Monday, 11 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua

akuongeza la 11 nami naliongeza
11) katika kuimarisha demokrasia kudhibiti uanaharakati usio na tija ila unaashiria kuturudisha nyuma kwa kisingizio cha Haki za binadamu.
--------------------------------------------
On Mon, 4/11/16, 'mashakamakana' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
To: "'Msambichaka Bart' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, April 11, 2016, 12:14 PM

Kwa michango ya namna hii tutafika.
Naimani mh. rais wetu yamemfikia mawazo yako mazuri.
Ikifikia wakati katiba inaundwa, wajumbe wa baraza
lisijumuishe wabunge waliopo madarakani na wastaafu na
wanasiasa ili kulinda maslahi ya nchi. Posho pia ya bunge
ipunguzwe ili kupata wabunge wa bunge maalum wenye uzalendo
kwa maslahi ya nchi na ustawi wake.

'Msambichaka Bart' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Haya tunayoyatoa ndiyo maoni yetu ya kuifanya Tanzania
ijitegemee haraka, kinyume chake ni kuifanya Tanzania
ichelewe zaidi kujitegemea. Kwa ufupi tukitaka tujitegemee
ni lazima tuyafanye (mengine tayari Rais ameanza kuyafanya)
yafuatayo:
1) Usimamiaji mzuri wa matumizi ya mapato ya serikali
2) Uimarishaji wa misingi ya demokrasia na kuheshimu uhuru
wa raia ili wananchi waungane kwa lengo moja la kujenga nchi
yao. Uchafu ule uliofanyika Zanzibar utafutiwe suluhisho
haraka
3) Usimamiaji mzuri wa ukusanyaji kodi za serikali kwa njia
rafiki
4) Kuhakikisha kuna watu wenye uwezo na ubunifu TRA ili
kuepukana na mawazo duni kuwa ukiweka kodi nyingi na kubwa
ndiyo mapato ya serikali yanaongezeka. Kodi utititiri na
kubwa zinadidimiza uwekezaji na ukuaji wa uchumi. Nchi kama
Dubai, Hong Kong zimeendelea haraka kutokana na kuwa na kodi
ndogo. Kodi ndogo kwa Tanzania kutaifanya Tanzania kuwa kuwa
mahali pa kufanyia manunuzi kwa nchi nyingi majirani zetu
5) Serikali izungumze na waagizaji wakubwa wa bidhaa toka
mataifa ya kigeni iwaulize ni lini wataanza kuzalisha
Tanzania bidhaa hizo hizo wanazoagiza toka nje. Iwasaidie
waagizaji hao wa bidhaa toka nje ili wawe wazalishaji
6) Wazalishaji wa ndani ambao uzalishaji wao ni mdogo waitwe
wazungumze na serikali ili kujua ni nini kinawazuia kuwa
wazalishaji wakubwa. Kama tatizo ni mtaji wasaidiwa kupata
mitaji kwa serikali kuwekeza katika makampuni hayo na
baadaye wafanyakazi na wananchi wengine wanunue hisa za
serikali. Kama tatizo ni soko, kwa bidhaa ambazo serikali
ina uwezo wa kuzitumia, serikali inunue bidhaa kutoka kwa
wazalishaji wa ndani
7) Serikali na taasisi zake zote, walazimishwe kununua
mahitaji yao kutoka kwa wazalishaji wa ndani isipokuwa pale
tu ambapo hazipatikani. Wazalishaji wa ndani wasaidiwe
katika kuongeza ubora wa bidhaa zao.
8) Rais na wote wenye mamlaka waepuke kabisa teuzi za nafasi
mbalimbali kama zawadi kwa misimamo ya kisiasa au urafiki na
undugu uliopo baina yao
9) Serikali ijenge mifumo imara ya kitasisi inayoweza
kusimamia kila jambo ili utendaji kazi kwa misingi ya
uadilifu na weledi uwepo wakati wote bila ya kujali nani
amekuwa kiongozi mkuu
10) Serikali ijenge mahusiano mazuri na jamii ya kimataifa
ikiwemo wahisani wetu wa miaka mingi. Bado tunawahitaji ili
tuweze kujitegemea kwa haraka, la muhimu ni kutambua kuwa
kila msaada tunaopewa utuelekeze kwenye kujitegemea kuliko
kutufanya kuwa watu wa kusaidiwa milele.
10) Mwanzo wa yote ni Katiba nzuri. Rasimu ya katiba ya
Warioba, yenye mapendekezo yenye hekima toka kwa wananchi
iwekewe utaratibu wa kujadiliwa upya baada ya kuchakachuliwa
na watu wachache wasio na nia njema na Taifa letu.

Bart

-------- Original Message --------
Subject: RE: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua
Hatua
From: 'mashakamakana' via Wanabidii
To: 'ananilea nkya' via Wanabidii
CC:


Watanzania wote tunatakiwa tumuunge
mkono mh.Rais wetu kwa hii sera ya nchi kujitegemea.
Watanzania tushikane kuanzia ktk kaya vitongoji hadi taifa.
Sidhani kama mh. rais wetu akipelekewa maoni ya jinsi ya
kujitegemea hawezi kupuuza. kukosoa bila kutoa suluhisho
haijengi hata kama kazi yako ni mkosoaji. wachangiaji wengi
ktk mitandao ya kijamii hatutegemei wahisani kukidhi
mahitaji ya familia zetu. Chaguzi zimekwisha tumpelekee mh.
rais maoni yetu ya kuijenga mchi ijitegemee na tufanye kazi

'ananilea nkya' via Wanabidii wrote:

>Mkinga,
>Hoja yako ni nzito. Nami niongezee kwamba, nchi kuamua
kujitegemea kunawezekana tu pale demokrasia inapokuwa siyo
ya figisufigisu, ubabe, dharau na ulaghai wa mchana kweupe.
Kilichofanyika hapo Zanzibar tupende tusipende kitatugharimu
Watanzania wote. Hii ni kwa sababu nchi kuweza kujenga
vuguvugu la kuelekea kujitegemea ni lazima, pamoja na mambo
mengine, kuwe na marishiano na maelewano siyo tu ya
kijamii na kisiasa kwa wananchi wote Tanzania Bara na
Tanzania Visiwani bali pia maelewano (normalized
relationship) kati ya Tanzania waliotutegemea (maana
hawatupi chochote bure) nasi kuwategemea (maana wanachuma
sana kwetu). Kujigamba na ubabe ubabe kama wa Mugambe ni
lazima utaigharimu Tanzania. Siku zote nimesema kama hayo
maamuzi ya Zanzibar yalikuwa
>ni ya Rais Dr John Magufuli hapo rais wetu alikosea na
kama yalikuwa ni mipango ya waliomtangulia, basi kwa kujua
au kutokujua wameiingiza serikali ya Magufuli mkenge-- maana
kama alikusudia kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo na
kuijenga Tanzania katika katika kuanza kujitegemea maamuzi
ya Zanzibar yatakuwa kwa kiasi chake yamekwaza maana ni yeye
at



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment