Wednesday 19 June 2013

[wanabidii] Tamko la watetezi wa Haki za Binadamu kuhusu hali ya usalama Arusha

KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU 
KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013


Mtandao wa Wateteziwa Hakiza Binadamu unaounganisha asasi za kiraiazinazotetea haki za binadamu zaidi ya mia moja, pamoja na mashirikawananchama Mkoani Arusha, tumesikitishwa na kushtushwa sana nakauli iliyotolewana Waziriwa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera,Uratibuna Bunge) William Lukuvi dhidi ya asasi zakiraia.

Katika kauli yake Bungeni tarehe 17 mwezi Juni, akizungumzia tukio la bomu d hidi ya wafuasi waChama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), Lukuvi ameendeleza kile ambacho kwa mudamrefu serikalii liyopomadarakani imekuwa ikikifanya yaani kutumia lugha mbaya zakuwachonganisha wateteziwa hakizabinadamu na asasiza kiraia kwa ujumla na kuwaita kwamba niwachochezi, vibaraka wa upinzani na lugha nyingine zenye dhihaka.

"Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la Polisi,kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini askari, kuwafanya raia wasiwapeushirikiano askari na hatimaye kuwa na taifa ambalo halitawaliki," alisema Lukuvi

Kauli kama hii kutolewa kiongozi mkubwa wa serikali tena katika Bunge la Tanzania ni kejeli kwawaliopoteza ndugu zao Mjini Arusha, na ni kauli
ya vitisho dhidi ya asasi zisizo za kiserikali nchini. Nchi yetu imekumbwa na kasumba ya viongozi kuacha kutatua dalili zinazoashiria upotevu waamani na kutaka kuonyesha kuwa asasi za kiraia na makundi mengine ndio chanzo cha matatizohayo. Kauli kama za Mh Lukuvi zimeshatolewa ndani ya miezi sita iliyopita na mawaziri na viongoziwenginewasiopungua watano. Waziri Kagasheki alizishutumu wazi wazi asasi za kirahia zinazoteteahaki za wafugaji Loliondo kuwa ni wachochezi wa mgogoro huo, wakati huo huo Naibu waziri waArdhi aliendeleza shutuma na vitisho hivyo dhidi ya Asasi zinazotetea rasimali ardhi nchini.

Tunamsihi Lukuvi, atambue kuwa imani ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi nchini haijawahikuondolewa na asasi za kiraia, bali huondolewa na matendo ya kidhalimu ya jeshi hilo dhidi yawanachi na vyama vyao. Jeshi la polisi litaweza kurudisha imani kwa wananchi endapo tu litaachakutumika na watawala kwa maslahi binafsi na kisiasa na sio kwa kauli za kubeza zitolewayo naviongozi wa serikali dhidi ya asasi za kiraia na makundi mengine.

Itakumbukwa kwamba hivi karibuni katika uchaguzi wandani wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania ,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, aliwatahadhrisha wanaCCM wasiendelee kulitegemea Jeshi la Polisi kamanguzo yake kisiasa.

Viongozi waache mzaha katika hali ya usalama wa Taifa kwa sasa kwani hakuna anaependa amaniya Taifa itoweke. Hadi sasa matukio ya kutishia amani ya Nchi yamekuwa yakishika kasi bila kuona jitihada za makusudi za kukomesha hali hiyo. Toka kushambuliwa kwa wahariri Saed Kubeneana Ndimara Tegambwage, kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka, kuuwa kwa Mwangosi, Mwenyekitiwa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, kuuwa kwa mapadre na mashekh, mlipuko wa Olasit dhidi ya waumini wa Kanisa katoliki, migogoro ya kidini na mengineyo, hakuna hata limojalillilopatiwa ufumbuzi wa kudumu.

USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI

Mtandao pia unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima uhuru waandishi wa habari, nakuwafukuza waandishi wa habari katika mikusanyiko ya mjini Arusha.Mtandao unalisihi jeshi laPolisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten Ashiraf Bakari, aliyekamatwa tarehe 18/6/2013 katikaeneo la Soweto alipokuwa akichukua picha za matukio ya jeshi la polisi dhidi ya raia waliopigakambi katika viwanja. Tunaalani kitendo cha jeshi la polisi kumkamata bwana Ashirafu aliekuwa navitendea kazi pamoja na kitambulisho chake cha uandishi wa habari.

WITO WETU

  1. Tunamsihi Waziri Lukuvi aifute kauli yake dhidi ya asasi za kirai aambazo kimsingi kwamujibuwa utendaji kazi zao ni Watetezi wa Hakiza Binadamu katika fani mbalimbali na hawahusiki kwanamna yoyote ile katika hali ya sasa ya uvunjufu wa amani unaondelea nchini.
  2. Aidha tunaomba asasi kwa upande wao zisijihusishe naitikadi yoyote ya kisiasa baliwaendeleekuwatumikia Watanzania waitikadizote bilaubaguzi wowote.
  3. Jeshi la polisi mkoani Arusha limwachie mwandishi wa chanel Ten bwana Ashiraf Bakari, nakuwapa uhuru waandishi kureport habari yoyote.
  4. Viongozi wote wakiwemo wa madhebu mabalimbali walaani vikali hali inaoyoendelea Arushakwa sasa.
  5. Balozi mbalimbali na Mashirika mbalimbali kukemea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamuunaoendelea Mjini Arusha.
  6. Viongozi watambue kazi za asasi za kirai na kuzieshimu na kuacha kuwaita wachochezi

Tarehe, 19/06/2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment