WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea Nkya
Mmoja wa watu waliosoma makala yangu Raymond Mauki, makala niliyoandika kwamba CCM ilimtoa Edward Lowassa kafara kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond ili chama hicho kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa na CCM ni chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu maswali mawili.
Kwenye malaka hiyo iiliandika kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi hapa nchini kuwa maskini. Nilitoa mfano wa serikali ya CCM kuwa fisadi kusimamia wizi wa fedha za umma kwenye akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana 2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni serikali ya CCM yenyewe ilihusika lakini walidanganya umma kwamba muhusika ni Edward Lowassa.
Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa fisadi wa Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona. Nilisema pia kwamba hivi sasa nchi imejaa ufisadi unaofanywa na watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo hata mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli wanayejidai ni mtu msafi akichaguliwa yerikali yake italazimika kufanya ufisadi penda asipende. Na yeye mwenyewe Magufuli amekaririwa akisema kwamba ataika mfano marais waliomtangulia.
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa fedha za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba ni malofa na wapumbavu ni lazima wananchi wafanye mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025 kwa kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba .
Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu ni haya ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?
Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao kupitia uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni mkubwa na muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao wakijitokeza kusikiliza kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga kura na wakaipigia kura UKAWA wataleta mabadiliko. Hivyo kila mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze kitambulisho chake cha kupiga kura(kichinjio).
Afanye hivyo kwa kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako (ni silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi au mgambo hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n chako. Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya kanga, kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.
Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake waipigie kura UKAWA kwa sababu ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu zinazogusa maisha ya wanawake moja kwa moja.
Kwanza UKAWA wana agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo Kikuu. Hili ni muhimu kwa sababu elimu ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa zima.
Pili UKAWA wana agenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Moja ya jambo muhimu katika Katiba ya wananchi ni kuweka uhusiano mpya kati ya viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi kujitajirisha kwa mali za umma huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.
Fedha za nchi zinazotafunwa na watawala wachache zitatumika kwa mfano kuboresha elimu, huduma za afya,maji, umeme, kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya watu ajira. Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya kuhakikisha uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.
Kashalika Katiba Mpya italeta usawa wa kweli wa kijinsia nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri uchaguzi wa 2020 kwa kutoa idadi sawa wanawake na wanaume madiwani kwenye kata na idadi sawa ya wabunge wanawake na wanaume majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.
Utaratibu wa viti maaluma utatumika kwa watu wenye ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa mbunge mwanamke na mwanaume. Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a kweli kuhusu usawa wa kijinsia unaotakiwa Tanania ili nchi yetu na watu wake waondokane na umaskini.
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama vinajinasibu eti vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea mwenza au mgombea wa Urais. Ni sawa lakini hiyo ni geresha ya danganya toto kwa sababu kwa mfumo wa sasa ambapo usawa wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba wanawake wanatumika tu kama wanaume kupitisha sheria na sera za maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.
Usawa wa jinsia wa kweli na wa kudumu hauwezi kufikiwa hapa nchini bila Katiba Mpya ya wananchi kuandikwa na kuweka misingi ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya kugombea na kushinda sawa na wanaume majimboni na kwenye kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake na wale wote wanaofanya kampeni UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli kwamba wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague UKAWA ndio waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.
Swali la Pili: Watanzania tufanye nini kuzuia CCM kuiba kura uchaguzi wa mwaka huu 2015? Mimi napendekeza yafuatayo:
Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM mnaouchukia kuona watu wengi wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri wa kupindukia, kinachotakiwa kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo wa kubadilisha maisha ya kimaskini wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza kitambulisho chako (kichinjio) na siku ya kupiga kura tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA kwa sababu wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA wana ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini unaotengenezwa kwa serikali ya CCM kukwapua fedha za wananchi na jeuri ya kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM kujifanya chama dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura maana hakuna ukombozi wenye kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila wananchi wenyewe kushiriki kuleta mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la kura.
Umaskini wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa ajira ya kuwapatia walio wengi wasio watumishi wa umma fedha za kujikimu. Watumishi wengi wa umma mfano walimu, madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa mshahara isiyokidhi mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.
Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda mrefu. Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache wakiugua wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa nchi za nje.
Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo mbinu mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu wenye ubora na wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile wanaheshimiwa, kuthaminiwa na kulipwa vizuri.
Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya dola hasa polisi kutumika kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi yetu bado iko kwenye ukoloni.
Pili: Kila kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi wengi anapaswa kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji, mtaa , polisi , mgambo au mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.
Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili wasipige kura ya kuwaletea mabadiliko kwa kuikataa CCMambayo utawala wake umewafanya wananchi wengi kuwa malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali ya CCM wakijilipa fdha za wananchi na kupata utajiri wa kukufuru.
Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni maana pengine hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki kuu ambazo nyingine zilibebwa kwa tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na kama ni nguo vaeni ni mali yenu lakini usimpe tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini wataifanya miaka 5 ijayo.
Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA awaeleze wananchi ukweli huu. Wananchi wakiujua ukweli kuhusu chimbuko la matatizo yanayowakabili kuwa ni serikali ya CCM kama taasisi kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka, wananchi wataelewa na watapiga kura kikamilifu kuleta mabadiliko—kuchagua UKAWA kuendesha serikali tuone miaka mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini. Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu na Katiba Mpya uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama kwa kuzingatia sera za maendeleo umaskini unaowasumbua Watanzania wengi hautaondoka nchini.
Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na maisha ya mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki, hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi ikamilike. Maana kwenye uchaguzi wakala ukipepesa ukipepesa macho kidogo tu wajanja wanachakachua.
Nne: UKAWA kuweka mawakala makini ambao siyo mamluki wa CCM-- watu jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio wengi wanaoteseka na maisha duni. Kura ni hesabu kwa mtu asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu ni rahisi sana KUDANGANYIKA maana hataweza kusoma na kuelewa kilichoandikwa.
Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza kuvumilia njaa ikibidi kukaa bila kula na kunywa kwa zaidi ya saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa kuendekeza ulaji na unywaji wakiwa kazini kwenye vituo vya kupiga kura, waliagiza vinywaji na vyakula na vinywaji. Lakini wajanja waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na walikuja kuamka uchaguzi ulikuwa umewisha na kura za mgombea wao ambaye alikuwa anapendwa na watu amekwishaibiwa kura zake wakiwa usingizini.
Ninachosema hapa ni kwamba uchaguzi ni wa mwaka huu ni mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo wanaCCM wengi tu) na kikundi cha watawala wa CCM wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.
Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini kwetu.
Sita: UKAWA wahakikishe inawaelekeza mawakala wake mambo muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura. Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha wanachukua kwa usahihi matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.
Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni kuhakikisha waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na Rais hawachakachui matokeo. Umma ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna kinachoshinda nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Ninaruhusu Makala hii ichapishwe na yeyote anayetaka. Lengo ni kuelimishana ili kuleta mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM
Mama Nkya nimekuelewa sana
sana na sana, siku zote nimekuwa nikifuatilia harakati zako
ila sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa kuwaambia
watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake
haijalishi yupo wapi, ana nafasi gani kwa jamii au yupo
upande gani kisiasa. Ulichokiandika ni very simple and very
true hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga ulichokiandika
tena wakitumia data za uongo kabisa. Ni ukweli uliowazi kuwa
watanzania wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na nashukuru
yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo kimoja cha
redio(clouds fm), watanzania wa leo wanahitaji mabadiliko
chanya na wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya mawili,
Je, tufanye nini watanzania lei hii ili kuzuia kabisa
mchezo wa ccm kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu?
Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za
leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?
Asante
na ubarikiwe sana,
RAYMOND
MAUKIKIGAMBONI,
DAR ES SALAAM.
From:"ananilea nkya
ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
[Attachment(s) from ananilea nkya
included below]
LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO
Na Ananilea Nkya
Nimeandika hoja hii baada ya kusoma na kusikia hoja
zinazotolewa na baadhi ya Watanzania kwamba eti CHADEMA ,
CUF, NCCR-Mageuzi na NLD -vyama vinavyounda UKAWA kwa
kumsimamisha Edward Lowassa kugombea Urais vimepoteza
usafi wa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi.
Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA kumsimamisha
Lowassa kuwa mgombea urais wamecheza kama Pele. Tena
wanastahili pongeze kubwa maana walitumia akili kali na
saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa ilicheza
mchezo mchafu kisiasa kuwatumia wapinzania kumpakazia
Lowassa ufisadi na hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
Lowassa kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha ufisadi.
Wanaodhani CHADEMA na UKAWA wamekosea pengine hawajaelewa
kuwa tangu upepo wa mabadiliko wa kukataliwa mfumo chama
kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu ulipoanza kuvuma
duniani kote mwishoni mwa miaka ya 1980, baadhi ya wanaCCM
hawajakubali kwa dhati kabisa ukweli huo na kuamini kwamba
CCM inaweza kupunzishwa kuongoza nchi angalao kwa miaka
mitano.
Hasa baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
imebaki na viongozi ambao hawako tayari kutumia ujasiri
kuongoza mabadiliko kwa amani. Baadhi ya vongozi wanaojali
zaidi maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli kama
hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere kuwa bila CCM
imara—Tanzania itayumba kujidanganya wenyewe na kudanganya
wananchi.
Wanasahau kwamba Mwalimu Nyerere kama mwanafalsafa na
mwanasiasa makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri kwa
faida ya taifa na wananchi kulingana na hali halisi ya
wakati husika kwa kusoma upepo wa wananchi. Kwa mfano
Nyerere aliwahi kusema CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
na Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
madarakani.
Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1992 alionyesha mfano kwamba
maslahi ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa wanaCCM wengi
waliokuwa wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi --kuharakisha
maendeleo ya wananchi.
Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila mwanaCCM
anayechaguliwa kuwa Rais, kwa kuogopa kulaumiwa kwamba eti
kama CCM haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
lawama za kufanya CCM iondoke madarakani, serikali zote za
CCM baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka duaniani zimekuwa
zinajihusisha na ufisadi.
Serikali ya CCM imekuwa ikikwapua kwa wizi wa wazi mabilioni
ya fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi zinafanyika kama
geresha tu—kudanganya wafadhili na mataifa kuwa Tanzania
ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi.
Mfano uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini ya Rais
Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki Kuu Akaunti
ya EPA shilling bilioni 133 ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
madarakani Rais Kikwete.
Mwaka jana 2014 serikali ya CCM chini ya Kikwete ilikwapua
shilingi bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta escrow Benki
Kuu kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda uchaguzi wa
serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaofanyika tarehe 25
Oktoba mwaka huu 2015.
CCM wakishaingia madarakani jambo muhimu kuliko yote Rais na
serikali yake analolifanyia ni kubuni ufisadi wa kuipatia
CCM fedha na mbinu nyingine za kuiwezesha CCM ibaki
madarakani uchaguzi unaofuta. Hakuna kazi muhimu ya
kuwaondolea wananchi umaskini inayofanyika kwa kiwango na
juhudi kubwa.
Kwa sababu hiyo, kikundi kidogo cha watawala, wengi wakiwa
ni kutoka CCM na familia zao wamejikuta wakinufaika kwa kuwa
matajiri kufuru kwa muda mfupi ili hali wananchi wengi
wakibaki maskini na mafukara wa kutupa.
Mfano wabunge (kikundi cha watu wasiozidi 400) wengi wakiwa
ni wanachama wa CCM kila mmoja analipwa si chini ya
milioni 10 kila mwezi kama mishahara, wacha marupurupu na
posho za vikao vya kamati, posho za safari na mamilioni
mafao kila baada ya miaka mitano. Lengo wawe na fedha
nyingi za kununua kura za wapiga kura maskini uchaguzi
unaofuata CCM ibaki madarakani.
Ndiyo sababu kila mwananchi wakiwepo watu muhimu kama walimu
wa vyuo vikukuu na madaktari hivi sasa nao wameamua kuwa
wanasiasa.
Zaidi baadhi ya wanaotafuta madaraka ya kisiasa wanatumia
mbinu chafu sana ikiwa ni pamoja na ushirikina wa kuuwa
watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) waweze kupata nafasi
ya kuingia katika kundi la watawala—kupata utajiri wa
kutisha katika kipindi cha miaka mitano.
Mfamo Wabunge waliomaliza muda wao mwaka huu 2015 kila
mmoja ameondoka na kiinua mgongo zaidi ya shilingi milioni
200. Hii ni kufuru katika nchi inayojinasibu kuwa ni
maskini na inapita huko na huko duniani kuomba misaada!
Hata hivyo kwa kadri ufukara unavyoendelea kuwatafuna
wananchi wengi, na kwa kadri uelewa wa wananchi
wanaoteseka kwa umaskini unavyoongezeka kwamba CCM na
utawala wa serikali yake ndicho chanzo cha umaskini wao,
CCM imebaini kuwa haiwezi tena kushinda uchaguzi kupitia
sanduku huru la kura kwa kutegemea kete moja tu—kununua
wananchi mafukara peke yake.
Hivyo katika miaka ya hivi karibuni CCM imeanza kuendesha
siasa za maji taka—kuchafuana wao kwa wao na hatimaye
wameamua kutoana kafara-lengo kuu likiwa ni kuzuia wananchi
wasitumie sandundu la kura kufanya mabadiliko—kuchagua
vyama vingine kuongoza nchi.
Hivyo Rais Kikwete, hata kama ndani ya umungu wa moyo wake
hakubaliani na CCM inavyotumia ubabe kukataa mabadiliko
kinyume na asili ya binadamu, amekuwa akifanya mambo
kutimiza matakwa ya baadhi ya wanaCCM —kujaribu kuzuia
mabadiliko—ili tu kuepuka lawama- amalize muda wake bila
kuonekana ndiye kasababisha wananchi kuipunzisha CCM uongozi
kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa kufanya hivyo Rais Kikwete amejikuta akiporwa ujasiri
wake aliokuwa nao kama mwanasiasa ambaye Mwalimu Nyerere
alimuamini.
Kumbuka Mwalimu Nyerere alinukuliwa na gazeti la Nipashe na
Majira 26/5/95 akisema baada ya Rais Mwinyi baadhi ya
vijana ambao alikuwa anaona wana nia ya dhati kabisa na
uwezo mkubwa wa kuongoza Tanzania ni Benjamin Mkapa, Jakaya
Kikwete na Edward Lowassa.
Lakini kwa Kikwete kukubali kuyumbishwa na wana CCM wachache
wasiokubali mabadiliko anaonekana kufumbia macho utekelezaji
wa kile mwanafalsafa Mwalimu nyerere alichokisema---kwamba
Watanzania wanataka mabadiliko.
Mfano Rais Kikwete alipata fursa ya kusimamia mabadiliko kwa
kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
Lakini kikundi kidogo cha wahafidhina ndani ya CCM
kilimtisha akajikuta anaweka pembeni ujasiri wake aliokuwa
nao wa kusimamia mabadiliko hayo muhimu kwa maendeleo ya
taifa hili.
Kama uamini jiulize ni kwa nini Kikwete aliachia Bunge la
Katiba lililojaa asilimia 80 ya wanachama likazika Rasimu
ya Katiba ya wananchi pale Dodoma mwaka jana 2014 -- Rasimu
ambayo ingeleta Katiba yakuweka misingi ya kuleta
madadiliko Tanzania—mabadiliko ya kuhakikisha kikundi
kidogo cha watawala hakijitajirishi kwa ufisadi na kujigawia
mali za umma huku mamilioni ya wananchi wakibaki maskini na
mafukara wa kutupa?
Baada ya Kikwete kupoteza fursa ya kuleta mabadiliko kwa
kuandika Katiba Mpya, umma uliofukarishwa umeendelea
kupata uelewa kuwa CCM na serikali yake ndicho chanzo cha
umaskini wao.
Hivyo ili kuendelea kubaki madarakani serikali ya CCM
imekuwa ikijihusisha na ufisadi ili ipate fedha za
kuwarubuni walala hoi wakati wa kampeni za uchaguzi.
Mfano mwaka 1995 Rais Benjamini Mkapa alijikuta serikali
yake ikifanya ufisadi katika akaunti EPA (bilioni 122)
zilizotumiwa na CCM kumuweka Kikwete madarakani.
Ukitafakari utaona kwamba katika ufisadi Tegeta escow,
serikali ya CCM imekapua billion 306 mara tatu ya ufisadi wa
EPA mwaka 1995 ilipokwapua bilioni 122 ili kipate fedha
nyingi zaidi la kuwalaghai wapiga kura mafukara ambao
wameendelea kupata uelewa kuwa CCM inaiba fedha za umma
kununua wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi.
Hivyo serikali ya CCM inayoongozwa na Kikwete ambayo
imeshuhudia nguvu ya wananchi kudai mabadiliko ikiwa kubwa
kuliko wakati mwingine wowote, inajaribu kila mbinu chafu na
safi ili CCM ibaki madarakani baada ya uchaguzi mwaka
huu.
Ndiyo sababu serikali ya CCM kupitia msemaji wa chama
hicho Nape Nnauye imeanza kuwaambia Watanzania kuwa CCM
lazima ishinde uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni kwa
kutumia goli la mkono (wizi au lolote lile chafu).
Zaidi Rais Kikwete amefikishwa mahali pabaya
kulazimika kubuni mchezo mchafu kujaribu kuwadanganya
Watanzania kuwa eti CCM na serikali yake ni safi,
haijihusishi na ufisadi unaofukarisha wananchi isipokuwa
wanachama wachache wa CCM ndio mafisadi.
Ili kujaribu kutafuta kujenga uhalali wa CCM kubaki
madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka huu 2015, Kikwete
amejikuta akilazimika kumtoa kafara Lowassa kwa
kumpakazia ufisadi wa Richmond.
Wananchi wanauliza kama Lowassa alikuwa ndiye mhusika wa
Richmond ni kwa nini Spika wa Bunge Anna Makinda (mmoja
wa watawala wa CCM), hakuagiza tume ya Bunge iliyoongozwa
na Mbunge wa CCM Harrison Mwakyembe kumhoji Waziri Mkuu
Edward Lowassa?
Pili wananchi wanahoji kama CCM haijamtoa Lowassa kafara
kwa kumbebesha ufisadi wa chama hicho ili kupumbaza hasira
ya wananchi dhidi ya ufisadi wa CCM kwenye uchaguzi wa
Oktoba mwaka huu 2015 ni kwa nini Rais Kikwete alikubali
Waziri wake Mkuu Edward Lowassa ajiuzulu kwa ufisadi wa
Richmond 2008 wakati ufisadi wa kutisha ulifanywa na
serikali ya CCM kwenye akaunti ya Tegeta escrow 2014
Kikwete aliwatetea mawaziri waliogawiwa fedha hizo na Ikulu
ilikuwa ndiyo mtuhumiwa namba moja?
Mimi si mwanasiasa wa chama chochote cha siasa hapa nchini
ninachoangalia ni chanzo cha umaskini wa wananchi wengi
Tanzania.
Ndiyo sababu Watanzania wengi nikiwepo mimi mwenyewe kwa
sababu tulipewa habari nusu nusu zilizotolewa kimkakati na
serikali ya CCM kuhusu kashfa ya Richmond kumpakazia
Lowassa ufisadi, tulipubwazwa tukaisaidia CCM kumchafua
Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond.
Lakini baadhi ya wananchi walianza kujua kuna ukweli
uliofishwa kuhusu Richmond pale TV moja ilipokuwa imemwalika
Lowassa aotoe yake ya moyoni live siku chache baada ya
kujiuzulu, lakini kipindi hicho cha TV kikafutwa ghafla.
Hata hivyo ukweli huo umekuja kujulikana mwezi Julai mwaka
huu Lowassa alipotoa hadharani baada ya kuachana na CCM na
kujiunga na CHADEMA.
Sasa wananchi wamefahamu kuwa CCM chini ya serikali ya
Rais Kikwete iliamua kumtoa Lowassa kafara kwa kumpakazia
ufisadi wa Richmond ili kuiokoa CCM isiadhibiwe vikali
na wananchi kwenye sanduku huru la kura –kwa ufisadi
alinawasababishia umaskini na ufukara.
Ndiyo sababu hivi sasa CCM na baadhi ya wanahabar
wanapakazia CHADEMA na UKAWA kuwa eti ni mafisadi
baada ya kumpokea Lowassa (kafara wa CCM) na kumpitisha
kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Isitosha hivi sasa kikundi cha watawala wachache wa
serikali ya CCM wanahaha na wanamzonga Kikwete azuie
mabadiliko kwa mkono kwa kufanya kila uchafu kupumbaza
Watanzania kwa kutumia kete ya eti Lowassa ni fisadi wa
Richmond hivyo hana sifa ya kugombea Urais wa Tanzania,
bali Magufuli ndiye mtu safi.
Wananchi wenye akili zao wanajiuliza hivi mwenye kashfa za
kifisadi kati ya Lowassa na Magufuli ni nani? Ni Lowassa
aliyepakaziwa Richmond au ni Magufuli aliyeongoza watawala
kujiuzia kwa bei chee nyuma za umma zilizogarimu wanannchi
mabilioni ya fedha?
Wananchi pia wanajiuliza kama Lowassa ni fisadi wa Richmond
ni kwa nini serikali ya CCM haijamshitaki mahakamani miaka
minane tangu ufisadi huo ulipotokea?
Hivyo pengine baada ya Lowassa kutafakari nafsi yake na
kuona kuwa CCM imemtoa kafara asigombee Urais ili kuzuia
mabadiliko, ameamua kufanya maamuzi magumu ya kuhama CCM
--kushiriki kuongoza masikini na mafukara wanaotafuta
mabadiliko.
Lowassa ameamua kutekeleza alichokitabiri Mwalimu Nyerere
kwamba CCM isipokubali kuongoza wananchi wapate mabadiliko
wanayoyataka—wananchi watayatafuta mabadiliko hayo nje
ya CCM.
Ni dhahiri CCM ilipoteza fursa adimu ya kuongoza wananchi
kwenye kuleta mabadiliko kwa kuandika Katiba Mpya-- kuweka
misingi ya kukomesha mfumo wa utawala unaowezesha watawala
kuwa matajiri wa kupindukia huku mamilioni ya wananchi
wakiwa mafukara na nchi ikinuka aibu ya umaskini wa
kijitakia ikiwa rasilimali nyingi za asili.
Wanaomchochea Rais Kikwete asikubali mabadiliko yachukue
mkondo wake, wameunda timu ya kampeni yanye wajumbe wengi
waliohusika kumpakazia Lowassa ufisadi wa Richmond ili eti
kwenye kampeni waendelee kumpaka ufisadi Lowassa, CHADEMA
na UKAWA wakidhani Watanzania hawana akili ya kutafakari.
Lengo lao ni moja. Wanajua kabisa kuwa kwa kutumia sanduku
huru la CCM haiwezi kuchaguliwa. Wanataka kutumia
kisingizio kuwa CHADEMA na UKAWA imechafuka eti kwa
kumsimamisha Lowassa Urais ambaye CCM imemtoa karafa –
kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond.
Lakini baada ya kupata salamu za wananchi kupitia mafuriko
yao kwenye kumtambulisha Lowassa kwamba wao wanaelewa fisadi
kamili ni CCM, sasa CCM imeshtuka imeanza kutumia polisi
kuwaadhibu wananchi. Pengine baadaye itatumia jeshi
kabisa.
Zaidi imeamua kujaribu kampeni za ardhini -nyumba kwa
nyumba, bila shaka kutumia mabilioni ya fedha serikali ya
CCM ilizokwapua Tegeta escrow kununua shahada na kura za
mafukara.
Kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu ndiko
ufisadi mbaya wa kisiasa unakofanyika—kununua, kutisha na
kuumiza wananchi mafukara.
Swali ni je Watanzania wangapi wapiga kura watakubali CCM
inapopita majumbani mwao kuuza shahada zao kwa sukari,
kanga au fedha hata kama CCM itaamua kumpa kila mpiga kura
shilingi milioni moja?
Ni mpiga kura gani atakayekubali KUDANGANYIKA kwa
kununuliwa na CCM kwa vijizawadi vya fedha nguo KUSALITI
mamilioni ya watanzania wanaoendelea kuteseka kwa ufukara
kila baada ya uchaguzi kwisha na CCM kubaki madarakani?
Wananchi pia wanauliza je mabilioni ya escrow yatawanunua
wajumbe wa NEC ili wavuruge daftari la wapiga kura, au
wachakachue kama uchaguzi wa 2010 au wataharibu daftari la
wapiga kura, mashine na vifaa vya kupigia kura, au
kuchelewesha kwa makusudi kufungua vituo vya wapiga kura
ili kuvuruga uchaguzi CCM ishinde kwa goli la mkono?
Kadhalika wananchi wanauliza wanaomshinikiza Kikwete
asikubali mabadiliko wakiona hilo haliwezekani je watamuua
Lowassa waliomtoa kafara au viongozi wa CHADEMA na UKAWA
waliompokea Lowassa na kumwezesha kufikia azma yake ya
kujitolea kuwatumikia watanzania ili kuvuruga uchaguziwa
mwaka huu?
Wananchi wanauliza maswali hayo baada ya kubaini kwamba
huenda wasiomtakia mema Kikwete astaafu kwa amani
wamejaribu kuwalaghai baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA ili
kujaribu kuvuruga UKAWA – lakini UKAWA kwa vile ni sauti
ya mafukara-sauti ya umma imeendelea kuwa moto mkali wa
nyika dhidi ya CCM.
Hivyo binafsi namshauri Rais Kikwete akubali kuwa baba wa
pili wa Taifa hili baada ya Nyerere kuondoka. Akubali
kusimamia wananchi watumie sanduku huru la kura kwenye
uchaguzi wa mwaka huu 2015 kupata mabadiliko ya uongozi
wanayoyataka.
Wananchi wana imani na UKAWA kwamba wakiingia madarakani
Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi itaandikwa.
Huo utakuwa ni mwanzo wa mabadiliko wanayoyataka
wananchi—kuhakikisha watawala hawajitajirishi kupindukia
kufisadi fedha za wananchi huku wananchi wengi wakibaki
mafukara. CHADEMA na UKAWA wasipotimiza hili na kuonyesha
kwa vitendo maendeleo watakayokuwa wameyaleta kwa miaka
mitano, ni lazima wananchi watatumia sanduku la kura
kuwapunzisha.
Ninaamini ni wenye kutetea maslahi binafsi tu ndiye
atakayemlaumu Rais Kikwete kwamba eti CCM isipochaguliwa
Oktoba 25, Kikwete atakuwa ni chanzo cha wananchi kuamua
kuipunzisha CCM kwa miaka mitano.
Nitakuwa wa kwanza kuwapinga watu hao na kumtetea Kikwete
hata kama ni kwa kuamua kuingia kwenye siasa kwa kujiunga
na CCM .
Hakika Rais Kikwete ukisimamia wananchi wazungumze kuhusu
hatma ya uongozi wan chi yao kwa kutumia sanduku huru la
kura bila CCM kuingiza mkono mchafu, wewe mwenyewe
ukistaafu utaishi kwa amani na furaha huku baadhi yetu
tukikuona kama baba wa Pili Taifa taifa hili, baada ya
Mwalimu Nyerere.
Mwisho ninaruhusu yeyote anayetaka kuchapisha au kutangaza
redioni natelevisheni niyoyoyaandika hapa TV au kuchapisha
na kuwasambazia Watanzania wote popote walipo ujumbe huu
afanye hivyo. Wanawaza kuwasambazia watu mitaani,
kwenyemikutano ya kampeni, mashuleni vyuoni popote
pale—lengo likiwa moja—sote Watanzania tuujue ukweli
kuhusu ufisadi na mchango wake katika kuwafanya Watanzania
waishi katika umaskini. Lakini muhimu kila Mtanzania ajue
hakuna mshindi wa kujisifu—mshindi ni nchi yetu Tanzania
na Watanzania wote.
MUNGU IBARIKI YANZANIA.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
__._,_.___
Attachment(s)
from ananilea nkya | View
attachments on the web
1 of 1 File(s)
LOWASSA KAFARA WA
CCM.docx
Posted by: ananilea nkya
<ananilea_nkya@yahoo.com>
Reply
via web post
•
Reply to sender
•
Reply to group
•
Start a New
Topic
•
Messages in this
topic
(1)
Visit Your Group
New Members
2
• Privacy • Unsubscribe • Terms of Use
.
__,_._,___
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment