Ninachangia kusema kuwa utafiti wao ni mzuri. ila, Muhimu unapozungumzia vyanzo vya maji na umbali kuvionyesha au kuvielezea na aina ya vyanzo vyenyewe vilivyo. Pia, kuonyesha na hayo mashamba ya mwekezaji na yao wanavijiji. Huenda mwekezaji anatumia tu mbinu za sustainable farming ambapo wao hawatumii ktk mashamba yao lakini wakitumikishwa-hufanya kazi inayohusu kilimo endelevu na hawaigi pia. Ajira mashambani-unaweza ukakuta hata hiyo ardhi nzuri shinyanga imetokana na mwekezaji kuweka mbolea ambayo wao ndio wanaikusanya kutoka boma zao na kumuuzia, kutumika kuichanganya na kuitandaza ila wao kwao ktk customary land na mashamba yao-kinyesi kinazalisha wadudu hakitumiki. Ndio wanakuja wageni tunawauzia ardhi halafu wao wanatuajiri kisha tunalalamika. Mimi nimepanda miti rafiki mazingira shambani kwangu. Mbegu unaokota tu kutoka miti hiyo ilipo popote pale. Pia, hubeba mbolea ya kuku na ya ng'ombe nanunua napeleka kwa lori, nimepata veltiva grass, guetemala grass, ninafanya terracing (matuta ya kukinga maji na kuchonga ardhi) na kupanda hayo majani ktk makinga maji-terraces. Nimepanda miti ilindayo ardhi ya kunduchi-salasala liliko shamba. Kuna maeneo wazi ya wenyeji mengi hayajalimwa machaka tu na mashamba ambayo ni sandy soils. Lakini huoni mwananchi kupiga makinga maji anaona kero/tatizo/karaha. Ila wanakuja kukata miti shambani kwangu, kukata majani (guetemala) kuuza kulishia mifugo lakini kwao bare land hawapandi. Inabidi upambane na watu wasing'oe guetemala ambayo wao wanaweza kuipanda na kupata hela kwa kuiuza na kurutubisha ardhi yao. Mbona anakuja kukata na kuuza? si anajua ubora wake ktk kupata pesa? Asingeyafuata!! Nimefanikiwa kupita SHY na kufanya kazi Lake zone hadi Serengeti Mkoa wa Mara; (1985-1988). Baadae (1994, 2003) na miradi mingi ya maji TZ mikoa mingine. Ninachangia kusema hivi kwa sababu wakati mwingine unakuta kuna vidimbwi vya maji na kuna visima vya maji ambavyo ni traditional water sources na ni cha Mzee Fulani kinaitwa-Kisima cha Mzee Juma au Mwanzage (kwa Mwanzage Well). Kisma cha asili hicho kinakuwa na masharti. Mfano-hakuna kuingia ktk mazingira ya kisima na viatu, hakuna kuchotea ndoo ya chuma bali kata ya kibuyu au ndoo ya plastic utakayoikuta au kata ya kifuu cha nazi (kama kuna minazi). Hii ni kuzuia kuingiza uchafu na kutu kuchafua maji. Sehemu nyingine sheria ni kulipia hela kidogo au kuchuma eneo adjacent to the well ktk kisima kipya. Hii ya kuchimba hutumika sana Serengeti na Musoma Vijijini ambako kuna wafugaji na kila kikundi cha wafugaji hujitahidi kuwa na lambo lao la maji kunyweshea mifugo. Wewe mwenye hitaji la maji mbona hujaweka juhudi na kundi lako kuwa na source yenu? Hivyo, traditional bylaws zinakwambia-wenzako wamechimba a land water reservoir wanachota ya kunywesha mifugo na matumizi ya nyumbani. Basi utoke jasho baada ya kuchimba kibarua eneo utakalopewa ndio uchote hiyo ndoo moja ya maji. Kila ndoo moja-kipande cha kuchimba. Sio dezo. Hii inafanyika. Huko Musoma rural utakuta kijiji kimoja mfano Masurura kina vibwaya na visima vya jadi 50+ kijiji kimoja na vimezungushiwa wigo wa mimea ya matete. Hii ni enzi hiyo ya 1985-1988 nilipofanikiwa kuwa huko Mara. Ni hivyo niliona maeneo ya Igunga vijijini, Magu, Bunda. Visima vya jadi hulindwa na tuliviboresha kwa kujengea mawe bila ya kutumia cement as a binder (Rock Wells). Ukiangalia wananchi wanaweza kuchimba na kujengea kisima chao kutumia mawe au tofari za kuchoma kwa kutumia mafundi wao na kulinda eneo na uchafunzi na huwa wanatunga sheria ndogo ndogo na wana adhabu pia za kimila. Ila, watatembea kilometa kadhaa kwenda kisima cha mzee Juma au bwawa chafu ambalo huingiza mifugo, kuoga humo na kufua. Tumenweteka. Visima vya pampu vya deep, medium deep na shallow wells Tanzania vilianzia Shinyanga na Morogoro na kiwanda cha pampu TZ kilikuwa Morogoro. lakini huko kumetokea uharibifu wa kung'oa nati za pampu kuweka ktk plau za ng'ombe na mikokoteni (Shinyanga). Morogoro lack og maintenance unakuta mabomba hayo butu whhite elephants vijijini mpaka kuelekea kilombero. Kupata maji toka pampu muhimu kwani wanalima huko Moro na kutumia pesticides. Matumizi ya madawa ya magugu na ya kuua ukungu katika mazao ya miti. Ukiangalia takwimu za kifafa zimepata kutokana na madawa haya ya magugu pamoja na ulaji wao wa nyama ya ngurue yenye tape worm. Morogoro yenye mito mingi na wet lands, wanachoma tofari za udongo na wamepata mafunzo vijijini ya kuchoma tofari kwa kutumia pumba za mpunga badala ya kumaliza miti. wanauza tofari sana lakini hawawezi kutumia kujengea visima kulinda uchafuzi. mawe ni mengi pia yale magumu na hutumia kwa foundation ya nyumba zao. Vijiji vingi pamoja na Morogoro Rural, Machimboni (mawe ya thamani au dhahabu) hata mjijini mikoani Mwanza (Igoma) tunakuta video za matusi na anayeonyesha anajali pesa tu. anaonyesha kwa watoto hapo sebureni. Pia kuna mabanda ya kuonyesha matusi hayo. Mfano. Kijiji cha Kisanga Morogoro Tarafa ya Mikumi Video za matusi kuangaliwa wakubwa na watoto lilikuwa tatizo no 1 mwaka 2008 katka shughuli za elimua ya ukimwi. Tulipowauliza kama mzazi anakuwepo, viongozi wanajua na wanatazama pia walisema ndio. lakini ni masuala ambayo yapo chini ya uwezo wao WAZAZI, WAZEE WA MILA, EXTENSION STAFF WA KATA HATA KAMA VIONGOZI WA KATA NA KIJIJI (mtendaji Kata, Kijiji na Diwani hawajali wapo corrupt). Waelimishaji jamii-wataalamu kushirikiana na wazee wa mila wanaweza wakakomesha. Ila inaonekana MILA NA MAADILI HAKUNA. Kiasi kwamba baba na mama watu wazima wanaweza kuangalia picha za malavidavi pamoja na watoto hata kama si watoto wao wa kwao wao wamefungia home-ni Upumbavu kukosa maadili. Ukiangalia, mwenye video hiyo ni mtu mwenye hela au madaraka na anatishia wanaomlalamikia. Wengine hufanya siri sebuleni kwao kupata hela. Katika machimbo ni mabanda ya kipato halmashauri ya Kijiji na Wilaya hukusanya mapato daily kama wanavyokusanya kwa wanaouza biashara za chakula barabarani katika uchafu. Vibanda vya video ni vya nyasi. Watoto hufanyakazi ya amalgamation ya dhahamu kupata ujira mdogo, kuponda mawe ili akapate shs 100 akaone video. hapo anachezea mercury inammaliza. anayemfanyisha kazi hii ya mercury ni mama au baba na anayemwonyesha picha za ngono ni baba au baba-anaganga njaa, mwachieni, kajiajiri!! NCHI INAKWENDA KUBAYA. Kuchangia huduma ya afya ni tatizo. hata kama mtu anakunywa pombe daily (ni tabia vijijini) lakini kutoa 2,000/= kwa card ya afya kwa watu 6 kutibiwa kwa mwaka na wanafunzi watano elfu 2 kwa mwaka ni tatizo. Binafsi, nimegharimia wanawake zaidi ya 20 kutibiwa Fistula bure CCBRT bila ya kupata msaada wa familia. Mume anasema alilipa mahari; familia ilidhania nina hela za mhisani ninataka kuzila peke yangu. Pamoja ya kuwaeleza kuhusu huduma ya bure CCBRT sina mhisani bado wakidhania hivyo. Baada ya kushonwa hao nikaachana nao. Utu wetu upo pembeni, tegemezi daima. Wachache sana walikubali kugharimia angalau nauli ya kuja dar. Kesi za ubakaji ndio zilishindikana, nimeeleza humu mara nyingi. Inasikitisha sana ndugu zangu. Unakuta usiri na aibu ya kukubali kutoa ushirikiano kwa dhati. hata wewe unayejitolea unachoka kupoteza nauli yako kufuatilia kesi au shauri, unaogopa kuuawa pia. Kuna kukubali kumaliza kienyeji na kuchukua rushwa au kumezea kuficha siri na aibu. Tulitibu watoto wengi wenye magonjwa ya zinaa na kuwafanyia ushauri nasaha. Ubakaji unatokea wakienda na kurudi shule, shamba kuliko kisimani kwani kuchota maji huenda wengi zaidi. Wafanyao ubakaji zaidi ni watu wazima. Ubakaji mwingi ndani ya nyumba wazazi kuwa shamba na kuwaacha watoto na ndugu zao wao huko miezi wakihamia ndege/wanyama pori kulinda mazao wezi wasiibe mpaka wavune. Pia jirani na tegemezi la kukopa dukani kuliko huo ubakaji wa wa nje ya nyumba. Pia kulaza watoto ba vijana wakubwa au watu wazima. Baadhi ya watoto kutumika kufanya biashara kilabuni, kuuza pombe na kuanza klamba vinywaji, biashara magulioni na kurudi usiku njia za mapori. baadhi ya vijiji hukataza wanafunzi kuuza biashara/pombe vilabuni lakini biashara hizo huonekana ndio njia ya kujikimu.Magazeti ya wiki iliyopita imetoa kesi za ubakaji nyingi pamoja na houseboy kubaka katoto ka miaka 6 na kesi za wanafunzi na jinsi wazazi wanavyoficha ukweli na kupeleka watoto kutibiwa hospitali binafsi bila kuchukua sheria. Pia wahusika wanavyokana tendo ambalo wamefanya na huwa huru pamoja na watoto kutoa vidhibiti. Denial hii ifanyiwe kazi na TGNP na kijamii mpaka wazazi wakubali kuwa wazi ili SOSPA na deski za jinsia zifanikiwe kufanya kinachotegemewa. --- On Mon, 10/6/13, Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment