Wednesday 26 June 2013

[wanabidii] UHALIFU HUU KARIBU NA MAENEO YA JESHI UDHIBITIWE

UHALIFU HUU KARIBU NA MAENEO YA JESHI UDHIBITIWE

Kuna matukio kadhaa yametokea karibu na maeneo ya jeshi ambayo yanalitia doa jeshi letu la ulinzi na usalama , naomba nitaje machache .

1 – Mbele ya Nyumba ya Mkuu wa zamani wa Majeshi 

Nyumba hiyo iko maeneo ya salasala , kiasi cha wiki kadhaa zilizopita wezi walifanikiwa kuiba kwenye duka linaloangaliana na geti ya kuingilia nyumbani kwa gen mbona na kutokomea gizani , siku nyingine walionekana baadhi ya wahalifu na pikipiki karibu na maeneo hayo lakini wakaondoka .
Maeneo ya salasala kumekuwa na wizi mkubwa wa watu wanaotumia pikipiki tena wanaiba muda wa jioni kuanzia saa 12 mpaka saa 2 tukio la karibuni ni mama mmoja kuibiwa alipokuwa kwenye sehemu yake ya biashara saa 1 usiku .

2 – Maeneo ya Mlalakuwa karibu na kituo cha Basi Mpakani .

Maeneo haya kuna mtu alipigwa usiku wa manane kwa tuhuma za kuvunja na kuiba kwenye dula la rafiki yake ambaye  ana duka hatua chache toka hapo , huyu jamaa wanasema ni polisi jamii , tulitegemea sehemu kama hii angalau kuwe na ulinzi wa uhakika hata wa kulinda watuhumiwa tu .

3 – Kaka Amuua Dadake 

Ni maeneo ya mlalakuwa siku chache zilizopita ambapo kaka alikuwa anamtuhumu dadake kwa kupoteza hela za maji , waligombana kwa masaa zaidi ya 3 huku wananchi wakiangalia hata pale walipopigana na kuachana wananchi waliendelea kujibanza .

Baadaye kaka mtu akaamua kumpiga dadake na stuli kichwani akamuuwa hapo hapo ,halafu akaondoka bila majirani wala mtu mtu yoyote kumfuata .
Ilikuwa bahati nzuri huyu mtu alionwa na dada yao mwingine maeneo ya ubungo wakati anatoka kibaha kwenda kwenye eneo la tukio ndio hapo askari wakaitwa haraka wakamtia mikononi .

Haya ni matukio machache lakini sio ya kupuuzwa hata kidogo haswa yanapotokea mdomoni mwa taasisi ambazo tunatemea saa zote na wakati wowote wawe tayari kulinda maeneo yao ya jirani na hakuna mtu yoyote anayejali wala kusema lolote .

Sasa vyombo vyetu viamke vianze kujiangalia upya kujilinda wao wenyewe ili wajenge imani yao kwa wananchi haswa wale wanaozunguka maeneo yao ,


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Uganda 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment