Tuesday 25 June 2013

[wanabidii] HII NDO TABIA YA WEZI

John 10:10 (NIV)
The thief comes only to steal and kill and destroy; I have come that they may have life, and have it to the full.
Yohana 10:10
Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu,mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Hii ndo tabia ya mwizi au wezi, kwanza kabisa wanaanza kwa KUIBA, maana ya kuiba ni kuchukua kitu kisicho mali yako bila ridhaa ya mmiliki wake (kwa mujibu wa tafsri yangu isiyo rasmi)
KUIBA kuko kwa aina nyingi mf:
Kuiba kwa kutumia nguvu, Kuiba kwa kutapeli, kuiba kwa kutumia ujinga wa mmiliki,  Kuiba kwa kusema au kuahidi uongo na usitekeleze n.k
Wezi wakifanikiwa katika azma yao na hiyo roho ya wizi ikikomaa huzaa kitu kingine amabacho ni KUCHINJA / KUUA
Hapa nia ya wezi huwa ni kuua kitu, mtu yeyote anayewafuatilia au anayekuwa kikwazo kwao, au anayeweza kusimama kama shahidi kutaka haki itendeke.
Hufanya hivi kwa njia mbalimbali mf: kukuua kimwili, kukufukuza kazi, kuangamiza biashara yako, kuharibu ndoa yako, kukufunga jela n.k
Wakifanikiwa katika hilo hawaishii hapo bali wanasonga mbele hatua ya kuanza UHARIBIFU.
Hapa uharibifu huwa wa aina nyingi maana hakuna anayewakataza au kuwakemea, kumbuka wameanza kuiba, wakachinja / wakaua sasa wanaanza kuharibu
Wanaharibu mifumo mizuri yooote iliyokuwepo ili  waweze kuendelea na uovu wao,hii ni pamoja na kujitengenezea mifumo mipya isiyohalali inayowalinda na kuwapendelea.
Wanaharibu uwezo wa mtu/ watu kufikiri na kuweza kujitambua (hasa mfumo wa elimu)
wanaharibu uwezo wa mtu/ watu kujiletea maendeleo/ kujitegemea maana wanataka wategemewe wao - watu wawe tegemezi na mifumo yao (uchumi)
Wanaharibu kila chema ulichonacho kwa njia mbalimbali.
Jamani ni jukumu letu kuwakataa hawa WEZI katika maisha yetu

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment