Lowassa akikumbuka kutubu, atasema nahili
KWA muda mrefu nimekaa kimya kusikiliza watu wakizungumza,na hasa mgombea urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne, vyaNCCR-Mageuzi, CUF na NLD chini ya umoja wao maarufu kwa jina la Ukawa, EdwardLowassa, na wapambe wake kuhusu ujenzi wa shule za sekondari za kata.
Kinachozungumzwa ni kwamba Lowassa ndiye mwanzilishi washule hizo huku baadhi ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 23,wakitangaza kuwa bila Lowassa wasingepata nafasi.
Vijana hao wanafikiri hivyo kwa madai kuwa ni Lowassa ndiyealiyekuna kichwa kubuni wazo hilo la kuanzishwa kwa shule za kata ambazo wanaUkawa walipokuwa katika Bunge la Tisa na hata la 10 walikuwa wakiziita shule zayeboyebo kwa madai kuwa hazifai kwa lolote lakini baada ya Lowassa kuingiaUkawa, sasa ni kete yao
kisiasa.
Maneno ya Lowassa na wapambe wake kuwa ndiye aliyefanya kazihiyo ni kupotosha ukweli na kufuta historia halisi ya nani hasa mbunifu wa wazohilo, mwezi Machi mwaka 2006.
Chimbuko la shule za kata
Kiini cha wazo la kuanzishwa kwa shule za kata kinahusishahistoria ndefu tangu utawala wa awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa, MwalimuJulius Nyerere, kupitia tume ya kupitia mfumo wa elimu ya Tanzania aliyoiundaNovemba, mwaka 1980, na kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwaka 1981.
Tume hiyo ilijulikana kama Tume ya Jackson Makweta, kamaMwenyekiti na Katibu wake alikuwa ni Musel Muze, na miongoni mwa wajumbe watume hiyo ni pamoja na maprofesa watatu na wajumbe wengine takriban tisa.
Sitaki kwenda kwa undani kuhusu kazi au hadidu rejea za tumehiyo kwa leo, lakini mojawapo ya mapendekezo ya msingi yaliyozaa wazo lakuanzishwa kwa shule za kata ni taarifa ya tume hiyo iliyokuwa na kurasa 354nje ya viambatanisho, iliyolenga kufanyia marekebisho mfumo mzima wa elimu wanchini, kwa kupanua kwanza elimu ya sekondari.
Katika mapendekezo hayo mojawapo ya hatua iliyopendekezwa naTume ya Makweta ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 1985, kila tarafa iwe nashule ya sekondari na baadaye kila kata ziwe na shule ya sekondari. Pia tumeilipendekeza baada ya miaka mitano, yaani mwaka 1990 upanuzi wa elimu ya juuuanze rasmi kwa kasi.
Katika pendekezo hilo, Tume ya Makweta iliitaka serikalikupandisha 'ngazi' vyuo vya ufundi vilivyokuwa maarufu kipindi hicho kama DarTec, Arusha Tec, Mbeya Tec, Musoma Tec kuwa vyuo vikuu, ili kuongeza nafasi yaelimu ya juu na kufanya Tanzania iendane na mataifa mengine katika elimu yajuu.
Kwa kuwa wakati huo kulikuwa na chuo kikuu cha umma kimojatu, Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na tawi lake dogo la Morogoro, tume piailipendekeza tawi hilo lipanuliwe kuwa chuo kikuu kinachojitegemea kazi ambayoilizaa matunda ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), mwaka1984.
Yapo mengi yaliyojiri katika taarifa ya Tume ya Makwetailiyowasilishwa kwa Rais Julius Nyerere, mwezi Machi mwaka 1982, ikiwamokuhakikisha Kiswahili na Kiingereza ndizo ziwe lugha rasmi za kutumiakufundisha katika ngazi zote ili kuwezesha Tanzania kwenda sawa na mataifamengine. Kwa kuwa sitaki kujadili kazi na utekelezaji wa tume, kwa ujumlasitakwenda mbali zaidi ya hapo kwa kuwa iko siku nitaandika juu ya utekelezajiwa maoni ya tume hiyo kwa wakati muafaka.
Mkapa na mapendekezo ya ya Makweta
Alipoingia madarakani Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa,mwaka 1995 alianza kutekeleza kwa vitendo maoni ya Tume ya Makweta kwa kubuniMpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Elimuya Sekondari (MMES).
Kwa wale wanaojua watakumbuka kuwa MMEM ililenga kupanuanafasi za shule za msingi na kuboresha mazingira ya shule ikiwa ni pamoja nakuwepo kwa vitendea kazi huku MMES, pia ikiwa na lengo hilo kwa shule zasekondari.
Ili kutekeleza azma yake kwa ufanisi mkubwa Rais Mkapa kamakiongozi wa nchi alielekeza kuwepo kwa awamu ya kwanza ya mipango hiyo yaaniMMEM na MMES, ambapo awamu ya pili iliangukia katika serikali ya awamu ya nne.
Kikwete na ujenzi wa shule za kata
Baada ya Serikali ya Awamu ya Tatu kukamilisha kazi yake nakukabidhi kijiti cha kuongoza nchi kwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya RaisJakaya Kiwete, Novemba 2005, Edward Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Waziri wa Elimu akiteuliwa Magareth Sittana Naibu wake akiwa Mwantumu Mahiza (wote hao wakiwa ni walimu).
Mwezi Machi mwaka 2006 kulifanyika mkutano wa watendaji waserikali katika Hoteli ya Blue Peal, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, kama ilivyo kwa ratiba ya wakubwaLowassa baada ya kufungua mkutano husika iliwadiwa wakati wa kunywa chai, NaibuWaziri wa Elimu Mahiza, alifanya kile kinachoitwa ujasiri kwa kumwomba WaziriMkuu wakati huo kumsikiliza kidogo ili amweleze shida yake kwa niaba ya waziriwake.
Katika maeelezo yake Mama Mahiza alimwambia Lowassa kuwa;"Sisi katika Mkoa wa Dar es Saalam tuna shida, tuna watoto waliofaulu lakinihawana nafasi ya kuendelea na masomo sasa tunaomba kutoa wazo la kuwapatianafasi lakini inahitaji ushauri wako mheshimiwa."
Baada ya maelezo hayo na ufafanuzi wa kina kidogo, Lowassaalimtaka Waziri na timu yake kufika ofisini kwake kesho yake saa nane mchanaili wamweleze kwa undani ni mikakati gani waliyokuwa nayo kuhakikisha watotohao wanaendelea na elimu ya sekondari, baada ya kufaulu lakini hawawezi kusomakutokana na ufinyu wa nafasi za sekondari kipindi hicho.
Nataka niweke wazi kuwa wakati huo, Mkoa wa Dar es Salaamulikuwa na shule za sekondari za serikali tatu tu. Leo mkoa huo una shule za sekondari112.
Ufaulu ulikuwa ni watoto 33,775 sawa na asilimia 71.2 katiya 47,459 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2005 ufauluuliotokana pia na maboresho ya MMEM huku MMES yakiwa bado hayajatekelezwa vyakutosha kwenda sambamba na ongezeko la ufaulu.
Kati ya wanafunzi 33, 775 waliofaulu ni watoto 25,457 tundio waliopata nafasi ya kuendelea na masomo hivyo kufanya wanafunzi 8,300kukosa nafasi ya kuendelea na masomo. Sitaki kueleza kwa undani mjadalauliokwepo kabla ya Mahiza kumvaa Lowassa kuhusu hali hiyo lakini nitagusia tukwa ufupi.
Kabla ya Naibu Waziri Mahiza kumvaa Lowassa, aliwaitawabunge watatu wa majimbo kupitia CCM Mkoa wa Dar es Salaam ambao wote badowapo, Abbas Mtemvu Jimbo la Temeke, Iddi Azan Jimbo la Kinondoni na Mussa AzanZungu Jimbo la Ilala, na kuwaambia hali halisi kuwa watoto zaidi ya 8,000wamefaulu lakini wamekosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari na hapo,Mahiza akawaeleza kuwa atamvaa Lowassa kumpa wazo la kuondokana na tatizo hilo.
Jibu la Lowassa kwa Mahiza
Baada ya maelezo hayo ya Mahiza kwenye chai, walipotoka hapowalikwenda moja kwa moja kujifungia ofisini yeye na wataalamu karibu wote wangazi ya juu hadi usiku wa manane, na kuingia tena alfajiri kwa ajili yakuandaa kile ambacho Waingereza wanakiita "paper" ya kwenda kwa Waziri MkuuLowassa saa nane mchana.
Takwimu zinaonesha kuwa saa 8 kamili mchana Magret Sitta,Mahiza na watalamu wao walitinga kwa Lowassa kuwasilisha paper ya nini tatizona ni nini wanachotaka kufanya kukabiliana na tatizo.
Walichowasilisha kwa Lowassa
Kwanza walitoa takwimu za ufaulu wa wanafunzi wa shule zamsingi kwa nchi nzima wakiainisha kila mkoa kuanzia waliofanya mtihani,waliochaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari na waliokosa nafasi kutokana naukosefu wa shule za sekondari.
Pili walitoa takwimu maalumu kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekeyake kutokana kuwa na idadi kubwa zaidi huku serikali nzima ikiwa katika Jijihilo kubwa Afrika Mashariki. Walitumia mfano wa Dar es Salaam kutaka kujengahoja yao ambayo kiini chake kilikuwa ni Mahiza kutaka kufanya mambo mawili.
Jambo la kwanza alilopendekeza Mahiza kwa Lowassa ni kuombakubadilishwa kwa sheria ili Wizara ya Elimu na Ufundi iruhusiwe kutumia fedhaza MMES awamu ya pili (MMES 2) kujenga shule mpya za sekondari kwa haraka iliwanafunzi wote waliokosa nafasi waendelee na masomo badala ya fedha hizokutumika kuboresha shule za zamani na kuwalipia ada watoto wanaotoka katikakaya masikini.
Pili alipendeleza wananchi wachangie kufyatua matofaili nakukusanya mawe, halmashauri za wilaya zichangie usafiri huku serikali kuukupitia MMES 2 ikipeleka fedha kwa ajili ya mabati, saruji na misumarikukamisha madarasa hayo.
Wakati huo MMES awamu ya pili ilikuwa na lengo la kujengashule 1,600 katika kipindi cha miaka mitano nchi nzima hatua ambayo badoisingesaidia kutatua tatizo kubwa lililokuwa limekumba taifa kwa wakati huolicha ya idadi hiyo kuwa ndogo mno kwa mahitaji ya nchi.
Mahiza alipata ujasiri huo kwa kuwa wakati huo alikuwaamemaliza kujenga shule ya sekondari ya sayansi kuanzia kidato cha tano hadicha sita, ikiwa na vitu vyote Bagamoyo, kwa mfumo wa ushirikiano kati yaserikali na wananchi hivyo alikuwa na uzoefu kuhusu kile alichopendekeza kwaLowassa.
Shule kama hiyo aliyojenga Mahiza zilitakiwa kujengwa katikakanda zote 11 za
elimu nchini japo leo sitaki kujadili kama zipo kweli auimebakia hiyo ya Mahiza peke yake.
Kutokana na 'paper' hiyo Lowassa aliguswa na mpango huo nakutoa ruhusa kwa Wizara ya Elimu kuanza kutekeleza mpango huo japo ilimchukuamuda mrefu kumwelewa Mahiza.
Kwa ufupi huo ndio mwanzo wa ujenzi wa shule za sekondari zakata, sasa swali langu la msingi hapa ni je, kati ya Mahiza kwa maana ya Wizaraya Elimu na Lowassa, nani aliyeanzisha shule za sekondari?
Nataka Lowassa atuambie ukweli kuhusu hili na akiwa kamamkristo mzuri atubu katika hili. Lakini pia awaombe radhi Watanzania kwakujitwalia sifa isiyomhusu bila kuwataja wahusika wakuu.
Lowassa angesema kuwa yeye ni miongoni mwa watendaji waserikali walioshiriki kuhimiza ujenzi huo wala isingekuwa shida na walanisingediriki kushika kalamu yangu inayopatika kwa nadra siku hizi kutokana nakubanwa na majukumu mengine ya kitaifa, kuandika juu ya hili.
Najua, natambua na nasema wazi kuwa mwaka 2007 baada yaBunge la mwezi wa pili, Lowassa kama Waziri Mkuu alimsaidia Rais Kikwetekuratibu mgawanyiko wa mawaziri wote nchi nzima kusimamia uamuzi wa Wizara yaElimu kuhakikisha shule hizo za kata zinakamilika na watoto wote waliofaulukupata nafasi ya kuendelea na masomo wanapata fursa hiyo.
Uamuzi huo pia ulitokana na malalamiko kutoka kwa wabungewengi kuwa watoto wamefaulu hawana pa kwenda, mimi nilikuwepo bungeni naanayenipinga akachukue hansard (kumbukumbu rasmi) za Bunge na orodha yawaandishi wa habari waliokuwapo wakati huo bungeni.
Lakini nikimnukuu Lowassa na mpambe wake namba mbiliFrederick Sumaye, ambaye alikuwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa miaka 10, alisema wazi kuwa hakuwa na nguvu ya kufanya lolote ndio maanawalishindwa
kufanya mabadiliko wanayotaka sasa.
Sasa swali langu kwa Lowassa kama kweli hiyo ndio halihalisi kumbe hata usimamizi wa mawaziri kwenda mikoani ilikuwa amri ya RaisKikwete na si yeye?
Na kama sivyo basi yeye Lowassa na Sumaye watueleze wazikuwa kama walikuwa na mamlaka makubwa ya kuanzisha vitu kama hivyo navikafanikiwa kumbe yale yote wanayodai walishindwa ilikuwa ni uzembe wao, hivyoLowassa hafai kuwa Rais kwa kuwa alishindwa?
Na kama sivyo basi, mafanikio ya shule za kata tumpeMwantumu Mahiza/ Wizara ya Elimu na Rais Kikwete kama kiongozi wa nchi,aliyetoa kibali cha kubadilishwa kwa sheria, taratibu na kanuni za matumizi yafedha za MMES -2. Mimi nasubiri Ikulu ya sasa kabla ya kuingia Rais mpya, basiRais Kikwete ampe Mahiza tuzo ya ubunifu na kutekeleza maoni ya Tume ya Makwetavinginevyo mnaficha ukweli wa historia.
Tusisahau kuwa moja ya pendekezo la Tume ya Makweta ambayoMahiza alisaidia ubunifu katika utekelezaji ni upanuzi wa elimu juu yaani vyuovikuu kuanzia mwaka 1990. Kazi hiyo imefanyika na leo kila mmoja anashuhudianafasi ya elimu ya juu. Sasa tunapigania ubora wa elimu na si nafasi ya elimu.
Nimalizie makala yangu kwa kusema tufanye siasa kwa lengo lakuomba ushindi lakini tuwaambie Watanzania ukweli tukimhofia Mungu tunayemtajakuwa yuko pamoja nasi kila siku, kwani iko siku tutajibu kila neno tunalotamka.
Tusisahau kuwa kadri tunavyotumia udhaifu wa Watanzaniawalio wengi kutojua kufanya utafiti wa mambo muhimu na kuwaaminisha uwongo kamahuo kwa maslahi ya kwenda Ikulu, ndivyo tunavyozidi kubomoa taifa badala yakujenga kwa kuwa
tutakuwa na wananchi wengi wasiojua ukweli kuhusu nchi yao namatokeo yake ni kukosekana kwa uzalendo kwa kuwa hawajui historia halisi yamambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayowahusu.
Siasa za uwongo, za ubinafsi kama hizi ndizo zinatufanyatuamini kuwa Kenya na Uganda wanatuzidi kwa kila kitu jambo ambalo si
kweli.Nimeshuhudia mara nyingi wataalamu kutoka Kenya na Uganda wakitiririka Mamlakaya Mawasiliamo Tanzania (TCRA) kuja kujifunza vitu na mbinu mbalimbali kuhusuuendeshaji masuala ya mawasiliano na teknolojia mpya hapa kwetu.
Nimeshuhudia vijana wa Tanzania wakibuni mbinu za kisasajinsi ya kutumia teknolojia kama Maxmalipo inayoongoza, lakini leo ukimuulizakijana wa Tanzania kuhusu ubunifu huo, atakwambia ukitaka kujua mambo mengikuhusu teknolojia nenda India au Afrika Kusini. Kisa kajazwa uongo na wanasiasawanaojitafutia ufalme. Tuache siasa za uongo tuseme ukweli, tujenge taifamadhubuti kwa maslahi yetu sote. –
Chanzo Raia Mwema
0 comments:
Post a Comment