Monday 21 November 2016

Re: [wanabidii] MAKONDA TULIA UNYWE DAWA

Ndio yale tunayosema wengine:
Serikali inapotoa vibali vya biashara haramu kama bar kuwa na shisha; vifaa vinapitia wapi ambako havikaguliwi kabla ya kuingizwa nchini?

Haya na haya ya Kubeti. Kila kona siku hizi kuna majumba/halls za kubeti. Sasa hii betting/gambling kila kona haikuona kuwa ni mchezo mchafu? Vinana na watu wazima wapo hapo kutwa wanakunywa na kucheza kamali hawafanyi kazi. Betting katika nchi ya Vibaka mtaani, vijana wasio ajira unategemea uchumi wa viwanda utafanikiwa?


Tunafanya makosa kwa vibali na leseni zisizo zingatia maadili tunajali pesa tu. Bar kila kona kila baada ya nyumba tatu Bar ya pombe, video, music za makelele majumbani mitaani; pembeni mwa nyumba ya kuishi watu mtaani mtu kaweka karakana ya nondo kusagwa, kuchunwa na ya mbao inayopakwa dawa zinazoingia majumbani na kusababisha afya mbaya watu wanavuta hewa za kemikali na kubwia vumbi la mbao na chumba. Bado hiyo daladala na bajaji, bodaboda zinapita mtaana na loud music! Usalama gani ndani ya bus la mtaani loud music? Dreva atasikia lini warning toka gari nyingine?Hata upigiwe simu ukipokea hamsikilizani. Watoto wadogo, watoto matumboni exposed to noise nyumbani, ndani bus, mtaani. Wanapata buses hizo wanaona wahusika; mtaani police wanaona na kusikia makelele hayo ya magari na bodaboda inapita inapiga kona za mapambo!

Itakuwa hiyo ya Shisha-Cha mtoto hicho! Wanapanda bangi vijijini mashamba makubwa police kupoteza muda kwenda kuyafyeka. Maiti zinasafirishwa na unga tumboni na bangi ndani ya gunia juu vitunguu! Kutaka hela na utajiri rahisirahisi na kila kiingiacho mijini na vijijini ni halali!?

Tusiporekebisha sasa kisheria na kimatendo ya kweli-tutajenga taifa la baadae la vijana zombie, vilema wengi wa umri mdogo na mkubwa watakaohitaji kutunzwa. Mmiliki wa Shisha ni mzazi anaona yanayoendelea hajali utu bali pesa tu.

Ndio hao si Shisha tu bali magulio ya kuuza watoto wa kike na wakiume.
Inakokwenda Bongoland ni kubaya-wazazi kuwajibika kidogo, utaifa umezamishwa topeni ndani ya kubeti issues zinazoonekana wazi ni kinyume na sheria na maadili.

Nilikuwa ninapita tu!!

On Mon, 21/11/16, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] MAKONDA TULIA UNYWE DAWA
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 21 November, 2016, 11:15

MAKONDA TULIA UNYWE DAWA

Na Happiness Katabazi

WIKI Iliyopita Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda
Mara Kadhaa amenukuliwa Katika vyombo Vya Habari akisema
yeye ameiita hidi kadri ya uwezo wake Kupambana na matumizi
ya dawa za kulevya ikiwemo Shisha lakini Jeshi la Polisi
limekuwa likisita kuwachukulia Hatua.

Makonda alitoa tuhuma hizo Mbele ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Katika Uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa
upatikanaji wa Umeme Katika Mkoa wa Dar Es Salaam dhidi ya
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon Sirro
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda .

Kuwa Mara kwa Mara amekuwa akimuuliza Sirro Kuwa Mbona
wananchi wanampatia taarifa wauzaji wa Shisha bado wanatamba
na Sirro Amekuwa akimjibu Kuwa Hali  ni shwari .

Makonda aliwashushia tuhuma Makamanda hao Wawili
Wamelambishwa ile hongo aliyoikata kutoka kwa
wafanyabiashara wale wa Shisha ndiyo maana wanasita
kuwachukulia Hatua wauzaji wa Shisha.Shisha imepigwa
marufuku kutumiwa hapa nchini.

Mkuu Huyo wa Mkoa Alidai kuna wafanyabiashara 10 bila ya
kuwataja majina walimfuata  wakitaka Kumhonga
Sh.Milioni 50 kila mwezi ,lakini alikataa.


Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa
alimtaka   Makonda aache Kulalamika badala
yake akatekeleze maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu wa
serikali.

Kauli hiyo Makonda dhidi ya makamanda hao wa polisi
imeibua  mjadala  katika jamii huku wengine
wakitofautiana na yeye vikali.

Kwa upande wa Jeshi la polisi Makao Makuu Kamanda Robert
Boaz mwishoni mwa wiki alizungumza na umma na akasema
taarifa hizo za tuhuma za Rushwa  dhidi ya makamanda wa
jeshi Lao  wamesikia na jeshi hilo limefikia uamuzi wa
kuanza kufanyia uchunguzi tuhuma hizo ( Inquiry).

Kwanza Napongeza Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kwa uamuzi
huo wa uweledi wa kuchukua Hatua za kufanya uchunguzi wa
tuhuma hizo zilizotolewa barabarani yaani Kwenye vyombo Vya
Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda.

Aidha pia Kifungu  cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa
Makosa ya Jinai 2002 , kinatoa mamlaka kwa Ofisa wa
Polisi  kuhoji mashahidi,watuhumiwa au mtu yoyote
ambaye Polisi inaitaji  kupata maelezo yake kutokana na
tuhuma au uchunguzi wa jambo lolote .

Hivyo Jeshi la Polisi wapo sahihi kufanyia uchunguzi taarifa
hizo zilizotolewa na Makonda wiki iliyopita.

Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya  Mwenendo wa Makosa ya
Jinai ya Mwaka 2002 ,kina Mtaka mtu yoyote ambaye anafahamu
taarifa za kutendeka au kutaka kutendeka kwa tukio ka
Uhalifu apeleke taarifa hizo Katika mamlaka husika za
kiserikali ili zifanyiwe Kazi na  akishindwa kufanya
hivyo atashitakiwa kwa kosa lolote chini ya Sheria ya Kanuni
ya Adhabu sura ya 16  ya Mwaka 2002.

Tumuulize Makonda yeye Kabla ya ile Sherehe ya Uzinduzi wa
Mradi wa umeme  aliyotoa tuhuma hizo nzito dhidi ya
Makamanda Hao wa Polisi  alishazipeleke taarifa hizo za
watu wale walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha
Katika mamlaka gani za kidola?

Makonda ana anakofia Ya Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam na
kofia ya Pili ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambaye Mkuu wa Mkoa
husika ndiyo Mwenyekiti , baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo
ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ), Jeshi la Polisi,
Usalama wa Taifa ( TISS) ,TAKUKURU ,Uhamiaji ,Magereza na
vyombo vingine.

Namuuliza Makonda alivyokuwa akiendesha vikao vya Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa na kofia ya
Mwenyekiti wa Kamati hiyo alishawahi kuwasilisha taarifa
zake hizo za  wafanyabiashara 10 aliyodai eti walifika
ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha  kila mwezi ili
aachane na mapambano ya Shisha?

Makonda uliwai Kuwasilisha  taarifa Katika Kamati ya
Ulinzi na Usalama kuwa  Kamanda  Sirro
anasita   kuchukua Hatua dhidi ya 
wafanyabiashara hao na uenda ile hongo iliyokataa kutoka kwa
wafanyabiashara wale wa Shisha   uenda
imewapitia?

Makonda uliwahi kuwasilisha mezani  taarifa Katika
Kamati hiyo unayoiongoza  Kuwa Jeshi la Polisi kupitia
RPC- Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu Biashara
ya Shisha?

Maana kupitia mahojiano yako na Redio Clouds umesikika
ukisema Mara kadhaa umekuwa ukipewa taarifa na Jeshi la
Polisi kupitia Kamanda Sirro Kuwa Shisha Hakuna Dar Es
Salaam na kwamba Jeshi la Polisi lomefanikiwa 
Kudhibiti Shisha  wakati wewe Makonda umekuwa ukipewa
taarifa na wananchi wanaoichukia  Shisha Kuwa Shisha
ipo ,na ukaenda kukamata na vielelezo unavyo .

Kama uliiwasilisha  Taarifa hizo katika Kamati ya
Ulinzi na Usalama Tueleze. Taarifa hizo zilijadiliwa ?

Na wajumbe wa Kamati hiyo walijibu nini ulivyosasilisha
taarifa hizo walikujibu nini ?Je wajumbe  wa 
Kamati Walisema hawatafanyia Kazi ?Au Walisema watafanyia
kazi?Walikupa tarehe ya mwisho ya kujifanyia Kazi
'deadline'?

Nafahamu Hilo Swali kwa mwana Usalama aliyefundwa akafundika
hawezi lijibu hadharani ila kwakuwa wewe Makonda ni
Mlopokaji na hufahamu majukumu ya kofia zako zote mbili
unaweza ni jibu hilo swali.

Au Makonda ndiyo ameamua  kuleta Habari
zako   za Kimbea ,majungu ,kujipendekeza
Mbele Waziri Mkuu Majaliwa ?Ili uonekane
wewe   ni mfanyakazi bora kuliko  Jeshi
Polisi kupitia makamanda wao Sirro na Kanda ? Upuuzi mtupu.

Je tukisema wale wahongaji hawakurudi tena kukuletea 
ile Rushwa   ndiyo maana umeamua Kusema
taarifa hizo hadharani? Mbona walivyokufuata ofisini kwako
hukujitokeza hadharani kutuambia kuna wafanyabiashara 10 wa
Shisha wamekufuata ofisini kutaka wakuhonge kiasi hicho cha
Fedha na ukakataa?

Kama uliamua kunyamaza kimya wakati walipokufuata kutaka
kukuhonga Fedha kama unavyodai ,Tukuulize ni kitu sasa
kimesukuma utoboe Siri hiyo hadharani hivi sasa?

Hivi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hasa ya Mkoa wa Dar Es Salaam,
Ina uwezekano mkubwa ikawa imefungwa CCTV kamera.

Hivyo ni vyema Makonda atoe  ushirikiano
atakapotakiwa  kufanya hivyo aseme  Hao
wafanyabiashara wa Shisha walikuja Lini ofisini kwake , ili
watu wanaohusika  na CCTV Kamera waweze kuwabaini kwa
sura ikibidi na mazungumzo Yao  ili ithibitike ni kweli
walifika ofisini wake?walitaka Kumhonga kiasi hicho cha
Fedha ?Na Hao watu 10 wasakwe wako jiwe waseme ni kweli
walitaka Kumhonga Makonda kama Makonda alivyodai Mbele ya
Umma?

Aiingi akilini Mkuu wa Mkoa mzima anasema 
wafanyabiashara Hao haramu eti walifika ofisini kwake ,
anawafahamu  kabisa ni wafanyabiashara haramu ,.

Akakaa na kufanya nao mazungumzo ofisini
kwake   hadi wakamtajia  na kiasi cha
fedha watawachmpa  halafu yeye  Mkuu wa Mkoa
ambaye lazima Atakuwa  na walinzi ashindwe 
Kuwaeleza walinzi Hao wawakamate wafanyabiashara Hao ambao
yeye  amejinasibu  Kuwa anawajua  ni
wanafanya Biashara hiyo haramu ya Shisha.

Na katika mtazamo wa yeye  kama Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Hilo suala la
yeye  kutaka kuhongwa kiasi hicho cha Fedha na
wafanyabiashara hao haramu 10  Narudia tena kumuuliza
aliwasilisha   mezani taarifa hiyo ?

Inaoenekana Makonda alikuwa  nania ovu ya kutaka
kuzipokea maana  kama alikuwa  hatamani 
kuzipokea hizo Fedha kwanini hukuwasilisha taarifa
hizo  za yeye  kutaka kuhongwa Kwenye Kamati ya
Ulinzi Usalama ya Mkoa ambayo yeye ndiyo Mwenyekiti?

Kwanini umesubiri Waziri Mkuu aje Kwenye sherehe za Uzinduzi
wa Maboresho  Upatikanaji wa Umeme Dar Es Salaam ,ndiyo
useme Hilo?

Makonda kijana mwenzangu umeacha  Mashaka mengi sana
Katika hili kwa sisi wananchi wako wa Mkoa wa Dar Es Salaam
unaotuongoza .

Umeonyesha  hujui wajibu wako  kwasababu wewe
Ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na
wewe ndiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo .Hufahamu sehemu ya
kutoa taarifa au kushitaki ?

Unasubiri shughuli za uzinduzi wa mradi maboresho ya umme
ndiyo ushitaki hadharani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa? Ni
dhahiri hutufai maana tayari umeishapata doa.

Nina mashaka na uwezo wake wa kiutendaji na uwezo wake wa
kuchanganua mambo.Makonda umetuacha na maswali kama anajua
majukumu yake ya Ya kofia ya Mkuu wa Mkoa na kofia ya
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Nashawishika kusema kuwa Makonda kama RC ,Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa ,akiwa pia ndiyo
anayesimamia utendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam hafahamu
majukumu yake  tena hata kwa wale watendaji wake wa
Moja kwa Moja yaani wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Na Pia Makonda kupitia matamko yake mbalimbali kuhusu sakata
hilo ameonyesha hafahamu Maadili ya Kazi yake Kwani kama
Angekuwa anajua Maadili ya kiongozi mwenye hadhi ya
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
asingethubutu kupayuka Yale aliyoyatamka hadharani dhidi ya
Kamanda Sirro na Kaganda pia asingethubutu kwenda Redio
Clouds kwenda kuzungumzia ule upuuzi aliouongea kupitia
Redio hiyo.

Nasema ni upuuzi kwasababu Makonda kama Kweli an ajitambua
yeye ni nani,ana madarakani siku ile ile aliposikia Waziri
Mkuu Majaliwa alivyomshushua mbele za watu kwa kumtaka
Makonda aache kulalamika afanyekazi na atekeleze maagizo
toka viongozi wa juu, alivyosikia Kamanda Sirro
alipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa operesheni
ya kukamata waharifu wa makosa ya aina mbalimbali ikiwemo
wauza dawa mbalimbali za kulevya imekuwa ikifanyika na
inaendelea kufanyika na kwamba majarada ya uchunguzi wa
watuhumiwa hao polisi wameyapeleka ofisi ya Mwanasheria Mkuu
kwaajiili ya hatua zaidi za kisheria na tayari na maana
polisi hawana mamlaka ya kufungulia washitakiwa kesi za
jinai mahakamani mwenye jukumu hilo ni Mkurugenzi wa
Mashitaka ( DPP) .

Na ni kweli kifungu cha 9 cha Sheria ya Taifa ya Huduma ya
Uendeshaji wa mashauri ya Jinai Na. 27 ya Mwaka 2008 ,
inasema DPP ndiyo mwenye Mahakama ya Kufungua na kuendesha
Kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya serikali.

Na aliposikia Jeshi la Polisi Makao Makuu Kupitia Kamanda
Boaz Kuwa
Jeshi la Polisi  limeanza kufanyia uchunguzi wa shutuma
za Makonda dhidi ya Makamanda wake Sirro na Kaganda, RC
-Makonda angefunga  mdomo wake kwa kunyamaza
kimya  kimya lakini sijui ni Utoto ,ulimbukeni
akaendelea kuongea tu Mara kuhojiwa Redio Clouds Mara
kunukuliwa na Gazeti moja akitamba Kuwa ataendelea
kuwachongea. Aibu gani hii jamani!

Ni wakati mwafaka wa Makonda arudishwe darsani ili akapewe
mafunzo yatakayomwezeka kufahamu majukumu yake ya Uenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na majukumu ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam.

Waswahili wanasema Dalili za Mvua ni Mawingu. Hivyo kama Leo
hii Mwenyekiti Huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama RC
Makonda ameshindwa kutumia majukwaa sahihi ( Proper Forum)
yakupeleka malalamiko yake badala yake anatumia vyombo Vya
Habari na kusubiri kudandia mkutano wa Waziri Mkuu kulalama
tena mambo mengi ambayo ambayo yanapandikiza Chuki baina ya
wananchi na Jeshi la Polisi Kuwa Jeshi la Polisi ndiyo
linalowalea wauza Shisha kwasababu ha liwachukulii Hatua
basi ipo siku Makonda Atakuja kuropoka mambo Siri ya vikao
Vya Kamati ya Ulinzi Usalama kupitia Vyombo Vya Bahari kwa
Lengo la kutaka kujionyesha yeye ni mchapakazi kuliko
watumishi wengine wowote .

Na ushahidi ni Yale mahojiano aliyoyafanya  a Redio
Clouds ambayo Clip yake ninayo ambayo Makonda kwa kinywa
Chake anamtuhumu Sirro ambaye ni mjumbe wake wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama Kuwa amekuwa alimpa taarifa za uongo
kuhusu Biashara ya haramu ya Shisha.

Sasa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo analalamikia mjumbe wake
wa Kamati hiyo hadharani tena Kwa zaidi ya Mara Moja , ni
wazi RC Makonda Hana Imani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum
ya Dar Es Salaam ambalo ndilo Hilo Hilo Askari wake
wanamlinda nyumbani anakoishi na ofisini.

Lakini hata kama ni kweli Kamanda Sirro alikuwa akikupa
taarifa za uongo kuhusu Shisha ,Sirro na wewe Makonda wote
ni wateule wa Rais John Magufuli .Je Makonda ulishawahi pia
kwenda kumweleza Rais Magufuli,au boss wa Sirro ambaye ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi Kuwa Sirro amekuwa akikupa taarifa
za uongo na auridhishwi na Utendaji wake?

Makonda umedai Jeshi la Polisi limekuwa likisita kuchukulia
Hatua wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya, hivyo Jeshi
la Polisi Leo Hii likiibuka na takwimu za Kuonyesha Jeshi
Hilo limekuwa likichukua Hatua Kabla hata ya wewe kufikiri
wa au wewe kufikiria utakuja Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es
Salaam sura yako Utaiweka wapi?

Maana Mimi ni shahidi mahakamani nimekuwa nikishuhudia
Mkurugenzi wa Mashitaka aliwashitaki watuhumiwa mbalimbali
wa makosa ya dawa kulevya ambao Chanzo cha washitakiwa Hao
kushitakiwa ni walidaiwa Kutenda makosa hayo na walikamatwa
na Jeshi la Polisi.

Elewa Uhalifu ulikuwepo toka enzi na Enzi na serikali ya
awamu ya tano imeukuta na itauacha na haiwezi kuukomoesha
maana kila kukicha wahalifu wanabuni mbinu mpya za kufanya
Uhalifu.

Hivyo hata wewe Makonda Biashara ya dawa kulevya umeikuta
hapa Dar Es Salaam na Duniani kwa ujumla.Usijidanganye Huna
Nguvu wala mamlaka ya Kupambana nayo kwasababu Huna Mafunzo
ya kutambua hizi dawa za kulevya, kukamata wenye hiyo
taaluma wapo ndani ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha
Kuthibiti Dawa za Kulevya Chenye Ofisi zake Barabara ya
Kilwa Dar es Salaam.

Umejitapa kupitia Redio Clouds  Kuwa umekamata dawa za
kulevya aina ya Shisha . Mina Kuuliza una Hakika gani hizo
ni dawa za kulevya?

Hivi hizo unazodai ni Shisha ulizokimata zikichukuliwa
zikapelekwa kwa wataalamu wakazikagua kitaalamu Kisha wakaja
kutoa ripoti Kuwa hizo siyo Dawa za kulevya utasema
nini?Acha wenye taaluma za Kupambana na dawa za kulevya
wafanyakazi Yao.Wewe taaluma hiyo Huna.

Mkuu wa Mkoa Mzima unaacha kushughulika na mambo makubwa
makubwa unaamua kujigeuza 'korokoroni 'unaenda kukamata
Shisha na vifaa Vya Kuvutia Shisha wakati Polisi wenye vyeo
Vya chini wa kufanyakazi ya ukamataji wapo na wala
hawakueleza  wameshindwa kukamata hivyo wa naomba
utasaidie.

Hivi Hao wahalifu wa Shisha unawaowafuta Fuata hadi Kwenye
vijiwe vyao Vya Kuvuta Shisha na bangi wakikumwagia Kinyesi
usoni utalia na nani?

Fanyakazi yako uliyotumwa na vyombo Vya Ulinzi na Usalama
ambayo ndiyo wenye taaluma ya Ulinzi na Usalama wafanyakazi
Yao kwa Uhuru .Heshimu wakubwa wako ,Chagua matamshi ya
kuzungumza Mbele ya hadhara dhidi ya viongozi wenzako.

We bado ni kijana Mdogo sana bado unaitaji kulelewa na
wanasiasa wenzako,wanausalama hivyo haina maana wewe
kujiingiza Katika msuguano na Jeshi la Polisi kupitia
Kamanda Sirro na Kaganda. Kushangaa siku Moja kitendo hicho
kikaja kukugharimu.

Aidha Makonda kaa chini ujitathimini na utafakari
hicho  ulichokifanya ambacho kutokana na matamshi yako
ambacho kimezusha mjadala  na kufanya watu Tutulie
Mashaka uwezo wa Utendaji wako .

Kisha wewe binafsi ujiulize Je ulikuwa sahihi wakati
ukifanya hayo uliyoyafanya  kwa mujibu wa maadili ya
kofia zako mbili za kimadaraka. Kisha ujipime wewe mwenyewe
mwisho uchukue maamuzi. 

Nimalize makala hii kwa kukushauri Makonda  Kuwa '
Usiwe na haraka kuliko Upesi'. Mji huu wa Dar Es Salaam Una
Masharti hadi ufanikiwe ,sio kuvaa Masharti /Suti ukajiona
wa maana . Acha tabia na kutaka kujipatia Umaarufu wa chee
kwa mambo yasiyo na tija .
Naomba kutoa hoja.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.com
0716 774494
21/11/2016


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment