Wednesday 26 June 2013

[wanabidii] Kagame , Uhuru na Museveni wamtega JK

Katika kile kilichozua minong'ono mingi miongoni mwa wachambuzi wa mambo ni kitendo cha marais watatu wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana katika kikaoo kizito cha kujadili mambo yanayohusu maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao. Hali hiyo imewashangaza wengi kwani hawakuwashirikisha marais wa Tanzania na Burudi kama washirika wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wapo wanaodadisi kuwa uamzi wao kama viongozi wa nchi kuwa na mikakati ya pamoja ya kupambana na umasikini wa wana Afrika mashariki ni jambo la heri na la kupongezwa kwa sababu hakuna mtu atakayewaletea maendeleo ya kweli wana Afrika Mashariki isipokuwa wao wenyewe kuwa na mikakati thabiti ya kujikwamua kiuchumi.

Aidha wadadisi wa mambo wameshangazwa na hatua ya kutokujumuishwa kwa marais wa Tanzania na Burudi ikiwa ni pamoja na rais wa Sudan Kusini ambaye anatajwa kuwa mdau mkubwa kutokana na ukweli kwamba bomba la mafuta yanayopatikana Sudani ya kusini litajengwa mpaka Kenya.

Haijafahamika wazi kama marais hao ambao hawakuhudhuria kikao hicho hawakualikwa au laa! Hii inatokana na kauli ya Rais Mseveni aliyenukuliwa akinukuu maandiko ya Biblia, "…….Wanapokusanyika watu zaidi ya mmoja , pamoja basi kuna jema …", alisikika Rais Mseveni mara alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kutokuwepo kwa Marais wengine wa Afrika Mashariki.

Wadadisi hawajaishia hapo tu, wengine wamebashiri huenda Kenyatta anatafuta marafiki watakao watakaomuunga mkono kuhusiana na kesi inayomkabili katika mahakama ya kimataifa. Pia wapo wanaodhania kuwa, Rais Kikwete amekuwa na mahusiano zaidi na Rais Obama jambo ambalo huenda limetia dosari pia.

Itakumbukwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kauli za kukinzana baina ya Rais Kikwete na Rais Kagame. Yote haya ni porojo tu ambazo majibu sahihi labda wanayo marais wa Tanzania, Burundi na Sudani Kusini kwa kutokushiriki kwao!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment