Sunday 6 November 2016

RE: [wanabidii] RAIS MAGUFULI BADILIKA

Siyo kwenye spelling tu, bali hata grammar.Anapaswa kuwa precise.

Hakieleweki kitu i.e. makosa ni mengi mno.

Huyu dada haelezeki hafundishiki na hakubali kukosolewa

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Selemani Rehani
Sent: Saturday, November 05, 2016 4:28 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RAIS MAGUFULI BADILIKA

 

Uandishi wako una makosa makubwa ya lugha. Hivi kweli wewe ni Mwandishi makini unafanya makosa ya kiuandishi kama haya! Unaandika neno 'udhoefu' badala ya 'uzoefu'!. Nakushauri kabla ya kuchapisha tafuta mtu akusaidia kurekebisha makosa ta kiuandishi, vinginevyo ni aibu kwako. Unaonekana kanjanja. Selemani Rehani.

 

 

 

Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

 

 

-------- Original message --------

From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>

Date: 05/11/2016 12:34 (GMT+03:00)

To: WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>

Subject: [wanabidii] RAIS MAGUFULI BADILIKA

 

RAIS MAGUFULI BADILIKA

Na Happiness Katabazi

EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Kitabu cha Ezekieli kinachopatikana Ndani ya Biblia kwasababu Leo Rais Dk.John Maguli anatimiza Mwaka mmoja tangu alipo apishwa 5/11/2015 Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Makala hii ambayo itajadili mazuri,  mazuri yaliyofanywa,Udhahifu iliyojitokeza na nitatoa ushauri / mapendekezo yangu ya mambo gani yarekebishwe ili taifa liweze kupiga Hatua zaidi Katika Kipindi cha Mwaka mmoja wa Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli.


Hakuna Siri  Kuwa  Katika kampeni za uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 ,Mimi niliutangazia umma Kuwa nitafunga mkono mgombea wa urais wa CCM ambaye alikuwa Dk.Magufuli ambaye alifanikiwa na ndiyo amekuwa rais wa Tanzania kwasasa .

Wakati nilipotangaza uamuzi huo wa Kumuunga mkono mgombea urais wa CCM ,pia nilisema licha Katika kampeni hizi Nitamuunga mkono mgombea urais wa CCM pia uchaguzi ukimalizika mgombea Huyo akafanikiwa akiwa rais wa nchini, nitaendelea Kumuunga mkono kwa Hali yoyote ile na sitamuonea haya kumkosoa kupitia kalamu yangu pindi ninapoona anatoka nje ya mstari.

Uamuzi wangu huo uliwakera wale ambao walikuwa wanaichukia CCM na walikuwa wakinitukana  matusi ya nguoni, kunitolea lugha za vitisho mkebehi na kusababisha nikabadili nyendo zangu ki aina  na wengine walidiriki kunipachika jina la Happiness Katabazi ni ' Hawali wa Magufuli 'ndiyo maana nampigia  debe lakini ukweli ni kwamba Magufuli hanifahamu hata kwa sura. Nimewasamehe bure ila walichobakiza hivi sasa wananitania jina ' Happiness Katabazi ni Mrs Magufuli ' na Mimi nawajibu sawa Magufuli ni My Husband'.

Turejee Kwenye  mada yetu ya Msingi.Kwanza kabisa Nakupongeza Rais Magufuli Leo kuweza kutimiza Mwaka mmoja ukiwa madarakani ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kukupa Afya hadi umefikisha umri huo pia nipongeze Timu yako yaani watumishi wa ngazi zote unapofanya nao Kazi Kwani Katika Kipindi hiki cha Mwaka mmoja kuna baadhi ya mambo ya maana nimeyafanya ambayo yanastahili pongezi nanitayataja hapa chini.

Jambo la kwanza ni la chini ya serikali ya Magufuli ,Watanzania tumefundishwa uchumi/ Kubana matumizi.

Hapa namaanisha Kuwa tangu Magufuli Aingie madarakani upatikanaji wa fedha umekuwa mgumu kwa wananchi waliowengi kwasababu mbalimbali na hili kumethibitishwa na Gavana wa Benki Kuu Professa Benno Ndullu hivi karibuni.

Hali hiyo imesababisha Leo hii Watanzania tuondokane na tabia ya kutumia Fedha Katika matumizi yasiyo ya lazima, Umuhimu.

Pia Hali hiyo imetufanya tuwe na nidhamu na fedha tunazozimiliki au tunazotarajia kuzipata kwasababu Tayari tumeishaona ukizifuja  Fedha hivi sasa kuzipata tena siyo Kazi rahisi.

Tuwe wa kweli hapo awali Watanzania Wengi  tulikuwa Hatuna nidhamu ya matumizi ya Fedha, ukipata Fedha Leo wakati mwingine unaziingiza Katika matumizi yasiyo na Umuhimu kwa wakati ule kwasababu unauhakika Kesho utapata Fedha kirahisi na kweli Fedha ilikuwa nyingi mitaani na mikononi mwa watu tofauti na ilivyo hivi sasa. Hali hiyo ina faida zake na Hasara pia Hilo pia tulijue.

Pili, Utawala wa serikali ya awamu ya Tano umeondoa ile Hali ya baadhi ya genge la watu kujiona wao wapo juu ya Sheria kuliko wengine.

 Napongeza Katika Hilo Kwani hapo awali Kabla ya serikali hii kuingia madarakani kuna baadhi ya wananchi wenzetu walikuwa wakiwafanyia baadhi ya wananchi wenzao mambo yasiyofaa kwakigezo wao wapo juu ya Sheria na wanajua na viongozi.

Katika Kipindi hiki kwa uchunguzi wangu Hali hii ni kama imepungua kila mmoja anaogopa kujitapa Kuwa atakufanyia uhuni na huwezi kumfanyia chochote kwasababu anafahamia na vigogo serikalini.

Tatu, serikali ya awamu ya tano ndani ya muda mfupi imeweza kununua Ndege ili kutoa huduma na kuongeza pato la taifa.Napongeza licha siyo kipaumbele kwa Watanzania waliowengi Kwani ni Watanzania Wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua Ndege.

Nne, watu wamekuwa na Mwamko mkubwa wa kulipa kodi mbalimbali kwakuogopa kushughulikiwa na serikali.Napongeza hili.Licha hata Katika Enzi za Utawala wa Serikali ya Rais Mstaafu Kikwete watu walikuwa Wakilipa kodi pia .

Tano,Bar za kuuza Pombe zenye leseni za kufanya Biashara mwisho saa Sita usiku kweli Bar nyingi nimeshuhudia ndani ya Kipindi ya serikali ya awamu ya tano kweli zinatekeleza agizo la kufayabiashara kwa mujibu wa leseni zao zinavyowataka hazikeshi kama zamani licha kuna baadhi ya bar hizo zina funga bar hizo Polisi wakipita wanaona zimefungwa ila zinawaingiza vyumba Vya ndani   wateja wake wanaendelea Kunywa Pombe kama kawaida.

Hata hivyo lile agizo la rais Magufuli alilotaka mchezo wa Pulltable usichezwe wakati wa kazi nikama halitekelezwi kwa vitendo kwani katika uchunguzi wangu baadhi ya bar ,watu wamekuwa wakicheza mchezo huo kama kawaida wakati wa kazi na kuuza Pombe muda wa kazi wakati wa hawana leseni ya kuuza pombe muda wakazi licha wafanyabiashara wengine wanauza kwa vificho.

Kwa asilimia 50 Napongeza Katika hili licha utekelezaji huu unawakera wanywaji Pombe wanaopenda Kunywa Pombe mchana hadi usiku wa manane na pia wafanyabiashara wa Bar Kwani wafanyabiashara Hao wanadai linawakoseshea wateja Wengi.

Tano,ni dhamu Katika baadhi ya Ofisi za watumishi wa umma imerejea Kwani kuna baadhi ya watumishi umma walikuwa hawana nidhamu Katika Ofisi zao na walikuwa hawatoi huduma kwa wananchi inavyotakiwa kwasababu tofauti ikiwemo Rushwa, jeuri,dharau au Ujinga wao tu.

Licha Katika hili la nidhamu ,napenda nisema Kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma tangu Magufuli Aingie madarakani wamekuwa wakifanyakazi kwa nidhamu ya woga wa kumuogopa Magufuli atafukuza kazi ,kuwasimamisha, au,kuwakaribia mbele za watu hivyo wamekuwa wakitenda Kazi kwa hofu badala ya taaluma zao na hili ni jambo Moja baya sana Kwani mtu anayefanya kazi kwa hofu,nidhamu ya woga mtu Huyo hawezi kufanyakazi vizuri mwisho wa siku ataaribu Kazi.

Licha Mara Kadhaa Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akiwata watumishi waache hofu wafanyakazi na kwamba mtu ambaye si mchafu kwanini awe na hofu?. Ukweli ni kwamba baadhi ya watumishi wa umma hivi sasa  hofu .

Katika maumbile ya ki binadamu lazima tukubaliane kwamba binadamu wote hatulingani kuna wanaojiamini ,hawana hofu na kitu chochote hata kama anatenda matendo machafu lakini kuna binadamu mwingine tena wengine ni wasomi wazuri tu lakini hawajiamini ,ni Waoga wapo tayari kuacha kufanyakazi kwa umakini lakini kwa woga walionao wanaamua kufanyakazi chini ya Kiwango kwa Lengo la kumfurahisha kiongozi .

Watu wa aina hii wapo Katika Jamii yetu. Ila Kwasisi tunaosali Biblia inasema hofu ni dhambi.

Sita, Hali ya Usalama wa nchi ni shwari kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo matukio ya hapa na pale ya Uhalifu lakini vyombo Vya dola vinajitahidi kadri ya uwezo wake kukabiliana na matukio hayo na moja ya ushahidi wa Hilo tangu serikali ya awamu ya tano ingie madarakani Mara kwa Mara tumeshuhudia Makamanda wa Polisi wa Mikoa Kadhaa waliripotiwa kutoa taarifa Kuwa Askari Polisi wa Mikoa Yao wamefanikiwa kuwaua kwa risasi watu waliwashuhuku Kuwa ni majambazi Kabla ya watu Hao kutekeleza matendo ya ujambazi na baadhi ya mapolisi kujeruhiwa na Kuuwawa Katika mapambano hayo na kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.

Saba, Katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha Utawala wako Rais Magufuli ameonyesha nia ya  kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ,kwasababu mikutano yako na viongozi mbalimbali ya Kimataifa iliyofanyika Ikulu Dar Es Salaam,Rais Magufuli umekuwa ukitumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano.

Oktoba 24 Mwaka huu,Mfamle wa Morocco ,Mohamed VI. Julai 10 Mwaka huu Waziri Mkuu wa India ,Narendra Modi .Machi 8 Mwaka huu, Rais wa Vietenam,Trouung Tan Sang.

Oktoba 2 Mwaka huu,Makamu wa Rais wa Cuba ,Savador Antonio , Julai Mosi Mwaka huu , Rais wa Rwanda ,Paul Kagame ,Oktoba 12 Mwaka huu, Rais wa Congo ,Joseph Kabila wote waliwasili nchini kwa tarehe hizo nilizozitaja hapo juu na walifanya mazungumzo na Rais Magufuli ambapo Rais Magufuli alitumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.

Nakupongeza Katika hili Kwani unakuza lugha ya Kiswahili kama kiongozi wa nchi inayozungumza lugha ya Kiswahili.

Nane, Mwamko wa elimu bure imeongeza usajili wa wanafunzi Kwani wanafunzi 800,000 wamedahiliwa  ndani ya Miezi miwili.Inaelezwa Kuwa Januari Mwaka huu,wanafunzi wa darasa la kwanza milioni 1.8 sawa na asilimia 84.5 walidahiliwa kujiunga Darasa la kwanza tofauti na Mwaka na Mwaka Jana ambao wanafunzi 128,000 tu ndiyo walidahiliwa.

Wanafunzi waliojiandikisha na elimu ya kidato cha kwanza wameongezeka  kwa asilimia  26  .

Na kila mwezi serikali inatoa Sh.bilioni 18.77   kwaajili ya kwenda kutekeleza elimu bure licha inachangamoto zake.


Aidha Katika Mpango wa elimu bure pia  Julai 14 Mwaka huu, Rais Magufuli Alizindua Mpango wa ugawaji wa madawati Kwenye majimbo y uchaguzi nchini,alisema tangu atoe agizo la kila Halmashauri inapaswa kuhakikisha shule zake zina madawati ya kutosha ,wananchi ,Wadau na Mashirika mbalimbali waliitikia kwa Mwamko.


Tisa,serikali imeongeza mikopo ya elimu ya juu kutoka Sh Bilioni 340 Mwaka 2015/2016 hadi Sh .Bilioni 483 Mwaka huu wa Fedha na Tayari mikopo hiyo imeanza kutolewa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Vya vikuu licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale.

Kumi,Julai 7 Mwaka huu, ilibaini Mabadiliko madogo ya sheria zilizoandikwa ( The Written Laws ( Miscellaneous Amendments ) Act 2016 Act No.3 of 2016'.

Mabadiliko hayo yalifuta  baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasomeka Katika ki fungu cha 18  (a,b) Magistrates Court Act, ambacho kilikuwa kinatoa mamlaka kwa Mahakama za Mwanzo kusikiliza kesi zenye thamani ya Sh.Milioni tano kushuka chini  na Act  (CAP .11 ) ambapo Kifungu cha 20 kilichofanyia marekebisho ya Kifungu cha 18 ,Mahakama za mwanzo zimepewa mamlaka kusikiliza Kesi zenye thamani ya sh.milioni 30 badala ya sh.milioni tano.ni jambo la kupongeza Kwani litasaidia kuondoa mrundikano wa Kesi Katika Mahakama za Wilaya ,Mikoa na Mahakama Kuu kwasababu Kesi hizi zitakuwa zinasikilizwa Mahakama za Mwanzo na kumalizika kwa haraka.

Aidha imekuwa ikielezwa Kuwa  uchumi wa nchi yetu mwaka jana ulikuwa wa asilimia 7  ,mwaka huu tumekusudia ukue kwa asilimia 7.2.

  Mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 7 hadi asilimia 4.5. Ni Ishara nzuri sote tushirikiane tufikie Malengo tuliyojiwekea.Ni jambo Jema.

MAPUNGUFU

Pungufu la kwanza ambalo tayari limeishamtia doa na linazidi kumpaka matope   Rais wetu ni hili la wananchi Wengi wamekuwa wakituhumu serikali yake inakandamiza Demokrasia waziwazi ,rais Magufuli wakati mwingine anatoa kauli za kibabe ,serikali yake inaua upinzani ukilinganisha na serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Kikwete ambapo watu walikuwa huru kutoa maoni Yao kwa huru.

Ibara ya 18(a) ya Katiba ya nchi, inasema ; " Kila mtu anao Uhuru wa Kuwa na maoni na kueleza fikra zake".

Hivyo Kimsingi mtakubaliana na Mimi  Kuwa haki ya watu kutoa maoni ni ya Kikatiba .

Wakosoaji wa serikali ya Magufuli na hata wale wanaoiunga mkono serikali na CCM kadri siku zinavyozidi kwenda Mbele chini kwa chini wamekuwa wakilalamika serikali ya awamu ya tano siyo rafiki kwa watu wanaotoa maoni Kwani baadhi ya watu wanaojaribu kutoa maoni Yao wamekuwa wakikamatwa  na kufikishwa mahakamani na mmoja alifungwa huko Arusha na mmoja alishinda Kesi Na wengine bado Kesi zao hazijamalizika huko mahakamani.

Siyo Siri tena siyo wasomi, watu wenye udhoefu wa mambo mbalimbali, wanasiasa ,wanaharakati na wananchi wa kawaida baadhi yao wameingiwa na woga  ya kutoa maoni Yao hadharani Kuhusu kutoa ushauri unaousu mambo mbalimbali yanayojenga nchi kwa hofu ya Kukamatwa na vyombo Vya dola na kushitakiwa.

Lakini mapema wiki hii Kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma, tumeshuhudia baadhi ya wabunge wa CCM ,Hussein Bashe, Mbunge wa Solwa ,Ahmed Ally Salum ,Mbunge wa Jimbo la Mtera ,Livingstone Lusinde walipongeza jitihada za serikali lakini waliikosoa serikali kwa Nguvu zote kwa uwepo wa uhaba wa mzunguko wa Fedha na mambo mengine mengi.

Wewe Magufuli ndiyo Rais wa nchi ,mwisho wa siku sifa Mbaya  au nzuri hata kama matendo hayo yalisababisha upate sifa nzuri au Mbaya hukuyatenda wewe Moja kwa Moja yametekelezwa na wasaidizi wako basi zitaelekezwa kwako .

Hivyo minashauri kwanza wewe binafsi na vyombo vyako vya ulinzi hasa Jeshi la Polisi katika baadhi ya mambo muwe wavumilivu  na mstahimilivu pale mnapoona  baadhi ya wananchi wenu  wakitoa maoni ya kutofautiana na wewe na serikali unayoiongoza.

 Maoni Yao yapi me kama yanalengo la Kujenga yachukue yafanyiwe kazi kama ni ya kipuuzi achana nayo na siyo kila Mwananchi anayetoa maoni ambayo yanawakera ni lazima mshitaki mahakamani, wengine wapuuzeni serikali iendelee kuchapa Kazi .

Magufuli wakati mwingine Jifunze uvumilivu kutoka Kwa Mtangulizi wako Rais  Mstaafu Kikwete ambaye alibezwa,kudharauliwa na picha za uchi zenye sura uchi aliyengenezewa zinafundikwa Kwenye Mtandao maarufu wa picha chafu wa THE UTAMU ,ambayo ulifutwa na wataalamu .

Rais Kikwete alivumilia yote Akaamua kuchapa Kazi licha ya kuwepo kwa mapungufu lakini Kazi alizozifanya za kimaendeleo wakati akibezwa na kudharauliwa na Watanzania hadi msafara wake kupopolewa kwa mawe Mkoani Mbeya ndiyo Leo hii wewe Magufuli una zindua  na kuendeleza Miradi hiyo iliyoanizishwa serikali ya awamu ya nne ya Rais Kikwete ambapo wewe ulikuwa ni Waziri wa Ujenzi.

Wakati mwingine kukaa kimya ni Jibu la Mjinga.Na ukikaa kimya utayahepuka Mengi.Wale wale waliokuwa walimtukana na kumdhalilisha Kikwete alipokuwa madarakani Leo hii bila aibu wamejitokeza kwenye vyombo vya habari wanasema wa namkumbuka na wanatamani hata sasa hivi Kikwete arudi Kuwa Rais wewe utoke maana serikali yako Ina minya Demokrasia na I wanaletea umaskini.

Na wananchi wale wale Katika kampeni waliokuwa wakikushangilia wewe kadri siku zinavyozidi kwenda wameanza kukuchukia na wengine hawataki hata kukuona na nikiweka Habari zinazokuhusu wewe Kwenye ukurasa wangu wa Facebook ,blog hawataki kuziona wanasema zina wachafu a hata kulike hawataki na nikikaa Katika vijiwe ambavyo  nilikuwa nikienda kukaa Katika Kipindi cha kampeni kwaajili ya kakupigia debe tena baadhi Yao ndiyo hawataki kusikia jina Lako na matusi wana kutukana na Mimi wananitukana na wamekupachika jina unaitwa (KIVURUGE) .

KIVURUGE maana yake wewe uliopo chaguliwa Kuwa Rais ndiyo umekuja kuvuruga kila kitu ( MVURUGAJI) Maisha Yao yamekuwa magumu kwasababu yako,umewabomolea nyumba,safari umefuta ,posho za muda wa nyongeza wa kazi umezifuta .Minachekea sina mbavu naambulia  kuyakoga matusi.


Hadi uimalize Miaka Kumi panapo Uhai serikali yako ikawafungulia Kesi za uchochezi watu wangapi Mahakamani?

 Kwani wakituolea maneno ya shombo/ kukudhihaki  wanakuchubua ngozi au ndiyo wa nafanya nafasi yako ya Rais ikome? Yesu  alidhihakiwa Msalabani na hadi Leo kuna binadamu wanatenda matendo na kutoa maneno ya kumdhihaki Mungu wazi wazi lakini wala Mungu awatoi Uhai,anawavumilia na anawapasha muda wa kutubu dhambi zao mwisho wa siku wanakuja kumrudia Mungu na Hao Hao walikuwa wanamdhihaki Mungu wakageuka Kuwa mashabiki wa kubwa wa Mungu wanakuwa Askari wa Yesu Wanahubiri Injili.


Achana nao waambie Hao Askari wako washughulike na mambo makubwa makubwa licha kwa Yule anatumia lugha za matusi kukosoa achukuliwe Hatua.

Magufuli Kumbuka ni vyombo hivi hivi Vya dola vilimvimbisha kichwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar ,Dk.Salimin naye kweli akavimba kichwa Leo hii Dk.Salim yuko peke yake Zanzibar  na Maradhi yake ya macho.Kuwa makini .

Nimefanya mahojiano yangu kwa Siri na madereva BodaBoda Kabla ya kuandika makala hii kila Nilipokuwa nikipanda pikipiki zao makusudi nilikuwa naanza mada za siasa na kuwahoji hii Hali ya kisiasa ikoje na Je Biashara Yao hivi sasa inakwenda vizuri ukilinganisha na Enzi za Kikwete .

Madereva wengine waliniambia kama niachane na hizo story hawataki kunisikia maana eti Magufuli kamwaga Mashushushu ambao madereva Hao wanawaita "Vihelehele" nao wamejigeuza abiria wanawachota akili madereva BodaBoda na wakibai ni madereva Hao wanaisema vibaya serikali wanawakama hivyo wanasema serikali ya Magufuli ya Moto" hawataki kuzungumzia Habari hizo licha Biashara Yao siyo nzuri sana ukilinganisha na Enzi za Kikwete Kwani hivi sasa abiria wao wa zamani wamekuwa hawapandi pikipiki zao kwa Wingi kama zamani wa nawaeleza Kuwa   Fedha " Magufuli kabana".


Hivyo baadhi nilizungumza hata wananchi wa kawaida wanasema wameamua kukaa kimya waone  mwisho wake utakuwa je.Na wengine wana mawazo mazuri tu ila wana hofu na serikali ya awamu ya Tano itawakamata .

Kwa mtazamo wangu Katika Kipindi hiki cha Mwaka mmoja, nimeona Rais Magufuli amekuwa akipenda kuzungumza kupita kiasi / kuwatolea lugha za ukali  Hadharani baadhi ya watendaji wake wa chini kabisa  mambo ambayo kama rais wa nchi kiuungwana na kidiplomasia hapaswi yamtoke kinywani Mwake Mbele ya hadhara .

Mifano ni mingi ila nitaiweka michache hapa, mfano Oktoba 17 mwaka huu, alipokuwa akiongoza Mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho wa mwili wa marehemu aliyekuwa Meya wa Jiji  la Dar Es Salaam, Dk.Didas  Massaburi, Msemaji wa familia ya marehemu Katika risala yake pamoja na mambo mengine alisema marehemu aliacha Mke mmoja .

Lakini Rais Magufuli alipopata fursa ya kuzungumza kweli alitoa maneno ya busara kwa watoto wa marehemu nay akubali lakini Rais Magufuli akatofautiana na msemaji wa familia Kuwa marehemu aliacha Mke mmoja akasema yeye anafahamu Kuwa marehemu Dk.Masaburi ameacha zaidi ya wake wanne  na watoto zaidi ya 20.

Sawa inawezekana ulipata taarifa za Siri Kuwa kuna mchezo mchafu wa baadhi ya wake ,watoto wa marehemu kutaka kudhulumiwa au kutotambuliwa lakini kweli Rais wa nchi unasimama Mbele ya umati wa watu  kuzungumzia mambo binafsi ya marehemu Dk.Masaburi?

Kauli yako hiyo inaweza kusaidia wake na watoto marehemu Masaburi wasigombanie mgawanyo wa mali lakini pia inaweza isisaidie pia kwani Tayari hapo kuna mchanganyiko wa mama tofauti na Damu tofauti na kila mmoja Ana hira zake na roho yake hivyo anaweza Kuzuka mtoto au Mke akazusha zogo la Kugombea mgawanyo wa Mali za marehemu na Mifano Hipo mingi Kwani hata baadhi ya watoto wa marehemu Mzee Mfaume Kawawa bila haya baba Yao alipofariki walimuanzishia vurugu Mke wa marehemu Kawawa na vyombo Vya Habari tuli ripoti tukio Hilo .Sitaki Hilo litokee Kwa familia ya mtani wangu Marehemu Dk.Masaburi.

Kweli Rais mzima wa Tanzania Mbele ya umati wa watu vyombo Vya Habari Vya Kimataifa vipo Unazungumzia   mambo binafsi ya marehemu Masaburi hata kama Angekuwa ni rafiki yako vipi kiasi gani?


Siyo kwa kiasi hicho.Kama ulitaka ujumbe wako ufike ungempa basi hata Mwenyekiti wa CCM Mkoa alisemehe Hilo  basi hata Ungetuma wasaidizi wako waende kwenye familia ya marehemu wakufikishie nasahaa zako .Badilika .

Mfano mwingine hivi karibuni Rais Magufuli ulitembelea Bandari ukiwa umevalia suruali,Kofia,shati jeusi na ulipofika Katika kitengo Kimoja, ukawa unamtaka kiongozi wa kitengo kile apige picha mizigo iliyokuwa nje halafu kompyuta za kitengo kile halafu hapo hapo uzione zile picha palepale.

Yule kiongozi wa kile kitengo cha Bandari kila alivyokuwa akijitahidi kukuelekeza kwamba ile Idara yake haiwezi kupiga picha ya mizigo iliyopo nje Moja kwa Moja kwasababu Idara yake inapokea picha za aina hiyo kutoka Katika Idara nyingine inayojitegemea ambayo ina kiongozi wake ambayo imeishapiga picha za mizigo inazituma picha hizo katika Idara yake lakini bado Rais Magufuli ulionyesha mashaka waziwazi na kutoridhika na maelezo Yale kwasababu ulionekana ukisema hivi' kama kompyuta hizi ni mbovu semeni, nataka mnionyeshe picha za mizigo iliyopo pale nje Mara Moja ....' Baada ya Yule Mkuu wa kitengo Kusimamia taaluma yake wewe Rais Magufuli Ukaondoka Katika kitengo hicho kwa haraka '.

Mimi sikupenda kile kitendo ulichokifanya Kwani licha ya Yule Mkuu wa kitengo bandarini kutumia lugha ya Upole kukupa maelekezo wewe ulikuwa ukionekana kuongea kwa Ukali ,na Kuonyesha kama vile ulitilia Mashaka maelezo ya Yule Mkuu wa kitengo na ukasema hata wewe hiyo Kazi ya mizani unaifahamu fika.

Rais Magufuli Kumbuka Hao watumishi wa umma nao wanastahili utu, heshima na wenyewe pia ni wanaume na wanawake zao majumbani,watoto na wakwe wanaheshimika hivyo sivyema ukafika Katika maeneo Yao ya Kazi na kuanza kuwahoji baadhi Yao kwa kutumia lugha za Ukali ambazo zina wafanya baadhi ya watumishi ukiwa unawahoji kuingiwa na uwoga ,kudhalilika Mbele ya Jamii kupitia Televisheni .

Ibara ya 12(2) Katiba ya nchi inasema ; " Kila mtu anastahili heshima ya kutambua uwa na kuthaminiwa utu wake".

Kitendo kile uchokifanya hakioendezi kwa jamii ya waungwana Kwani pia kitasababisha watu kupunguza molari ya kufanyakazi kwasababu ya kisasi cha kutolewa maneno ya makali na Mkuu wa nchi,Kumbuka nao ni binadamu hawajataliwa nyongo.

Katika Hilo la bandarini la Huyo Mkuu wa kitengo uliyokuwa unamshinikiza akuonyeshe picha za mizigo iliyopo bandarini.Minakushauri ingekuwa busara na bado Hujachelewa unaweza kumuita Mkurugenzi wa Bandarini na wale wakuu wa vitengo vile ulivyotembelea Ikulu uwaeleze wewe unataka hivyo vitengo vifanye Kazi kwa mtindo ambao unaoutaka wewe ambao labda Mataifa mengine wanafanya hivyo Kisha wape muda waseme hadi lini watakuwa wametekeleza Kisha wakuletee ripoti ya utekelezaji.

Ulipotembelea bandarini ulisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea Bandarini hapo akaamuru baadhi ya mashine zinunuli we lakini hadi wewe umeenda bandarini bado hazijanunuliwa na ukasema Fedha zipo.

Labda nikuulize Rais Magufuli hivi unafahamu kuwa Sheria ya Manununuzi ya Umma ipo na inafanyakazi na usipoifuata unashitakiwa na ukipatikana na hatia unafungwa?


 Mali za serikali lazima zinunuliwe kwa kufuata tarabu za Sheria ya Manunuzi ya Umma, Leo hii Mkurugenzi wa Bandari hawezi kukurupuka kununua hivyo vifaa walivyotakiwa wanunue na Waziri Mkuu, wewe Rais Magufuli bila kufuata Taratibu za Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Akikiuka Taratibu za Manunuzi ya Mali ya umma kwa Kigezo eti Waziri Mkuu,Rais Magufuli alisema hadharani basi  ajiandae kufikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ama Mahakama zingine kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababishia serikali Hasara kwasababu Mlikiuka matakwa ya Sheria ya Manunuzi na Jela mtakwenda peke yenu Hao wanasiasa waliyokuwa wakiwapa maelekezo hamtokuwa nao watakuwa majumbani mwao wamelala na wake zao,nawafahamu vizuri sana wanasiasa akili zao.

Akili kumkichwa nunue Mali za serikali kwa kufuata Taratibu za kisheria Puuzeni mashinikizo ya ununuzi kutoka kwa mabosi wenu ambayo hayapo Katika mfumo wa maandishi.

Na Mifano ipo Si ya Kutafuta waliokuwa vigogo wa SUMA JKT ,aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege David Mattaka, Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS , Charles Ekelege ambaye huyu hata gerezani alifungwa na Kesi zao nimeziripoti vizuri sana  pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam.

Mfano Mwingine Rais Magufuli hivi karibuni ulipoenda  kutembelea Shirika la Ndege ATCL na ukawahutubia pamoja na mambo mengi ulivyozungumza nayo ambayo ya aonyesha umedhamiria kuliongezea Nguvu Shirika Hilo uliongea maneno ambayo kama Rais hakupaswa kuyasema .

Rais Magufuli ulisema kuna wake wa mawaziri bila kuwataja majina yao wanafanyakazi hapa ATCL na ATCL inafanya vibaya wao bado wanang'ang'ania tu. 

Mimi sikufurahishwa na Kauli hii Kwani Kauli hiyo inaweza kutafsiri wa Kuwa wake Hao mawaziri ndiyo wa nasababisha ATCL isifanye vizuri .

Lakini baada ya muda Kauli hiyo ili zusha mijadala Katika Jamii na baadhi ya vyombo Vya Habari vikaamua kwenda kufanya uchunguzi ndani ya ATCL kubaini Hao wake wa mawaziri ni nani lakini walibaini Mke wa waziri ni mmoja tu ambaye ni Mke wa Waziri wa Ardhi ,William Lukuvi ambaye ni  Germina  Lukuvi ambaye aliajiwa hapo Mwaka 1987 Kabla hajaona   na Lukuvi.

Mama Lukuvi alihojiwa na baadhi ya vyombo Vya Habari akaeleza jinsi alivyojiunga na ATCL hadi hivi sasa alipo. Lakini siku Chache baadaye Mama Huyo aliamua kuandika barua ya kuacha Kazi kwa Hiari yake.

Simfahamu huyu mama ila nafikaga katika Moja ya Duka linaloelezwa Kuwa ni lakwake katika Jengo la Benjamin Mkapa kununua vipodozi Vyangu .

Kwanza Nampongeza sana kwa uamuzi wake wa kuachakazi hiyo namedhihirisha ni mwanamke makini sana, anajua kusoma alama za Nyakati na anaamini Kuwa anaweza  vile vile kupata riziki na kuendesha Maisha hata kama Hana  ajira ya serikali.

Hivi Katika akili ya kawaida Rais wa nchi alienda  ATCL kazungumza maneno kama hayo licha anakutaja jina ,hivi mamlaka nyingine za juu zinaongoza ATCL zingekuwa zinamchukuliaje huyu Mke wa waziri Angeendelea kufanyakazi Katika Shirika Hilo?

Maana watu wengine ni kama machizi hapa nchini Rais akiongea jambo hawana muda wa kulitafari ndiyo wanalichukulia ni Sheria, Kigezo cha kusurubu wengine Kumbe wakati mwingine Rais anaweza kukosea maana na yeye ni binadamu.

Kwahiyo hapo Tunajifunza pia Rais anaweza akapewa taarifa za uongo ambazo bila kujua akazitumia kutolea maamuzi ambayo yataumiza baadhi ya watu na baadaye Rais anakuja  kubaini taarifa zile alizopewa awali  akazitumia kutolea maamuzi Fulani zilikuwa za uongo na wakati huo uamuzi wa Rais uliotokana na taarifa za uongo umeishaaribia watu Maisha Yao na Kuwaumiza na kuwachafua Katika Jamii.

Masononeko ya Mama Lukuvi Mbele za Mungu hay atakwenda bure ipo siku Mungu atamlipia.

Mfano mwingine wa Rais Magufuli Kuonyesha Anaongea sana na kuamini sana baadhi ya taarifa za kupelekewa Vyanzo vyake kana kwamba hizo taarifa alizichunguza alizutafuta yeye binafsi  wakati akitakiwa Kumbe taarifa hizo anapewa na vyombo vyake ni  siku ile Magufuli alipitembelea  Benki Kuu ,pamoja na mambo mengine alisema ndani ya BOT kuna wafanyakazi hewa Kauli iliyoshtua Wengi na baadhi ya watu kuanza kuitazama  tofauti BOT.

Lakini siku Chache baadaye Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alihojiwa na Gazeti la Mtanzania ,Kuwa ni je ni kweli BOT kuna wafanyakazi hewa .

Gavana Ndulu ambaye ni Mchumi   mbobezi alimtaka Huyo Mwandishi aliyemuuliza Swali Hilo kwanza   aende akamhoji Huyo aliyemweleza Kuwa ndani ya  BOT kuna wafanyakazi hewa.

Na taarifa toka ndani ya BOT zinaeleza ndani ya BOT Hakunaga wafanyakazi hewa ndiyo maana hadi Leo hatujasikia Zoezi la kusaka Wafanyakazi hewa limebaini ndani ya BOT kuna wafanyakazi hewa.

Mfano mwingine wa Rais Magufuli Anaongea sana ni hivi karibuni alivyofaya  ziara yake Zanzibar na kuwahutubia  wananchi wa Zanzibar .  mambo mengi ya kujenga na kusisitiza upendo ,mshikamano Umoja  lakini Rais alishindwa kujizuia hisia zake na kujidhiirisha yeye ni mtu wa kulipa  kisasi jambo ambalo Mungu halipendi Kwani jukumu la kulipa kisasi ni la   Mungu.

Rais Magufuli alisema hivi atoe mkono wake halafu mtu aukatae Kisha mtu Huyo aliyoikataa kuupokea mkono wake aje kutaka mkono wake umsainie Nyaraka zake  yeye hatoweza kusaini Nyaraka za mtu Huyo kwasababu eti alikataa kupokea mkono wake wakati alipo msalimia.

Itakumbukwa Kuwa Katika msiba wa marehemu Aboud Jumbe Mwaka huu huko Zanzibar ,Rais wa Zanzibar Dr.Ally Mohammed Shein walikutana ana kwa ana mpinzani wake Maalim Seif Sharif Hamad na Dk.Shein alikuwa akimsalimu Seif kwa njia ya kumshika mkono lakini inaelezwa Kuwa Seif alikataa kupokea mkono wa Dk.Shein kwasababu anazozijua yeye.

Vyovyote Iwavyo, mtu yoyote aliyeshiba Mafundisho ya dini, muungwana na Rais wa nchi hakupaswa kutoa Kauli kama hiyo hadharani ambayo ni wazi inaonyesha ni mtu asiye na desturi ya kusamehe,uvumilivu na mtu mwenye kinyongo kwa mtu anayefikiri amekosea wakati Mungu Mwenyewe ni mvumilivu,anasamehe na Mungu anatukaza kulipa visasi kwanini jukumu la kulipa visasi kwa watesi wetu ni lake.

Ni hatari Kuwa na Rais wa nchi anayetoa Kauli kama hii hadharani zinazoonyesha ni mtu mwenye kinyongo na mlipa visasi   kwa mtu atakayebaini atakwenda kinyume na matakwa yake.

Maalim Seif ni Makamu wa Pili  Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ana Stahili zake anatakiwa kuzipata kwa mujibu wa Sheria sasa mtu anayefikiri Sawasawa hawezi Kutamka hadharani Kuwa kwakuwa amekataa kupokea mkono wake basi siku Seif akitaka kutibiwa nje ya nchi hatoidhinisha Maombi yake .

Kukataa Kupokea salamu ya mtu siyo kosa kisheria linaloweze sababisha mtu ashitakiwe au Rais amnyime mtu Stahili zake anazostahili kwa mujibu wa Sheria kisa amekataa kupokea mkono wake.

Rais Magufuli alipokuwa akihutubia wananchi wa Kaliua Katika mikutano yake  ya kampeni za urais CCM Mwaka 2015  alinukuliwa akifanikiwa akisema akifanikiwa Kuwa  Rais wa Tanzania ataakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati na kwamba hatokubali kuona wanafunzi wamefika tayari vyuoni na bado hawajapatiwa mikopo ,waliowacheleweshea wanafunzi hao mikopo atawashughulikia.

Lakini tumeshuhudia Katikati ya Oktoba Mwaka huu, kulizuka mvutano wa ,Wanafunzi  wa baadhi wa Vyuo Vikuu  wakilalamikia utaratibu mbovu wa mikopo kwa Mwaka huu Tayari walikua wameishafika vyuoni .

Haki iliyosababisha Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa Mradi wa mabweni wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam,    Oktoba   Mwaka huu, alikiri  kutokea kwa dosari za kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo na kuitaka Bodi ya Mikopo kajipange sawa sawa iondoe hizo dosari  na hadi sasa hajamchukulia Hatua mtu yoyote aliyesababisha dosari hizo.

Lakini ushahidi wa Video unaonyesha ni Magufuli huyu huyu Kwenye kampeni zake za CCM Mwaka 2015 alisema akiwa Rais ole wake anatakaye mcheleweshea mwanafunzi wa Chuo Kikuu mikopo atamshughulikia na video ipo inayomuonyesha akisema hayo wakati wa kampeni za kusaka urais.

Ila kwakuwa amekiri dosari ni vyema, ila hii inatufundisha binadamu hasa wanasiasa tuwe na tabia ya kuweka Akiba ya maneno.

Tusipende kuzungumzia mambo ambayo hatutayafikia kuyapata au kuyatenda  Kuwa nikipata kitu Fulani nitafanya hivi Mara vile tena Mbele za watu mwisho wa siku ukipata hayo madaraka unashindwa kutekeleza kwa vitendo Yale uliyoyasema Kabla hujapata madaraka hayo.Ni Mbaya sana Kwani wakati mwingine ni Kigezo Kimoja wapo kinachokuondolea sifa ya kuaminiwa Taratibu.


Mapema kabisa wakati umeshika madaraka ya urais ulitamka hadharani Kuwa  utahakikisha unawabana wale waliokuwa wanaishi Maisha kama wapo pepo ili waanze kuishi kama mashetani.

Hii Kauli ni Mbaya sana  Kwani  Mungu Mwenyewe anasamehe Saba Mara sabini na hat hivyo   Mtoa riziki ni Mungu .Vidole vyenyewe Vya mikono havilingani kuna virefu na vifupi hivyo kuna matajiri na masikini.

Hivyo mtu Kuwa Tajiri siyo dhambi na Kuwa masikini siyo dhambi yote ni mipango ya Mungu. Unaweza usiwe Tajiri lakini ukawa Kinara wa Kutenda dhambi na kuvunja Sheria.

Hadi  sasa Hakuna Mahakama yoyote nchini hadi sasa haijamkuta  na hatia mshitakiwa  yoyote  wa Kesi za wizi,uhujumu uchumi au matumizi Mabaya ya madaraka walioshitakiwa katika utawala wako Kwani kwa mujibu wa Ibara ya 107A ( 1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 , inasema ; " Mamlaka yenye Kauli ya mwisho ya Utoaji Haki Katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama'. 

Na Mungu hapendi watu wake aliyowaumba waishi kama mashetani sasa wewe  Rais wetu huu uhalali wakutaka watu walioumbwa na Mungu waishi kama mashetani umepata wapi?Ni Mungu gani huyo Kakupa madaraka hayo ya kuwafanya watu aliyowaumba waishi kama mashetani?

Hagai 1:7-8 Katika Biblia Mungu anasema  ; " Nami nitatikisa Mataifa yote ,na vitu vinavyotamaniwa na Mataifa yote vitakuja ,nami nitaijaza nyumba hii utukufu ,asema Bwana wa Majeshi . Fedha ni Mali yangu na dhahabu na dhahabu ni Mali yangu ,asema Bwana wa Majeshi".

Hivyo kwa mujibu wa nukuu hiyo ya Kitabu cha Hagai 1:7-8  ,Mungu anatumbia Kuwa Fedha Mali na dhahabu ni Mali yake siyo Mali ya binadamu. Ndiyo maana kuna Msemo maarufu usema binadamu Hana mamlaka ya Kuzuia riziki za watu ila anachelewesha tu.

Licha hii aimaanishi watu wanahusika na vitendo Vya kuhujumu uchumi wa nchi wakichukuliwe Hatua ,Nasema wachukuliwe Hatua kwa Taratibu za Sheria za nchi.

Jambo jingine ni ule uamuzi wako wa Kuzuia wakuu wa Mikoa, Wilaya wasiende kushiriki sherehe za kilele za Kuzima Mwenge Mkoani Simiwi dakika za mwisho wakati taasisi ulifahamu kuwepo kwa sherehe hizo
Posho Simiwi , kuwafanyia viongozi wako  wameadhirika,waathirika kisaikolojia .na Hao


MAPENDEKEZO

Ili Rais wetu Magufuli ondokana  na tabia ya kuongea mambo ambayo hayafai  kutamkwa kwa umma na mtu mwenye hadhi ya Rais wa nchi.

Ni vyema sasa Wasaidizi wa Rais wajenge utaratibu wa kumbana Rais awapo Kwenye baadhi ya shughuli mbalimbali za kiserikali awe anazungumza kupitia hotuba zilizoandaliwa na wasaidizi wake Kwani kama Hilo halitofanyika ipo siku tusije kushangaa Rais akatoa maneno ambao yataleta Shida.

Maana Kauli za Rais ni nzito jamani na wakati mwingine zinaweza kutumika kuanzisha mchako wa kutunga Sheria mbalimbali .

Pendekezo la pili, Nashauri kama Rais Magufuli kama alishawahi kuhudhuria kozi ya Diplomasia ,sawa na kama hadi sasa bado haja pelekwa kuudhurulia kozi ya Diplomasia basi hajachelewa .

Uandaliwe  utaratibu wa kumtafutia walimu wa Mafunzo hayo   ili wamfundishe zaidi mambo ya kidiplomasia ambayo pia yatamsaidia Kuwa na subira ,uvumilivu Katika Utendaji Kazi wake ikiwemo wakati akitoa matamshi yake Mbele ya umma na jinsi ya Kutenda Kazi za watumishi wake wa umma bila kutolea watu Kauli za Ukali ambazo baadhi ya watu wanasema Kauli za aina hiyo zinatolewa na ' WAKUDA' ,hazipaswi kutolewa na mtu mwenye hadhi ya Rais wa nchi.

Katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Mwaka huu Dodoma, muda mchache baada ya kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu ,Rais Mstaafu Dk.Jakaya Kikwete  Katika hotuba yako uliongea mambo mengi na mipango mingi unayopanga kuifanya ndani ya CCM na Moja ya Kauli yako ulisema unawaomba wananchi wakuombee uwe na moyo wa uvumilivu kwasababu moyo wa uvumilivu kama aliyokuwa nayo Rais Kikwete wa kuvumilia watu unaona wanakwenda nje ya mstari kama wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mwaka Jana Katika mkutano wa kumchagua mgombea mmoja wa CCM ili awe mgombea urais wa CCM .

Ambapo  baadhi ya wajumbe Katika mkutano ule wakati Mwenyekiti wa CCM Enzi hizo Rais Kikwete alipokuwa akiingia ukumbini baada ya Jina la aliyekuwa Kuwa Kada wa CCM ambaye alikuwa na wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono kukatwa jina lake waliamua kuimba ' Tunaimani na Lowassa oya oya oya...badala ya kuimba Tunaimani na Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano' .

Magufuli alitamka wazi wazi Kuwa yeye ndiyo angelikuwa ni Mwenyekiti wa CCM halafu wajumbe wa mkutano wanamfanyia vile as ingeweza kuwavumilia angewashughulikia kikamilifu. Kwa Kauli hiyo ni uthibitisho Kuwa Rais Magufuli Hana moyo wa uvumilivu kwa wale wanaotenda mambo ambayo hayapendi.

Hata hivyo ni hatari pia kwa Rais wa nchi kutamka hadharani Kuwa Huna moyo wa kuvumilia watu unaowaona wanakwenda kinyume na wewe au Sheria za nchi Kwani Kumbuka Shetani naye yupo Kazini hajalala ,unapoanika Udhahifu wako huo kwa umma na wewe ni kiongozi wa nchi tambua Kuwa kuna watu ambao wanauwezo wa kukufikia wewe na unawaamini sana Kumbe wengine wana roho za kishetani,wachonganishi,watu wanaotaka kulipiza visasi dhidi ya watu ambao hawawezi kukufikia wewe wakaja kwako wakakujaza maneno ya umbea ,fitna dhidi ya ha watu na kwakuwa wewe Tayari umeishaanika Udhahifu wako hadharani Kuwa Huna roho ya uvumilivu utawaamini unakurupuka utaamuru washughulikiwe au wewe wewe Mwenyewe utoe uamuzi wa Kuwafukuza Kazi au utengue Teuzi zao.

Na hili linawezekana sana maana hii nchi kuna watu shetani amewabariki Kauli ,kila wanapokwenda kupeleka uzushi,uzandiki dhidi ya wenzao wanasikilizwa na kuaminiwa sana baadaye na baadhi ya watu wale Wahanga wa uzushi wameishaumia na kuharibiwa Maisha Yao ndiyo ukweli unakuja kujulikana Kuwa walisingiziwa .

Wewe Magufuli ni shahidi Katika hili ,na Mimi pia ni shahidi Katika hili na mfano  mzuri ni wa jinsi Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu ,mashetani wachache ndani ya serikali ya awamu ya nne walivyomharibia Maisha yake na kumfanya Aisha Maisha mateso ,Fedhea kwa uzushi tu na Kesi ya uhujumu uchumi wakambakia pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  siku chache tatu tangu Rais Kikwete alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza.

Llakini kwakuwa Balozi Mahalu ana rekodi ya uadilifu ndani na nje ya serikali na ni shabiki namba Moja wa Mungu tatizo Hilo akimkabidhi Mungu na ndani ya serikali ile ile ya Kikwete kwa Siri kuna maofisa wa serikali walijitokeza kumpiga nia kwa Nguvu zote hadi akashinda Kesi hiyo ambayo iliandika historia hapa nchi ambapo mmoja wa shahidi wa Mahalu alikuwa ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye alifika mahakamani kutoa ushahidi wa kumtetea Mahalu na alishinda serikali ikaumbuka .

Binafsi Nilipokuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania nilipata fursa ya kuripoti Kesi hii mwanzo hadi mwisho Katika ngazi ya Mahakama Kuu pia hata DPP alipokata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam pia niliiripoti Kesi hadi siku DPP wa enzi hizo alikuwa Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alipoamua kuifuta rufaa hiyo kwasababu alikuwa Hana Haja ya kuendelea kumpatia rufaa Balozi Mahalu na Grace Martin.

Hivyo nakushauri sana kila siku omba Mungu akupe moyo wa subira, uvumilivu ,Hekima kikweli kweli Mungu atakupatia kwani ukisoma Kitabu cha 1 Wafalme  3 :5-14 katika Biblia ,utaona Mfalme Selemani aliomba Mungu ampe hekima na alimpa.Binafsi ,Kiongozi wa Kanisa ninalosali la Elshadai Temple lililopo Boko Basiaya Dar Es Salaam, linaloongozwa na Nabii ,Kanali Mstaafu, Bruno Kinunda na waumini wote Kabla ya kuanza ibada ya Jumapili tu nakuombea Ulinzi,Hekima ,busara na uvumilivu Katika kuongoza taifa hili na Mimi ndiyo niliyoenda Kwa Siri kumweleza Nabii Kinunda aongezee maneno ya Busara,Hekima na uvumilivu wakati tukikuombea Kwani hapo awali alikuwa akituongoza kukuombea kwa kukuomba Mungu akupe Ulinzi ,Afya njema .

Hekima ,uvumilivu ,busara  vitakusaidia sana kuondokana na Hali kuongea sana hadharani mambo ambayo kama Rais Hupaswi kuyatoa kinywani mwako.

Wapuuzi wachache wanaweza Kusema makala hii ina Lengo la kukudhihaki, Si kweli Kwani hata Mimi kwa asilimia Fulani nilikuwa na tabia kama yako ya kutaka jambo Fulani lifanyike kwa wakati huo huo haraka tena nilikuwa Mkali sana na watu waliniogopa sana na hiyo Hali ilisababisha nikose vitu vingi Vya maana .

Kwa Kuwa nia yangu ilikuwa ni njema ya kutaka wahujumu wa nchi hii na wavunja Sheria wachukuliwe Hatua kupitia makala mbalimbali nilizokuwa  naziandika, Na wakati huo nilikuwa sijitambui Kuwa hiyo Hali niliyonayo ya Pupa,jazba ya kutaka vitu vifanyike haraka bila kuvuta subira nilikuwa nakosea sana na kugeuka Kituko Mbele ya wasomi wa Sheria .

Ndipo mtu mmoja ambaye alikuwa Ni Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambaye alipokuwa DPP nilifanya kazi sana na Ofisi yake kwa kuripoti Kesi zao bila kuchoka, ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kulibaini Hilo tatizo langu la Kuwa na pupa ,kutokuwa na uvumilivu pindi ninapokuwa nimekerwa na wavunja Sheria ,ha kujificha alinieleza Hilo tatizo langu na akaniambia kama nipo Tayari kuondokana nalo kwanza nikiri Mimi binafsi kwa Mungu silitaki tatizo Hilo liendelee kuwepo Ndani ya mwili wangu na akaniambia nijiendeleze kielimu na ya kuchoka Mara kwa Mara kunifundisha mbinu ya kuondokana na tatizo Hilo kwa zaidi ya Miaka Saba yote a lilipokuwa DPP .

Haikuwa Kazi rahisi kwakwe kunio ndoa Katika hicho kilema cha kukosa uvumilivu,Kuwa na Pupa lakini alifanikiwa kwa asilimia 90  na asilimia 10 zilizobakia zilikwenda kuondolewa na Mzee wangu ambaye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo( UB) ambaye ni Boss wangu ,Profesa Costa Ricky Mahalu Kwanini Mimi ni Ofisa  Habari wa Chuo hicho,ambaye muda wote Mahalu amekuwa akiniambia Mimi na wasomi wenzake Happiness Katabazi ana akili sana ila hakuwa amepata mwongozo wa kupata elimu tangu alipokuwa Mdogo na kwamba ataakikisha ananisaidia ananisaidia nijiendeleze kielimu na niachane na tabia ya pupa Katika kuchukua maamuzi,niwe mfumo livu,subira na kumtegemea Mungu kwasababu siyo Siri sisi waandishi wa Habari Wengi ni wachangamfu kupita kiasi na ni waongeaji kupita kiasi na bila Kuwa na tabia hizo huwezi Kujenga marafiki/ Vyanzo Vingi Vya Habari na hutopata taarifa nyingi .

Balozi Mahalu ni Mwanasheria ambaye amebobea Katika Sheria za Kimataifa na ni Mwanadiplomasia vile vile , University of Bagamoyo walitaka niache Kazi Gazeti la Tanzania Daima ili niende University of Bagamoyo kama Ofisa Habari wa Kwanza wa hicho hadi sasa ni Ofisa Habari wa hicho chuo ,Balozi Mahalu siyo mwongeaji sana Kumbe alinibaini ni tatizo la kukosa uvumilivu,kushindwa kuvumilia ninapokasirishwa na sijui mambo ya Diplomasia hata chembe.

Nakumbuka Boss wangu Mahalu alimuita Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayeshughulikia Taaluma, Dk.William Kudoja na Aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtaro akawaambia Happiness ni binti mwenye akili na uwelewa mpana wa mambo hivyo hili mwisho wa siku asije kukitia aibu chuo kwa kukukosa uvumilivu kuropoka inabidi atafutwe mwalimu anayefundisha kozi ya Protocol and Etiquette amfunishe kozi hiyo peke yake hapa chuoni ili aondokane na tabia za ajabu ajabu.

Kweli alitafutwa Mwanadiploma Mkongwe Mstaafu ambaye aliwahi kufayakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ambaye amewahi kuwa Mhadhiri wa kozi ya Diplomasia Katika Chuo cha Diplomasia ,Mr.Edward Kadiri aliletwa chuoni hapo na kunifundisha kozi hiyo ya muda mfupi Mimi peke yangu Katika maeneo yafuatayo ;

1. Diplomatic and Consular Relations and Practices,
2.Diplomatic ,Official and Social Protocol.
3.Diplomatic,Official and Social Etiquette


Kadri  siku alivyokuwa alinifundisha mhadhiri huyo Mr.Edward Kadiri nilifikiri a zile tabia za kishenzi kishenzi za kuropoka,kukosa uvumilivu ninapokerwa nilizokuwa nikizifanya  Kabla Jaji Feleshi  kunikosoa , Mr.Kadiri ajaanza kunifunda  na nikajiona nilikuwa ni mpumbavu  wa Hali ya juu na nikakubali kuzidi kujishusha kwako pindi wanaponirekebisha pindi ni endapo ofisini kwako,kwa njia ya simu  na kubadilika na nilipomaliza kozi hiyo nilienda kuwashukuru  kwa maboss wangu Kuwa kozi ile imenisaidia sana kuniondolea kilema cha kukosa uvumilivu ,kuropokaropoka walicheke sana na wa kafurahi lakini Leo maboss wangu wanajivunia Kuwa Fedha waliyonilipia ya kujisomesha kozi hiyo Fupi ya Diplomasia imesaidia kumjengea uwezo Ofisa Habari wao ambaye ni Mimi na wamekiri imenibadilisha tabia yangu.

Aidha Jaji Dk.Feleshi ambaye ni miongoni wa wanasheria wachache wabobezi katika Sheria ya Sayansi ya Jinai na,Balozi Mahalu ambao ni Wanasheria kitaaluma  waliniakikishia wataendelea kunishape niondokane na ule ulemavu wa kupayuka payuka,kukosa uvumilivu na Kuwa na papara wa kaniambia kwakuwa nilikuwa Mwanafunzi wa Shahada ya Sheria ninakutana na Alternative Dispute Resolution (ADR ) na kwamba somo Hilo pia litachangia kuniondolea hicho kilema cha kuropoka,kukosa uvumilivu na kukataa kusikiliza wenzangu wanasema nini pindi ninapopandwa na jazba.

Hakika Nilipokuwa mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu 2016 , Somo la ADR Nilifundishwa na Mwanasheria Aghatha Lend .

Ndani ya kozi  Hiyo kuna Topiki Moja ya kutatua Migogoro nje ya Mahakama na Hatua zake .

Kwakweli nililifuatulia kwa makini kozi  hiyo na nikajifunza Kuwa msuluhisi/Mtoa Haki yoyote Yule   anatakiwa kwanza asiwe na upande,awe anajua kutunza Siri,awe mvumilivu,afuate Taratibu Katika kuendesha mambo ya kisuluhishi kwakweli hapa napo palinisaidia sana kunitibu tatizo langu.


Lakini  wakati nikipitia Hatua zote hizo la kutibu tatizo langu Hilo Kila ninapenda Kanisani kusali na n ikamkabidhi Nabii jina langu nanikaorodhesha Shida zangu kwa maandishi Kuwa anapokuwa anaomba kwa muda wake namimi ninapokuwa naomba nyumbani na kanisani naomba Mungu aniondolee tatizo la kuropoka,anipe uvumilivu,subira na kweli namshukuru Mungu hivi sasa nimebadilika hata mtu akinitukana Leo hii naweza kuvumilia nisimjibu au naweza Kumjibu sentensi Fupi ambayo itafamnya ajione yeye ni shetani  Hana akili na mwishowe atataka kuanzisha vurugu na Mimi nitamkwepa.

Nimelazimika kuanika Hatua hizo nilizo pita kumaliza tatizo langu Hilo la kukosa uvumilivu kwa watu wanaokukosoa au wanaovunja Sheria ,papara,kuropoka ili liwe Funzo kwako Rais Magufuli ambaye Mara Kadhaa kwa kinywa Chako umesema Huna moyo wa uvumilivu kwa wanaokosea,na pia wengine wasiyokuwa na moyo wa uvumilivu,Hekima ambao wanataka wabadilike wajifunze kupitia Mimi maana tatizo Hilo lilinisababishia ni kukosa mambo mengi mazuri nanilikuwa sitambui kama nakosea nilikuwa najiona Mimi ndiyo Mwamba napatia Kumbe nakosea Kwani unaweza kumrekebisha mtu unayefikiri anakosea kwa sauti ya Upole tu na akalelewe vizuri kuliko kumkaripia na kumuonyesha ubabe.

Tatu, Rais Magufuli ameishagundulika Kuwa nia yake ni njema ya kutaka kuiletea  taifa hili maendeleo na Mimi binafsi sitaacha Kumuunga mkono kwa harakaharaka .

Ila  Nashauri Rais kuanzia hivi sasa apunguze au aache kutoa Kauli mara kwa mara hadharani za Kulalamika Kuwa nchi unayoiongoza  ndiyo imekithiri kwa ufisadi na kwamba kila eneo linanuka ufisadi.

Hakuna ubishi kuna baadhi ya Sekta zilikuwa zikiandamwa na tuhuma chafu licha siyo zote na siyo wafanyakazi wote wa umma ni wachafu ,wapo wasafi na waadilifu kwa Taifa Lao na ndiyo maana muda wote wamefanya kazi serikali kupitia taaluma zao na uadilifu wao hadi wewe ukawa Rais wa nchi na Leo unatimiza Mwaka mmoja.

Siyo sifa kwa kiongozi wa nchi kusimama majukwaani iwe Kwenye shughuli za Kitaifa,nyuma za ibada  Kulalamika Kuwa nchi hii imekithiti kwa ufisadi.Kwani wewe ndiyo baba mwenye nyumba unavyosimama nje ya nyumba Yako/ majukwaani unalalama Kuwa watoto wangu ni Malaya sana ,unategemea hata kama kuna mwanaume jirani alikuwa anataka kuwachumbia Hao watoto wako Atakuja kweli kuchumbia watoto wako?

Kwanini hao watoto wako usiwaite ndani ukawakanya kama mzazi kwa lugha za stahaa watakuelewa.

Hawezi kwasababu Tayari baba mwenye nyumba umeishatamka mtaani Kuwa watoto wako ni Malaya sana.

Hivyo basi hata kwa wewe Rais ambaye Leo unatimiza Mwaka mmoja tangu uwe Rais ,achana na Kasumba ya kurudiarudia tena Hilo neno la kwamba Tanzania ufisadi ulikithiri,Mara Watanzania ni Wapiga Dili Kwani ukumbuke Mataifa mengine yapo macho yanafuatilia kila unachokozungumza wanakipa na kukiranyiakazi na mwisho wa siku Watanzania Mbele ya sura ya Dunia tutakuwa hatuaminiki tena kwasababu ya Kauli zako unazozitoa Mara kwa Mara wakati wanaotenda mambo hayo machafu ni wachache siyo Wengi .

Usije ukashangaa hata baadhi ya wawekezaji wengine wanaogopa Kuja kuwekeza hapa nchini kwasababu ya Kauli zako za kila Mara Kuwa kila sehemu Katika nchi kuna Wapiga Dili.Na Wapiga Dili kila nchi wapo umewakuta utawaacha .


Sasa hivi hao ' wazee wa mishemishe 'nikama wanausoma mchezo unaocheza ,wa nakuvutia kasi tu na hivi bado una safari ndefu Katika Kipindi Chako cha urais lazima  ' watakufurahisha' .

Kuna watu hapa duniani wao Maisha Yao yote ni kupiga Dili tangu vijana, wa nazeeka ndiyo shughuli zao hizo utawawezea wapi?Utawabana wachache kwa muda Fulani wengine hutafanikiwa kuwabadili tabia Kwani hizo tabia za kufanya Mishemishe,kupiga Dili zipo Kwenye Damu Yao.

Nne, Acha kuzungumza hadharani Kuwa wanaolalamika  Maisha magumu hivi sasa walikuwa ni 'Wapiga Dili' Utawala uliopita. Siyo kweli Kuwa wote wanaolalamika Maisha ni magumu Katika Utawala wako eti wote ni Wapiga Dili siyo kweli ni uongo wa wazi Kwani siyo Siri tena kila pembe hivi sasa watu wanalalamika Maisha yamekuwa magumu Kwani upatikanaji wa Fedha mitaani umekuwa ni mgumu kwasababu mbalimbali .

Kweli miongoni mwa Wanaolalamika walikuwa ni 'Wapiga Dili',lakini kuna hata wafanyabiashara halali tunawajua, wafanyakazi wa Sekta za umma na binafsi wanapata kipato halali na uadilifu wao hautiliwi shaka wanalalamika pia na huo ndiyo ukweli Kuwa upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu hivi sasa kwasababu wewe Rais Magufuli ulitangaza serikali yako imeanza kwa kubana matumizi kwakufuata posho, safari.

Watumishi wa umma pamoja na kulipwa mishahara pia posho za vikao, safari ndiyo zilikuwa zina wasaidia kuwapunguzia makali ya Maisha ambayo wanayaona hivi sasa.

Hivyo Huyo aliyekwambia utamke siku ya sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kuwa wanaolalamika Mara kwa Mara  ugumu wa upatikanaji wa Fedha ni wachache ndiyo hao wachache walizoea vya dezo.

Ukweli ni kwamba kadri siku zinavyozidi kusonga Mbele wanaolalamika wanazidi kuongezeka hivyo siyo wachache na kwamba ni Wapiga Dili peke yake ,hivyo waliyokupa taarifa Kuwa wanaolalamika ni wachache amekudanganya sana.


Serikali ndiyo yenye hela Ikiziminya Fedha zake na isipofanya manunuzi kwa wingi,ikafuta safari,posho kwa watumishi wake  ni wazi watu wanaotegemea kufanyabiashara na serikali watateteleka na wengine wanasema wameishateteleka  kiuchumi na huo ndiyo ukweli Leo hii baadhi ya mahoteli yanakosa wateja Wengi kama zamani,zinashindwa kujiendesha kwasababu serikali haipeleki tena mikutano yake Katika baadhi ya Hoteli za watu binafsi kama zamani.

Kuna hata watumishi wa umma wengine ni wateule wako,viongozi wa dini ,watu wazima na heshima zao ambao uadilifu wao hautiliwi Mashaka nao pia wanalalamika Kuwa mzunguko wa Fedha tangu Rais Magufuli ulipoingia madarakani hadi sasa umekuwa mgumu mno na Mimi binafsi naungana nao Kuwa ni kweli Hali ya upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu sana kwasababu wewe Mwenyewe Rais Magufuli umenukuliwa serikali yako inabana matumizi na umesema utaendelea kubana matumizi .

Na kama Mnasema ni Wapiga Dili/ mafisadi ndiyo wanalalamika Hali ya Maisha na upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu Mbona hivyo vyombo vyako Vya Ulinzi Usalama haviwakamati basi Hao Wapiga Dili/ wahalifu?

 Tano, Katika fikra zako kuanzia sasa acha kutoa Kauli zinaonyesha wazi Kuwa upo kwaajili ya kuwasaidia na kuwatetea sana watu masikini .Hii Kauli umekuwa ikiirudia Mara kwa Mara .

Nakukumbusha wewe ni Rais wa Watanzania wote Maskini,matajiri na watu wenye kipato cha Kati.Hata matajiri pamoja na utajiri wao nao wanashida zao tena ukute Shida zao ni kubwa kuliko masikini.

Ibara 13(4) ya Katiba ya nchi inasema ; " Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya Sheria yoyote au Katika utekelezaji wa Kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi".


Napendekeza kaa na vyombo vyako mtijitafakari kwanza ni kwanini hivi sasa baadhi ya wananchi wamekuwa na woga wa kujitokeza adharani kutoa maoni Yao kuhusu serikali yako kwa Madai Kuwa serikali hii haitaki  kukosolewa na ukiikosoa unashitakiwa?

Mkishabaini fanyeni mbinu ya kuondoa hiyo Hali kwa wananchi wenu maana hivi sasa hata wasomi pia wanafahamu mambo mengi mazuri ambayo wakiyatoa adharani yataisidia kuleta maendeleo Katika taifa letu Lakini wanaogopa kuyatoa adharani kwa Kigezo cha kuanza kufatiliwa na serikali ya Magufuli.

Binafsi naona  kuna Chanzo kikichosababisha baadhi ya wananchi Hao kukutwa na Hali hiyo na Kuishia kunung'unika chinichini, kwa kuandika maoni Yao kwa njia ya mafumbo,wengine kukaa na madukuduku Yao kifuani  wa kuogopa kutoa madukuduku /maoni Yao hadharani kwa Sababu eti watakamatwa na wengine wa nadiriki Kuita ni ya kidikteta.

Kwani Rais Magufuli utambue jambo Moja binadamu yoyote huwezi kumzuia asifanye jambo analolitaka kujifanya ana uwezo wa kutumia njia yoyote ile kufikisha ujumbe kama ni wabunge wa CCM, watumishi wa umma ambao wanaogopa hawaridhiki na mambo yanavyoendeshwa na serikali wanaweza kuwapatia taarifa viongozi wa vyama Vya upinzani au watu wenye sauti Katika Jamii wa siyoogopa wakapaza sauti kwaniaba Yao bila wewe Kufahamu na ujumbe ukafika kwa Jamii vizuri tu na Dalili hizo nimeanza kuziona .

Pendekezo jingine, naomba serikali ya awamu ya tano uwezekano wa kuibadilisha hii sera ya Utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwasababu hayo Masharti yaliyomo Katika hiyo sera ni ya Kibaguzi na yenye Lengo la kutaka kundi Fulani la vijana wa nchi hii wasipate elimu ya juu kwa Kigezo eti walivyokuwa wakisoma shule za Sekondari rekodi zao zinaonyesha walikuwa wakisoma Sekondari za kulipigia kwa gharama kubwa hivyo wazazi wao wanauwezo wa kifedha wa kuwalipia elimu ya Chuo Kikuu na hivyo hawastahili kupewa mkopo.Huu ni ushenzi wa Hali ya juu na au vumiliki.

Kwasababu mambo uenda ya kubadilika Leo Mzazi /Miezi/mfadhili wa mtoto anaweza Kuwa na kipato cha uhakika kama mshahara ,Biashara ,au Mali zisiozamishika ambazo ndiyo zikawa ni Chanzo Chake cha kipato kwa wakati huo kilichomuwezesha kwa wakati huo kumsomesha mtoto shule za Msingi, Sekondari za kulipia .

Lakini Ilipofika wakati mtoto Huyo amefanikiwa kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu hivyo Vyanzo Vya Mapato Vya Huyo Mzazi,Mlezi, mfadhili vimekufa kwasababu mbalimbali ikiwemo kufilisiwa, nyumba kubomolewa na serikali ,kufukuzwa Kazi au kustaafu hivyo anajikuta anashindwa kumlipia Ada ya Chuo Kikuu mtoto Huyo wakati huo sera ya Bodi ya Mikopo nayo inasema haiwezi kumpatia mkopo kwasababu rekodi zinaonyesha eti wazazi wake ni vigogo wanauwezo wa kumlipia Ada na sababu nyingine kuwa hawasomi kozi zenye kipaumbele chakupewa mkopo.Hatari sana.

Hivi mtu anataka mkopo akope kwanini serikali inashindwa kuweka utaratibu wa kuwawekea dhamana wanafunzi Katika mabenki ili mabenki Iweze kuwapa mikopo wanafunzi Hao waweze kusoma Kisha wakarejesha mikopo hiyo?

Tunajitapa kila kukicha Tunataka taifa hili liwe la wasomi wakati sera ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ni ya Kibaguzi?

Kwa hiyo mtoto akose Haki yake ya Kikatiba ya kunufaika na Rasilimali za taifa hili kwa Kigezo eti Mzazi wake anauwezo wa kumsomesha mara eti kozi aliyoichagua siyo miongoni mwa kozi zenye vipaumbele .  Wazimu wa aina yake ndiyo huu.

Enzi taifa hili halina Fedha wala Miradi mingi ya maendeleo ,serikali ilikuwa ikiwa peleka wanafunzi kusoma vyuo vikuu Leo hii taifa hili limepiga Hatua za kimaendeleo Tunaambiwa makusanyo ya kodi yameongezeka yanaibuka Masharti kibao Kandamizi ya kunyima wanafunzi mikopo .


Pendekezo jingine ,naomba utambue kwamba kila jambo /uamuzi unaofanya kwa maslahi ya taifa hili kama unavyoeleza fahamu fika lina faida na Hasara zake. Uamuzi wa Kufuta safari za nje ,posho za vikao na posho muda wa ziada wakazi una faida na Hasara pia Hilo ulijue.

Katika mazungumzo yangu ya baadhi ya watumishi wa umma Wengi tu toka Ofisa mbalimbali wanasema uamuzi wako wa Kufuta posho ya muda wa ziada wa Kazi umewaondolea molari ya kufanya Kazi kabisa na tangu ulipotangaza Kufuta hizo posho za Muda wa ziada wa Kazi ,Wawapo Kazini akili zao na Nguvu nyingi wanazielekeza Katika shughuli zao Binafasi za kuwaingizia kipato kwasababu kwanza mshahara wa watumishi wa umma ni Mdogo na tangu uwe Rais wa nchini, hujawaongezea mshahara unategemea wao wanaishi vipi ?

Nani kweli nimekuwa nikifika Katika Ofisi za umma mbalimbali hivi sasa ikifika saa 9:30 Alasiri kila mfanyakazi anafunga virago vyake anaondoka hata kama Kazi alipopewa na boss wake Hajazimaliza ,wanaziacha kiporo na wengine wa nadiriki Kusema kwa Kauli hizi za vitisho zinazotolewa na baadhi ya watawala Kuwa asiyetaka Kazi na aache pia zimewafanya baadhi ya watumishi Kuwa na hofu ya kufukuzwa Kazi jambo ambalo siyoni kama lina Tina kwa taifa kwasababu Kimsingi tukubaliane Utendaji wa Kazi n wa kushirikiana .


Ni kweli una nia ya kutaka kuleta maendeleo Katika taifa hili ni vizuri ila naona kama speed yako ni Kali sana hivyo nilikuwa nakushauri ukumbuke ule Msemo usemao 'kawia ufike' , nenda Taratibu na Timu yako Katika baadhi ya maamuzi  Utendaji tutafika salama Kwani harakahara haina baraka.Tanzania haiwezi Kuwa kama Japan Leo hii.

Kwani ukumbuke hata Rais Kikwete alikiri hadharani Kuwa amestaafu urais ameweza Kutenda mambo ya kimaendeleo kwa kadri ya uwezo yake na yale ambayo alishindwa kutekeleza anatuachia mrithi wake ayatekeleze

Pendekezo jingine nakushauri Tazama upya uamuzi wako wa kuondoa Fedha Katika mabenki ya Kibiashara na Kisha Fedha hizo ukaamuru ziamishiwe Benki Kuu .

Misiyo mchumi ila nimeshuhudia baadhi ya watu wakikosoa uamuzi wako huo kwa Madai Kuwa unaathiri uchumi kwasababu Benki Kuu haifanyi Biashara.

Lazima ulipata  ushauri huo na wachumi lakini wachumi nao ni binadamu wanaweza kukosea hivyo Huna budi tena kukaa na wachumi wengine  idi mradi ujiridhishe wachumi Hao ni wazalendo kweli ,pia kaa na wakuu wa mabenki ambayo yalikuwa yakikaa na hizo Fedha ukaziamishia Benki Kuu wakupe maoni Yao kwamba Je tangu hilo agizo Lako litekelezwe Benki hizo na wananchi wamenufaika vipi na wameadhirika kwa kiasi gani?Je ushauri wao ni upi kwako Je agizo Lako Hilo liendelee Kubaki  kama lilivyo au ul itengue?

Na kama fikra zako zilikutuma Kuwa kuamisha Fedha toka Kwenye mabenki ya kawaida ukaziamishia Fedha hizo Benki Kuu  kwa Kigezo Kuwa Fedha za umma zikikaa Benki Kuu zitakuwa salama zaidi, kwa asilimia Fulani  utakuwa unakosea sana kwasababu hata Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA)  zilikuwa zikitunzwa kwa muda mrefu Katika Benki ya Taifa ya Baishara ( NBC) lakini baadaye serikali ya Rais Benjamin Mkapa iliamuru Akaunti hiyo uamishiwe Benki Kuu na Fedha hizo zitunzwe ili mwisho wa siku wanaodai Fedha hizo wakija kuzidai serikali iwalipe.

Mwisho wa siku watu wenye akili zao ' wasiyotaka  Ujinga', waliingia ndani ya Benki Kuu wanashirikiana na Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu wakazichota kwa nafasi mabilioni ya shillingi ya Fedha za EPA tena wengine walitumia Nyaraka Fedha na walinufaika nazo vizuri sana mwisho wa siku baadhi Yao walishitakiwa Katika Mahakama ya Kisutu akiwemo Kada wa CCM, Rajabu Maranda ambaye alishitakiwa kwa jumla ya kesi tano za wizi wa fedha za EPA alifungwa Katika baadhi ya Kesi Akakaa gerezani kwa muda mfupi ,Rais Kikwete alimpatia msamaha  Katika baadhi ya Kesi hivi ,Kesi nyingine alishinda hivi sasa yupo uraiani anaendelea na Maisha .

Sasa kama Kigezo Chako cha kuamisha Fedha Katika mabenki yetu ukaziamishia Benki Kuu kwaajili ya eti Benki Kuu kuna Ulinzi zaidi nau kukwepa liba kubwa katika hayo mabeni ya kati kwa asilimia Kadhaa unajipotosha Kwani nchi hii kuna watu washenzi sana na hawawezekani na hutakaa uwaweze maana walishashindikanaga muda mrefu kwa wazazi wao ,Jela hawaliogopi,Polisi ndiyo nyumbani Kwao na wala hawana hofu na Mungu.


Aidha nakushauri Kuwa makini sana na baadhi ya watu wanaokusifu hadharani kwa kila jambo unalotenda baadhi Yao ni wanafki tena wazandiki wakubwa maana baadhi Yao wana kusifia hadharani wakikaa na sisi pembeni wanakukandia hatari.

Nakushauri usiwachukie wala kuwawekea visasi wale wote wanaokosoa baadhi ya matamshi na matendo yako kwa nia ya Kujenga .Tazama vigezo walivyotumia kukukosoa ,mapendekezo Yao kama yanalengo ya Kujenga yachukue yafanyie Kazi Kwani tukubaliane Kimsingi wewe ni Rais wa nchi ni binadamu kama sisi ,kuna wakati unakosea ,unafanya vizuri lazima wananchi wako tukueleze na uwe Tayari kujifunza,kubadilika.

Kuanzia sasa nakushauri uache kuendelea kutamka hadharani Kuwa 'utaunda Mahakama ya Mafisadi' licha nafahamu Mahakama hiyo ambayo wewe ndiyo umepachika  jina Hilo kwasababu kitendo cha Kuita majukwaani  Mahakama hiyo ya  mafisadi ni Tayari kwamba wale washitakiwa wote watakao Kuwa wanaoshitakiwa Katika Mahakama hiyo Tayari watakuwa wameishahukumiwa Katika macho ya Jamii Kuwa ni Mafisadi Kabla ya Mahakama hiyo haijatoa hukumu yake  .

Ikumbukwe kuwa  Ibara ya 107A (I) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, inasema hivi " Mamlaka yenye Kauli ya mwisho ya Utoaji Haki Katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama'.

Leo hii kupitia Kauli zako mbalimbali Katika kampeni za kuomba uchaguzi we Kuwa Rais ,na ulivyokuwa Rais umetaka Mahakama hiyo ianzishwe na kweli imeanzishwa  mwisho Mahakama hiyo sasa watu tunaofikiri Sawa sawa tunajiuliza Rais wa nchi Magufuli na baadhi ya watu Mahakama hiyo wamejipachika  jina Hilo huku mitaani,majukwaani Kuwa Mahakama hiyo ni Mahakama ya mafisadi lakini Je ikija kutokea washitakiwa Hao mliokwisha hukumu Kuwa ni mafisadi wakija kushinda Kesi zao Katika Mahakama hizo Je sura Zenu mtaziweka wapi?

Maana Sheria ni kitu kingine kabisa na porojo za wanasiasa ni  Kitu kingine .S iyo  mwisho wa siku upande wa Jamhuri ushindwe  kupeleka ushahidi thabiti mahakamani kuhusu Kesi hizo zitakazofunguliwa Katika Mahakama hiyo mnayoiita huku mitaani 'Mahakama ya Mafisadi ',washitakiwa wakishinda  hizo Kesi Nyie wanasiasa msije kuanza kupaka matope Mahakama hiyo Kuwa Imepokea Rushwa na inahujumu serikali ya awamu ya tano maana hiyo tabia mnayo sana  wanasiasa wapenda sifa za kijinga.

Pendekezo jingine naomba Timu yako msikilize nakuofanyia Kazi haya Madai ya baadhi ya wananchi ,wabunge na wafanyabiashara kwamba zile kodi za ushuru wa mizigo ni nyingi za viwango vyake ni Vya juu ukilinganisha na viwango Vya kodi Vya Mataifa mengine Hali inayosababisha baadhi ya wafanyabiashara wa Mataifa mengine wasipitishe mizigo Yao Katika Bandari yetu.

Binafsi siyo mtaalamu Katika eneo hili ila napenda kufanya majadiliano na watu wa Kada mbalimbali na kufuatilia mijadala mbalimbali kadri siku zinavyozidi kwenda watu wamekuwa walilalamikia na Kamati Moja ya Bunge ilishatoa mapendekezo yake ziondolewe zitaletea Shida taifa,hivyo Nashauri wataalamu wa eneo hili wafanye utafiti wa kubaini Madai hayo ya wanaolalamika kodi hizo yangu kweli wowote au laa.

Kumekuwa na malalamiko ya mzunguko hafifi wa Fedha ,Nashauri serikali iongeze juhudi za kulipa  Madeni ya ndani ili hela iingie Kwenye mzunguko .

Minakwambia usipo badilika na kuanza Kuwa na moyo wa uvumilivu wa kuvumilia kuona au kusikia yale usiyoyataka kusikia siku ukistaafu akiingia madarakani Rais mwingine na Rais Huyo Akaamua Kuja na Taratibu zake mpya na kuanza Kubomoa Misingi uliyoyaacha unaweza kujikuta unazirai kitandani kwasababu ni lazima utakasirika kupita kiasi Kwani ukitumia Nguvu nyingi kuirekebisha nchi na Utaiweka Kwenye mstari huku ukiamini mrithi wako atakayekuja atayaendelea uliyoyaacha halafu asiyaendeleze .

Omba Mungu akupe uvumilivu na kunyamaza na ndiyo maana tunaambiwa Mwanaume ameumbewa na Koromeo hili awe kuhifadhi baadhi ya mambo maana nchi hii ni kubwa unaongoza watu wa kila aina wengine ni machizi huwezi kufanikiwa wote waende au waishi unavyotamani wewe waishi .Mimi nakuombea Hilo.

Ukae ukijua huku mitaani pia umepachikwa jina la ' Rais Mlopokaji au Rais Lopolopo' . Yaani manaake hata sisi mashabiki wako hiyo tabia yako ya kuropoka mambo ambayo kistaarabu hayapaswi Kusemwa na mtu kama wewe mwenye hadhi ya urais wa nchi, na inatutukanisha sana,tu najikaza kwamba eti tulimpigia debe Rais ' Mlopokaji' ,Saa Mbovu yaani Kichaa.


Ni Mungu peke yake asiyebadilika  ila binadamu tunajadilika.Rais Magufuli badilika  la Katika baadhi ya madhaifu niliyoyainisha hapo juu yanayokuhusu wewe binafsi  utafanikiwa zaidi na sitaacha kuinga mkono serikali unayoiongoza inanitokana na CCM  .

Ila sikufichi tabia yako ya kutamka  baadhi ya maneno yasiyopaswa  kuyatamka na mtu  kama wewe mwenye hadhi ya Rais kwa Kigezo Chako kile unachokitumiaga use macho ' eti huo ndiyo ukweli,tuwe wa kweli' siipendi tena siipendi kabisa.

Rais wa nchi ana hadhi yake tena kubwa tu na lazima ajitofautishe na watendaji wake wa chini  na wananchi wengine wakawaida kabisa.

Rais Magufuli Hupaswi kuzungumzia masuala ya vitafunwa Katika sherehe zinazofanyika  Ikulu  kwa Kigezo eti unabana matumizi,watu wale Korosho warudi makwao.Hiyo Idara ya vitafunwa,vinywaji siyo yako inawenyewe wache wenye Idara hiyo waizungumzie.

Leo unatimiza Mwaka mmoja tangu    ulipoapishwa 5/11/2015 Kuwa Rais wa awamu ya tano.

Ninaamini haya madhaifu niliyowataja na mengine ambayo sijayataja Katika makala hii ondokana nayo Kwani Tunaweza Kusema labda ulionyesha Udhahifu huo kwasababu ulikuwa ni mgeni na Ikulu na mgeni wa Cheo cha Urais.Badilika utakuwa bora zaidi Kwani nitafurahi zaidi kama utaandokana hiyo tabia ya kuongea maneno ambayo wewe kama Rais Hupaswi kuyatamka hadharani .

Kwani utambue nchi hii unaongoza watu wasomi wa taaluma tofauti,wenye uzoefu na wajuzi wa mambo mbalimbali kuliko wewe kila unachokifanya au kukiongea hadharani wanakipima na kunijadili Katika maeneo Yao na wengine wamekuwa wakiku sanifu sana wewe hujui .Badilika.

Kuanzia Leo tuna hesabu ule ushamba ,ugeni wa urais, Ikulu umekutoka hivyo umekua sasa hivyo basi baadhi ya mambo achana nayo na ukubali kujishusha ili watu 'wakushape 'uwe Rais bora zaidi Kwani pia huku mtaani jina jingine umepachikwa unaitwa ' ONE MEN SHOW' .

Yaani eti wewe Rais Magufuli ' ONE MEN SHOW ' unajifanya unajua kila kitu  wakati Hakuna binadamu anayefahamu kila kitu.

Misina Hakika na Hilo Kuwa wewe ni ONE MEN SHOW  kwasababu sipo karibu na wewe ila jichunguze kama ni kweli acha hiyo tabia Kwani itakukosesha mengi kutoka kwa watu ambao wanafahamu baadhi ya mambo wanataka wakueleze au kukufundisha ili uwe kuyatumia Katika Utawala wako ufike Mbali  hawataki. Kumbuka bado una safari ndefu .

Mwisho wa siku Ibara ya 37.-(1) ya Katiba ya nchi  inasema hivi ; " Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote".

Hivyo hulazimishwi na Sheria yoyote kufuata ushauri wangu niliyotoa Katika makala hii ila nimeitimiza wajibu wangu kama mwanachi wa nchi wa kutoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977  na pia nimeitimiza wajibu wangu kama Mkristo kama tulivyotakiwa na Mungu Katika  Kitabu cha
EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Mungu ibariki Tanzania

0716 774494
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com

5/11/2016.


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment