"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".
Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa
From: ananilea nkya ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]
Sent: 01/09/2015 21:36
To: Wanazuoni@yahoogroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
Cc: WANA BIDII; Paschally Mayega
Subject: RE: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15[1Attachment]
Ndugu Saru
Neno mabadiliko katika muktadha wa uchaguzi Tanzania mwaka huu 2015 linatumika kumaanisha wananchi kuchagua serikali mpya tofauti na serikali ya CCM iliyoko madarakani ambayo ilikataa kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Serikali Kitiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba hiyo pamoja na mambo mengine itaweka misingi mizuri ya kuwepo usawa wa kijinsia katika uongozi hasa 50 kwa 50 wabunge wanawake na wanaume majimboni. Pia itaweka misingi ya kuzuia serikali kuwa chanzo ufisadi wa fedha za umma. Mfano ufisadi wa mwaka jana 2014 wa Tegeta escrow bilioni 306, ufisadi wa Richmond bilioni 172 mwaka 2008 na ufisadi wa EPA bilioni 133 mwaka 2005 na hakuna aliyefikishwa mahakamani.
Katiba Mpya pia itaweka misingi itakayozuia watawala wachache wakijitajirisha kwa kutumia fedha za wananchi kujilipa mishahara mikubwa, mafao na marupurupu wakati watumishi wengine wa umma madaktari, wauguzi, walimu, polisi na wananchi wengi wakibaki maskikini. Mfano mbunge kulipwa mshahara shilingi milioni 10 mkwa mwezi na mafao zaidi ya shilingi milioni 200 baada ya kustaafu miaka mitano tu ya utumishi. huku ni kutajirisha kikundi kidogo cha watu katika nchi huku wengi wakibaki mafukara.
Nimeandika kwamba kwa vile vyama vinavyounda UKAWA vina agenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi, wapewe kura. Hayo ni maoni yangu baada ya kusoma dondoo za ilani za vyama mbali mbali vinavyotafuta ridhaa ya kuchaguliwa hapo Oktoba 25 mwaka huu 2015. Nimesema pia kuwa serikali ya UKAWA wasipotimiza ahadi hiyo miaka 5 ijayo wananchi watapiga kura watawaondoa madarakani. Bila wananchi kufanya mabadiliko ya uongozi na kuweka uongozi utakaoandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi siasa za vyama vingi Tanzania zitaendelea kuongeza umaskini wa wananchi na nchi yenyewe huku mali zetu zikiwa zinaporwa na wawekezaji kwa kwenda mbele.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Tue, 9/1/15, Surumedia majiydsuru@gmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com> wrote:
Subject: RE: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]
To: Wanazuoni@yahoogroups.com, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, wanabidii@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Tuesday, September 1, 2015, 5:39 PM
Mama yangu Nkya umetumia muda
wako mwingi kupiga kampeni kwenye jukwaa la wanazuoni. Mambo
uliyoyazungumza ni mazuri sana kwenye uwanja wa siasa lakini
siyo kwenye jukwaa ambako wengi wanajijua na wanafanya
upembuzi makini kuhusu hatima ya Taifa badala ya hatima ya
makundi ya wasakatonge. Naomba ujikite zaidi kwenye mambo ya
msingi na hatima ya taifa. Kwa mfano Unazungumzia mabadiliko
bila ku-define neno mabadiliko. Maswali yangu kwako ni:
Mabadiliko ni nini? Je! Mabadiliko maana yake ni kuwapa
UKAWA kuongoza nchi tu na si zaidi ya hapo? Je ikitokea
tetemeko la ardhi siyo mabadiliko? Je, nchi ikivamiwa na
maadui kupitia wasaliti wa uhuru wetu siyo mabadiliko? Kama
UKAWA walitumia miaka nane kutudanganya kwamba Lowassa ni
fisadi, lakini wakatumia siku moja kumsafisha na
kutudanganya kwamba Lowassa si fisadi tutawaamini vipi
kwamba hawatabadili kauli zao kama walivyobadili kwa maslahi
ya kundi hilo la UKAWA? Hivi unaposema mnataka katiba ya
wananchi, je wale wabunge walioshiriki kwenye Bunge la
Katiba hawakuchaguliwa na nchi wa Tanzania kutoka majimbo
yote? Je, wao (wabunge) walikuwa raia wa nchi gani? Hao
wananchi sura zao ni tofauti na hawa tunaowajua sisi raia wa
Tanzania? Hivi mtu ambaye hayupo UKAWA siyo mwananchi wa
Tanzania? Wewe umesema haupo Chama chochote kwa sababu huna
kazi ya Chama chochote au fikra zako na imani yako haipo
kwenye Chama chochote? Kama utadai UKAWA siyo Chama, je!
UKAWA wafuasi wake hawana Chama? Kama hawana Chama basi pia
hawana haki ya kutafuta uongozi wa nchi hii kwa njia ya
sanduku la kura!
"Ni
bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini
ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa
kimya".
Baba
Nouman,
Bongonyika, East
AfricaFrom:
ananilea
nkya ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]
Sent:
01/09/2015
17:26
To:
Wanazuoni@yahoogroups.com;
mabadilikotanzania@googlegroups.com;
wanabidii@googlegroups.com
Cc:
WANA
BIDII; Paschally
Mayega
Subject:
[Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE
NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]
WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea Nkya
Mmoja wa watu waliosoma makala yangu Raymond Mauki, makala
niliyoandika kwamba CCM ilimtoa Edward Lowassa kafara
kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond ili chama hicho
kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa na CCM ni
chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa
kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu
maswali mawili.
Kwenye malaka hiyo iiliandika kwa serikali ya CCM ndiyo
fisadi wa fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi
hapa nchini kuwa maskini. Nilitoa mfano wa serikali ya CCM
kuwa fisadi kusimamia wizi wa fedha za umma kwenye
akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana
2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni
serikali ya CCM yenyewe ilihusika lakini walidanganya umma
kwamba muhusika ni Edward Lowassa.
Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa fisadi wa
Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona.
Nilisema pia kwamba hivi sasa nchi imejaa ufisadi
unaofanywa na watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo hata
mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli wanayejidai ni
mtu msafi akichaguliwa yerikali yake italazimika kufanya
ufisadi penda asipende. Na yeye mwenyewe Magufuli
amekaririwa akisema kwamba ataika mfano marais
waliomtangulia.
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM
kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa fedha
za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku
wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena
watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba ni
malofa na wapumbavu ni lazima wananchi wafanye
mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025 kwa
kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba .
Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu ni
haya ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati
hizi za leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?
Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha
yao kupitia uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni mkubwa na
muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao wakijitokeza kusikiliza
kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga kura na
wakaipigia kura UKAWA wataleta mabadiliko. Hivyo kila
mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze
kitambulisho chake cha kupiga kura(kichinjio).
Afanye hivyo kwa kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote
kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako (ni
silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu
mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi
au mgambo hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n chako.
Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya kanga,
kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke
USIDANGANYIKE.
Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho
lakini nasisitiza wanawake waipigie kura UKAWA kwa sababu
ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu zinazogusa
maisha ya wanawake moja kwa moja.
Kwanza UKAWA wana agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo
Kikuu. Hili ni muhimu kwa sababu elimu ndiyo msingi wa
maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike,
familia na taifa zima.
Pili UKAWA wana agenda ya kuandika Katiba Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi. Moja ya jambo muhimu
katika Katiba ya wananchi ni kuweka uhusiano mpya kati ya
viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi
kujitajirisha kwa mali za umma huku mamilioni ya wananchi
wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.
Fedha za nchi zinazotafunwa na watawala wachache
zitatumika kwa mfano kuboresha elimu, huduma za
afya,maji, umeme, kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya watu
ajira. Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya
kuhakikisha uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya
maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.
Kashalika Katiba Mpya italeta usawa wa kweli wa kijinsia
nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri uchaguzi wa
2020 kwa kutoa idadi sawa wanawake na wanaume madiwani
kwenye kata na idadi sawa ya wabunge wanawake na wanaume
majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa
mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.
Utaratibu wa viti maaluma utatumika kwa watu wenye
ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa mbunge
mwanamke na mwanaume. Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a
kweli kuhusu usawa wa kijinsia unaotakiwa Tanania ili nchi
yetu na watu wake waondokane na umaskini.
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama vinajinasibu eti
vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea
mwenza au mgombea wa Urais. Ni sawa lakini hiyo ni geresha
ya danganya toto kwa sababu kwa mfumo wa sasa ambapo usawa
wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba wanawake
wanatumika tu kama wanaume kupitisha sheria na sera za
maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi
wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.
Usawa wa jinsia wa kweli na wa kudumu hauwezi kufikiwa
hapa nchini bila Katiba Mpya ya wananchi kuandikwa na
kuweka misingi ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa
vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya
kugombea na kushinda sawa na wanaume majimboni na kwenye
kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya
nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake na wale wote wanaofanya
kampeni UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli
kwamba wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha yao
wachague UKAWA ndio waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda
ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa
kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya
wananchi.
Swali la Pili: Watanzania tufanye nini kuzuia CCM kuiba
kura uchaguzi wa mwaka huu 2015? Mimi napendekeza
yafuatayo:
Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM
mnaouchukia kuona watu wengi wanateseka kwa umaskini na
watawala wachache wana utajiri wa kupindukia, kinachotakiwa
kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo wa
kubadilisha maisha ya kimaskini wanayoishi mamilioni ya
Watanzania, ni kutunza kitambulisho chako (kichinjio) na
siku ya kupiga kura tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda
kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja
unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA
kwa sababu wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA wana ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na
maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya
kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini
unaotengenezwa kwa serikali ya CCM kukwapua fedha za
wananchi na jeuri ya kupora madaraka ya wananchi—yaani
CCM kujifanya chama dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki nzima
hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate
tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura maana hakuna ukombozi
wenye kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi wengi
ambao hupatikana katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa
bila wananchi wenyewe kushiriki kuleta mabadiliko hayo
kupitia sanduku huru la kura.
Umaskini wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa
ajira ya kuwapatia walio wengi wasio watumishi wa umma
fedha za kujikimu. Watumishi wengi wa umma mfano walimu,
madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa
mshahara isiyokidhi mahitaji ya msingi kama vile chakula,
mavazi na malazi.
Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda
mrefu. Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji, watu
kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache wakiugua
wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa nchi
za nje.
Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina
chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo
mbinu mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu wenye
ubora na wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile
wanaheshimiwa, kuthaminiwa na kulipwa vizuri.
Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi
kunakojidhihirisha kwa vyombo vya dola hasa polisi
kutumika kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi yetu
bado iko kwenye ukoloni.
Pili: Kila kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura
anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi wengi anapaswa
kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na
asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe
mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji,
mtaa , polisi , mgambo au mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa wanapita nyumba kwa
nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba
kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na kuwaogopesha
wananchi wanaotaka mabadiliko ambao Rais Mstaafu Benjami
Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.
Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili
wasipige kura ya kuwaletea mabadiliko kwa kuikataa
CCMambayo utawala wake umewafanya wananchi wengi kuwa
malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali ya CCM
wakijilipa fdha za wananchi na kupata utajiri wa kukufuru.
Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula
watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni
walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni maana
pengine hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka
jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki kuu ambazo
nyingine zilibebwa kwa tandarusi. Ni fedha za wananchi
kuleni na kama ni nguo vaeni ni mali yenu lakini usimpe
tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine
na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini
wataifanya miaka 5 ijayo.
Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA awaeleze wananchi ukweli
huu. Wananchi wakiujua ukweli kuhusu chimbuko la matatizo
yanayowakabili kuwa ni serikali ya CCM kama taasisi
kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka,
wananchi wataelewa na watapiga kura kikamilifu kuleta
mabadiliko—kuchagua UKAWA kuendesha serikali tuone miaka
mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini.
Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu na
Katiba Mpya uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia
sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama kwa
kuzingatia sera za maendeleo umaskini unaowasumbua
Watanzania wengi hautaondoka nchini.
Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na maisha ya
mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki,
hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu
wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya
kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi ikamilike. Maana
kwenye uchaguzi wakala ukipepesa ukipepesa macho kidogo tu
wajanja wanachakachua.
Nne: UKAWA kuweka mawakala makini ambao siyo mamluki wa
CCM-- watu jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua kusoma,
kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya
walio wengi wanaoteseka na maisha duni. Kura ni hesabu kwa
mtu asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu ni rahisi sana
KUDANGANYIKA maana hataweza kusoma na kuelewa
kilichoandikwa.
Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye
anaweza kuvumilia njaa ikibidi kukaa bila kula na kunywa
kwa zaidi ya saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa
kuendekeza ulaji na unywaji wakiwa kazini kwenye vituo vya
kupiga kura, waliagiza vinywaji na vyakula na vinywaji.
Lakini wajanja waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo
dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na walikuja
kuamka uchaguzi ulikuwa umewisha na kura za mgombea wao
ambaye alikuwa anapendwa na watu amekwishaibiwa kura zake
wakiwa usingizini.
Ninachosema hapa ni kwamba uchaguzi ni wa mwaka huu ni
mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo
wanaCCM wengi tu) na kikundi cha watawala wa CCM
wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.
Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini wakiamua
kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa
CCM uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara ya
kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi Tanzania.
Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi wanaoishi maisha ya
kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni kubwa
kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi
nchini kwetu.
Sita: UKAWA wahakikishe inawaelekeza mawakala wake mambo
muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.
Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha wanachukua kwa usahihi
matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri
kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.
Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni kuhakikisha
waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na
Rais hawachakachui matokeo. Umma ukiwa unafuatilia
0 comments:
Post a Comment