Tuesday, 1 September 2015

[wanabidii] RE: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]

Mama yangu Nkya umetumia muda wako mwingi kupiga kampeni kwenye jukwaa la wanazuoni. Mambo uliyoyazungumza ni mazuri sana kwenye uwanja wa siasa lakini siyo kwenye jukwaa ambako wengi wanajijua na wanafanya upembuzi makini kuhusu hatima ya Taifa badala ya hatima ya makundi ya wasakatonge. Naomba ujikite zaidi kwenye mambo ya msingi na hatima ya taifa. Kwa mfano Unazungumzia mabadiliko bila ku-define neno mabadiliko. Maswali yangu kwako ni: Mabadiliko ni nini? Je! Mabadiliko maana yake ni kuwapa UKAWA kuongoza nchi tu na si zaidi ya hapo? Je ikitokea tetemeko la ardhi siyo mabadiliko? Je, nchi ikivamiwa na maadui kupitia wasaliti wa uhuru wetu siyo mabadiliko? Kama UKAWA walitumia miaka nane kutudanganya kwamba Lowassa ni fisadi, lakini wakatumia siku moja kumsafisha na kutudanganya kwamba Lowassa si fisadi tutawaamini vipi kwamba hawatabadili kauli zao kama walivyobadili kwa maslahi ya kundi hilo la UKAWA? Hivi unaposema mnataka katiba ya wananchi, je wale wabunge walioshiriki kwenye Bunge la Katiba hawakuchaguliwa na nchi wa Tanzania kutoka majimbo yote? Je, wao (wabunge) walikuwa raia wa nchi gani? Hao wananchi sura zao ni tofauti na hawa tunaowajua sisi raia wa Tanzania? Hivi mtu ambaye hayupo UKAWA siyo mwananchi wa Tanzania? Wewe umesema haupo Chama chochote kwa sababu huna kazi ya Chama chochote au fikra zako na imani yako haipo kwenye Chama chochote? Kama utadai UKAWA siyo Chama, je! UKAWA wafuasi wake hawana Chama? Kama hawana Chama basi pia hawana haki ya kutafuta uongozi wa nchi hii kwa njia ya sanduku la kura!

"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".

Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: ananilea nkya ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]
Sent: ‎01/‎09/‎2015 17:26
To: Wanazuoni@yahoogroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
Cc: WANA BIDII; Paschally Mayega
Subject: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]

 
[Attachment(s) from ananilea nkya included below]

WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea Nkya

Mmoja wa watu waliosoma makala yangu Raymond Mauki, makala niliyoandika kwamba CCM ilimtoa Edward Lowassa kafara kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond ili chama hicho kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa na CCM ni chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu maswali mawili.

Kwenye malaka hiyo iiliandika kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi hapa nchini kuwa maskini. Nilitoa mfano wa serikali ya CCM kuwa fisadi kusimamia wizi wa fedha za umma kwenye akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana 2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni serikali ya CCM yenyewe ilihusika lakini walidanganya umma kwamba muhusika ni Edward Lowassa.

Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa fisadi wa Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona. Nilisema pia kwamba hivi sasa nchi imejaa ufisadi unaofanywa na watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo hata mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli wanayejidai ni mtu msafi akichaguliwa yerikali yake italazimika kufanya ufisadi penda asipende. Na yeye mwenyewe Magufuli amekaririwa akisema kwamba ataika mfano marais waliomtangulia.

Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa fedha za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba ni malofa na wapumbavu ni lazima wananchi wafanye mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025 kwa kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba .

Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu ni haya ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?

Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao kupitia uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni mkubwa na muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao wakijitokeza kusikiliza kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga kura na wakaipigia kura UKAWA wataleta mabadiliko. Hivyo kila mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze kitambulisho chake cha kupiga kura(kichinjio).

Afanye hivyo kwa kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako (ni silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi au mgambo hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n chako. Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya kanga, kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.

Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake waipigie kura UKAWA kwa sababu ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu zinazogusa maisha ya wanawake moja kwa moja.

Kwanza UKAWA wana agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo Kikuu. Hili ni muhimu kwa sababu elimu ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa zima.

Pili UKAWA wana agenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Moja ya jambo muhimu katika Katiba ya wananchi ni kuweka uhusiano mpya kati ya viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi kujitajirisha kwa mali za umma huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.

Fedha za nchi zinazotafunwa na watawala wachache zitatumika kwa mfano kuboresha elimu, huduma za afya,maji, umeme, kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya watu ajira. Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya kuhakikisha uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.

Kashalika Katiba Mpya italeta usawa wa kweli wa kijinsia nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri uchaguzi wa 2020 kwa kutoa idadi sawa wanawake na wanaume madiwani kwenye kata na idadi sawa ya wabunge wanawake na wanaume majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.

Utaratibu wa viti maaluma utatumika kwa watu wenye ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa mbunge mwanamke na mwanaume. Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a kweli kuhusu usawa wa kijinsia unaotakiwa Tanania ili nchi yetu na watu wake waondokane na umaskini.

Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama vinajinasibu eti vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea mwenza au mgombea wa Urais. Ni sawa lakini hiyo ni geresha ya danganya toto kwa sababu kwa mfumo wa sasa ambapo usawa wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba wanawake wanatumika tu kama wanaume kupitisha sheria na sera za maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.

Usawa wa jinsia wa kweli na wa kudumu hauwezi kufikiwa hapa nchini bila Katiba Mpya ya wananchi kuandikwa na kuweka misingi ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya kugombea na kushinda sawa na wanaume majimboni na kwenye kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake na wale wote wanaofanya kampeni UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli kwamba wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague UKAWA ndio waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.

Swali la Pili: Watanzania tufanye nini kuzuia CCM kuiba kura uchaguzi wa mwaka huu 2015? Mimi napendekeza yafuatayo:

Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM mnaouchukia kuona watu wengi wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri wa kupindukia, kinachotakiwa kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo wa kubadilisha maisha ya kimaskini wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza kitambulisho chako (kichinjio) na siku ya kupiga kura tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA kwa sababu wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA wana ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini unaotengenezwa kwa serikali ya CCM kukwapua fedha za wananchi na jeuri ya kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM kujifanya chama dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura maana hakuna ukombozi wenye kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila wananchi wenyewe kushiriki kuleta mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la kura.

Umaskini wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa ajira ya kuwapatia walio wengi wasio watumishi wa umma fedha za kujikimu. Watumishi wengi wa umma mfano walimu, madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa mshahara isiyokidhi mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.

Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda mrefu. Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache wakiugua wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa nchi za nje.

Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo mbinu mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu wenye ubora na wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile wanaheshimiwa, kuthaminiwa na kulipwa vizuri.

Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya dola hasa polisi kutumika kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi yetu bado iko kwenye ukoloni.

Pili: Kila kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi wengi anapaswa kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji, mtaa , polisi , mgambo au mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.

Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili wasipige kura ya kuwaletea mabadiliko kwa kuikataa CCMambayo utawala wake umewafanya wananchi wengi kuwa malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali ya CCM wakijilipa fdha za wananchi na kupata utajiri wa kukufuru.

Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni maana pengine hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki kuu ambazo nyingine zilibebwa kwa tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na kama ni nguo vaeni ni mali yenu lakini usimpe tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini wataifanya miaka 5 ijayo.

Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA awaeleze wananchi ukweli huu. Wananchi wakiujua ukweli kuhusu chimbuko la matatizo yanayowakabili kuwa ni serikali ya CCM kama taasisi kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka, wananchi wataelewa na watapiga kura kikamilifu kuleta mabadiliko—kuchagua UKAWA kuendesha serikali tuone miaka mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini. Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu na Katiba Mpya uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama kwa kuzingatia sera za maendeleo umaskini unaowasumbua Watanzania wengi hautaondoka nchini.

Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na maisha ya mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki, hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi ikamilike. Maana kwenye uchaguzi wakala ukipepesa ukipepesa macho kidogo tu wajanja wanachakachua.

Nne: UKAWA kuweka mawakala makini ambao siyo mamluki wa CCM-- watu jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio wengi wanaoteseka na maisha duni. Kura ni hesabu kwa mtu asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu ni rahisi sana KUDANGANYIKA maana hataweza kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza kuvumilia njaa ikibidi kukaa bila kula na kunywa kwa zaidi ya saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa kuendekeza ulaji na unywaji wakiwa kazini kwenye vituo vya kupiga kura, waliagiza vinywaji na vyakula na vinywaji. Lakini wajanja waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na walikuja kuamka uchaguzi ulikuwa umewisha na kura za mgombea wao ambaye alikuwa anapendwa na watu amekwishaibiwa kura zake wakiwa usingizini.

Ninachosema hapa ni kwamba uchaguzi ni wa mwaka huu ni mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo wanaCCM wengi tu) na kikundi cha watawala wa CCM wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.

Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini kwetu.

Sita: UKAWA wahakikishe inawaelekeza mawakala wake mambo muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura. Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha wanachukua kwa usahihi matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.

Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni kuhakikisha waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na Rais hawachakachui matokeo. Umma ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna kinachoshinda nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ninaruhusu Makala hii ichapishwe na yeyote anayetaka. Lengo ni kuelimishana ili kuleta mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM


Mama Nkya nimekuelewa sana
sana na sana, siku zote nimekuwa nikifuatilia harakati zako
ila sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa kuwaambia
watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake
haijalishi yupo wapi, ana nafasi gani kwa jamii au yupo
upande gani kisiasa. Ulichokiandika ni very simple and very
true hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga ulichokiandika
tena wakitumia data za uongo kabisa. Ni ukweli uliowazi kuwa
watanzania wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na nashukuru
yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo kimoja cha
redio(clouds fm), watanzania wa leo wanahitaji mabadiliko
chanya na wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya mawili, 
 Je, tufanye nini watanzania lei hii ili kuzuia kabisa
mchezo wa ccm kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu?
Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za
leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha? 
Asante
na ubarikiwe sana,
RAYMOND
MAUKIKIGAMBONI,
DAR ES SALAAM.

From:"ananilea nkya
ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]


 









[Attachment(s) from ananilea nkya
included below]


LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO



Na Ananilea Nkya



Nimeandika hoja hii baada ya kusoma na kusikia hoja
zinazotolewa na baadhi ya Watanzania kwamba eti CHADEMA ,
CUF, NCCR-Mageuzi na NLD -vyama vinavyounda UKAWA kwa
kumsimamisha Edward Lowassa kugombea Urais vimepoteza
usafi wa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi.



Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA kumsimamisha
Lowassa kuwa mgombea urais wamecheza kama Pele. Tena
wanastahili pongeze kubwa maana walitumia akili kali na
saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa ilicheza
mchezo mchafu kisiasa kuwatumia wapinzania kumpakazia
Lowassa ufisadi na hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
Lowassa kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha ufisadi.




Wanaodhani CHADEMA na UKAWA wamekosea pengine hawajaelewa
kuwa tangu upepo wa mabadiliko wa kukataliwa mfumo chama
kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu ulipoanza kuvuma
duniani kote mwishoni mwa miaka ya 1980, baadhi ya wanaCCM
hawajakubali kwa dhati kabisa ukweli huo na kuamini kwamba
CCM inaweza kupunzishwa kuongoza nchi angalao kwa miaka
mitano.



Hasa baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
imebaki na viongozi ambao hawako tayari kutumia ujasiri
kuongoza mabadiliko kwa amani. Baadhi ya vongozi wanaojali
zaidi maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli kama
hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere kuwa bila CCM
imara—Tanzania itayumba kujidanganya wenyewe na kudanganya
wananchi.



Wanasahau kwamba Mwalimu Nyerere kama mwanafalsafa na
mwanasiasa makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri kwa
faida ya taifa na wananchi kulingana na hali halisi ya
wakati husika kwa kusoma upepo wa wananchi. Kwa mfano
Nyerere aliwahi kusema CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
na Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
madarakani.



Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1992 alionyesha mfano kwamba
maslahi ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa wanaCCM wengi
waliokuwa wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi --kuharakisha
maendeleo ya wananchi.



Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila mwanaCCM
anayechaguliwa kuwa Rais, kwa kuogopa kulaumiwa kwamba eti
kama CCM haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
lawama za kufanya CCM iondoke madarakani, serikali zote za
CCM baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka duaniani zimekuwa
zinajihusisha na ufisadi.



Serikali ya CCM imekuwa ikikwapua kwa wizi wa wazi mabilioni
ya fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi zinafanyika kama
geresha tu—kudanganya wafadhili na mataifa kuwa Tanzania
ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi.



Mfano uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini ya Rais
Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki Kuu Akaunti
ya EPA shilling bilioni 133 ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
madarakani Rais Ki


[The entire original message is not included.]

0 comments:

Post a Comment