Thursday 27 June 2013

[wanabidii] Hivi Tanzania kuna SWAT (Special Weapons And Tactics Teams) ?

Habari!
 
Siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wimbi la ujambazi wa kutumia silaha, uporaji (wa kutumia silaha), utekwaji, ujangili, wizi wa magari pamoja na matishio ya kigaidi (kama tunavyosikia kila siku kwenye vyombo vya habari).
 
Nakumbuka kuna siku nilikua hospitali ya mwananyamala, na wakati nikiwa hapo kuna majambazi waliojeruhiwa na askari waliletwa hapo kwa matibabu. Nilimsikia askari mmoja (simfahamu jina wala simkumbuki sura) akisema "huyu aliyepigwa risasi kifuani "ametusumbua sana".
 
Gari zilizokuja ni mbili, moja ni "defender" nyeupe fupi (ilibeba askari "kanzu" wasiovaa sare) na nyeusi ndefu (ilibeba askari waliovaa sare za FFU).
 
Cha-kushangaza ni kwamba katika askari wote hao waliokuwa wamevaa nguo "rasmi" zenye kuwalinda "body armour" hawakuzidi hata watatu. Pia magari yao sio bullet proof (not armoured vehicle).
 
Nakumbuka pia (sikumbuki mwaka gani) maeneo ya Kawe DSM askari wa jeshi la polisi waliokuwa katika patrol walishambuliwa na watu wasiojulikana na walipoteza maisha!
 
Sasa basi, kinachonishangaza zaidi askari hao hao wa "defender" wakisaidiana na FFU hutumika kukabiliana na purukushani zote zinazotokea. Kwenye kuzuia vurugu za wananchi huwa wanatumika. Pia kuna siku niliwakuta Magomeni askari wa defender wamesimamisha DCM lililosadikiwa kuwa lilibeba pombe haramu ya gongo. Hawakuwa na "sare".
 
Kuna siku nilikua mkoani (jina limehifadhiwa), kwenye mataa kuna gari ndogo ilivamiwa na majambazi waliokuwa kwenye pikipiki na silaha. Raia wema walipiga simu na matokeo yake walikuja askari wa kawaida na FFU tena wengi wao hawakuwa na "body armour". Kuna askari wa usalama barabarani alijaribu kusaidia lakini alikoswa na risasi na aliamua kukimbia (kwakua hakuwa protected au hakuwa amejiandaa kupambana kulingana na mazingira).
 
Kuna siku nilishuhudia askari wa tatu wa kawaida wametumwa kumkamata "mtuhumiwa" nyumbani kwake. Duh, walipigwa sana. Yaani askari wetu waliowengi hawana uwezo wa "hand to hand combat"
 
Turudi kwenye kazi za SWAT
 
Their duties include: confronting heavily-armed criminals; performing hostage rescue and counter-terrorism operations; high risk arrests; and entering armored or barricaded buildings. Such units are often equipped with specialized firearms including submachine guns, assault rifles, breaching shotguns, sniper rifles, riot control agents, and stun grenades. They have specialized equipment including heavy body armor, ballistic shields, entry tools, armored vehicles, advanced night vision optics, and motion detectors for covertly determining the positions of hostages or hostage takers, inside enclosed structures. Source
 
Nyongeza
  1. Huwa hawapigi risasi hovyo-hovyo (they target), their motto is basically "to protect and to serve"
  2. in many cases they do not target / harm unarmed civilian(s)
  3. they do all they can to eliminate the threat with maximum efficiency and less time
  4. wanatumia "akili" na sio mabavu (hawavamii nyumba bila kuwa na michoro au ramani"
  5. wanatumia tekinolojia (surveillance systems and other tracking devices, etc)
  6. SWAT huwa wanafanya mazoezi kila siku.
Hitimisho:
  1. hivi SWAT wapo Tanzania?
  2. hutumika wakati gani?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment