwa wananchi kwa ajili ya na kwa
manufaa ya wananchi wenyewe.
Kwa kuzingatia haya, nchi haikuhitaji, na bado
haihitaji
Katiba mpya kwa wakati huu, ila ipo haja isiyohojika ya
kuifanyia marekebisho ya hapa na pale Katiba iliyopo
kwa
kuondoa ibara zinazopwaya au zinazokinzana (repugnant
provisions) na mnyumbuliko wa demokrasia
kwa mazingira ya sasa.
Serikali ya Awamu ya Nne ilitishika na kusalimu amri
kwa
"mungurumo" wa mbali wa kudai Katiba mpya bila
sababu
wakati ikijua ubora wa Katiba iliyopo, ila kwa sababu
ya
"uzembe" wake wa kuruhusu maovu ya kijamii
tuliyoyataja
kutamalaki.
Uzembe huo ulisababisha kujipaka matope na uchafu wa
kila
aina ama kwa kushiriki au kwa kunyamazia maovu hayo
kufikia
kile anachosema kila mara Rais wa awamu ya tano, John
Pombe
Joseph Magufuli (JPM), kwamba, "nchi iliendeshwa
kihovyo
hovyo tu kana kwamba hapakuwa
na (viongozi) serikali".
Kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Tume ya Warioba kwa
njia
ya Rasimu ya Katiba ni kuboresha na kufafanua kwa fikra
na
"mantiki" pana zaidi ya yaliyo bora yaliyomo katika
Katiba ya 1977 pamoja na namna ya utekelezaji kwa
uthabiti,
na kwa kuziba au kuondoa mapungufu
tuliyokwishaelezea hapo mwanzo.
Ni Rasimu iliyohusisha "akili" bora za ainaaina
zinazofahamika hapa nchini, zenye fikra za kimapinduzi,
utu
na usawa wa binadamu na wa kijamii na ambayo kama
ingepita
ilivyo, bila ya shaka yoyote ingetoa Katiba bora na ya
aina
yake kumfanya Mtanzania aishi
bustani ya Edeni bila hofu wala mawaa, badala ya
kuendelea
kuishi kwenye "shamba la bibi" ilivyo sasa, kwa kila
mtu
kuishi kadri ya ukali wa meno yake kuweza kurarua na
kupora
kiharamia awezavyo, bila kujali wanyonge na mafukara wa
nchi
wa kufukarishwa na
mfumo.
Rasimu hii ilikuwa tishio kwa maslahi ya mfumo wa
kifisadi
uliotaka kubakia na uliofanya nchi "kuendeshwa
kihovyo
hovyo tu kana kwamba hapakuwa na serikali".
Waingereza wana msemo, kwamba, "give a dog a bad name
and
it will be killed", yaani, "mpe mbwa jina baya na
atauawa". Haraka haraka mafisadi wa nchini na wa
kimataifa
walivuta pumzi kukusanya nguvu kuiangamiza rasimu hii
kwa
kuipa tume na baadhi ya wajumbe
wake majina mabaya mabaya ionekane ya "majahili"
na
rasimu hiyo kuwa haifai.
Kanuni na taratibu za kutunga Katiba zikapindwa bungeni
kuhakikisha kwamba inanyumbulishwa na kusukwasukwa
mithili
ya meli ndani ya tufani na kupoteza mwelekeo wa Katiba
iliyokusudiwa.
Kisha, kwa matumizi ya hoja za nguvu; ubaguzi wa
kiitikadi
wa kubumba; ushawishi wa kilaghai na matumizi ya pesa
chafu
kwa kushirikisha ubepari wa ndani na wa kimataifa,
tabaka
hili la kifisadi lililewesha bangi sehemu kubwa ya
Bunge
Maalum la Katiba kiasi
cha kupanua midomo na kulishwa kila aina ya
"mvinyo",
vinywa vimewaachama mithili ya makinda ya ndege, huku
likijipa bila uhalali wa kisheria, mamlaka ya kuandika
lenyewe "Katiba Inayopendekezwa" kwa kutupilia
mbali
sehemu kubwa ya maoni ya wananchi.
Matokeo ya ubabe huu yalikuwa ni pamoja na kunyofolewa
kwa
sehemu kubwa, misingi ya usawa wa kijamii, tunu za
taifa,
maadili ya taifa, usimamizi wa rasilimali za taifa kwa
manufaa ya wananchi wote na uwajibikaji wa viongozi ili
kusimika kile kinachoweza kuitwa
"jamii ya kitabaka".
Baada ya kunyofolewa kwa sehemu kubwa mengi mema kwenye
Rasimu ya Tume ya Warioba, "Katiba Inayopendekezwa"
ya
wababe wa ufisadi na mawakala wa ukoloni mamboleo, si
tu
kwamba iliweka rehani demokrasia na uhuru wa nchi na
raia
kwa ubeberu mpya, bali pia inasaliti
yaliyo mema katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977
kuturejesha
"utumwani" kwa Farao, Misri.
Pengine, na huenda JPM aliyaona mapema haya kiasi cha
kupata
ujasiri wa kuhoji kwenye mkutano wake na wahariri wa
vyombo
vya habari nchini hivi karibuni akisema, "Je, mliwahi
kunisikia wakati wa kampeni zangu nikitaja lolote juu
ya
Katiba?".
Maadam wababe wa ufisadi bado wana ushawishi mkubwa wa
kilaghai juu ya mkondo wa Katiba nchini kwa kushirikiana
na
vigogo wengi ambao bado wapo ndani ya mfumo wa
serikali,
mwendelezo wowote wa "Katiba Inayopendekezwa" hauna
maana tena kwa sababu utaipeleka
nchi pabaya kwa matakwa ya wababe hao.
Acha muda upite kwa jambo hili, hadi umma
utakapofunguka
macho kuona uchafu uliokuwa ukilishwa ili kuchangamkia
mchezo huo wa kifo. Na maadam sehemu kubwa ya Katiba
iliyopo
ina mengi mazuri ila kwa sababu tu ilibezwa kwa maslahi
ya
kitabaka; JPM hana sababu
ya kukosa usingizi juu ya "mwongozo" wa kufanyia
kazi
ila kwa kuzingatia na kuheshimu mema yaliyomo.
Wananchi (mimi nikiwa mmoja wao) baada ya kuona kuwa
maovu
ya kijamii yanavuma na kunyamaziwa wakati Katiba
iliyopo
ikivunjwa bila hofu kwa wavunjaji kuwajibishwa,
walifikia
kutamani kuwa na kiongozi "kichaa" kidogo, dikteta
mwema
(benevolent dictator) ainyooshe
kwanza nchi japo kwa awamu moja tu kwa kuwashikisha
adabu
wote wenye kuchezea demokrasia, uhuru na haki za raia,
hata
kama ni kwa "kuweka pembeni" kidogo baadhi ya
vifungu
vya Katiba nzuri iliyopo.
Tangu mwanzo, serikali haikuwa na nia njema na suala la
Katiba mpya ila kuziba ombwe la uongozi kwa njia hiyo
kufuatia kutamalaki kwa ufisadi, rushwa na demokrasia
duni
na hivyo kuelekea kuipa nguvu kambi ya upinzani dhidi
ya
serikali iliyokwenda likizo kuchapa
usingizi.
Ni wazi pasingekuwa na hoja ya upinzani juu ya maovu
haya
kama uongozi ungetekeleza wajibu wake vyema kwa kuongozwa
na
Katiba iliyopo, na hivyo pia pasingezuka hoja ya Katiba
mpya.
Ndiyo maana, baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia
madarakani na kujitoa mhanga kupambana na maovu haya,
kambi
ya upinzani imeishiwa hoja na madai ya Katiba mpya
kukosa
mantiki. Hebu angalia mifano hii kuona ilivyokuwa.
Ukiona serikali madarakani inaatamia kwa mbawa zake
maovu
yenye kuhujumu nchi, kupora au kuibia serikali mapato
na
kuwakingia kifua wafanyabiashara wahujumu wa uchumi,
wakishirikiana na wanasiasa ili wasiguswe; hapo elewa
kwamba, serikali hiyo imejiweka rehani
kwa wenye fedha, mafisadi na maharamia wa uchumi wa
nchi.
Ukiona kuibuka kwa tabaka la wafanyabiashara
kuchangamkia
nafasi za uongozi wa chama na serikali kwa udi na uvumba
na
kwa kupenyeza nguvu ya fedha kupata uongozi, fahamu
kwamba
demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria unayoyoma
na
kukaribisha utajiri (fedha)
kununua madaraka na uongozi, na uongozi kuwa sehemu ya
kundi la kimafia la kupora utajiri wa nchi, hata kama
nchi
itakuwa na katiba bora kupita zote duniani.
Chini ya awamu hii, yaonesha kama vile JPM anawaambia
viongozi wa aina hii, wauze kwanza vyote walivyo navyo
na
kisha wamfuate katika kuutafuta ufalme wa kisiasa, kwa
maana
hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa pamoja, yaani watu
na
mali.
Nakwambia, subiri uchaguzi mkuu ujao (2020) uone; zaidi
ya
nusu kati yao hawatachukua fomu, maana walizoea vya
kunyonga
na sasa vya kuchinja hawaviwezi. Hapo, iko wapi hoja ya
Katiba mpya?.
Ukiona uchumi wa nchi unahama mikononi mwa wananchi
kwenda
mikononi mwa wajanja wachache; rasilimali za taifa
kuporwa
na "wawekezaji" wa kigeni bila hofu kwa kushirikiana
na
mawakala wao wa ndani; elewa kwamba nchi iko hatarini
kugeuzwa "shamba la bibi", kwa
kila mtu kurarua na kupora kadri ya ukali wa meno
yake.
Ukiona viongozi wa kitaifa wakiutangazia umma kwa
ulaghai
kwamba uchumi wa taifa unapaa wakati wananchi wakizidi
kufukarika kuliko mwanzo, na eti kwamba wasiokubaliana
na
uongo huo ni "wavivu wa kufikiri" au wapinzani wa
chama
na serikali; fahamu kwamba hizo
ni dalili za serikali kujiweka mbali na wananchi wake
na
kuwa "mwenye shibe (viongozi) hamjui mwenye njaa".
Ukiona serikali inapuuza maoni ya wananchi na kusikiliza
ya
wenye pesa na wenye madaraka; elewa kwamba serikali
hiyo
imelewa madaraka; itanyanyasa vyombo vya habari na
wanahabari kwa changamoto zao za "kuuamsha umma".
Lakini ilivyo leo, mambo yanaonekana kugeuka, kwamba
kiongozi wa awamu ya tano (JPM), anaonekana kuongozwa
na
kauli mbiu na hekima ya Rais, mwanademokrasia wa zamani
wa
Marekani, Abraham Lincoln, kwamba "Kwa kuungwa mkono
na
umma (si na mafisadi na majambazi
ya kisiasa) naweza kufanya jambo lolote; lakini bila
hivyo
na mbele ya upinzani wa umma, siwezi kufanya lolote".
Kauli mbiu hii inakidhi ule msemo wa Kilatini "Vox
Populi,
Vox Dei", yaani, "Sauti ya Wengi ni Sauti ya
Mungu".
Pengine ni kwa sababu hii, kwamba JPM mara nyingi
hachoki
kuwaomba wananchi wamwombee kwa Mungu amlinde katika
harakati hizi. Kwa nini?.
Hapa tena, Shabaan Robert anaonekana kumpa sala JPM kwa
shairi "NILINDE", linapokuja suala la kutetea na
kulinda
maslahi ya taifa katikati ya ufisadi uliotamalaki.
Kwenye
shairi hilo, Shaaban Robert anasema:
"Ni
weledi wa kusema, watu wa leo
Na
elimu na hekima, si haba kwao
Bali
hawana huruma, katika moyo
Na
fahari (kwa taifa) na heshima
ni
chache kwao tamthili ya wanyama,
mfano
wao kisha waweza kuuma, sumu wanayo
E
Mungu mwenye uzima, nilinde nao".
Na tumuombee sote kwa Mungu afanikishe vita hii bila hoja
ya
Katiba mpya.
Raia mwema
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment