Monday, 11 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua

Tangu mjadala huu umeanza sijawahi kumsikia kiongozi yeyote akisema hatutaki misaada na tunaweza kujitegemea kuanzia sasa.
Nilichokisikia na kukihisi ni:
Kukataa kuburuzwa kwa kufanya mambo kuridhisha MCC ili watupe misaada.
Mimesikia kuwa serikali bajeti yake ijayo itapunguza kiwango cha utegemezi wa misaada.
Nimesikia viongozi (Rais) wakisema misaada wakati mwingine inaambatana na masharti yasiyotekelezeka.
Nimeona utayari wa viongozi kuwa tayari kwenda tutakavyokwenda bila kuburuzwa ikitokea misaada ikaambatana na masharti.

Mimeona juhudi za serikali ya sasa kuongeza ukusanyaji wa mapato
Nimeona juhudi za serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza mapato yetu sehemu zinazoongeza tija.
Nimeona serikali ikiongeza uwajibikaji katika utumishi wa umaa.

Nimesikia pia viongozi wetu (idara ya upinzani) ikiichachamalia viongozi 'waliosema' Tanzania inaweza kujitegemea sasa.
Nimesikia hawawataji viongozi waliosema hivyo na kuashiria kuwa wanachokisema hakipo.

Wote tunakubaliana kuwa Tanzania haiwezi kujitegemea bila msaada wa nje wa namna yoyote ule.
Nimeshuhudia watanzania tukipingana kati ya wanaotaka tutegemee misaada kwa masharti yoyoteyale na wale tunaosema hapana misaada ya masharti tuikatae kama hayatupeleki tunakotaka.

Ninaamini kuwa:
Kamam ikitokea tukawekewa vikwazo vya kiuchumi na wapuuzi wa ulimwengu huu kama ilivyowahi kutokea kwa nchi fulani Nchi inao viongozi wanaoweza kuipitisha katika kipindi hicho na tukakivuka kwa heshima. Ninaamini pia kuwa katika kipindi hicho vibaraka wapo tayari kuajiriwa na watakaotuwekea vikwazzo hivyo.
Ninaamini kuwa jambo pekee linaloweza kutusumbua ni hao wapuuzi wakiamua kuja kutafuta silaha za maangamizi kama walivyofanya Iraq.
Ninaamini pia kuwa kunza watu waioelewa kuwa hawa wanaojifanya wanatusaidia hawana nia njemaa na sisi. wao ni nia zao ovu tu wala sio kutusaidia
Elisa

--------------------------------------------
On Sun, 4/10/16, 'Bart Mkinga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, April 10, 2016, 7:31 PM

Kati mijadala iliyochukua muda wa wengi hapa
katika majukwa mengi ni:
Je,
Tanzania inaweza kujitegemea ghafla leo baada ya kuwa
tegemezi kwa miaka yote?


Ukifuatilia utagundua kuwa watu wengiwasio na Elimu ya
uchumi ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuelezea
kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea kwa 100% hata kuanzia
leo. Lakini

wataalam wa uchumi na viongozi wa serikali wameeleza kuwa
Tanzania bado
tunahitaji kusaidiwa ili kuweza kusimama kwa miguu yetu kwa
100%. Baadhi
ya wachumi na watendaji wa serikali wamelisema hilo wazi na
wengine
wamenyamaza kimya kwa kukosa ujasiri wa kutamka kile
wanachokijua kuwa
Tanzania haina uwezo wa kujitegemea kwa 100% kwa ghafla,
japo uwezo huo
upo kwa siku za mbeleni kama tutakuwa na mipango thabiti.



Magufuli alipozungumzia kuhusu kujitegemea alitoa kauli
tata, alisema
Tanzania ina uwezo wa kujitegemea, na ilistahili kuwa donor
country,
hakusema tunaweza kujitegemea kuanzia sasa. Hakusema
tutakuwa donor
country kuanzia sasa. Na nina uhakika Magufuli kamwe
hatathubutu kutamka
kuwa Tanzania tayari tunaweza kujitegema kuanzia sasa, japo
uwezekano
upo.Tafsiri yangu ni kuwa alimaanisha kuwa uwezo huo tunao
japo
hatujitegemei, na je ni lini tutajitegemea, na kwa mipango
ipi? Ndiyo
jambo tulilostahili hasa kulijadili.



Miongoni mwa hatua za kuelekea kujitegemea ni hiyo ya
kusimamia
ukusanyaji wa kodi, kuongeza uwekezaji, kufanya kazi kwa
bidii, kuwa na matumizi mazuri ya fedha za
serikali, uwajibikaji, kujenga mifumo na utengenezaji wa
sera zinazolenga kujitegema. Hayo hayatokei kwa kulala na
kuamka.



Kujitegemea ni process, siyo kila siku unasaidiwa katika
kila kitu:
barabara unajengewa, maji unaletewa, wagonjwa wako wote wa
HIV wanapewa
ARV na wageni, uzazi wa mipango unasaidiwa, huduma ya Mama
na Mtoto
unalipiwa, umeme unajengewa, madaraja unajengewa, mafunzo ya
watendaji
wako unagharamiwa, mafunzo ya majeshi unasaidiwa, silaha za
kivita
unanunuliwa, n.k., halafu uamke tu na kusema kuwa kuanzia
kesho
najitegema. Utakuwa kichaa! Mwenye hekima lazima atatuambia
kuwa katika
process ya kujitegemea, tunaanza kujitegemea na nini.
Tunatarajia
tuambiwe kuwa katika mwaka huu wa fedha barabara zetu zote
tunazijenga
wenyewe,
mwaka mwingine atatuambia maendeleo ya sekta ya kilimo
yanagharamiwa na
sisi wenyewe, n.k.



Ni ukweli huu ndiyo unaofanya wataalm wote wa uchumi au
kukaa kimya au
kuishia tu kusema, tunasikitishwa kukatiwa misaada,
tunatarajia watoaji
wa misaada watafikiria upya uamuzi wao, na wengine kuamua
kukaa kimya.
Ila wale wasiojua hata A ya uchumi kama wanabaki wanapiga
kelele za kujifurahisha kuwa tunaweza kujitegema kuanzia
sasa.



Zimbabwe ilikuwa na uchumi imara zaidi ya mara 10 ya uchumi
wa Tanzania.



Zimbabwe inachimba madini mengi kuliko Tanzania. Zimbabwe
ina migodi ya
kisasa ya precious metals kama gold, na ilikuwa nayo hata
kabla ya
Tanzania. Inachimba base metals kama Nickel, Copper, Zinc na
Lead.
Tanzania hatuna migodi ya madini hayo, copper kidogo inatoka
pale
Bulyanhulu kama by-product.



Zimbabwe ni nchi inayoongoza katika uchimbaji na uuzaji wa
madini ya Lithium katika Afrika.



Zimbabwe inachimba industrial minerals kama limestone,
dolomites na phosphates.



Zimbabwe ni nchi ya pili Duniani katika uchimbaji na uuzaji
wa madini ya platinum (white gold).



Zimbabwe ina viwanda vya aina mbalimbali vinavyozalisha
bidhaa zaidi ya 6,000.



Ni kutokana na uchumi huo imara wa Zimbabwe, Mugabe alifanya
jeuri,
akiiamini uchumi wake imara ungeweza kusimama wenyewe bila
ya
kuyategemea mataifa ya Ulaya Magharibi na Amerika akijidai
kuwa maumuzi ya kuwanyang'anya ardhi walowezi alikuwa
analinda
uhuru wa Taifa lake.
Zimbabwe hata wananchi wa vijijini walikuwa hawajui kununua
nyanya
zilizowekwa barabarani kwenye mchanga kama Tanzania,
walikuwa wananunua kwenye super
markets zilizokuwa zimeenea nchi nzima.



Leo Zimbabwe haina hata sarafu yake yenyewe, inatumia dola
ya marekani
na Randi ya Afrika Kusini. Je hapo sasa Zimbabwe imekuwa na
uhuru zaidi
au imepoteza uhuru wake? wananchi wake, tena wasome
waliishia kuuwawa
huko Afrika Kusini walikokuwa wameenda kubangaiza maisha.
Nilipokuwa
Afrika Kusini nilizungumza na baadhi ywa hudumu (waiters) wa
mahoteli ya
Afrika Kusini, wengi walikuwa Wazimbabwe, wengine ni walimu
wa
sekondari, wengine ni wauguzi, walikuwa clinical oficcers,
wanaona aheri
wakafanye kazi ya uhudumu wa hoteli Afrika kusini kuliko
kufundisha
sekondari au kutibu wagonjwa nchini Zimbabwe.
Hivi
kwa Zimbabwe kuamua kutumia sarafu za wale wale
uliosema wanakuingilia uhuru wako, ni uhuru zaidi? je,
Watanzania
tunataka tufike huko? Namsihi Rais Magufuli azisikie sauti
zetu hizi,
watanzania wana asili ya unafiki wanapoongea na mkubwa,
watakusifia hata
pale unapokosea.



Watanzania tuna ule msemo kuwa mwenzio akinyolewa wewe tia
maji,
tusijifanye ni Vinjekitile tunapigwa risasi tunakufa ndugu
wanaotuona tunakufa
wanasema risasi hizo zimegeuka maji na damu inayomwagika ni
maji.
Binadamu mwenye akili hujifunza kupitia makosa ya mwenzake.
Tusiwe kama
nyumbu ambao wanaona aliyetangulia anaingia kwenye mto,
analiwa na mamba
mmoja, na yeye anaamini hatakamatwa kwa sababu yule mamba
ameshiba kwa
kumla yule nyumbu wa kwanza bila ya kujua mto una mamba
wengi.



Tanzania nchi maskini kabisa, tena kwa mbali ukilinganisha
na Zimbabwe
haina uwezo wa kushindana na haya mataifa makubwa kwa
kiburi, yatubidi tuwe werevu,
twende nao kwa urafiki na uelewano, huku tukiendelea
kujenga uwezo wetu
wa kujitegemea. twende kwenye uhalisia, tusipelekwe na sifa
au mihemuko
ya kisiasa.



Tunataka utawala wa Magufuli ufanikiwe, kufanikiwa kwa
utawala wake ni
unafuu kwa watanzania na kufanikiwa kwa Tanzania kama taifa.
Tunakuomba
Magufuli, fanya jitihada zako zote, ujenge uhusiano wa
karibu na ulio
imara na jamii ya kimataifa. Tofauti ya kuwa na mahusiano
mazuri na
mahusiano mabaya gharama yake ni kubwa mno. Zimbabwe
kimaendeleo imerudi
nyuma zaidi ya ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Mpe maelekezo
Waziri wako
wa Mambo ya nje kuwa tunataka mahusiano mazuri na jamii ya
kimataifa,
tunataka misaada yote iliyosimamishwa tuipate ili itupe
nguvu ya kuweza
kujitegemea haraka, tuitumie misaada hiyo kama mbegu tukijua
kuna siku
itatoweka.
Msambichaka Mkinga



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment