Maskini Lesian. Unakaa na kutarajia Trump aaishwe kama rais wa Marekani aje kukusaidia Tanzania?????
--------------------------------------------
On Sat, 11/19/16, 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya isubiri nchi inyooshwe
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, November 19, 2016, 12:33 PM
Triump atawakomesha hata
hawa wanalazimisha matokeo kua wameshinda ili waendelee
kutoa mi amri tu kumbe alieshinda mwingineee,nyie subirin
'Reuben Mwandumbya'
via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Lessian;Shambulia
hoja sio kushambulia mimi.
Never
believe that Trump is for others than American
interests.Jiandae
kupokea wadogo zako wanaodeki vyoo kule America then wakija
Bongo wanasema ni Mameneja huko ughaibuni.Trump
akishika moto na wengine watamfuata,hapo ndipo moto utawaka
Jomba. Reuben
On Saturday, November
19, 2016 11:39 AM, 'Lesian' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Katiba iliopo ni'mbovu
reuben.....inawapa watu mamlaka ya ajabu anateua hadi
wajumbe wa nyumbakumi...hawa ma dcs wa n sasa kama si
upotevu wa pesa......
Katiba iliopo ni nzr
kwa watu kama kina reuben tu wqnaofagilia kila jambo ilmradi
limesemwa na kusimamiwa na ccm
Hawanaga
mawazo mbadala na hawatak,'na maana yake hawataki kuona
mbele na trump kaja atawanyooshen subirin mnaokomaa
madarakan navyma vyenu kaja komesha..teh teh
'Reuben Mwandumbya'
via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mbegu;Sio
kwamba inji haina Katiba kabisa,itanyooshwa na katiba
iliyopo.Katiba
iliyopo sio kwamba ni mbaya kabisa kwamba sawa na haipo,
mabadiliko ya katiba yana sehemu chache za kuboresha na
kuongeza.Uhuni
uliokuwepo/uliopo umetokana na kutofuata Katina, shaeria na
kanuni zake i.e. lazier free Reuben
On Thursday, November
17, 2016 7:42 PM, Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
wrote:
Nchi itanyooshwa kwa sheria zipi? Kwa utaratibu upi?
Kwa utashi wa mtu binafsi? Ametumwa na nani?
Sent from Samsung
tablet.
-------- Original message --------
From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: 17/11/2016 10:36 (GMT+03:00)
To: ELISA MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Magufuli kasema yote: katiba mpya
isubiri nchi inyooshwe
Serikali
za Wanyama na ndege au Wadudu;
Ndani
zina taadhima, kama kwamba maabudu;
Na
watu wenye hekima, siku hizi hawamudu
Madaraka
na heshima, heri mnyama na mdudu
Vinywa
vimewaachama, tamu imekuwa ngwandu
Na
heshima imehama baki taka na mashudu
Na
madhara na dhuluma miungu ya kuabudu
(Shaaban
Robert; katika "Kielelezo cha Fasili")
SHAABAN Robert katika shairi nililonukuu hapo juu, anaelezea
madhara ya Uongozi na Viongozi wanapokosa maono, hekima na
heshima kwa wananchi akisema, inapokuwa hivyo heri Serikali
za Wanyama, Ndege au Wadudu zina taadhima kuliko za viongozi
wenye kukithiri
kwa dhuluma na kujigeuza miungu watu.
Japo gwiji hilo la ushairi Afrika Mashariki alikuwa
akiandikia zama zake zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo
fukuto la ufisadi, rushwa, kutoweka kwa uzalendo, uadilifu,
maadili ya uongozi na ubinyaji wa demokrasia ilivyo sasa
halikuwa jambo lililopevuka, lakini
utabiri wake wa kinabii kwa yajayo hayo wakati huo ulikuwa
sahihi na ndiyo yaliyoikaba koo nchi yetu hivi leo.
Ilivyo leo, na kama tunavyoambiwa na wataalamu wa siasa na
sayansi ya jamii kwa ujumla, suluhisho la maovu haya ya
kijamii ni kwa njia ya Katiba ya nchi itakiwayo na itokanayo
na wananchi wahanga wa maovu hayo, kwa njia ya maoni na kura
ya maoni.
Pengine ni kwa sababu hii miaka ya karibuni, na hasa
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwamba suala la Katiba mpya
lilikuwa ajenda moto, na zaidi kwa vyama vya upinzani
vilivyodai kuwa Katiba iliyopo imepitwa na wakati kwa sababu
iliandaliwa katika mazingira
tofauti na ya sasa miaka 40 iliyopita.
Tangu mwanzo, Serikali, kupitia Mwanasheria wake Mkuu (AG)
na mara nyingi pia kupitia waziri mwenye dhamana ya mambo ya
Katiba na vigogo wengine wa chama tawala, ilitamka wazi
kuwa, "Katiba mpya si ajenda ya serikali madarakani",
tamko lililochukuliwa na wengi
kama sawa na kujaribu kuzuia mafuriko kwa viganja vya
mkono.
Hatimaye mwaka 2012, serikali ilisalimu amri kwa
"mafuriko" hayo kwa kuteua Tume ya Kupendekeza "Rasimu
ya Katiba", chini ya uenyekiti makini wa Jaji Joseph Sinde
Warioba kwa matarajio kwamba Katiba hiyo mpya ingetumika kwa
mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba 2015.
Hadi kipindi hicho na mpaka sasa, nchi yetu ilikuwa na moja
ya Katiba bora Afrika Mashariki – Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo ukiondoa
mapungufu machache kadhaa yaliyomo, likiwamo lile la harufu
ya chama kimoja; madaraka makubwa
ya Rais (Mhimili wa Utawala) dhidi ya mihimili mingine –
Bunge na Mahakama na baadhi kuhusu Muungano, ilitosha na kwa
utoshelevu mkubwa katika ujenzi wa demokrasia na utawala
bora nchini.
Ni mwananchi gani mpenda demokrasia ya kweli bila kificho,
anaweza kubeza ubora usio na mshindani wa Katiba hii kwa
mambo muhimu inayotetea, kama vile, "malengo muhimu na
misingi ya shughuli za serikali madarakani" (ibara 6 –
11); na "Haki ya Usawa na Wajibu
wa Serikali kwa Raia" (ibara 12 – 30) ambayo Katiba za
nchi nyingi hazina?.
Ibara hizi za Katiba zina umahiri wa pekee kutokana na
ukweli kwamba zilitungwa na kupewa nguvu na msukumo enzi za
utawala ulioweka mbele mambo kama vile uwajibikaji na
maadili kwa viongozi; usawa wa binadamu na wa kijamii, utu
na dhana nzima ya uchumi/utajiri
wa nchi kuwa mikononi mwa wananchi kwa ajili ya na kwa
manufaa ya wananchi wenyewe.
Kwa kuzingatia haya, nchi haikuhitaji, na bado haihitaji
Katiba mpya kwa wakati huu, ila ipo haja isiyohojika ya
kuifanyia marekebisho ya hapa na pale Katiba iliyopo kwa
kuondoa ibara zinazopwaya au zinazokinzana (repugnant
provisions) na mnyumbuliko wa demokrasia
kwa mazingira ya sasa.
Serikali ya Awamu ya Nne ilitishika na kusalimu amri kwa
"mungurumo" wa mbali wa kudai Katiba mpya bila sababu
wakati ikijua ubora wa Katiba iliyopo, ila kwa sababu ya
"uzembe" wake wa kuruhusu maovu ya kijamii tuliyoyataja
kutamalaki.
Uzembe huo ulisababisha kujipaka matope na uchafu wa kila
aina ama kwa kushiriki au kwa kunyamazia maovu hayo kufikia
kile anachosema kila mara Rais wa awamu ya tano, John Pombe
Joseph Magufuli (JPM), kwamba, "nchi iliendeshwa kihovyo
hovyo tu kana kwamba hapakuwa
na (viongozi) serikali".
Kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Tume ya Warioba kwa njia
ya Rasimu ya Katiba ni kuboresha na kufafanua kwa fikra na
"mantiki" pana zaidi ya yaliyo bora yaliyomo katika
Katiba ya 1977 pamoja na namna ya utekelezaji kwa uthabiti,
na kwa kuziba au kuondoa mapungufu
tuliyokwishaelezea hapo mwanzo.
Ni Rasimu iliyohusisha "akili" bora za ainaaina
zinazofahamika hapa nchini, zenye fikra za kimapinduzi, utu
na usawa wa binadamu na wa kijamii na ambayo kama ingepita
ilivyo, bila ya shaka yoyote ingetoa Katiba bora na ya aina
yake kumfanya Mtanzania aishi
bustani ya Edeni bila hofu wala mawaa, badala ya kuendelea
kuishi kwenye "shamba la bibi" ilivyo sasa, kwa kila mtu
kuishi kadri ya ukali wa meno yake kuweza kurarua na kupora
kiharamia awezavyo, bila kujali wanyonge na mafukara wa nchi
wa kufukarishwa na
mfumo.
Rasimu hii ilikuwa tishio kwa maslahi ya mfumo wa kifisadi
uliotaka kubakia na uliofanya nchi "kuendeshwa kihovyo
hovyo tu kana kwamba hapakuwa na serikali".
Waingereza wana msemo, kwamba, "give a dog a bad name and
it will be killed", yaani, "mpe mbwa jina baya na
atauawa". Haraka haraka mafisadi wa nchini na wa kimataifa
walivuta pumzi kukusanya nguvu kuiangamiza rasimu hii kwa
kuipa tume na baadhi ya wajumbe
wake majina mabaya mabaya ionekane ya "majahili" na
rasimu hiyo kuwa haifai.
Kanuni na taratibu za kutunga Katiba zikapindwa bungeni
kuhakikisha kwamba inanyumbulishwa na kusukwasukwa mithili
ya meli ndani ya tufani na kupoteza mwelekeo wa Katiba
iliyokusudiwa.
Kisha, kwa matumizi ya hoja za nguvu; ubaguzi wa kiitikadi
wa kubumba; ushawishi wa kilaghai na matumizi ya pesa chafu
kwa kushirikisha ubepari wa ndani na wa kimataifa, tabaka
hili la kifisadi lililewesha bangi sehemu kubwa ya Bunge
Maalum la Katiba kiasi
cha kupanua midomo na kulishwa kila aina ya "mvinyo",
vinywa vimewaachama mithili ya makinda ya ndege, huku
likijipa bila uhalali wa kisheria, mamlaka ya kuandika
lenyewe "Katiba Inayopendekezwa" kwa kutupilia mbali
sehemu kubwa ya maoni ya wananchi.
Matokeo ya ubabe huu yalikuwa ni pamoja na kunyofolewa kwa
sehemu kubwa, misingi ya usawa wa kijamii, tunu za taifa,
maadili ya taifa, usimamizi wa rasilimali za taifa kwa
manufaa ya wananchi wote na uwajibikaji wa viongozi ili
kusimika kile kinachoweza kuitwa
"jamii ya kitabaka".
Baada ya kunyofolewa kwa sehemu kubwa mengi mema kwenye
Rasimu ya Tume ya Warioba, "Katiba Inayopendekezwa" ya
wababe wa ufisadi na mawakala wa ukoloni mamboleo, si tu
kwamba iliweka rehani demokrasia na uhuru wa nchi na raia
kwa ubeberu mpya, bali pia inasaliti
yaliyo mema katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 kuturejesha
"utumwani" kwa Farao, Misri.
Pengine, na huenda JPM aliyaona mapema haya kiasi cha kupata
ujasiri wa kuhoji kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo
vya habari nchini hivi karibuni akisema, "Je, mliwahi
kunisikia wakati wa kampeni zangu nikitaja lolote juu ya
Katiba?".
Maadam wababe wa ufisadi bado wana ushawishi mkubwa wa
kilaghai juu ya mkondo wa Katiba nchini kwa kushirikiana na
vigogo wengi ambao bado wapo ndani ya mfumo wa serikali,
mwendelezo wowote wa "Katiba Inayopendekezwa" hauna
maana tena kwa sababu utaipeleka
nchi pabaya kwa matakwa ya wababe hao.
Acha muda upite kwa jambo hili, hadi umma utakapofunguka
macho kuona uchafu uliokuwa ukilishwa ili kuchangamkia
mchezo huo wa kifo. Na maadam sehemu kubwa ya Katiba iliyopo
ina mengi mazuri ila kwa sababu tu ilibezwa kwa maslahi ya
kitabaka; JPM hana sababu
ya kukosa usingizi juu ya "mwongozo" wa kufanyia kazi
ila kwa kuzingatia na kuheshimu mema yaliyomo.
Wananchi (mimi nikiwa mmoja wao) baada ya kuona kuwa maovu
ya kijamii yanavuma na kunyamaziwa wakati Katiba iliyopo
ikivunjwa bila hofu kwa wavunjaji kuwajibishwa, walifikia
kutamani kuwa na kiongozi "kichaa" kidogo, dikteta mwema
(benevolent dictator) ainyooshe
kwanza nchi japo kwa awamu moja tu kwa kuwashikisha adabu
wote wenye kuchezea demokrasia, uhuru na haki za raia, hata
kama ni kwa "kuweka pembeni" kidogo baadhi ya vifungu
vya Katiba nzuri iliyopo.
Tangu mwanzo, serikali haikuwa na nia njema na suala la
Katiba mpya ila kuziba ombwe la uongozi kwa njia hiyo
kufuatia kutamalaki kwa ufisadi, rushwa na demokrasia duni
na hivyo kuelekea kuipa nguvu kambi ya upinzani dhidi ya
serikali iliyokwenda likizo kuchapa
usingizi.
Ni wazi pasingekuwa na hoja ya upinzani juu ya maovu haya
kama uongozi ungetekeleza wajibu wake vyema kwa kuongozwa na
Katiba iliyopo, na hivyo pia pasingezuka hoja ya Katiba
mpya.
Ndiyo maana, baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia
madarakani na kujitoa mhanga kupambana na maovu haya, kambi
ya upinzani imeishiwa hoja na madai ya Katiba mpya kukosa
mantiki. Hebu angalia mifano hii kuona ilivyokuwa.
Ukiona serikali madarakani inaatamia kwa mbawa zake maovu
yenye kuhujumu nchi, kupora au kuibia serikali mapato na
kuwakingia kifua wafanyabiashara wahujumu wa uchumi,
wakishirikiana
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment