Monday 3 June 2013

RE: [wanabidii] Rwanda’s reaction to Pres. Kikwete’s statement is shochking

Sidhani kama kuna mtu anayekubaliana na msemo wa "right or wrong my country first" lakini suala ni je, kuna "wrongness" gani kwenye ushauri/mawazo ya Rais wa Tanzania kwa Wanyarwanda huku tukizingatia yafuatayo:
1. Ilikuwa forum ya kutoa mawazo - siyo hotuba ya amri.
2. Tanzania siku zote huunga mkono utatuzi wa migogoro kama sera yetu.
3. Baada ya miaka 19 - hao jamaa wa Kigali wanataka waendelee kupigana ili iweje? Si wameshashindwa?
4. Kwani ni lazima kufuata ushauri? Sasa kwa nini watukane?
 
Aidha, kulinganisha suala hili na suala la Kenya na Al Shabaab si haki. Hakuna fursa yoyote ya mazungumzo kwenye hili na hakuna hata mtu anayejulikana kwamba huyu ndiye kiongozi. Hawa ni wahuni tu wa mambo ya kiarabu.
 
Kulinganisha na suala la Nyerere kukataa kuongea na Idi Amin nako si haki pia. Turejee kwenye historia. Nyerere hakukataa kuongea na Amin na ndiyo maana Siad Barre alitukutanisha Mogadishu na tukasaini mkataba kwamba hatutaweka majeshi yetu mpakani. Amin aliuvunja.
 
Lakini pia, Nyerere aliwaambia viongozi wa OAU (mwenyekiti akiwa Jaffery Nimeiri), na wale wa nchi za Afrika - hasa waliotuma wajumbe kama Nigeria, Ghana na wengine waliotuma ujumbe kama Kenya, kwamba wamwambie Amin afanya haya:
1. Aondoe majeshi yake; 
2. Alipe fidia;
3. Aape kwamba hataivamia Tanzania tena;
4. Aache chokochoko.
 
Hakuna aliyefanya hivyo. Amin naye hakufanya chochote. Kwa maneno mengine Nyerere na Tanzania tulinyimwa fursa ya kuumaliza mgogoro ule kwa amani. Mkumbuke kuwa Amin alishawahi kutuvamia kwa mabomu kabla na aliwahi hata kumkamata RPC wa Kagera na kumuua. Kudai kwamba Nyerere/Tanzania tulikataa mazungumzo au njia ya amani ni kuukwepa ukweli wa historia. 
 
Kutoa mfano wa Komoro nako si sahihi kwa sababu Kanali Bakari aliombwa na AU afanye mazungumzo, aache uasi lakini alikataa. Waziri Membe alizungumza naye (subiri kitabu kitakachochapishwa kiitwacho "Our chairmanship") na alimwambia kwa nini usiache haya mambo na mkamaliza kwa amani? Kanali Bakari alikataa. Sasa mazungumzo ya amani yangefanyikaje?
 
Kwenye suala la Rwanda na wagomvi wake tunapaswa kujua kwamba iwapo wataendelea hivi hivi, iko siku mauaji mengine makubwa yatatokea lakini pia kuna haki gani kuwalaumu hata watoto waliozaliwa baada ya mauaji ya 1994 na ambao leo ni wapiganaji wa msituni huko? Kweli Waafrika hatuwezi kumaliza shida zetu kwa kuzungumza? Sasa wameshafanikiwa nini hadi sasa? Rwanda ni nchi ndogo kuliko msitu walikojificha hawa jamaa, hili balaa litaisha lini?
 
La msingi ni kwamba walipewa ushauri mzuri na hakuna mtu amethibitisha kwamba ushauri huu ni kinyume cha sera ya Tanzania au ni mbaya; kwa hiyo tusichanganye matatizo yetu ya ndani ya masuala ya nje.
 
Rwanda washike adabu yao; hakuna nchi iliyowabeba kama Tanzania na hata huyu balozi wao hapa Washington DC alisomea uhandisi Mlimani pale bure bure akisema kwao ni Nzega. Muulizeni James Mbatia anamjua.
 
Matinyi.
 

From: kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] Rwanda's reaction to Pres. Kikwete's statement is shochking
Date: Sun, 2 Jun 2013 18:19:10 +0000

Ndiyo  maana mimi najikuta nikishawishika kuwa na wasi wasi labda "vision" ilikuwa kuwafurahisha Wafaransa na wazee wa FDLR na kuwafanya kuona umuhimu wa CCM kuendelea kuwa madarakani Tanzania hata baaday a2015 na hasa  ikiwa   inaendelea kuwa chini ya ushawishi wa watoa ushauri kama huu... Uchanguzi 2015 utaitaji pesa nyingi jamani kuwaonga wanahabari na wanasiasa wasidhubut kuendekeza  ushabiki na ukweli kama   wa akina Mwangosi  na hata  akina Kibanda... Sijui lakini sidhani haikukwepo  "vision"...ndio maana ushauri wenyewe ulitolewa katika hotuba badala ya mazungumzo ya ana kwa ana Na umefuatiwa na postings  kwenye mitandao iliyoandikwa kwa Kiingereza cha ushawishi mkubwa!!!!...
 
Labda lengo lilikuwa kumfanya Kagame akasirike  na akina FDLR wafurahi....na Watanzania wamtetee Rais wao na kumuita Kagamne majina mabaya kama  vile kusema  ni "mtoto" mtikutu. (spoiled child) hasiyestahili kutembelewa na Baraka Obama.. Yaani kwa vile Rwanda ni ndogo kwa umbo basi na Rais wake eti naye ni bwana mdogo na hasitahili kumsema vibaya Rais wa Tanzania ambaye ni bwana mkubwa...mwenye eti uzoefu wa kusuluhisha migogoro kama ule "mkubwa sana" wa Comoro....Ahahah!!!
Mwl. Lwaitama 

Date: Sun, 2 Jun 2013 13:22:28 -0400
Subject: Re: [wanabidii] Rwanda's reaction to Pres. Kikwete's statement is shochking
From: emuganda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hivi, niwaulizeni wajuzi. Kagame akikaa na interahamwe na Museveni akae na Kony, what is the end game?
What did Kikwete envisage? Huwezi kutoa ushauri kama hauna vision ya suluhisho.
What is the vision?
em

2013/6/2 RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>


Matinyi hatubishani bali tunatumia haki yetu ya msingi ambayo wewe ni mtetezi wake kujadiliana. Kama wamewatukana hivi ijumaa na jumamosi ile website ya matusi iliyokuwa chini ya Maelezo kablya kufutwa jioni ilitoka wapi kama siyo Tanzania? Kuna matusi kama yale tona toka kwa watu wa serikali ambao wanafundisha jirani yao tolerance? Kwa nini ulazimishe watu wakubali ushauri wako na wao hawataki? Kama wanapigana miaka kumi na sita na nchi yao inakwenda sawa wewe ambaye hujapigana vita tangu miaka ya thamanini mna tofauti  gghani maana wote mnakwenda na bakuli kwa wakubwa kuomba vyandarua?

    Kama mchambuzi tunayekuamini tunataka katika hili tumia hiyo Bongo inayonoa wazungu huko uliko kuzama kwa kina na kuachana na ujanja ujanja huu wa bongo.




------------------------------
On Sat, Jun 1, 2013 2:43 PM GMT-12:00 Mobhare Matinyi wrote:

>Hatuna haja ya kubishana au kudhani kuwa udhaifu wa chochote kile kilichopo Tanzania unaweza kuwapa watu au mtu wa Rwanda haki ya kututukana sisi kupitia kwa Mkuu wa Nchi yetu. Rwanda hawana adabu na hawana sababu wala haki ya kuropoka kama wanavyofanya sasa. Tusichanganye matatizo yetu ya ndani ama hasira zetu za mambo ya siasa za ndani mwetu ya wajibu wetu wa kulinda na kuitetea heshima ya taifa letu pale linapotukanwa na matoto matundu. Hakuna hata mtu mmoja atakayetuona kuwa tu watu wa maana kwa kuwasaidia wakorofi kulitukana taifa letu. Ni aibu kumsaidia adui kukushambulia wewe mwenyewe. Rwanda hawana adabu - kama tunataka kuwa wakweli wa yote yaliyopita; hawana adabu.
>
>Matinyi.
>
>> Date: Sat, 1 Jun 2013 19:13:01 -0700
>> From: rmgamba2000@yahoo.com
>> Subject: Re: [wanabidii] Rwanda's reaction to Pres. Kikwete's statement is shochking
>> To: wanabidii@googlegroups.com
>>
>>
>>
>> Kivamwo kabla ya kuandika tafiti kwanza haya yote uliyouliza yamo mtandaoni na majibu yake ni rahisi sana siyo kama unavyofanya short cut.
>>
>>   Ikiwa unadiriki kusema Kabila senior hakusaidiwa na hawa wanaoitwa waasi leo then kuna tatizo katika utafiti wako. M23 ni the same faction iliyojulikana zamani kama CNDP iliyokuwa ikiongozwa na Jean Bosco Ntanganda mpaka Machi 23 2009 walipotia sahihi makubaliano ya amani. Ntaganda msaidizi wake alikuwa Sultani Makenga

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment