-------- Original Message --------
Subject: RE: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
From: 'mashakamakana' via Wanabidii
To: 'ananilea nkya' via Wanabidii
CC:
Watanzania wote tunatakiwa tumuunge mkono mh.Rais wetu kwa hii sera ya nchi kujitegemea. Watanzania tushikane kuanzia ktk kaya vitongoji hadi taifa. Sidhani kama mh. rais wetu akipelekewa maoni ya jinsi ya kujitegemea hawezi kupuuza. kukosoa bila kutoa suluhisho haijengi hata kama kazi yako ni mkosoaji. wachangiaji wengi ktk mitandao ya kijamii hatutegemei wahisani kukidhi mahitaji ya familia zetu. Chaguzi zimekwisha tumpelekee mh. rais maoni yetu ya kuijenga mchi ijitegemee na tufanye kazi
'ananilea nkya' via Wanabidiiwrote:
>Mkinga,
>Hoja yako ni nzito. Nami niongezee kwamba, nchi kuamua kujitegemea kunawezekana tu pale demokrasia inapokuwa siyo ya figisufigisu, ubabe, dharau na ulaghai wa mchana kweupe. Kilichofanyika hapo Zanzibar tupende tusipende kitatugharimu Watanzania wote. Hii ni kwa sababu nchi kuweza kujenga vuguvugu la kuelekea kujitegemea ni lazima, pamoja na mambo mengine, kuwe na marishiano na maelewano siyo tu ya kijamii na kisiasa kwa wananchi wote Tanzania Bara na Tanzania Visiwani bali pia maelewano (normalized relationship) kati ya Tanzania waliotutegemea (maana hawatupi chochote bure) nasi kuwategemea (maana wanachuma sana kwetu). Kujigamba na ubabe ubabe kama wa Mugambe ni lazima utaigharimu Tanzania. Siku zote nimesema kama hayo maamuzi ya Zanzibar yalikuwa
>ni ya Rais Dr John Magufuli hapo rais wetu alikosea na kama yalikuwa ni mipango ya waliomtangulia, basi kwa kujua au kutokujua wameiingiza serikali ya Magufuli mkenge-- maana kama alikusudia kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo na kuijenga Tanzania katika katika kuanza kujitegemea maamuzi ya Zanzibar yatakuwa kwa kiasi chake yamekwaza maana ni yeye ataonekana mbabe kwa vile ndiye ndiye mwenye usukani wa nchi kwa sasa.
>
>Hakika, kama ulivyosema, mtu ambaye aliwahi kuitembelea Zibwambe miaka ya mwanzoni mwa 90 akienda leo lakima atakumbuka Mwalimu Nyerere akichombambia Mugabe wakati anaapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Nyerere alimwambia hivi. Robert Mugambe; umeipokea Bimbabwe ikiwa nchi ya asali na maziwa, angalia usinogewe utawala ukaivuruga nchi hii. Angeinuka Mwalimu leo; sijui Mugambe angejichimia wapi Wazimbabwe wameikimb ia nchi yao wamekuwa wakimbizi katika nchi za Afrika na Ulaya. Nchi ilikuwa inaongoza kwa kuwa na shule nzuri Afrika leo ni balaa etu uhuru--uhuru wa wachache kuneemeka kwa kisingizio walipigania uhuru? Kwani ukoloni ni sura au matendo ya kinyonyaji ambayo hayana rangi, dini wala itikadi ya siasa?
>
>Ananilea Nkya
> E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
>--------------------------------------------
>On Sun, 4/10/16, Herment Mremawrote:
>
> Subject: RE: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
> To: "wanabidii@googlegroups.com"
> Date: Sunday, April 10, 2016, 5:55 PM
>
> #yiv1989413591
> #yiv1989413591 --
> .yiv1989413591hmmessage P
> {
> margin:0px;padding:0px;}
> #yiv1989413591 body.yiv1989413591hmmessage
> {
> font-size:12pt;font-family:Calibri;}
> #yiv1989413591 Ndugu
> Mkinga
>
> Ninaunga mkono hoja.
> Tuombe Mungu Rais Wetu alione hilo. Na kwa kuongezea Raisi
> angeweza kuwahamasisha Watanzania watoe mawazao yao ni nini
> kifanyike ili hii nchi itoke kwenye hili tope la umaskini.
>
>
> Ajaribu kukusanya haya
> mawazo kutoka nje ya watu wanaomzunguka na walio kwenye
> mfumo kwani walioko kwenye mfumo wamechoka kifikra na
> ubunifu na wanaona vibaya kukubali kuwa wameshindwa.
> Walioko kwenye mfumo wanapigana kufa na kupona kutetea
> walichofanya na wanachofanya wakiogopa kuonekana kuwa
> wameshindwa.
>
> Tunahitaji
> mfumo wa kufikiria nje ya uwigo. Tatizo ni nani asimimie
> hilo zoezi bila kuwa na vested interest. Tatizo kubwa letu
> Watanzania ni kuwa Watanzania ambao wana nia ya dhati kutoka
> rohoni kuboresha na kubadilisha maisha ya watanzania ni
> wachache mno ambao hawatoshi kuleta mabadiliko na mapinduzi
> ya kifikra yanayotakiwa.
>
> Lakini uzuri tumeanza tunazungumza, watu
> wanatusikiliza, wengine tunaandika na wachache wanasoma na
> kidogo kidogo tunapanda mbegu ya mabadiliko na iko siku hizi
> mbegu zitachipua, na kuwa mti wa matunda ambayo nayo yatatoa
> mbegu ambazo nazo zitaanguka ardhini na kuendelea
> kuchipua. Baada ya muda mfupi tu ninaamini tutakuwa na
> mapinduzi ya kiakili, kisaikologia, kiuchumi, na kijamii.
>
> Tusikate tamaa tuendeleaa
> kupambana
>
> Ahsante
>
> Herment A. Mrema
>
> Date: Sun, 10 Apr 2016
> 16:31:09 +0000
> From:
> wanabidii@googlegroups.com
> To:
> wanabidii@googlegroups.com
> Subject:
> [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua
>
> Kati
> mijadala iliyochukua muda wa wengi hapa katika majukwa mengi
> ni:
> Je,
> Tanzania inaweza kujitegemea ghafla leo baada ya kuwa
> tegemezi kwa miaka yote?
>
>
> Ukifuatilia utagundua kuwa watu wengiwasio na Elimu ya
> uchumi ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuelezea
> kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea kwa 100% hata kuanzia
> leo. Lakini
>
> wataalam wa uchumi na viongozi wa serikali wameeleza kuwa
> Tanzania bado
> tunahitaji kusaidiwa ili kuweza kusimama kwa miguu yetu kwa
> 100%. Baadhi
> ya wachumi na watendaji wa serikali wamelisema hilo wazi na
> wengine
> wamenyamaza kimya kwa kukosa ujasiri wa kutamka kile
> wanachokijua kuwa
> Tanzania haina uwezo wa kujitegemea kwa 100% kwa ghafla,
> japo uwezo huo
> upo kwa siku za mbeleni kama tutakuwa na mipango thabiti.
>
>
>
> Magufuli alipozungumzia kuhusu kujitegemea alitoa kauli
> tata, alisema
> Tanzania ina uwezo wa kujitegemea, na ilistah
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment