Tuesday 4 June 2013

Re: [wanabidii] Story; Tendwa Akipa Usajili wa Kudumu Chama Kipya cha 21

Nawatakia mafanikio katika safari yao ya kushika dola ila nafikiri ipo haja ya kutafuta kifupi (abbreviation) kingine kwa ajili ya jina la chama. Neno CHAUMWA katika kiswahili laweza kuwa na tafsiri isiyoleta matumaini kwa watu watakaotaka kujiunga.

Tendwa anaposema chama hakina migogoro na kinakaa miaka kadhaa bila hata ya kuwa na diwani sijui kama ana ufahamu mzuri wa vyanzo vya migogoro ndani ya vyama vya upinzani. Migogoro iliyo mingi ndani ya vyama vya upinzani ina mikono ya walio madarakani. Ipo haja ya kutunga sheria ya kuwaadhibu watakaopatikana na hatia ya kupandikiza watu ndani ya vyama vya wenzao ili waanzishe migogoro na hatimaye kuvidhoofisha vyama hivyo.

Tumeona watu wakipandikizwa na kuanza kubwabwaja maneno ya uzushi kwa nia ya kuvidhoofisha vyama pinzani, au kununuliwa ili wahame vyama fulani na kujiunga na chama chenye sera ya kujijenga kwa kuvihujumu vingine. Tendwa anatakiwa kuziona rushwa za namna hii na kuzifanyikia kazi kama amedhamiria kuvisaidia vyama vyote kujijenga kwa usawa. Wakati akiangalia uwezekano wa kutunga sheria ya kuvibana vyama vinavyotumia matusi aangalie pia uwezekano wa kuboresha sheria ya rushwa zinazotolewa kwa baadhi ya wanachama vipandikizi wenye lengo la kuvihujumu vyama pinzani. Lakini pia sina uhakika kama aliwekwishasema lolote juu ya matusi yanayotumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama wakiwemo wabunge.

Ni kosa na aibu kwa chama chenye nguvu kutumia mikakati ya kuhujumiana kwa sababu watu wamewekeza nguvu, mali, muda na akili zao ili kuanzisha vyama na hivyo chama au mtu yeyote anayekihujumu chama  cha wenzake bora akachukuliwa hatua if Tendwa is to be fair


2013/6/5 Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com>

Tendwa Akipa Usajili wa Kudumu Chama Kipya cha 21, CHAUMMA

Na  Thehabari.com

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) huku akivitaka vyama vya siasa kufuata sheria na kuepuka kuwa vyanzo vya vurugu na uchochezi wa migogoro.

Tendwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwakabidhi cheti cha usajili wa kudumu viongozi wa chama kimpya cha kinachojulikana kama Chama cha Ukombozi wa Umma.

Alivitaka vyama vya siasa kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kushika dola na hata kama itashindikana kwao, basi kuhakikisha wanapata nafasi za uwakilishi wa wananchi zikiwemo za udiwani, ubunge pamoja na uongozi wa serikali za mitaa kwa mujibu wa taratibu za nafasi hizo.

Alisema kwa sasa vipo vyama vya siasa ambavyo licha ya kuwa na usajili wa kudumu na uongozi mzuri usio na migogoro vimeshindwa kutimiza malengo ya msingi ya chama kwa kushika nafasi za uwakilishi maeneo anuai kwa mujibu wa utaratibu.

"…Vyama hivi unakuta hawana mbunge, hawana diwani, hawana viongozi serikali za mitaa, kijiji na kwingineko lakini ukiangalia wana viongozi wazuri hawana migogoro ndani ya chama, haya sio madhumuni ya chama cha siasa," alisema Tendwa.

Aidha aliwataka viongozi wa CHAUMMA kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze kutimiza malengo ya chama na kuwawakilisha wananchi maeneo mbalimbali ya uongozi kisiasa. Alisema katika mapendekezo mapya ofisi yake inafikiria kuanza kuvipunguza vyama ambavyo licha ya kuwa na usajili havifanyi chochote kama ilivyo kwa madhumuni ya kuanzisha chama.

"Sheria inafanyiwa marekebisho, chama kikikaa ndani ya miaka mitano hakijafanya chochote tunafikiria kukifuta, kiongozi wa chama akitukana miezi sita unafungiwa kwa muda…maana hatuwezi kuruhusu matusi, vurungu na masuala mengine yasiokuwa na msingi ndani ya vyama vya siasa," alisema Tendwa.

Hata hivyo amesema katika mapendekezo yao ya mabadiliko ya katiba wamependekeza mambo mengi ikiwemo sasa kuruhusu vyama kujiunga na kufanya shughuli za siasa kama ilivyo kwa nchi za Kenya, Afrika Kusini, Lethoto na nchini Namibia.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu Mwenyekiti wa muda wa CHAUMMA, Wallance Mayunga alisema wamejipanga vizuri katika kuwatumikia wananchi na chama chake kinatambua changamoto zilizopo nchini katika uongozi, utendaji na utawala hivyo kina nia ya kuleta mabadiliko.

Nafasi ya Katibu Mkuu wa muda wa CHAUMMA inashikiliwa na Shaffii Abed huku Hamad Tao akiwa ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa nchama hicho.

~Imeandaliwa na www.thehabari.com


________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment