Saturday 1 June 2013

Re: [wanabidii] Re: Ombi la Rais Kikwete la Walimu wa baadhi ya masomo kutoka Jamaica lakubaliwa

Haka kanchi kalipata uhuru lini hivi?

--- On Sat, 6/1/13, Limbe <geelimbe@hotmail.com> wrote:

From: Limbe <geelimbe@hotmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: Ombi la Rais Kikwete la Walimu wa baadhi ya masomo kutoka Jamaica lakubaliwa
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, June 1, 2013, 1:19 AM



On May 30, 1:27 pm, Abdalah Hamis <hamis...@gmail.com> wrote:
> Jamaica imeahidi kuisaidia Tanzania kwa kuipatia walimu wa hisabati na
> sayansi na pia imesema kuwa itatoa kocha wa kufundisha mchezo wa
> riadha kwa nia ya kusaidia maendeleo ya mchezo huo nchini Tanzania.
>
> Aidha, nchi hizo mbili zimeahidi kuongeza ushirikiano katika nyanja
> mbali mbali na kuangalia uwezekano wa Tanzania kufungua aina ya
> uwakilishi katika Kisiwa hicho cha Caribbean katika miaka miwili
> ijayo.
>
> Makubaliano hayo kati ya Tanzania na Jamaica yalifikiwa usiku wa
> Jumapili, Mei 26, 2013, katika mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya
> Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu
> wa Jamaica, Mama Portia Simpson Miller.
>
> Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Hotel ya Sheraton mjini
> Addis Ababa, Ethiopia, viongozi hao wawili walikubaliana kuwa Jamaica
> itaangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania kwa kutoa walimu wa
> kufundisha hisabati na masomo ya sayansi.
>
> Rais Kikwete alikuwa Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 tokea
> kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Juni 25, mwaka 1963 na Mkutano wa 21
> wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU wakati Mama Simpson Miller alikuwa
> mmoja wa viongozi mashuhuri wa nchi mbali mbali duniani walioalikwa
> kuhudhuria sherehe hizo.
>
> Katika mazungumzo hayo, Mama Portia Simpson Miller ambaye aliapishwa
> kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica Januari 5, mwaka jana, 2012 baada ya chama
> chake cha Peoples National Party (PNP) kushinda uchaguzi mkuu nchini
> humo, alimwuliza Rais Kikwete jinsi gani Jamaica inavyoweza kuisaidia
> Tanzania.
>
> "Mawili makubwa ambayo mnaweza kutusaidia – moja ni walimu wa hisabati
> na masomo ya sayansi kama mnao wa kutosha na pia kocha wa riadha ili
> tuweze kufufua upya mchezo huo ambao Tanzania ilikuwa inatamba duniani
> katika miaka ya 1970," alisema Rais Kikwete.
>
> Mama huyo alimwahidi Rais Kikwete kuwa Jamaica inao uwezo wa kusaidia
> katika maeneo yote mawili. "Hili la walimu tutaliangalia mara moja
> nikirejea nyumbani. Tutasaidia kwa kadri inavyowezekana kwa sababu
> najua fika juhudi zako kubwa ambazo umekuwa unafanya katika eneo hili
> la elimu na mafanikio makubwa ya jitihada zako."
>
> Kuhusu kocha wa riadha, Mama Simpson Miller amesema kuwa na hilo
> halina pingamizi kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Michezo kwa miaka
> mingi na kuwa kwa sasa Wizara ya Michezo iko kwenye Ofisi yake ya
> Waziri Mkuu. "Nilikuwa Waziri wa miaka mingi wa michezo katika nchi
> yangu na kwa sababu ya umuhimu wa michezo, nimeamua kuiweka shughuli
> ya michezo katika Ofisi yangu ya Waziri Mkuu."
>
> Jamaica ni moja ya nchi zinazoongoza katika mchezo wa riadha duniani
> ikiwa imetoa wanariadha wengi mabingwa wa dunia akiwamo bingwa wa sasa
> wa Olimpiki na dunia katika mbio fupi za mita 100 na 200 – Usain Bolt.
>
> Imetolewa na:
> Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
> Ikulu.
> Dar es Salaam.
> 27 Mei, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment