Hizi hazikuletwa na utalii wa JK. Hata maelezo ni kutokana na kuoekana Tz inapiga vita rushwa. Tuneweza kuzipata bila rais kwenda huko--------------------------------------------
On Mon, 9/28/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Stop press: Tanzania yapeta tena katika mpango wa kupata mabilioni ya MCC
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 28, 2015, 4:39 PM
Hii ni moja tu ya
faida za safari za rais Kikwete nchi za nje
On Sep 28, 2015 2:16 PM,
"'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Stop press: Tanzania yapeta tena katika mpango wa
kupata mabilioni ya MCC
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sasa ni Rasmi: Tanzania kupata mabilioni mengine ya MCC
·-Yafaulu mtihani wa kupata bilioni 992.8 za kuboresha
sekta ya umeme
·-Yafanikiwa baada ya kutimiza masharti yote likiwemo la
kupambana na rushwa
·-Zitaanza kutolewa mwakani baada ya kupigiwa kura na Bodi
ya MCC
Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili
ya fedha za
maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la
Millennium Challenge
Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na
kunufaika na
mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC
kupiga kura ya
kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa
MCC-2.
Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015,
kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, na
Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano
uliofanyika katika
Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa
na watumishi
waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais
wa
Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria
shughuli za
mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
"Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania
imetimiza
masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa
MCC - 2, ikiwa
ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania
inachukua hatua za
dhati kupambana na rushwa," Bi. Hyde amemwambia Rais
Kikwete na viongozi
wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa
Zanzibar,
Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.
Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika
mkutano wake
wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake,
Waziri wa Mambo
ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu
kipengele pekee
kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC
kuwa ni
kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua
hatua stahiki
kukabiliana na janga hilo la rushwa.
MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza
masharti ya
kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za
maendeleo na pia
imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC
imeridhishwa na
hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.
Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi
duniani, fedha
za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na
pia nchi
husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo
ambayo
inaitaka igharimiwe na fedha hizo.
Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na
Waziri wa Fedha
wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi
wa Biashara
wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la
Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa
anaikaimu Bwana
Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa
Taasisi ya
International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.
Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani
katika Tanzania
wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC-1.
Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi
kupelekewa
muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo
chini ya
mpango wa uwekezaji wa MCC-2 yatakwenda katika kuboresha
huduma za umeme
katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika
vijiji vingi
zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa
wanapata
umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya
asilimia hiyo
imetokana na msaada wa MCC-1.
Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi
cha dola za
Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa
kutilia
maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni
1.46) ambazo
zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata
jumla ya dola za
Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika
kipindi cha
miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa
mwakani, 2016.
Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho
kilikuwa kiasi
kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya
Mpango huo
wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2
Tanzania itakuwa
ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za
maendeleo chini
ya MCC duniani.
Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga
Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na
Namtumbo-Songea-Mbinga.
Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za
maji kwa
ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika
kusambaza umeme
katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara.
Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya
kusafirisha
umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania
Visiwani na pia
zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na
baadhi ya
barabara za Unguja kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Septemba, 2015
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment