Lakini jamani hayo maneno kasema Lowasa mmeyakubali siku anao watuhumu wakikanusa mnasemaje?
Kwenye mkanganyiko kama huo ndiyo huwa kuna haja ya mahakama.
Kwani katika hali ya kawaida unategemea Lowasa aseme nini?
Walewale
On Aug 1, 2015 10:41 PM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- Kama Lowasa akipona la Richmond anaweza kujiosha na fedha alizokuwa akizisambaza makanisani na misikitini na kwingineko?? alipoulizwa akasema anachangiwa na rafiki zake. lakini hakujibu lengo la marafikizake hao ni nini. Bado anaungwa mkono kwa saabu ya kujibu la richmond?
--------------------------------------------
On Sat, 8/1/15, Ireneus Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] RE: [Mabadiliko] NINAMUUNGA MKONO LOWASSA KUGOMBEA URAIS
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, August 1, 2015, 10:45 AM
Mama
Nkya
Haya yote Ni marudio Tu. Tumeshayasikia
tokea vinywa mbali mbali.
Kwanini mnapindisha ukweli? Huyu huyu Dr Slaa
alisema kuwa Ana ushahidi kuhusu Richmond Na Yuko tayari
kuuwasilisha mahakamani kama tu ENL atapelekwa kwa
pilato.
Mbona hamuhoji hayo
tena au siyo ya msingi sababu Mkaskazini huyu keshakuwa
malaika na automatically msafi kwa kubadili jezi? Hawa jamaa
ni wajanja wamecheza na nyakati wamehit kwenye msumari wa
moto ukiwa haujapoa. Watu wamecheza na fursa adimu. Kimsingi
wana malengo tofauti. Huyu ana hasira ya kuikomoa CCM hawa
wanacheza na akili hiyo kujijenga kisiasa zaidi kwani
popularity itaongezeka, status itapanda, watavuna wafuasi
wengi at ago na si lazima waingie ikulu but watakuwa
wamegain sana hata kuongeza wabunge 50 from the current
number.
Next move atakuja
Chenge. Ukihama CCM si unatakasika automatic? Huyu bwana ana
team oliyojiuzuru naye. Sijawasikia wao kuhama au wanapima
upepo bado hadi ufanyike uchaguzi. Hawa wote ndani ya Ukawa
ni watukufu na wasafi hivi karibuni watajoin majeshi na
kubadili jezi. Hawa hawa waliokuwa wanawaponda
watawashangilia sana na kuwaita majembe!
Ninaamini Mbowe, Slaa,
Lipumba, Mbatia, na UKAWA top yote hawampendi ENL ila
wametumia fursa hii kuachieve strategy zao za kisiasa. Time
will tell. Kumsafisha au kutomsafisha haihusu sana.
Washasema ilikuwa ni mambo ya kisiasa zaidi so watapima
matokeo baadaye! Muhimu ni kugain tu kwa sasa kabla ENL
hajarudi kwenye normal senses.
Tutaona mwisho wa haya... Heri sisi
tusiofungamana na kipande yoyote.... Tunahitaji mabadiliko
ya kweli sio ya kinafiki. Msituchanganye! Jana mlikuja
kivingine, Leo mnakuja hivi kesho hatujui mtakuja na lipi.
Tuonyeshe dira na dhamira sio mikakati ya fursa za zimamoto.
Umesababisha mke wa mtu aachwe, alipopewa
talaka tu, eti ndio na wewe unatangaza ndoa halafu eti
tukuchangie. Tutafika? Siasa mchezo mchafu!From:
'ananilea
nkya' via Mabadiliko Forum
Sent:
01/08/2015
01:21
To:
mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc:
WANA
BIDII
Subject:
[Mabadiliko] NINAMUUNGA MKONO
LOWASSA KUGOMBEA URAIS
Mimi Ananilea Nkya tatizo langu kubwa kwa
Lowassa lilikuwa ni ufisadi wa Richmond uliotafuna zaidi ya
shilingi bilion 172 za wananchi. Baada ya kusikia kauli yake
alipohojiwa na wanahabari siku alipojiunga na CHADEMA, na
baada ya kujiridhisha kuwa kama alikuwa amehusika na ufisadi
wa Richmond leo angelikuwa jela kama Yona na Mramba,
namuunga mkono kugombea Urais. Naamini hata Dr Slaa
amemkubali Lowassa kuwa mgombea Urais wa vyama vinanyounda
UKAWA baada ya kujiridhisha kuwa mamlaka ya juu ilimbebesha
Lowassa kashfa ya Richmond ili kunusuru serikali nzima
kuanguka.
Lakini zaidi
nimeongeza imani yangu kwa Lowassa baada ya kubaini kuwa
hata Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere alimuona kama
kijana makini mwenye maono na dhamira safi ya kuwatumikia
Watanzania. Mwaka 1995 wakati Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
anamaliza muda wake mwandishi wa habari Mwita Matinyi
alimuliza Mwalimu Nyerere alikuwa anafikiri ni nani angeweza
kumrithi Mwinyi kuiongoza Tanzania. Mwalimu alijibu Matinyi
hivi. Nanukuu:
Ni kweli Mzee Mwinyi
anaondoka lakini ndani ya CCM kuna viongozi wengi wenye sifa
za kuwaongoza Watanzania, kikubwa tu awe na dhamira kwa
mfano wapo wakina Warioba, Mzee Msuya na Mark Bomani na wapo
vijana hodari na wenye upeo mkubwa sana kama Mkapa, Kikwete
na Lowassa ni jambo la heri sana CCM kuwa na watu kama hawa
(Majira 26/5/1995) ukurasa wa 3; na Nipashe 26/5/95 ukurasa
wa 3).
Pia nikiwa ripota
Radio Tanzania Dar es Salaam niliwahi kufanya kazi na
Lowassa katika miaka ya 90. Nilivyouona utendaji wake wa
kazi zama hizo nashawishika kwamba anafaa kuwa kiongozi wa
nchi yetu. Nilishuhudia akijituma kweli kweli kwenye kazi za
umma zama hizo.
Kadhalika
namuunga mkono Lowassa kwa sababu hagombei Urais kupitia
chama cha CCM ambacho kinakumbatia mfumo wa kuwadhawau na
kuwafukarisha wananchi huku watawala wachache wakineemeka
kwa kutumia rasilimali za nchi kama vile nchi hii ni mali ya
watawala, familia zao na marafiki za. Ninaamini kwa kugombea
Urais kupitia UKAWA, CCM itapunguziwa dharau na jeuri yake
dhidi ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya mwisho kuhusu
hatma ya nchi yetu. Mfano CCM mwaka jana 2014 ilionyesha
dharau kubwa sana kwa wananchi kwa kuizika Rasimu ya Katiba
iliyotengenezwa kwa kutumia maoni ya wananchi wakati fedha
zaidi ya bilioni 130 zilitumika. Kwa kutumia mabilioni hayo
bila Katiba Mpya kupatikana ni kufisadi mali za wananchi
mchana kweupe. Haikubaliki.
Vile vile namuunga mkono Lowassa kwa kwa sababu
anaukataa hadharani umaskini wa kuchongwa ambao watawala
wanautumia kwa faida yao ili waendelee kuwanunua wananchi
mafukara wakati wa uchaguzi na wakishapata madaraka
waendelee kujineemesha na mali za nchi.
Nchi yetu siyo maskini bali watawala
wanaendekeza matakwa ya wawekezaji (wakoloni wa zama hizi za
utandawazi wizi) ambao wanaliibia taifa rasilimali nyingi na
na hatimaye nchi za wawekezaji hao (donors)wanawapoza
watawala kwa vijimisaadaa uchwara. Ni aibu sana kwa kiongozi
wa Tanzania kijipitisha nchi moja hadi nyingine Marekani,
Ulaya, China, India na Ausralia n.k kutembeza bakuli (omba
omba kama matonya vile) huku nchi yetu ikiwa na rasilimali
tele. Tena wakati watawala wanakwenda kuomba eti wanapanda
ndege daraja la kwanza. Huu ni wenda wazimu. Ni kuiaibisha
Tanzania na Afrika.
Sina
chama cha siasa ninachofungamana nacho kwa sasa, lakini
namuunga mkono Lowassa kugombea Urais kupitia UKAWA kwa
sababu naamini akiwa Rais wa nchi yetu upuuzi huu wa
kuendekeza umaskini kwa kuomba omba nchi za nje huku tukitoa
mali za nchi honyo hovyo kwa wageni na kuamini kuwa
maendeleo ya nchi yetu yataletwa kwa misaada kutoka nje,
kutakomeshwa. Naamini hata hao wakoloni wa zama hizi za
utandawazi wizi wanajua Lowassa hatachekacheka nao.
Lakini zaidi namuunga mkono
Lowassa kwa sababu Watanzania wakiridhia kwenye sanduku huru
la kura hapo Oktoba awe Rais wa Tanzania, vyama vinavyounda
UKAWA vitasimamia kuhakikisha kuwa mamlaka ya wanannchi
hayaporwi hivyo hovyo tena. Kwa hiyo Rasimu ya Katiba ya
wananchi itaheshimiwa na nchi yetu itapata Katiba Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi. Kwa kufanya hivyo taifa
hili litaanza kupiga hatua kubwa ya kuondoa ufukarishwaji wa
wananchi walio wengi unaofanya na watawala wa CCM kwa
kushirikiana na wakoloni wa zama hizi za utandawazi wizi.
Naridhia andiko langu hili
lichapishwe na yeyote anayetaka
Ananilea
Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Unapokea
Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la
'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye
Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more
options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Mabadiliko Forum" group.
To
unsubscribe from this group and stop receiving emails from
it, send an email to
mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to
mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit
this group at
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit
https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1438381307.95951.YahooMailBasic%40web121006.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment