Thursday, 20 June 2013

[wanabidii] Sikika: Bado kuna uhaba wa Alu katika vituo afya nchini

Vituo 920 kati ya 5,079 ambavyo ni sawa na asilimia 18.11 vimeripotiwa kutokuwa na aina yoyote ya dawa Mseto ya kutibu malaria (ALu) 'zero stock' hadi kufikia Juni 19, 2013. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa SMS for life wa Wizara ya Afya ambao hutoa uhalisia wa uwepo wa dawa za Alu katika vituo vya huduma za afya vya umma Tanzania bara.

Taarifa za upungufu huo zinakinzana na habari za hivi karibuni zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari zikimnukuu Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisema kwamba kuna akiba ya kutosha ya dawa za Alu kwa kutibu malaria nchi nzima. 

Taarifa hizo sio tu kwamba zinakinzana na takwimu za sasa katika mtandao wa SMS for Life, lakini pia zinapingana na tamko la Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi la  Februari 16 mwaka huu, alipokiri kuwepo kwa uhaba wa ALu nchini, na hivyo kuahidi kulifanyia kazi tatizo hilo, kwa kusambaza dawa kwa haraka katika vituo vilivyoripotiwa kuwa na uhaba mkubwa wakati huo. Waziri Mwinyi alinukuliwa akisema, "Serikali imekiri kuwepo upungufu wa dawa ya kutibu malaria ya mseto (ALu) kutokana na kuchelewa kufika baada ya kuagizwa."

Licha ya Wizara kutumia nguvu na muda mwingi kukanusha taarifa za uhaba wa dawa za ALu zinazotolewa na Sikika, ukweli unabaki kwamba bado kuna uhaba wa dawa hizi katika baadhi ya vituo vya huduma za 
afya. 

Hata hivyo, Sikika inatambua kuwepo kwa mabadiliko kidogo tangu ianze kutoa taarifa za upungufu huo kupitia vyombo vya habari (28/01/2013). Uhaba wa ALu ulikuwa ni asilimia 26 wakati huo na kwa sasa umefikia 18.11%. 

Ingawa matarajio yetu ilikuwa ni kuona uhaba wa Alu ukitoweka kabisa, lakini kwa bahati mbaya hali bado si nzuri hasa katika mikoa hiyo ambayo imekuwa ilivyoripotiwa mara nyingi na Sikika kuwa na uhaba mkubwa. Miongoni mwa wilaya katika mikoa zilizokuwa na uhaba mkubwa wa Alu ni; Geita (70%), Ukerewe (66%) katika mkoa wa Mwanza, Mbinga (55%), Songea (31%) katika mkoa wa Ruvuma, Nzega (61%), Urambo (32%) katika mkoa wa Tabora naBunda (59%), Rorya (52%) katika mkoa wa Mara.

Kulingana na ripoti ya ruzuku ya Global Fund-Tanzania (2013), Tanzania imekuwa ikipatiwa fedha za kutosha kutoka Global Fund (GF) kwa ajili ya mapambano dhidi ya Malaria. Fedha  zilizopitishwa kwa ajili ya Malaria kutoka GF ni dola za kimarekani milioni 350,320,838/ (2012/13 FY) na hivi sasa dola za kimarekani milioni 307,675,487/- tayari zimeshatolewa na kutumika.

Ripoti hiyo ya Global Fund-Tanzania (2013), pia inaonesha kwamba takriban dola za Marekani milioni 60,657,059/- ziliidhinishwa kununua Dawa Mseto aina ya ACTs na dola za Marekani milioni 44,869,885/- sawa na asilimia 74 tayari zilishatolewa. Licha ya fedha hizi kutolewa, uhaba wa dawa ya Alu bado unaendelea.
Ni matarajio yetu kwamba Wizara itaelekeza zaidi juhudi zake kwenye kusambaza dawa ili kuhakikisha uhaba huo unapungua au kuisha hadi kufikia asilimia sifuri. Kwa sasa, bado uhaba wa ALu upo, hususani katika mikoa ileile ambayo awali iliripotiwa na Sikika kuwa na ukosefu mkubwa wa dawa hizo.

Si lengo letu kuendeleza malumbano na Wizara ya Afya lakini tunaishauri kwa mara nyingine tena iwajibike zaidi kwa watanzania kwa kununua na kusambaza dawa hizi kwa wakati ili kupunguza vifo vitokanavyo na Malaria kwa watanzania wasio na hatia.

Mr. Irenei Kiria
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, S.L.P. 12183, Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/06/sikikabado-kuna-uhaba-wa-alu-katika-vituo-afya-nchini.html#ixzz2WlaLeVEN

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment