Wednesday 20 April 2016

Re: [wanabidii] Tanzania bila misaada haiwezekani: Misaada bila masimango inawezekana

Nadhani kuna universal translation ya human rights. Tumesaini mikataba ya UN kuhusu haki za binadamu.
Kunaweza kuwepo tafsiri tofauti kuhusu demokrasia lakini hatima yake ni utawala uliosimikwa na watu kwa niaba ya watu.
Pili sidhani kuna taifa lolote limetoa misaada kwa masimango. Huo ndio mtazamo wangu in a nutshell.
em

2016-04-20 10:27 GMT-04:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Mjadala huu unahitaji kujadiliwa  kwa makini.
Sijawahi kusikia kiongozi yeyote wa Taifa hili akisema Tanzania haihitaji kutumia misaada ya nje ili kuliendeleza Taifa. Na Kweli haiwezekani taifa lolote likaendelea au kutimiza malengo yake bila misaada. Marekani ilipotaka kuipiga Iraq ilibidi kukusanya majeshi mpaka ya Kenya. Ni misaada. Niliwahi kusikia kuwa Marekani inadaiwa kuliko mataifa yote duniani. Kinachoisaidia ni ujanja wa kuyaibia mataifa mengine na kuyahujumu ili iweze kulipia madeni yake. Na madeni ni misaada.
Nilichokisikia viongozi wetu wakisema ni kukataa misaada yenye masharti ambayo yanaumbua utu wetu. Mataifa hayo yanalazimisha kutafsiri kila kitu. Demokrasia watafsiri wao. Haki za Binadamu watafsiri wao na wakati mwingine hawataki uweke haki na wajibu wa binadamu. Hata uhuru wa taifa au tunu zake watafsiri wao. Tukisema Muungano wetu tutaulinda kwa vyovyote wanasema hapana. Demokrasia kwanza. Mfano marekani ilitumia mabavu kulazimisha muungano taifa moja wapo linalounga umoja huo lilipotaka kujitenga. USSR au Yugoslavia zilipoanza kusambaratika isingeweza kutumia mabavu. Kisa: Demokrasia.
Hizo tafsiri ndizo zilifanya MCC waamue 'kuinyika' Tanzania misaada. Walitaka tutumie akili zao kutafsiri uingiliwaji au utoingiliwaji wa uchaguzi Zanzibar. Walitaka tutumie tafsiri yao kuhusu makosa ya mitandao. Ninaposema tafsiri yao simaanishi kama wao wanavyotafsiri kwao, hapana kama wanavyotaka kutafsiri kwetu tu.
Walivyo wajanja wamesema misaada katika maeneo mengine kama Elimu na Afya vitaendelea. Naam vitaendelea. Ndio wanaamua tuanzishe chanjo gani mpya. Hazitegemei milipuko ya magonjwa iliyopo kwetu. Hapana. Ndiyo maana wakatusaidia chanjo ya kuharisha na Pneumonia. Niliwahi kumuuliza daktari mmoja kuwa kulikuwa na mlipuko wa nini mpaka tukasaidiwa chanjo hii. Akasema sijui. Na huyo alikuwa Mganga Mkuu wa Wilaya fulani nimeisahau. Hata sasa wametubadilishia chanjo ya Polio.
Kuna wakati myaka ya 90 Warundi waliwahi kutilia mashaka maziwa Fulani na wakasema warundi walio makambini wasipewe maziwa hayo. Sisi tukasema 'tupeni'. Yakasambaa kwetu.
Elimu ndiyo huelekeza mtu aende wapi. Inapotolewa utotoni ina-determine ukubwa wa mtu. Maeneo hayo hawawezi kuacha kufadhili hata mungeua watu kila siku. Nani ajuaye misaada hiyo itasaidia kuamua aina ya raia watakaokuwepo myaka 60 ijayo? Hata Osama walimpata kupitia chanjo ya watoto. Ulikuwa msaada wa USAID. USAID kumtafuta Osama ndiyo.
Lakini hoja yangu ni hii- Kuna watu wanasema hatuwezi kwenda bila misaada hata kama inaambatana na masimango. Nataka kuorodhesha watu wanaoogopa kutosaidiwa na kuwapima ni watu wa namna gani. Huko sio kutojitambua? Sisi na raslimali zetu tunahitaji misaada hata inayoambatana na masimango?
Ninaamini tunahitaji misaada. Lakini hatuhitaji misaada ya masimango. Ninaamini kuna mataifa duniani yanaweza kutusaidia. Tunahitaji kuangalia tunahitaji kusaidiwa wapi na nini. Naelewa kama tunasaidiwa kuchimba madini yetu. Kusaidiwa vyombo vya kisasa kumsaidia mkulima kurekebisha kilimo chake.
Sitarajii serikali makini kusaidiwa misaada kwa sehemu kubwa katika afya, chakula Elimu nk. Lazima uamue ni kitu gani usaidiwe katika maeneo hayo. Maeneo hayo taifa lazima liwe selective. Misaada mingine inaweza kuvuruga utamaduni wako na taifa likakosa identity. Sikiliza lafudhi za wasanii wetu. Ni makosa kufikiri wamepotea kwenye ulimi. Hapana upotevu umeanzia kichwani.
Misaada mingine si lazima ziwe grants. Hata mikopo nafuu. Mimi ninawashangaa wasomi wanaositasita na kutaka tuwe tayari hata kwa misaada ya masimango. Mwalimu Nyerere aliacha msaafu wa ripoti yake ya South Commission. Ushauri wake ambao naona Magufuli anaanza kuutekeleza unatosha kuliendeleza Taifa. Wapo watu wanaona misaada lazima itoke Marekani. Hapana. Singapore, Thailand, Vietman Rwanda, Kenya. Hao hawatatupa pesa. Watatukopesha mashine za kuwasaidia wakulima. Watatusaidia technologia ya kusindika mazao yetu. Watatusaidia technologia ya kuchimba madini yetu. Watatusaidia uzoefu Fulani. Viongozi wetu ambao hawakuzoea Muhogo ndio wanamsumbua Rais wetu. Kama tukisema misaada hii hapana lazima tuwe tayari ama kujibana mahala au kuyakosa mambo fulani. Ndio Muhongo aliousema Magufuli na watu wengine wakakosa kuelewa ana maana gani.
Elisa

  --

  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

   

  Kujiondoa Tuma Email kwenda

  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
 Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma

   

  Disclaimer:

  Everyone posting to this Forum bears the sole
 responsibility
  for any legal consequences of his or her postings, and
 hence
  statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree to this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

  ---

  You received this message because you are subscribed to
 the
  Google Groups "Wanabidii" group.

  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

  For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

 --
 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 Kujiondoa Tuma Email kwenda
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
 Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 Disclaimer:
 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 ---
 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.
 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment