Mgombea wa Urais kupitia UKAWA analia lia kumuomba Mbowe aje aongeze nguvu kwenye kampeni zake, inamaanisha nini? Kwangu ni vitu vitatu ama vinne vifuatavyo: cha kwanza, mgombea wa Urais wa UKAWA anahisi kama ametelekezwa na Mwenyekiti wa Chama chake na kwamba ana hisia kuwa Mbowe amepoteza imani ya ushindi, cha pili, Mbowe amebanwa sana jimboni na hivyo karudi kuimarisha jimbo ili asijekosa yote na kwamba haamini tena kama kuna uwezekano wowote ule wa kushinda Urais kwa mwaka huu. Hivyo, bora nusu shari kuliko shari kamili; cha tatu, mgombea wa Urais wa UKAWA hana imani na wanaomfanyia kampeni (akina Zero, Mgeja, Msindai, Masha et al) na yeye mwenyewe hana msuli wa kujifanyia kampeni (hotuba alizokuwa akitoa walau kwa dakika 6 sasa zimekuwa za dakika 1: 08 [ya jana]), na ya nne, ukweli kwamba hatutegemei mgombea wa Urais aanze kulia lia jukwaani mbele ya hadhara ya Hai kumtaka Mwenyekiti wa chama chake aje kwenye kampeni za Urais kuongeza nguvu huku angeweza kulizungumza hilo kwenye vikao vyao vya ndani vya tathmini (CP) inamaanisha kuwa Mwenyekiti amesusa na pengine ni kwa sababu alichokitarajia kutokana na mazungumzo yao hakijatokea...
Acha yote haya yatokee, kwa vyovyote vile, hili moja ni la uhakika, kwamba, kampeni ya CCM imeimarika, mgombea wake Ndg.#MagufuliMtendaji anaendelea na #HapaKaziTu, ana #Magufulika, na sisi wapambe wake tunamagufulika tu kumuunga mkono, nayo imekuwa viral, na hii inaashiria mafanikio makubwa zaidi ya haya yanayojionesha kwenye tafiti mbalimbali; wakati huo huo kampeni ya UKAWA iko hoi bin taabani na mgombea wake amechoka sana mpaka anachanganyikiwa kiasi cha kupotea podium pamoja na mengine ya kusikitisha na kufedhehesha yanayomtokea, na mpaka kufikia mwisho wa kampeni, CCM itakuwa ina uhakika wa ushindi wa zaidi ya asilimia 70!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment