Saturday 15 June 2013

[wanabidii] UPDATES KUTOKA MANYARA: MERRY NAGU NUSURA ACHOMWE MOTO.

Mary Nagu nusura achomwe moto akigawa rushwa ya uchaguzi! Ilikuwa hivi, makamanda wa CHADEMA wakiongozwa na Mbunge wa Karatu, Israel Natse na Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul, walitonywa na askari wa miguu wa Kata ya Bashanet, kuwa CCM wako mahali wameita watu na kuwafungia ndani ya nyumba wakiwapatia rushwa ili wamchague mgombea wao.

Makamanda wa Ki-iraq wakapiga yowe kuita wenzao. Nyumba ikazingirwa, watu wakitaka kuichoma moto, ndani yake akiwemo Nagu na Jitu Soni. CCM wana hali mbaya sana katika kata hiyo ambapo CHADEMA na mgombea wake, Lawrence Tara, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, wanakubalika sana. Polisi kutoka Babati mjini na vijijini ndiyo wamefanikiwa kumwokoa Nagu alfajiri ya leo, baada ya kuzingirwa usiku kucha.

Muda huu ndiyo Kamanda wa Anga, Mbowe anaelekea kata hiyo ya Bashnet kwenda kufunga kazi, kisha atakwenda Dongobesh, Makuyuni, kisha Arusha mjini, Uwanja wa Soweto Kaloleni.

» Kamanda Mbowe amemaliza mkutano wa Bashnet sasa ngoma Dongobesh, Mbulu. Kama ilivyokuwa jana Muheza ambako mikutano ya CCM na CUF ilikufa kwa watu kwenda kusikiliza mikutano ya CHADEMA, leo pia mkutano wa CCM hapa Bashnet umekufa, watu wamekimbilia kumsikiliza Mbowe.

• Mwenyekiti ametoa kauli nzito hapa Bashnet akionya mchezo mchafu wanaofanya CCM Monduli wa kuanza kukodi vijana ili wakawafanyie fujo watu wa CHADEMA, amesema kama vijana wa CHADEMA nao watapewa amri ya kulipiza matendo ya CCM itakuwa ni songombingo ambayo itaharibu nchi.

• CHADEMA hawako tayari kuona damu ya Mtanzania yeyote ili mtu mmoja awe diwani, lakini kwa mambo ya CCM kuanza kufanya vurugu huku vijana hao wakilindwa na polisi, itafika mahali haitakubalika! Amesema ''vijana wa CCM nchi nzima ni 10% wakati wale wa CHADEMA ni 90%, amewataka waache mara moja.

• Nape amepita hapa nusu saa kabla Mkiti Mbowe hajatua, watu walimzomea. Walikuwa na wapambe na masare yao. Mbowe alipofika, wananchi wachache waliokuwepo kwenye mkutano wake wakaondoka kwenda CHADEMA.

Chanzo: Tumaini Makene.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment