Friday, 21 August 2015

Re: [wanabidii] Mbeya wahoji uadilifu viongozi wa Ukawa

Naye Lowassa mwanae abakwe ndipo atakapo eleza vyema tofauti ya Shetia na Siasa


Sent from my LG Mobile


------ Original message------

From: 'jbifabusha' via Wanabidii

Date: Fri, 21 Aug 2015 6:56 PM

To: wanabidii@googlegroups.com;

Subject:Re: [wanabidii] Mbeya wahoji uadilifu viongozi wa Ukawa


Ebu nijuze Rais mamlaka yake ya kusamehe wafungwa yakoje kisheria?


Sent from Samsung Mobile



-------- Original message --------
From: 'leonard magwayega' via Wanabidii >
Date:
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mbeya wahoji uadilifu viongozi wa Ukawa


Kesi ya Babu Seya nilowatumia ni ya uamuzi wa Mahakama kuu. Sasa natuma ya Mahakama ya rufaa halafu tumpime Lowassa na Mbowe wake kama hawataingilia uhuru wa Mahakama.
Adv. Leonard Elias Magwayega (a.k.a Bob Leo)



On Friday, August 21, 2015 6:30 PM, leonard magwayega > wrote:


Hongera sana mwandishi wa habari hii gazeti la Raia mwema. Kimsingi hata mimi nilishtuka sana kumsikia Rais mtarajiwa akiahidi hadharani ku frustrate maamuzi ya Mhimili wa mahakama bila hata kusema atatumia sheria ipi. Tunajua Rais ana mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria nyingine. Lakini msamaha huo hautolewi kihorelahorela na kwa kosa lolote tu bila kufuata guideline zilizopo. Babu Seya kwa kosa aliloshtakiwa na kufungwa kwalo haliko na muda wa kifungo alichopewa (Maisha) halimo katika orodha ya makosa ya kusamehewa na kutolewa jela. Sijui huyu atakuwa ni Rais wa aina gani. Nadhani Lowassa amepoteza uwezo wa kutafakari kwa kina na anaoambatana nao pia ni laymen kwa mambo mengi tu achana kuwa laypersons wa kisheria tu.Huyo mwenyekiti wa CDM ndo layman wa mambo mengi sana na hata anayodhani anajua anayajua kijuujuu tu na nadhani hata washabiki wao wengi ni wa aina hiyohiyo. Wakipewa viroba, wakawekewa mafuta kwenye bodaboda, posho kidogo iso zidi 20000 wako tayari kuandamana na kushangilia lolote litokalo vinywani mwa hao wakubwa zao. Hivi wewe ambaye una mtoto wako wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 10 na kurudi chini hadi 6 anapobakwa tena kwa namna ile ya kuchangiwa na watu zaidi ya mmoja na akaharibiwa sehemu zake za siri mbele na nyuma utakuwa na ushujaa wa kumshangilia rais ajaye anyesema atawaachia huru wabakaji wa aina ya Babu seya? Mahakama ya Rufaa ndiyo chombo cha juu kabisa cha utoaji haki nchini kwetu na ina majaji weredi sana na kwa hiyo uamuzi wake ni wa mwisho. Leo unawezaje kuwa na rais ambaye anasisitiza kuwa ataingilia uhuru wa Mahakama? kwa wale msiojua hukumu hiyo ngoja niwatumie angalau mpate mawili matatu kisha tutaendelea na majadiliano ikiwa mtaona inafaa.
Leonard Elias Magwayega (Esq)



On Thursday, August 20, 2015 10:43 AM, 'Lesian Mollel' via Wanabidii > wrote:


Hizi mbwembwe tu bro emma subiri filimbi ipulizwe watakimbia wenyewe,ukawa tumejipanga vilivyo na jk atfute mbeleko yenye kamba ya katani original ambebee huyu mtu wake cc wwtunatasukumwa na nguvu ya umma,peeeoples
Lesian

Emmanuel Muganda > wrote:

Naona kampeni zimeshaanza. Lakini ngoma ya mwaka huu ni ngumu.
em

2015-08-19 7:07 GMT-04:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:

Felix Mwakyembe
 
  Chadema sasa wakwepa ajenda yaufisadi
    Kauli ya kumwachia Babu Seya yashtua polisi

MKUTANO wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) uliofanyikakatika viwanja vya Shule ya Msingi Luanda jijini Mbeya wiki iliyopita, umeachasimulizi na mikanganyiko miongoni mwa wakazi wa jijini hapa.
Umati uliohudhuria mkutano huo umeacha simulizi kutokana nawingi wa watu wakiwa kutoka wilaya zote za Mkoa Rukwa, Iringa na Ruvuma.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ujio waoulikuwa mahsusi kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa mgombea wao, Edward Lowassa,ambaye naye alihutubia mkutano huo kwa muda usiozidi dakika ishirini.
Hotuba ya mgombea huyo iliacha mkanganyiko pale alipotoaahadi ya kumwachia mwanamuziki nguli wa dansi nchini, Nguza Vickinganayetumikia kifungo baada ya kukutwa na hatia, ikiwamo ya kuwanajisi watoto.

Baadhi ya watu waliokuwapo mkutanoni hawakusubirikuitafakari ahadi ile baadaye, bali walianza mjadala muda ule ule, wakihojimantiki ya ahadi ya mgombea huyo kumwachia huru mtu ambaye hata Mahakama yaRufaa nchini ilimtia hatiani.

"…kumwachia Babu Seya tena, hii kali ya mwaka, wale majajiwa Mahakama ya Rufaa wako vizuri sana, asingekuwa na hatiawangemwachia,"alisikika askari mmoja wa Jeshi la Polisi aliyekuwapo mkutanonipale mara baada ya ahadi hiyo kutolewa.

Mbali ya ahadi hiyo yenye shaka kutoka kwa mgombea huyo waUkawa, ahadi yake hiyo, iwapo itatekelezwa, inatajwa kuwa ni sawa na uvurugajiwa utawala bora, lakini pia naye Mwenyekiti wa Chadema alifanya tukiolililodhihiri baadaye kuwa ni kituko cha aina yake.

Mbowe, kwa mbwembwe, aliwatangaza wanachama wapyawaliojiunga na chama hicho siku hiyo ya mkutano, na miongoni mwao ni wabungewawili waliomaliza muda wao, Mchungaji Luckson Mwanjale, Jimbo la MbeyaVijijini na Modestus Kilufi, Jimbo la Mbarali. Wote wakiwa kutoka CCM.
Hata hivyo ni Kilufi pekee aliyejitokeza uwanjani pale nakutambulishwa, wakati Mwanjale aliitwa mara kadhaa na Mbowe pasipo kutokeza.Akiwatambulisha, Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema; "walipokuwa katika chamachao cha zamani walitufanyia nanihino, tuwapokee!"

Mwenyekiti huyo aliitikiwa na umati uliokuwepo wakisemawapokee, lakini muda wote huo Mchungaji Mwanjale hakuwepo uwanjani hapo, hatuailiyosababisha Mbowe kutoa kauli nyingine tata akidai inawezekana mbunge huyoamechelewa kutokana na msongamano wa magari lakini angefika uwanjani hapo.

Kutokana na tukio hilo la kutangazwa na kutonekana,waandishi wa habari walianza kumtafuta Mwanjale ili kupata kauli yake naalipopatikana alionyesha kushangazwa na taarifa hizo za yeye kujiunga Chadema,akisema hajawahi kuwaza jambo hilo na kwamba asingeweza kujiunga na chama hichokabla ya kushauriana na familia yake.

Katika mahojiano yake na Raia Mwema kwa njia ya simu,Mchungaji Mwanjale alisema kuwa wakati msafara wa Lowassa ukiwasili katikaUwanja wa Ndege Songwe, naye alikuwepo akiwa pamoja na jamaa zake na kwa sababuni mtu wanayefahamiana alisalimiana naye.

Mchungaji Mwanjale anasema inawezekana lile tukio la yeyekusalimiana na Lowassa lilichukuliwa kimakosa na baadhi ya watu wakiwemoviongozi wa Chadema, kwamba kwao alikuwa amejiunga tayari na chama hicho.
"Makamo haya unaenda Chadema ili iwe nini, pamoja na makosaya chama, wengine kutotendewa haki, sina mawazo ya kuhama chama," alisemaMwanjale.

Wakati mchungaji huyo akikanusha, baadhi ya wadau wa siasaza Mbeya nao wanahoji mantiki ya kiongozi mkuu wa Chadema kutangaza jamboambalo hana uhakika nalo. Wanabainisha kuwa kama ni kweli hakukuwa namawasiliano basi viongozi hao wanawakosea wenzao staha.

Wakati Mchungaji Mwanjale akitangazwa kwenye mkutano wahadhara, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile naye alizushiwakuhamia Chadema lakini katika kipindi kifupi kiongozi huyo alikanusha, akisemahajawahi kuwazia jambo hilo na kwamba bado yupo CCM na hajabadilika.

"Kwa umri wetu huu, sio kuhama vyama, bali unampigia yuleunayemuona anafaa na mwenye uwezo wa kutuongoza," anasema Mzee Mwakipesilekatika mahojiano ya simu na mwandishi wetu, na kuongeza; "Lowassa tunafahamianana alikuwa kiongozi wangu, tumefanya naye kazi akiwa Waziri Mkuu mimi nikiwaMkuu wa Mkoa, tulikuwa naye bungeni kwa miaka 10, inawezekana watu wanatumiavibaya uhusiano wetu huo."

Taarifa za kuhama kwa wanasiasa hao zilikuwepo kabla ya ujiowa Lowassa Mbeya, na wote, sababu kuu ya kuzushiwa ikiwa ni ukaribu wao namgombea huyo wa Chadema.
"Tatizo Chadema wanatafuta watu wote waliokuwa jirani naLowassa akiwa CCM, wanachanganya urafiki na itikadi, huo ni udhaifu mkubwa,"anasema Charles Mwakipesile aliyekuwa miongoni mwa watangaza nia wa CCM na kushikanafasi ya tatu katika kuwania ubunge Jimbo la Mbeya Mjini.

Mwakipesile ambaye pia anashikilia nafasi mbalimbali zauongozi ndani ya CCM anasema kuwa wanachama wenzao wanaokimbilia Chadema baadaya kushindwa kwenye kura za maoni wanadhihirisha umamluki wao walipokuwa ndaniya chama hicho.

"Mtu amekuwa kiongozi wa miaka mitano, leo anaondoka baadaya kuanguka huku akitoa kashfa lukuki kwa chama kile kile alichokitumikia, niudhaifu mkubwa," anasema Mwakipesile na kuongeza; "….mimi nawaheshimu sanawanaohama bila ya msukumo wa kuanguka kwenye uchaguzi, hao ni wakomavu wakisiasa."

Chanzo cha ndani, waliokuwapo Uwanja wa Ndege Songwekumpokea Lowassa vinabainisha kilichojitokeza Mchungaji Mwanjali alipokwendakumsalimia Lowassa ni utani uliokuwepo akihamasishwa kuhamia Chadema nayeakajibu, "tupo pamoja."
Chanzo hicho kinabainisha kuwa yawezekana Chademawalichukulia kauli ile kama jibu la kukubali kwa Mchungaji huyo kuhamia kwao.Katika kuthibitisha hilo, chanzo hicho kinasema ndio maana hata Mbowe alitoa kaulimbili, kwanza akisema yupo hapa, kwa maana ya mkutanoni na ilipobainika hayupoakasema inawezekana amekwama njiani kutokana na msongamano wa magari.

Katika mkutano huo walikuwepo viongozi mbalimbali wa vyamavinavyounda Ukawa akiwamo, Mgombea Mwenza katika urais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Juma Duni, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Dk.Emmanuel Makaidi.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi alikuwa miongoni mwawazungumzaji katika mkutano huo, ambapo pamoja na mambo mengine alikituhumuChama Cha Mapinduzi (CCM), kuingiza mkoani humo shahada 5,000 za kupigia kurana kutishia akisema; "…wakijaribu kufunga goli la mkono tutatuma beki kuzuia,kule pembezoni akifunga tunakata kiganja kwa nyengo, mteule wa CCM kaingizwabweni la zeluzelu."

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alimshauri RaisJakaya Kikwete kuwa mtulivu na msikivu pamoja na chama chake katika kipindihiki. Pamoja na ushari kwa Rais Kikwete, aliwasihi pia wananchi wa Mkoa waMbeya kuhubiri amani ili uchaguzi uwe wa amani pasipo kubaguana.

Hata hivyo Mwenyekiti Mwenza kwenye Ukawa, Freeman Mbowealisema umoja huo hautapiga magoti kuwabembeleza Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) iwapo wataona wanaonewa bali watajibu kwa vitendo.
"Ukawa hatutopiga magoti tukiona tunaonewa, tutachukua…,"akajibiwa na umati uliohudhuria "action!"

Pamoja na ahadi yake ya kumwachia Babu Seya iwapo ataingiamadarakani, Lowassa pia aliahidi kulibadili Jiji la Mbeya na kuwa la kimataifapamoja na Uwanja wa Ndege wa Songwe nao uwe wa kimataifa. Nao baadhi yawasikilizaji katika mkutano huo wakasemezana wakihoji; "kwani sasa sio wakimataifa?"

Katika jambo lililowashangaza baadhi ya wafuatiliaji wasiasa mkoani humo, ni hatua ya viongozi wa Ukawa kukwepa ajenda yao ya ufisadi,ajenda iliyowajenga na kuwapambanua kama viongozi makini wanaochukizwa na halihiyo nchini ambayo imekuwa ikifichuliwa karibu kila mwaka na ripoti za Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Katika mkutano wa Mbeya, sio Mbowe wala Mbatia au Makaidialiyethubutu kutamka neno, fisadi au ufisadi. Hatua hiyo iliwafadhaishabaadhiya wapenzi wa mageuzi mkoani humo, wakibainisha kuwa wametelekezwa naviongozi wao.

"Watu wamepoteza maisha, Mwalukali alipigwa risasi hapa naleo hii ana ulemavu wa mkono, tuliwaamini kuwa wanapigania haki, tukaingiabarabarani, leo hii wamethamni pesa zaidi kuliko sisi, siasa chafu kabisahizi," alisikika mkazi wa Soweto beya akilalamika

Chanzo Raia Mwema Toleo la 419, 19 Aug 2015
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

0 comments:

Post a Comment