Monday, 11 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua

Kwa michango ya namna hii tutafika. Naimani mh. rais wetu yamemfikia mawazo yako mazuri. Ikifikia wakati katiba inaundwa, wajumbe wa baraza lisijumuishe wabunge waliopo madarakani na wastaafu na wanasiasa ili kulinda maslahi ya nchi. Posho pia ya bunge ipunguzwe ili kupata wabunge wa bunge maalum wenye uzalendo kwa maslahi ya nchi na ustawi wake.

'Msambichaka Bart' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Haya tunayoyatoa ndiyo maoni yetu ya kuifanya Tanzania ijitegemee haraka, kinyume chake ni kuifanya Tanzania ichelewe zaidi kujitegemea. Kwa ufupi tukitaka tujitegemee ni lazima tuyafanye (mengine tayari Rais ameanza kuyafanya) yafuatayo:
1) Usimamiaji mzuri wa matumizi ya mapato ya serikali
2) Uimarishaji wa misingi ya demokrasia na kuheshimu uhuru wa raia ili wananchi waungane kwa lengo moja la kujenga nchi yao. Uchafu ule uliofanyika Zanzibar utafutiwe suluhisho haraka
3) Usimamiaji mzuri wa ukusanyaji kodi za serikali kwa njia rafiki
4) Kuhakikisha kuna watu wenye uwezo na ubunifu TRA ili kuepukana na mawazo duni kuwa ukiweka kodi nyingi na kubwa ndiyo mapato ya serikali yanaongezeka. Kodi utititiri na kubwa zinadidimiza uwekezaji na ukuaji wa uchumi. Nchi kama Dubai, Hong Kong zimeendelea haraka kutokana na kuwa na kodi ndogo. Kodi ndogo kwa Tanzania kutaifanya Tanzania kuwa kuwa mahali pa kufanyia manunuzi kwa nchi nyingi majirani zetu
5) Serikali izungumze na waagizaji wakubwa wa bidhaa toka mataifa ya kigeni iwaulize ni lini wataanza kuzalisha Tanzania bidhaa hizo hizo wanazoagiza toka nje. Iwasaidie waagizaji hao wa bidhaa toka nje ili wawe wazalishaji
6) Wazalishaji wa ndani ambao uzalishaji wao ni mdogo waitwe wazungumze na serikali ili kujua ni nini kinawazuia kuwa wazalishaji wakubwa. Kama tatizo ni mtaji wasaidiwa kupata mitaji kwa serikali kuwekeza katika makampuni hayo na baadaye wafanyakazi na wananchi wengine wanunue hisa za serikali. Kama tatizo ni soko, kwa bidhaa ambazo serikali ina uwezo wa kuzitumia, serikali inunue bidhaa kutoka kwa wazalishaji wa ndani
7) Serikali na taasisi zake zote, walazimishwe kununua mahitaji yao kutoka kwa wazalishaji wa ndani isipokuwa pale tu ambapo hazipatikani. Wazalishaji wa ndani wasaidiwe katika kuongeza ubora wa bidhaa zao.
8) Rais na wote wenye mamlaka waepuke kabisa teuzi za nafasi mbalimbali kama zawadi kwa misimamo ya kisiasa au urafiki na undugu uliopo baina yao
9) Serikali ijenge mifumo imara ya kitasisi inayoweza kusimamia kila jambo ili utendaji kazi kwa misingi ya uadilifu na weledi uwepo wakati wote bila ya kujali nani amekuwa kiongozi mkuu
10) Serikali ijenge mahusiano mazuri na jamii ya kimataifa ikiwemo wahisani wetu wa miaka mingi. Bado tunawahitaji ili tuweze kujitegemea kwa haraka, la muhimu ni kutambua kuwa kila msaada tunaopewa utuelekeze kwenye kujitegemea kuliko kutufanya kuwa watu wa kusaidiwa milele.
10) Mwanzo wa yote ni Katiba nzuri. Rasimu ya katiba ya Warioba, yenye mapendekezo yenye hekima toka kwa wananchi iwekewe utaratibu wa kujadiliwa upya baada ya kuchakachuliwa na watu wachache wasio na nia njema na Taifa letu.

Bart


-------- Original Message --------
Subject: RE: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
From: 'mashakamakana' via Wanabidii
To: 'ananilea nkya' via Wanabidii
CC:


Watanzania wote tunatakiwa tumuunge mkono mh.Rais wetu kwa hii sera ya nchi kujitegemea. Watanzania tushikane kuanzia ktk kaya vitongoji hadi taifa. Sidhani kama mh. rais wetu akipelekewa maoni ya jinsi ya kujitegemea hawezi kupuuza. kukosoa bila kutoa suluhisho haijengi hata kama kazi yako ni mkosoaji. wachangiaji wengi ktk mitandao ya kijamii hatutegemei wahisani kukidhi mahitaji ya familia zetu. Chaguzi zimekwisha tumpelekee mh. rais maoni yetu ya kuijenga mchi ijitegemee na tufanye kazi

'ananilea nkya' via Wanabidii wrote:

>Mkinga,
>Hoja yako ni nzito. Nami niongezee kwamba, nchi kuamua kujitegemea kunawezekana tu pale demokrasia inapokuwa siyo ya figisufigisu, ubabe, dharau na ulaghai wa mchana kweupe. Kilichofanyika hapo Zanzibar tupende tusipende kitatugharimu Watanzania wote. Hii ni kwa sababu nchi kuweza kujenga vuguvugu la kuelekea kujitegemea ni lazima, pamoja na mambo mengine, kuwe na marishiano na maelewano siyo tu ya kijamii na kisiasa kwa wananchi wote Tanzania Bara na Tanzania Visiwani bali pia maelewano (normalized relationship) kati ya Tanzania waliotutegemea (maana hawatupi chochote bure) nasi kuwategemea (maana wanachuma sana kwetu). Kujigamba na ubabe ubabe kama wa Mugambe ni lazima utaigharimu Tanzania. Siku zote nimesema kama hayo maamuzi ya Zanzibar yalikuwa
>ni ya Rais Dr John Magufuli hapo rais wetu alikosea na kama yalikuwa ni mipango ya waliomtangulia, basi kwa kujua au kutokujua wameiingiza serikali ya Magufuli mkenge-- maana kama alikusudia kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo na kuijenga Tanzania katika katika kuanza kujitegemea maamuzi ya Zanzibar yatakuwa kwa kiasi chake yamekwaza maana ni yeye at

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment