Wednesday, 30 September 2015

[wanabidii] NATHAN MPANGALA ‘KIJASTI’ KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA UCHORAJI VIBONZO KESHO


Mchoraji vibonzo maarufu nchini Tanzania, Nathan Mpangala, ameandaa mazungumzo ya wazi yatakayofanyika katika Viwanja vya Nafasi Art Space, Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, kesho (Ijumaa) ambapo atazungumzia maisha aliyopitia katika vyombo mbalimbali vya habari akiwa kama mchoraji vibonzo.

 

Ili kunogesha tukio hilo, wahudhuriaji watapata nafasi ya kuuliza maswali au kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali atakayogusia.

 

Mazungumzo hayo yana malengo makuu matatu;

 

(i)            Kueleza maisha aliyopitia kama mchora vibonzo.

(ii)           Kukutana ana kwa ana na ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake                 wa vibonzo kwa ajili ya kufahamiana zaidi.

(iii)          Darasa huru kwa wachora vibonzo wanaochipukia kusikia maisha                       aliyopitia ili kuwatia moyo wafike alipofikia au kupita.

 

Mazungumzo hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio yataanza saa 10 alasiri ambapo watu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

 

Wakati huohuo, Mpangala ametoa rai kwa wachoraji vibonzo wote hasa waishio Dar es Salaam, wakongwe na chipukizi kuhakikisha wanahudhuria tukio hilo kwani ni fursa nzuri ya kubadilisha mawazo na kusemea taaluma yao.

 

Kwa maelezo zaidi 0713 262 902.

 


Nathan Mpangala
Editorial Cartoonist | Comic Artist | Illustrator | Animator | Blogger
Editorial Cartoonist: ITV Tanzania
Founder: Wafanye Watabasamu Initiative
P. O Box 7022,
Dar es Salaam,
TANZANIA.

Phone: +255 713 262 902

Links:

0 comments:

Post a Comment