Pole sana bw Malata na pia hongera kwa kutumia muda wako kutafuta michango ya mtu mmoja uliodhai kwufanya hivyo utakuwa umefanya utafiti wa maana. Kwa mtizamo wangu naona unamuda mwingi wa ziada kiasi kwamba badala ya kuandaa masomo ya wanafunzi wako unakwenda kushinda kwenye Maktaba kusoma michango ya mtu kwenye mitaandao ya kijamii. Na kutoka hapo unakuwa umefikia tamati ya mtu huyu anahitaji toba. Pengine nahitaji niwaza nje ya box, pengine ulitaka kufikisha ujumbe kwa mtu huyu kwamba habari zako zote ulizoandika zipo mahala na kuna siku zitakutia matatani? Na pengine ujumbe kwa watu wengine pia?
Nitaomba kumradhi kwa machache nitakayoandika hapo chini, sina maana ya kuwadharau wasomi wote, lakini kwa namna moja au nyingine unapopata watu wanaopoteza muda wa kwenda kusoma habari za michango ya mtu si ndipo sisi waafrika inapofika tamati ya kushughulikia vitu vya mtu ambavyo havina faida kwako wala kwa jamii yetu.
Kama kisa cha kufanya yote hayo ni kwa sababu ya utofauti ya itikadi, basi hata wewe bwana Malata unahitaji toba, kama unavyomshangaa nyani mwingine naye anakushangaa hivyo hivyo, kama unamuona u mwingine haeleweki kwa msimamo wake, naye atakuwa aa mana hiyo hiyo. Mara kadhaauna watjamvini wametoa ushauri mzuri sana, kwa tuvumiliana pale tunapokuwa na utofauti wa mawazo. Usiwe unaumia roho kwa kibano cha mtu unayemshabikia, kuna watu wa upande mwingine wanajisikia kama wewe mtu wao anapota kibano.
Miaka ya kale wafalme walikuwa wakn mstwa mbele kupigania himaya zao, siku hizi wao wapo majumbani na watu kama mimi na wewe ndiyo tunaweza tukatoana roho kwa kutetea huyo aliyepumzika kitandani mwake. Punguza ghadhabu, utasema huna ghadhabu, kitendo cha kweda kushinda maktaba kuna kitu kilikuwa kimekukera kiasi kwamba kila kikitu kwako kikwa hakinathamani hadi pale utakapopata ukweli juu ya mtu. Je tutegemee kualikwa kwenye ufuzuji wa research, wenzako wamefanya research kuhusu ganda la korosho.
On Sunday, 27 September 2015, 15:05, 'Malata.' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Fumbuka na wengine…!!!!
Nafikiri tunahitaji toba!! Toba ya kweli kwa Mungu wetu na mbele ya watu wetu. Hii inatokana na ukweli kuwa tumekuwa watu wazito kusema "hapana" kwa kile tunachokiamini na kulazimisha wengine wakubaliane na kile tunachokiamini kwa hoja nyepesi kabisa. Watu tulioaminika kuwa ni Public Intellectuals tumefika mahali tunaisaliti jamii yetu!!!? [Wasomi kizimbani?!!] Tumenaswa katika mikoba ya uchawi wa Giningi na kusahau kabisa uganga (Udaktari) ambao tumeusomea na kufuzu kwa viwango vilivyotukuka. Historia itatuhukumu!. Nakumbuka 2007 , usiku mmoja katika kumbukizi/tafakari ya maisha ya marehemu Prof. CSL Chachage niliwaeleza wanazuoni waliokusanyika kwa ajili ya tukio lile kuwa jamii yetu ipo katika kitu inaitwa " apocalyptic moment". Hali tata inayodhihirisha fumbo la maisha yetu . Fumbo hili ni kwamba, kuna pengo kubwa kati ya ukweli wa maisha yetu na jitihada za mantiki tunayotumia ili kuona ukweli huo . Unaweza kujisomea zaidi kwa kubonyeza HAPA
Hakika nimepata shida kidogo kipindi hiki.Nimelazimika wakati mwingine kushinda maktaba kujaribu kujiridhisha juu ya baadhi ya watu na michango yao hapa jukwaani na kuishia kufedheheka tu.Mfano mzuri ni mama NKYA!! Nimefanikiwa kupata makala zake za kutosha tu tangu 2010 hadi sasa.Yeye ni mmoja wa wale wanaohitaji TOBA kwa kweli.Kimsingi tumesahau wajibu wetu kwa jamii yetu, na historia itatuhukumu.
Kazi ya mja kunena.
______________________________
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
A D D R E S SWithout "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
John J. Malata
Secretary General,
Society Empowerment Agency
Mobile: +255 782366090Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment