Thursday 27 June 2013

[wanabidii] Tathmini ya miaka miwili ya Bunge: Wabunge wetu, Je! Waliwajibika?

Picture
Swali muhimu kwa mwananchi yeyote, Je, Mbunge wangu aliwakilishaje maslahi yangu Bungeni? Njia moja ya kutathmini utendaji wa Wabunge ni kutazama idadi ya ushiriki wao Bungeni.

Muhtasari unaoitwa Je, waliwajibika? Tathmini ya miaka miwili ya Bunge 2010-2012 uliyoandaliwa na Twaweza kwa kushirikiana na Centre for Economic Prosperity (CEP). 

Muhtasari unachambua data zinazopatikana kwenye tovuti ya Bunge, kuhusu ushiriki wa kila Mbunge wakati wa vikao vya Bunge. Bunge ndio mhimili wa demokrasia, likiwakilisha wapiga kura katika namna 
wanavyohusiana na dola. Twaweza na CEP zinatoa tathmini ya utendaji wa Wabunge kwa ujumla, kwa kila chama, kwa kila Mbunge na kwa aina ya ushiriki.

Uchambuzi umeonyesha kwamba Wabunge wanaotoka katika vyama vidogovidogo na vyenye viti vichache huwa na wastani wa juu zaidi wa ushiriki. Tathamini hii inazingatia ushiriki uliofanywa na Wabunge katika miaka miwili ya kipindi cha ubunge cha 2010 – 2015. Wabunge wanaweza kushiriki kwa namna tatu: kwa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza na kutoa michango. Katika namna zote hizi, TLP ambacho kina mbunge mmoja na NCCR-MAGEUZI watano, vilikuwa na kiwango kikubwa zaidi chaa ushiriki kwa Mbunge. Hata hivyo, ukiondoa vyama vidogovidogo vyenye chini ya asilimia 5 ya uwakilishi Bungeni, CHADEMA kinafanya vema zaidi, kikifuatiwa na CUF na CCM.

Endelea kusoma: bunge Tanzania utawala

Authors: Thomas Maqway
Editors: Youdi Schipper
Organizations: Centre for Economic Prosperity
Pakua nyaraka
---
Imenukuliwa kutoka: Twaweza.org
Translation in English: MPs in Tanzania: Did they perform? 


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/06/tashmini-ya-miaka-miwili-ya-bunge-wabunge-wetu-je-waliwajibika.html#ixzz2XQQBrIqG

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment