Sunday 16 June 2013

[wanabidii] Kilicho nyuma ya pazia kwenye mlipuko wa bomu mkutano wa CHADEMA Arusha

Wakuu.

Tunajadiliane kwa kina chenye weledi wa mantiki kuhusu mlipuko wa bomu ulio tokea kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha. Pamoja na mapenzi na itikadi zetu za kisiasa tutangulize maslahi ya nchi yetu mbele na kuiona tunu ya kuishi kuwa ndio shufaa pekee yenye kuweza kuondoshwa kwa mapenzi ya Mungu.

Lakini pia lazima tufungue milango yetu ya fahamu na kutafakari upya siasa zinazo toesha uhai wa wenzetu, lazima tutafakari upya tamaa ya kupenda madaraka na kufikia hatua hata ya kuwa tayari kutoa uhai wa mtanzania mwenzako, lazima tutafakari na kuzikanya nafsi zetu kuwa hakuna aliye mtanzania zaidi kuliko mtanzania mwingine linapo kuja suala la kutaka madaraka.

Yaliyotokea Arusha ni muendelezo wa matukio mabaya tuliyo wahi kuyasikia kwenye siasa za Tanzania. Tumesikia mengi mabaya na yanayo ogofya, lazima tusimame kama Taifa na kuweka kando itikadi za kisiasa na tukemee kwa sauti ya ukali hali hii ya kutoesha amani ya nchi yetu.

Baada ya kusema hayo, hebu tujiulize machache na tupate majibu ya kimantiki kwenye maswali hayo.

1. Hivi chadema walijitathimini kuwa wana enda kushindwa kwenye uchaguzi wa kata hizo na hivyo kuamua kuvuruga uchaguzi kama alivyo nukuliwa Nape kabla ya tukio akisema "Kuna chama kimepanga kuvuruga uchaguzi"?

2. Hivi chadema chenye wafuasi wengi wanao kiunga mkono mkoani Arusha kinaweza kujitupia mabomu ili kipate umaarufu wakati kesho yake walikuwa wanahitaji kuongeza kiongozi?

3. Baadhi ya majeruhi wamekutwa na matundu ya risasi (sio majeraha ya mabomu) kwenye miili yao, je bastola iliyo tumika niya nani? Na kwa nini Polisi walipa mabomu ya machozi badala ya kutoa msaada au kusaka mlipuaji wa bomu?

4. Miongoni mwa walio fariki kwenye mlipuko huo ni kiongozi wa chadema. Je chadema iliamua kufanya shambulio ili kiongozi wake au wawe na hivyo kipate huruma ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi huo? Na kwa nini mikutano ya chadema igubikwe na vifo au matukio mabaya hasa wanapo kuwepo polisi?!

5. Je tuendelee kuviamini vyombo vyetu vya usalama kwa haya yanayoendelea?! Kama ndio kwa nini na kama sio kwa nini? 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment