Monday, 24 August 2015

Re: [wanabidii] Maana ya upumbavu kwa mujibu wa Sugu na wengine wataalamu

Japo mimi sio mwana-UKAWA waka mwana-CCM, ila ni bayana kuwa aliyeandika hizi point 10 hapo juu NI MPUMBAVU. Kwa kuwa hakujiandika jina lake/sahihi yake mwishoni, naomba ndugu ELISA MUHINGO umsaidie kujitambua hivyo, na wewe ni vizuri ukawa unajizuia kuleta UPUMBAVU kwenye hili kundi (hata kama PERSONALLY umeufurahia)...

Kundi hili huwa napenda kulichukulia kama mahali pa watu WENYE AKILI TIMAMU, wanaopenda kujadiliana, kubadilishana mawazo na hata KUSHINDANA kwa kutumia AKILI zao na busara zao, lakini inakera pale inapoonekana wazi kwamba kuna watu wanajitahidi KWA MAKUSUDI kufanya mambo hayo kwa kutumia UPUMBAVU wao (badala ya akili zao na busara zao)...!!!

Nadhani ni vizuri mtu kuwa anatumia muda KUTAFAKARI na KUTOFAUTISHA ni mambo gani ambayo anaweza akayaongea "kijiweni" akiwa na "washikaji" na ni mambo gani anaweza akatumia muda KUYA-TYPE na KUYATUMA kwenye kundi lenye watu wengi na tofauti kama hili....

Kuwaita Mawaziri wakuu Wastaafu wa hii JAMHURI kuwa ni WAPUMBAVU, halafu ukawaona walio wateua kuwa wana akili, bila shaka na HUO NI UPUMBAVU mahiri.... Lakini yote hayo hayalisaidii hili taifa tunapoelekea kwenye Uchaguzi. Tujikite katika mambo ambayo yatajenga letu - kabla na baada ya uchaguzi.

Na kama kuna chama au kundi ambalo linadhani linaweza kunufaika kisiasa kwa KUTUNGA NA KUSAMBAZA UPUMBAVU, Basi hicho chama au kundi NI LA WAPUMBAVU...

BILLEGEYA, Mussa,
Twitter: @MBillegeya



Le Lundi 24 août 2015 14h43, 'lang'itomoni lokomoi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> a écrit :


Maana ya upumbavu kwa mujibu wa Sugu na wengine wataalamu

UKIWA UKAWA WEWE NI MPUMBAVU.

Kutokana na SUGU 2013 (BUNGENI) - alitoa maana ya upumbavu Kwa kusema hivi "NAOMBA TAIFA LIELEWE UPUMBAVU SIO TUSI, NI STUPIDITY, LACK OF KNOWLEDGE OF UNDERSTANDING"
Kwa wale wenzangu tusiojua Kiingereza (Sugu ana maana kukosa maarifa na uelewa ndiyo maana sahihi ya UPUMBAVU.

Hivyo UKAWA wote NI wapumbavu kwasababu zifuatazo

1. Kutanguliza FISADI papa kupambana na UFISADI.

2. Kuuza vyama vinne katika mnada mmoja na kutegemea Pesa za mabepari kufanya Kampeni bila kujua wanauza Nchi.

3. Kupambana na mfumo wa CCM kwa kutumia viongozi waliolelewa na mfumo wa CCM.

4. Kusahau kashfa na uchafu wote wa Lowassa ndani ya usiku mmoja.

5. Kuwataka Watanzania wenye ushahidi juu ya Lowasa waende mahakamani na kusahau kuwa walitutangazia wana ushahidi na kumtaka Lowassa kama anaonewa aende mahakamani.

6. UKAWA wote ni wapumbavu na marofa Kwa kupingana na kauli zao wenyewe juu ya UFISADI wa Lowassa.

7. UKAWA wote ni wapumbavu Kwa kushindwa kujua na kukemea ajenda ya siri iliyoanzishwa na chief Mareale na kuendelezwa na Mtei na 2012 kusimamia na Mpumbavu Joshua Nassari.

8. UKAWA wote ni wapumbavu kwa kushindwa kusimamia misingi ya uanzishwaji wa Ukawa na kuwapuuza waasisi wa UKAWA yaani Prof. Lipumba na Dr. Slaa.

9. UKAWA wote ni wapumbavu kwa kuwa kichaka cha kuficha wezi, mafisadi na wapumbavu wengine.

10. Ukiwa mwana UKAWA wewe NI mpumbavu Kwa kukubali kuburuzwa kama "mbuzi" na kushindwa kuhoji Lowasa NI msafi toka lini? Slaa, Mbowe, Lema, Mnyika, Lissu wanamtofautishaje Lowasa wa 2008 na 2015.

Jitafakari, Upo Ukawa hadi sasa? Basi wewe NI mpumbavu Kwa kushindwa kunielewa na kushindwa kujua nia ya mafisadi,Mabepari na wa walanguzi kumpeleka Lowasa ikulu.

Acha kuwa mpumbavu na lofa.

UKAWA NI

U - UMOJA
KA - KAMILI WA
WA - WAPUMBAVU
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment