Tunasubiri utumbuaji wa Lugumi!!
LKK
On Tuesday, April 19, 2016 9:12 PM, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
M4c ya MAGUFULI ni balaa, Ni Tsunami na mtikisiko ndani na je ya mipaka ya Tanzania na wazembe, wabadhirifu wahujumu na mafisadi wanaisoma namba na watazidi kuisoma namba kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.
Ndio wanaisoma namba kwa mabadiliko yanayotokea, wanawachanganya watu walio wengi huku baadhi yao wasijue la kufanya.
Watu wengi wanastushwa na kwa nafurahi a sana kwa mabadiliko haya huku
wachache wakichuki. " Ni afadhali wachache wakachukia kuliko umma wa watu milioni 40 nikiwakosesha, name nitajibu nini kwa Mungu?". Anasema Rais Magufuli akiwa kwao Chato siku za hivi karibuni.
Wakati wa kampeni mwaka jana Rais wetu alisikika akisema "Magufuli for Change" watu hawakumuelewa kwa vile kauli mbiu hiyo hutumiwa nan a CHADEMA wakimaanisha "harakati za kimabadiliko" yaani Movement 4 change, kwa kifupi M4C.
Mabadiliko ya M4C ya JPM yalianza mara tu baada kutingia ofisini Ikulu, JMP alianza kutembelea wizara za serikali kwa staili ya kushitukiza. Akakuta baadi ya watumishi hawakuwepo ofisini muda wa kazi kinyume na taratibu.
Kumbuka kwa wafanyakazi hewa huu, huu ni mtikisiko wa aina yake unaoonekana kuzikumba halmashauri nyingi katika Tanzania yetu, hayo ni mabadiliko ambayo hayajawahi kutokea.
Kwa mfano hadi wiki hii tunaambiwa kuna wafanya kazi hewa 300 Arusha pekee, na huko Shinyanga alipotumbuliwa Anna Kilango wanazidi kuongezeka mpaka sasa ni zaidi ya 100.
Swali linakuja mbona hakuna wafanyabiashara hewa wala wakulima hewa? Swali lingine ni mabilioni mangapi yameliwa tangu awamu ya pili yam zee Ruksa (Rais Mstaafu Mwinyi) mapaka sasa.
Haijawahi kutokea kuumbuka wala kuumbuliwa kwa watumishi ndani ya serikali hii ambao wengine hulipwa mishahara inayofikia milioni 40. Huku kima cha chini wengine wakilipwa elfu sabini kama sikosei.
Wanoishi kama maraika sasa wataishi kama shetani hadi kufikia mishahara ya juu shilingi milioni 15 tu. Hii haijawahi kutokea na hii ni M4C namaanisha Magufuli 4 Change. Wafanyakazi ama watumishi wa umma sasa wameanza kufanya kazi kwa weledi bila masihara,uzembe, uvivu na unafiki vimeanza kuondoka katika sekta za umma.
Angalau sasa wananchi tumeanza kula matunda ya M4C ya Magufuli kwa maana watumishi matumbo joto kwamba uklizubaa utatumbuliwa kama si kukatwa mguu kabisa. "Mimi sio kutumbua tu ikibidi nakata mguu kabisa" alinukuliwa JPM akisema hayo juzi juzi Chato akiongea na wananchi. Kama sio kuisoma namba basi umma usome alama za nyakati.
Sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari hususani runingani watumishi wa wengi wa umma wanakamatwa na hatia mbalimbali na kufunguliwa mashitaka mahakamani. Sasa naiona mahakama ya mafisadi ikianza kazi bila hata majengo yake kuanzishwa.
Kuna baadhi ya wizara hata sasa wanafanyakazi huku wakijua kuwa wanaweza kutumbelewa na kujikuta katika wakati mgumu kama bado watakuwa wanazembea kutoa huduma walioajiriwa kwao.
M4C ya Magufuli anasema hivi "kama mtumishi wa serikali una wasiwasi wa kutumbuliwa basi ondoka tu, na kama una wasiwasi ndio tiketi yako ya kuondolewa" mwisho wa kunukuu.
Hotuba yake aliyoitoa bungeni inadhihirisha kuwa huyu ni Magufuli 4 Change, kwani matendo yake yanajionyesha wazi. Utadhani katokea kwenye chama cha upinzani na hii haiwezi kusahaulika kamwe katika historia ya taifa hili.
Rais Magufuli alidiriki kuyaanika madudu mengi ya serikalini na ambayo yamezoeleka kudekezwa na viongozi wa wa juu wa nchi huku na wao wakiwa wamekaa na kumsikiliza akimwaga sera zake.
Kabla hatujakaa sawa siku ya sherehe ya uhuru nchii hii zikafika, wote tukachukua zana za usafi kusafisha miji yetu kwa kufutwa kwa sherehe hiyo na pesa zilizopangwa kwa sherehe hiyo zikachukuliwa na kupelekwa katika huduma nyingine za kijamii. Hiyo ndio Magufuli 4 Change.
Kajipambanua kuwa yupo tofauti na marais wenzake waliopita JPM' akapiga magwanda, kombati za kijeshi wakati akielekea katika kwenye sherehe za kuhitimisha mafunzo ya kijeshi huko Monduli – Arusha. Akizungumzia suala hilo mkuu wa Mjeshi, Davis Mwamnyange alisema kuwa hii ni heshima ya mkuu wan chi.
Ni Mabadiliko ya aina yake amabayo JPM hakutaka kujionyesha kwa watawala wa dunia hii mara tu baada ya kuapishwa kwakwe, hakutaka kwenda Marekani ' kula bata'. Mpaka sasa katembelea nchi moja tu ya Rwanda kwa maslahi ya taifa, huyu ndiye Magufuli 4 Change.
Juzi juzi TRA, ilitangaza kuongezeka kwa mapato yake hadi kufikia Trilioni moja na pointi tatu sawa na vile alivyokuwa amekisema M4C kuwa Tanzania ni tajiri sana wala hatuitaji kuwa ombaomba.
M4C ya Magufuli ni kwamba, kuisoma namba kwa kwenda mbele kwa kuwa matumizi ya fedha yameminywa sana. Kwamba kama watumishi wa umma wafanyie vikao vyao maofisini wapo wengi hawawezi kuenea wafanyie hata chini ya muembe.
Hakuna tena kwenda mahotelini ama kupanda ndege kwenda nchi za nje kufanya kikao kinachoihusu Tanzania kama ilivyokuwa imezoeleka huko nyuma watu kukutana Dubai kujadili maendeleo ya Tanzania.
M4C ya Magufuli mesababisha sherehe kupungua na bar nyingi hazipati wateja ukilinganisha na tawala za awamu mbili zilizopita katika nchi hii. Wengi wanalia pesa hakuna. Wengi wanaisoma namba maana walizoea 'Kupiga madili ya hela' Kinyume na utaratibu.
Aidha kutumbuliwa kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna Kilango Malecela nayo ni dalili nyingine kuwa M4C ya Magufuli haina mchezo wala masihara na wengi wataisoma namba bila kujali nyadhifa zao wala haiba zao za kisiasa. Kwani moto huu asio wa mabua watu wenyewe wanaona kuwa JPM hana UCCM hata chembe.
Onyo kali ameshalitoa M4C siku za karibuni akisema "Atakayejaribu kutukwamisha , atakwama yeye na sio mimi kutumbua majipu tu hata kukata mguu". Haya sasa kama sio kuisoma namba hapo kila mtu ajue kuwa mambo yamebadilika na Tanzania kumekucha.
Hongera Magufuli 4 Change.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment