Tuesday, 1 September 2015

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15

Mama Nkya umeshakwisha

On Sep 1, 2015 5:26 PM, "'ananilea nkya' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
WANANCHI WAFANYE NINI  WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea  Nkya

Mmoja wa  watu waliosoma  makala yangu Raymond Mauki, makala  niliyoandika  kwamba CCM ilimtoa  Edward Lowassa kafara  kwa kumpakazia ufisadi  wa Richmond  ili chama hicho  kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa  na CCM ni chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa  kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu  maswali mawili.

Kwenye malaka hiyo iiliandika  kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa  fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi hapa nchini kuwa maskini.  Nilitoa mfano wa serikali ya CCM kuwa fisadi   kusimamia  wizi wa fedha za umma kwenye  akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana 2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni serikali ya CCM yenyewe  ilihusika lakini walidanganya umma kwamba muhusika ni Edward Lowassa.

Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa  fisadi wa Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona.  Nilisema pia kwamba hivi sasa   nchi imejaa ufisadi unaofanywa na  watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo hata mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli  wanayejidai  ni mtu msafi akichaguliwa  yerikali yake italazimika kufanya ufisadi penda asipende.   Na yeye mwenyewe  Magufuli amekaririwa akisema  kwamba ataika mfano marais waliomtangulia.

Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM  kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa fedha za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena  watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba ni  malofa na wapumbavu ni lazima  wananchi wafanye mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025  kwa kutumia sanduku huru la kura  hapo tarehe 25 Oktoba .

Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu   ni haya  ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za  leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?

Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao kupitia   uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni mkubwa na muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao  wakijitokeza kusikiliza kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga  kura na wakaipigia kura UKAWA  wataleta mabadiliko.  Hivyo kila mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze kitambulisho chake   cha kupiga kura(kichinjio).

 Afanye hivyo kwa  kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako  (ni silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi au mgambo  hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n chako.  Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya kanga, kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.

Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake waipigie kura  UKAWA  kwa  sababu  ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu zinazogusa maisha ya wanawake moja kwa moja.

Kwanza UKAWA wana  agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo Kikuu. Hili ni muhimu kwa  sababu elimu ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa zima.

Pili  UKAWA wana agenda ya  kuandika Katiba  Mpya inayotokana na  maoni ya wananchi.  Moja ya jambo muhimu katika Katiba  ya wananchi ni  kuweka uhusiano mpya kati ya viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi kujitajirisha  kwa mali za umma huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.

Fedha za  nchi  zinazotafunwa na watawala wachache zitatumika  kwa mfano  kuboresha  elimu, huduma za afya,maji, umeme,  kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya watu  ajira.   Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya kuhakikisha  uwakilishi wa wanawake  kwenye vyombo vya maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.

 Kashalika Katiba  Mpya italeta usawa wa kweli wa kijinsia nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri  uchaguzi wa 2020  kwa kutoa   idadi sawa  wanawake na wanaume  madiwani kwenye kata  na  idadi sawa ya wabunge wanawake na wanaume majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.

Utaratibu wa viti maaluma utatumika  kwa watu   wenye ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa  mbunge mwanamke na mwanaume.  Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a kweli kuhusu usawa wa kijinsia  unaotakiwa Tanania ili nchi yetu na watu wake waondokane na umaskini.

Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama  vinajinasibu eti  vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea mwenza au mgombea wa Urais.  Ni sawa lakini hiyo ni geresha ya danganya toto  kwa sababu kwa mfumo wa sasa ambapo  usawa  wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba  wanawake  wanatumika tu  kama wanaume  kupitisha sheria na sera za maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.

Usawa wa jinsia  wa  kweli na wa kudumu  hauwezi kufikiwa hapa nchini  bila Katiba Mpya ya wananchi kuandikwa  na kuweka misingi ya kutekeleza  usawa wa jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya kugombea na  kushinda sawa na wanaume majimboni na kwenye kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake  na wale wote wanaofanya kampeni  UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli kwamba  wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague UKAWA  ndio waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.

Swali la Pili: Watanzania tufanye nini  kuzuia CCM  kuiba kura  uchaguzi wa  mwaka huu 2015?  Mimi napendekeza yafuatayo:

Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM mnaouchukia   kuona watu wengi  wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri wa kupindukia,  kinachotakiwa  kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo wa kubadilisha maisha  ya kimaskini wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza kitambulisho  chako (kichinjio)  na siku ya kupiga kura  tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA  kwa sababu  wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA   wana ajenda ya kuandika  Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini unaotengenezwa kwa  serikali ya CCM kukwapua fedha za wananchi  na jeuri ya kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM kujifanya chama dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura  maana hakuna ukombozi  wenye kuleta mabadiliko  katika maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana  katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila wananchi wenyewe  kushiriki  kuleta mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la kura.

Umaskini  wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa ajira ya kuwapatia walio wengi  wasio watumishi wa umma fedha za kujikimu.   Watumishi wengi wa umma  mfano  walimu, madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa  mshahara isiyokidhi mahitaji  ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.

Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda mrefu.  Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache  wakiugua  wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa nchi za nje.

Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina  chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo mbinu  mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu  wenye ubora na  wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile wanaheshimiwa, kuthaminiwa  na kulipwa vizuri.

Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya  dola  hasa polisi  kutumika  kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi yetu bado iko kwenye ukoloni.

Pili: Kila  kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi wengi   anapaswa kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji, mtaa , polisi  , mgambo au  mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa  wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko  ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.

Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili  wasipige  kura  ya kuwaletea mabadiliko  kwa kuikataa CCMambayo utawala wake  umewafanya wananchi wengi kuwa malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali  ya CCM wakijilipa fdha za wananchi  na kupata utajiri  wa kukufuru.

Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula  watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni  maana pengine  hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow  Benki kuu ambazo nyingine zilibebwa kwa  tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na kama ni nguo vaeni  ni mali yenu lakini usimpe tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini   wataifanya miaka 5 ijayo.

Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA  awaeleze wananchi ukweli huu. Wananchi wakiujua ukweli  kuhusu chimbuko la matatizo yanayowakabili  kuwa ni  serikali ya CCM kama taasisi kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka,  wananchi wataelewa na watapiga kura  kikamilifu kuleta mabadiliko—kuchagua  UKAWA  kuendesha serikali tuone miaka mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini. Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu na Katiba Mpya  uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama  kwa kuzingatia sera za maendeleo  umaskini unaowasumbua Watanzania wengi hautaondoka nchini.

Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na  maisha  ya mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki, hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu  wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi  ikamilike. Maana kwenye uchaguzi  wakala  ukipepesa ukipepesa macho kidogo tu wajanja wanachakachua.

Nne:  UKAWA kuweka mawakala makini  ambao siyo mamluki wa CCM-- watu  jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio wengi wanaoteseka  na maisha duni.  Kura ni hesabu kwa mtu asiyejua kusoma,  kuandika  na kuhesabu ni rahisi sana KUDANGANYIKA  maana hataweza kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza kuvumilia njaa ikibidi  kukaa  bila kula  na kunywa  kwa zaidi ya  saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa kuendekeza ulaji na unywaji  wakiwa kazini kwenye vituo vya kupiga kura, waliagiza vinywaji na  vyakula na vinywaji. Lakini wajanja  waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo  dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na  walikuja kuamka  uchaguzi  ulikuwa umewisha  na  kura za mgombea wao ambaye alikuwa anapendwa  na watu amekwishaibiwa kura zake wakiwa usingizini.

Ninachosema hapa ni kwamba  uchaguzi ni wa mwaka huu ni mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo wanaCCM wengi tu)  na kikundi cha watawala wa CCM wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.

Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM  uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi  wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni kubwa  kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini kwetu.

Sita:  UKAWA  wahakikishe inawaelekeza  mawakala wake mambo muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.  Mambo hayo ni pamoja na   kuhakikisha wanachukua kwa usahihi matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.

Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni kuhakikisha waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na Rais hawachakachui matokeo. Umma  ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna kinachoshinda nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ninaruhusu Makala hii ichapishwe na yeyote anayetaka. Lengo ni kuelimishana  ili kuleta mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie:  ananilea_nkya@yahoo.com



Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
 To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
 Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
 Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM


 Mama Nkya nimekuelewa sana
 sana na sana, siku zote nimekuwa nikifuatilia harakati zako
 ila sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa kuwaambia
 watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake
 haijalishi yupo wapi, ana nafasi gani kwa jamii au yupo
 upande gani kisiasa. Ulichokiandika ni very simple and very
 true hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
 wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga ulichokiandika
 tena wakitumia data za uongo kabisa. Ni ukweli uliowazi kuwa
 watanzania wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na nashukuru
 yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo kimoja cha
 redio(clouds fm), watanzania wa leo wanahitaji mabadiliko
 chanya na wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
 nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
 Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya mawili, 
  Je, tufanye nini watanzania lei hii ili kuzuia kabisa
 mchezo wa ccm kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu?
 Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
 kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
 nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za
 leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha? 
 Asante
 na ubarikiwe sana,
 RAYMOND
 MAUKIKIGAMBONI,
 DAR ES SALAAM.

  From:"ananilea nkya
 ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]"
 <Wanazuoni@yahoogroups.com>
 Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
 Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
 KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]


  









         [Attachment(s) from ananilea nkya
 included below]


       LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO



 Na Ananilea Nkya



 Nimeandika  hoja hii baada ya kusoma na kusikia  hoja
 zinazotolewa na  baadhi ya Watanzania kwamba  eti CHADEMA ,
 CUF, NCCR-Mageuzi  na NLD  -vyama vinavyounda UKAWA kwa
 kumsimamisha   Edward Lowassa kugombea Urais  vimepoteza
 usafi  wa kuongoza  mapambano dhidi ya ufisadi.



 Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA kumsimamisha
 Lowassa kuwa mgombea urais wamecheza kama Pele. Tena
 wanastahili pongeze kubwa maana walitumia akili kali na
 saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa ilicheza
 mchezo mchafu kisiasa kuwatumia wapinzania kumpakazia
 Lowassa ufisadi na hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
 Lowassa kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha ufisadi.




 Wanaodhani CHADEMA na UKAWA wamekosea pengine hawajaelewa
 kuwa   tangu upepo wa mabadiliko  wa kukataliwa mfumo chama
 kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu ulipoanza kuvuma
 duniani kote mwishoni mwa miaka ya 1980,  baadhi ya wanaCCM
 hawajakubali kwa dhati kabisa  ukweli huo na kuamini kwamba
 CCM inaweza  kupunzishwa kuongoza nchi angalao kwa miaka
 mitano.



 Hasa baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
 imebaki na viongozi ambao hawako tayari kutumia ujasiri
 kuongoza mabadiliko kwa amani.  Baadhi ya vongozi wanaojali
 zaidi maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli kama
 hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere kuwa bila CCM
 imara—Tanzania itayumba kujidanganya wenyewe na kudanganya
 wananchi.



 Wanasahau kwamba Mwalimu Nyerere kama mwanafalsafa na
 mwanasiasa makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri kwa
 faida ya taifa na wananchi kulingana na hali halisi ya
 wakati husika kwa kusoma upepo wa wananchi. Kwa mfano
 Nyerere aliwahi kusema CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
 na Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
 madarakani.



 Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1992 alionyesha mfano kwamba
 maslahi ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
 CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa wanaCCM wengi
 waliokuwa wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
 nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi --kuharakisha
 maendeleo ya wananchi.



 Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila mwanaCCM
 anayechaguliwa kuwa Rais, kwa kuogopa kulaumiwa kwamba eti
 kama CCM haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
 lawama za kufanya CCM iondoke madarakani, serikali zote za
 CCM baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka duaniani zimekuwa
 zinajihusisha na ufisadi.



 Serikali ya CCM imekuwa ikikwapua kwa wizi wa wazi mabilioni
 ya fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
 CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi zinafanyika kama
 geresha tu—kudanganya wafadhili na mataifa kuwa Tanzania
 ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi.



 Mfano uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini ya Rais
 Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki Kuu Akaunti
 ya EPA shilling bilioni 133 ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
 madarakani Rais Kikwete.



 Mwaka jana 2014 serikali ya CCM chini ya Kikwete ilikwapua
 shilingi bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta escrow Benki
 Kuu kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda uchaguzi wa
 serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaofanyika tarehe 25
 Oktoba mwaka huu 2015.



 CCM wakishaingia madarakani jambo muhimu kuliko yote Rais na
 serikali yake analolifanyia ni kubuni ufisadi wa kuipatia
 CCM fedha na mbinu nyingine za kuiwezesha CCM ibaki
 madarakani uchaguzi unaofuta. Hakuna kazi muhimu ya
 kuwaondolea wananchi umaskini inayofanyika kwa kiwango na
 juhudi kubwa.



 Kwa sababu hiyo,   kikundi kidogo cha watawala, wengi wakiwa
 ni kutoka CCM na familia zao wamejikuta wakinufaika kwa kuwa
  matajiri kufuru kwa muda mfupi ili hali  wananchi wengi
 wakibaki maskini na mafukara wa kutupa.



 Mfano  wabunge (kikundi cha watu wasiozidi 400) wengi wakiwa
  ni wanachama wa CCM  kila mmoja analipwa si chini ya
 milioni  10 kila mwezi kama mishahara, wacha marupurupu  na
 posho za vikao vya kamati, posho za safari na  mamilioni
 mafao kila baada ya miaka mitano.  Lengo wawe na fedha
 nyingi za kununua kura za wapiga kura maskini uchaguzi
 unaofuata CCM ibaki madarakani.



 Ndiyo sababu kila mwananchi wakiwepo watu muhimu kama walimu
 wa vyuo vikukuu na madaktari hivi sasa nao  wameamua kuwa
 wanasiasa.



 Zaidi baadhi ya wanaotafuta madaraka ya kisiasa wanatumia
 mbinu chafu sana  ikiwa ni pamoja na ushirikina wa kuuwa
 watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) waweze kupata nafasi
 ya kuingia katika kundi la  watawala—kupata utajiri wa
 kutisha katika kipindi cha miaka mitano.



 Mfamo Wabunge waliomaliza muda wao mwaka huu 2015    kila
 mmoja ameondoka na kiinua mgongo zaidi ya shilingi milioni
 200.  Hii ni kufuru katika nchi inayojinasibu kuwa ni
 maskini na inapita huko na huko duniani kuomba misaada!



 Hata hivyo kwa kadri ufukara unavyoendelea kuwatafuna
 wananchi wengi, na kwa kadri uelewa wa  wananchi
 wanaoteseka kwa  umaskini  unavyoongezeka kwamba CCM na
 utawala wa  serikali yake ndicho chanzo cha umaskini wao,
 CCM  imebaini kuwa haiwezi tena  kushinda uchaguzi kupitia
 sanduku huru la kura kwa kutegemea kete moja tu—kununua
 wananchi mafukara  peke yake.



 Hivyo katika miaka ya hivi karibuni CCM imeanza kuendesha
 siasa za maji taka—kuchafuana wao kwa wao na hatimaye
 wameamua kutoana kafara-lengo kuu likiwa ni kuzuia wananchi
 wasitumie sandundu la kura kufanya mabadiliko—kuchagua
 vyama vingine kuongoza nchi.



 Hivyo Rais Kikwete, hata kama ndani ya umungu wa moyo wake
 hakubaliani na CCM inavyotumia ubabe kukataa mabadiliko
 kinyume na asili ya binadamu, amekuwa akifanya mambo
 kutimiza matakwa ya baadhi ya wanaCCM —kujaribu kuzuia
 mabadiliko—ili tu kuepuka lawama- amalize muda wake bila
 kuonekana ndiye kasababisha wananchi kuipunzisha CCM uongozi
 kwa kipindi cha miaka mitano.



 Kwa kufanya hivyo Rais Kikwete amejikuta akiporwa ujasiri
 wake aliokuwa nao kama mwanasiasa   ambaye Mwalimu Nyerere
 alimuamini.



 Kumbuka Mwalimu Nyerere alinukuliwa na gazeti la  Nipashe na
 Majira 26/5/95 akisema   baada ya Rais Mwinyi  baadhi ya
 vijana ambao alikuwa anaona wana nia ya dhati kabisa  na
 uwezo mkubwa wa kuongoza Tanzania  ni Benjamin Mkapa, Jakaya
 Kikwete na Edward Lowassa.

 Lakini kwa Kikwete kukubali kuyumbishwa na wana CCM wachache
 wasiokubali mabadiliko anaonekana kufumbia macho utekelezaji
 wa kile mwanafalsafa Mwalimu nyerere alichokisema---kwamba
 Watanzania wanataka mabadiliko.



 Mfano Rais Kikwete alipata fursa ya kusimamia mabadiliko kwa
 kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
 Lakini kikundi kidogo cha wahafidhina ndani ya CCM
 kilimtisha akajikuta anaweka pembeni ujasiri wake aliokuwa
 nao wa kusimamia mabadiliko hayo muhimu kwa maendeleo ya
 taifa hili.



 Kama uamini jiulize ni kwa   nini  Kikwete aliachia Bunge la
 Katiba lililojaa asilimia 80  ya wanachama likazika Rasimu
 ya Katiba ya wananchi pale Dodoma mwaka jana 2014  -- Rasimu
 ambayo ingeleta Katiba yakuweka  misingi ya kuleta
 madadiliko Tanzania—mabadiliko ya kuhakikisha kikundi
 kidogo cha watawala hakijitajirishi kwa ufisadi na kujigawia
 mali  za umma huku mamilioni ya wananchi wakibaki maskini na
 mafukara wa kutupa?



 Baada ya Kikwete kupoteza fursa  ya kuleta mabadiliko  kwa
 kuandika Katiba Mpya,  umma uliofukarishwa  umeendelea
 kupata uelewa kuwa CCM na serikali  yake ndicho chanzo cha
 umaskini wao.



 Hivyo ili kuendelea  kubaki madarakani  serikali ya CCM
 imekuwa  ikijihusisha na ufisadi ili ipate fedha za
 kuwarubuni walala hoi wakati wa kampeni za uchaguzi.



 Mfano mwaka 1995 Rais Benjamini Mkapa alijikuta serikali
 yake ikifanya ufisadi  katika  akaunti EPA (bilioni 122)
 zilizotumiwa na CCM kumuweka  Kikwete madarakani.



 Ukitafakari utaona kwamba katika ufisadi Tegeta escow,
 serikali ya CCM imekapua billion 306 mara tatu ya ufisadi wa
 EPA mwaka 1995 ilipokwapua bilioni 122 ili kipate fedha
 nyingi zaidi la kuwalaghai wapiga kura mafukara ambao
 wameendelea kupata uelewa kuwa CCM inaiba fedha za umma
 kununua wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi.



 Hivyo serikali ya CCM inayoongozwa na Kikwete ambayo
 imeshuhudia nguvu ya wananchi kudai mabadiliko ikiwa kubwa
 kuliko wakati mwingine wowote, inajaribu kila mbinu chafu na
 safi ili CCM ibaki madarakani baada ya uchaguzi mwaka
 huu.



 Ndiyo sababu  serikali ya CCM  kupitia msemaji wa chama
 hicho Nape Nnauye imeanza kuwaambia Watanzania kuwa  CCM
 lazima ishinde uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni kwa
 kutumia goli la mkono (wizi au lolote lile chafu).



 Zaidi  Rais   Kikwete  amefikishwa mahali  pabaya
 kulazimika  kubuni  mchezo  mchafu kujaribu kuwadanganya
 Watanzania  kuwa eti  CCM na serikali yake ni safi,
 haijihusishi na ufisadi unaofukarisha wananchi isipokuwa
 wanachama wachache wa CCM ndio mafisadi.



 Ili  kujaribu kutafuta kujenga  uhalali wa CCM kubaki
 madarakani baada ya uchaguzi wa  mwaka huu 2015, Kikwete
 amejikuta akilazimika  kumtoa  kafara Lowassa  kwa
 kumpakazia  ufisadi wa  Richmond.



 Wananchi wanauliza kama Lowassa alikuwa ndiye mhusika  wa
 Richmond  ni kwa nini   Spika wa Bunge  Anna Makinda (mmoja
 wa watawala  wa CCM),  hakuagiza  tume ya Bunge iliyoongozwa
 na Mbunge wa CCM Harrison Mwakyembe kumhoji Waziri Mkuu
 Edward Lowassa?



 Pili wananchi wanahoji kama CCM haijamtoa Lowassa kafara
 kwa kumbebesha ufisadi wa chama hicho  ili kupumbaza hasira
 ya  wananchi dhidi ya ufisadi wa CCM kwenye uchaguzi wa
 Oktoba mwaka huu 2015  ni kwa nini  Rais Kikwete alikubali
 Waziri wake Mkuu  Edward Lowassa  ajiuzulu kwa ufisadi wa
 Richmond 2008 wakati ufisadi wa kutisha  ulifanywa na
 serikali ya CCM kwenye akaunti ya Tegeta escrow 2014
 Kikwete aliwatetea mawaziri  waliogawiwa fedha hizo na Ikulu
 ilikuwa ndiyo mtuhumiwa namba moja?



 Mimi si mwanasiasa wa chama chochote cha siasa hapa nchini
 ninachoangalia ni chanzo cha umaskini wa wananchi wengi
 Tanzania.



 Ndiyo sababu Watanzania wengi nikiwepo mimi mwenyewe kwa
 sababu  tulipewa habari nusu nusu zilizotolewa kimkakati na
 serikali ya CCM kuhusu kashfa ya Richmond  kumpakazia
 Lowassa ufisadi, tulipubwazwa tukaisaidia CCM  kumchafua
 Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond.



 Lakini baadhi ya wananchi walianza  kujua kuna ukweli
 uliofishwa kuhusu Richmond pale TV moja ilipokuwa imemwalika
 Lowassa aotoe yake ya moyoni live siku chache baada ya
 kujiuzulu, lakini kipindi hicho cha TV kikafutwa ghafla.



 Hata hivyo ukweli huo umekuja kujulikana mwezi Julai mwaka
 huu Lowassa alipotoa hadharani baada ya kuachana na CCM na
 kujiunga na CHADEMA.



 Sasa wananchi    wamefahamu kuwa  CCM  chini ya serikali ya
 Rais Kikwete iliamua kumtoa Lowassa kafara kwa kumpakazia
 ufisadi wa   Richmond  ili  kuiokoa CCM isiadhibiwe vikali
 na wananchi kwenye sanduku huru la kura  –kwa ufisadi
 alinawasababishia umaskini na ufukara.



 Ndiyo sababu  hivi sasa  CCM na baadhi ya wanahabar
 wanapakazia  CHADEMA  na  UKAWA  kuwa  eti ni mafisadi
 baada ya kumpokea Lowassa (kafara wa CCM)  na  kumpitisha
 kuwa mgombea wa  Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




 Isitosha hivi sasa kikundi  cha watawala wachache wa
 serikali ya CCM wanahaha na wanamzonga Kikwete azuie
 mabadiliko kwa mkono kwa  kufanya kila uchafu  kupumbaza
 Watanzania kwa kutumia kete ya eti   Lowassa ni  fisadi wa
 Richmond  hivyo hana sifa ya kugombea Urais wa Tanzania,
 bali Magufuli ndiye mtu safi.



 Wananchi wenye akili zao wanajiuliza hivi mwenye kashfa za
 kifisadi kati ya Lowassa na Magufuli ni nani?  Ni Lowassa
 aliyepakaziwa Richmond au ni Magufuli aliyeongoza watawala
 kujiuzia kwa bei chee nyuma za umma zilizogarimu wanannchi
 mabilioni ya fedha?



 Wananchi pia wanajiuliza kama Lowassa ni fisadi wa Richmond
 ni kwa nini serikali ya CCM haijamshitaki mahakamani miaka
 minane tangu ufisadi huo ulipotokea?



 Hivyo  pengine  baada ya Lowassa kutafakari nafsi yake na
 kuona kuwa CCM imemtoa kafara asigombee Urais  ili kuzuia
 mabadiliko, ameamua kufanya  maamuzi magumu  ya kuhama CCM
 --kushiriki kuongoza masikini  na mafukara  wanaotafuta
 mabadiliko.



 Lowassa ameamua kutekeleza alichokitabiri Mwalimu Nyerere
 kwamba CCM isipokubali kuongoza wananchi wapate mabadiliko
 wanayoyataka—wananchi watayatafuta mabadiliko hayo  nje
 ya CCM.



 Ni dhahiri CCM ilipoteza fursa adimu ya kuongoza wananchi
 kwenye kuleta mabadiliko kwa kuandika Katiba  Mpya-- kuweka
 misingi ya kukomesha mfumo wa utawala  unaowezesha watawala
 kuwa matajiri wa kupindukia  huku mamilioni ya wananchi
 wakiwa mafukara na nchi ikinuka aibu ya umaskini  wa
 kijitakia  ikiwa rasilimali nyingi za asili.



 Wanaomchochea Rais Kikwete asikubali mabadiliko yachukue
 mkondo wake, wameunda timu ya kampeni yanye wajumbe wengi
 waliohusika kumpakazia Lowassa ufisadi wa Richmond ili eti
 kwenye kampeni waendelee kumpaka ufisadi  Lowassa, CHADEMA
 na UKAWA wakidhani Watanzania hawana akili ya kutafakari.



 Lengo lao ni moja. Wanajua kabisa kuwa kwa kutumia sanduku
 huru la CCM  haiwezi kuchaguliwa. Wanataka kutumia
 kisingizio   kuwa  CHADEMA  na UKAWA imechafuka eti kwa
 kumsimamisha Lowassa Urais  ambaye CCM imemtoa karafa –
 kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond.

 Lakini baada ya kupata salamu za wananchi kupitia mafuriko
 yao kwenye kumtambulisha Lowassa kwamba wao wanaelewa fisadi
 kamili ni CCM, sasa CCM imeshtuka imeanza kutumia polisi
 kuwaadhibu wananchi. Pengine baadaye itatumia jeshi
 kabisa.



 Zaidi imeamua kujaribu kampeni za   ardhini -nyumba kwa
 nyumba, bila shaka kutumia mabilioni ya fedha serikali ya
 CCM ilizokwapua Tegeta escrow kununua shahada na kura za
 mafukara.



 Kwenye kampeni za   nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu ndiko
 ufisadi mbaya wa kisiasa unakofanyika—kununua, kutisha na
 kuumiza    wananchi mafukara.

 Swali ni je Watanzania wangapi wapiga kura watakubali CCM
 inapopita majumbani mwao kuuza shahada zao  kwa sukari,
 kanga au fedha hata kama CCM itaamua kumpa kila mpiga kura
 shilingi milioni moja?



  Ni mpiga kura gani atakayekubali KUDANGANYIKA  kwa
 kununuliwa na  CCM  kwa vijizawadi vya fedha nguo KUSALITI
 mamilioni ya watanzania  wanaoendelea kuteseka  kwa ufukara
 kila baada ya uchaguzi kwisha na CCM kubaki madarakani?



 Wananchi  pia wanauliza je mabilioni ya escrow yatawanunua
 wajumbe wa NEC ili  wavuruge daftari la wapiga kura, au
 wachakachue kama uchaguzi wa 2010  au wataharibu daftari la
 wapiga kura, mashine   na vifaa vya kupigia kura, au
 kuchelewesha kwa makusudi kufungua vituo vya wapiga kura
 ili  kuvuruga uchaguzi CCM  ishinde kwa goli la mkono?



 Kadhalika wananchi wanauliza wanaomshinikiza Kikwete
 asikubali mabadiliko wakiona hilo haliwezekani je watamuua
 Lowassa waliomtoa kafara au  viongozi wa CHADEMA na UKAWA
 waliompokea Lowassa na kumwezesha kufikia azma yake ya
 kujitolea kuwatumikia watanzania  ili kuvuruga uchaguziwa
 mwaka huu?



 Wananchi wanauliza maswali hayo  baada ya kubaini kwamba
 huenda  wasiomtakia mema Kikwete astaafu kwa amani
 wamejaribu kuwalaghai baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA ili
 kujaribu kuvuruga UKAWA – lakini UKAWA kwa vile ni sauti
 ya mafukara-sauti ya umma  imeendelea kuwa moto mkali wa
 nyika  dhidi ya CCM.



 Hivyo binafsi namshauri Rais Kikwete akubali kuwa baba wa
 pili wa Taifa hili baada ya Nyerere kuondoka. Akubali
 kusimamia wananchi watumie sanduku huru la kura kwenye
 uchaguzi wa mwaka huu 2015 kupata mabadiliko ya uongozi
 wanayoyataka.



 Wananchi wana imani na UKAWA   kwamba wakiingia madarakani
 Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi itaandikwa.



 Huo utakuwa ni mwanzo wa mabadiliko wanayoyataka
 wananchi—kuhakikisha watawala hawajitajirishi kupindukia
 kufisadi fedha za wananchi huku wananchi wengi wakibaki
 mafukara.  CHADEMA  na UKAWA  wasipotimiza hili na kuonyesha
  kwa vitendo maendeleo watakayokuwa wameyaleta kwa miaka
 mitano, ni lazima wananchi watatumia sanduku la kura
 kuwapunzisha.



 Ninaamini ni wenye kutetea maslahi binafsi tu ndiye
 atakayemlaumu Rais Kikwete kwamba eti CCM isipochaguliwa
 Oktoba 25, Kikwete atakuwa ni chanzo  cha wananchi kuamua
 kuipunzisha CCM  kwa miaka mitano.



 Nitakuwa wa kwanza kuwapinga watu hao na kumtetea Kikwete
 hata kama ni kwa kuamua  kuingia kwenye siasa  kwa kujiunga
 na CCM .



 Hakika Rais Kikwete  ukisimamia  wananchi  wazungumze kuhusu
 hatma ya uongozi wan chi yao kwa kutumia sanduku huru la
 kura  bila CCM kuingiza  mkono mchafu, wewe mwenyewe
 ukistaafu utaishi kwa amani na furaha huku baadhi yetu
 tukikuona kama baba wa Pili Taifa taifa hili, baada ya
 Mwalimu Nyerere.



 Mwisho ninaruhusu yeyote anayetaka kuchapisha au kutangaza
 redioni natelevisheni niyoyoyaandika hapa TV au kuchapisha
 na kuwasambazia Watanzania wote popote walipo ujumbe huu
 afanye hivyo. Wanawaza kuwasambazia watu mitaani,
 kwenyemikutano ya kampeni, mashuleni vyuoni popote
 pale—lengo likiwa moja—sote Watanzania tuujue ukweli
 kuhusu ufisadi na mchango wake katika kuwafanya Watanzania
 waishi katika umaskini.   Lakini muhimu kila Mtanzania ajue
 hakuna mshindi wa kujisifu—mshindi ni  nchi yetu Tanzania
 na  Watanzania  wote.



 MUNGU IBARIKI YANZANIA.



 Ananilea Nkya

  E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com





     __._,_.___

             Attachment(s)
 from ananilea nkya | View
 attachments on the web




          1 of 1 File(s)




       LOWASSA  KAFARA WA
 CCM.docx







         Posted by: ananilea nkya
 <ananilea_nkya@yahoo.com>




                           Reply
 via web post
                       •

                Reply to sender
           •

               Reply to group
           •
             Start a New
 Topic
           •
                             Messages in this
 topic
                 (1)
















     Visit Your Group


       New Members
       2






    • Privacy • Unsubscribe • Terms of Use






















   .







 __,_._,___






 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1441117556.40382.YahooMailBasic%40web121003.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment