Monday 24 June 2013

RE: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Mwigulu, Msigwa Na Hamu Ya Vurugu Mechi!

Shukrani sana mkuu. Tupo pamoja.

Date: Mon, 24 Jun 2013 16:20:04 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Mwigulu, Msigwa Na Hamu Ya Vurugu Mechi!
From: mjengwamaggid@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Jimmy,
Ahsante sana.

Ni mimi Maggid wa enzi za Fr Kalumuna pale Tambaza, 1983 - 87. Aisee, umenikumbusha mbali sana. Nilianzisha gazeti langu ' Tambaza News!'. Mhariri na ripota ni mimi mwenyewe!

 Ni kweli, Tambaza tulikwenda ziara ya michezo Usagara, Tanga. Niliingizwa kwenye msafara kama ' Ripota' wa shule. Nikiwa Tanga nikajituma mwenyewe kwenda mpaka mapango ya Amboni.

Niliporudi, mbali ya kuripoti matukio ya michezo, nikaripoti pia masuala ya kijamii na kitamaduni ikiwamo feature article ile yaAmboni.

Nimefurahi kujua kuwa nawe ulikuwa mmoja wa wasomaji wangu. Nakumbuka Second Master wetu Mwaipopo alikuwa mmoja wapo pia.

 We had really good time at Tambaza, as a strong and united family.  Kwenye maktaba yangu nina picha moja nikiwa   Amboni, Tanga enzi hizo . Nitairusha kwenye blogu yangu siku za karibuni.

Ahsante sana Jimmy kwa kunimbusha tulikotoka.

Maggid,
Iringa.

2013/6/24 Jimmy Mwanyakunga <jmwanya@hotmail.com>
Kwa kweli Maggid umenena. Vyombo vetu vya habari nadhani bado vipo chini kabisa ya viwango, au kwa kiasi kikubwa vinakumbwa na huu upepo wa kisiasa unaovuma kwa kasi wakitegemea kunufaika kwa njia moja au nyingine.

Hivi ni Maggid yule wa Tambaza enzi zile za Fr.K??? Du, nakumbuka uliandika makala moja ya mapango ya Amboni vijana walifanya ziara kule. Ah longtime... Big up kaka.

CC: mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
From: chongoloh@gmail.com
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari; Mwigulu, Msigwa Na Hamu Ya Vurugu Mechi!
Date: Mon, 24 Jun 2013 09:22:32 +0300
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Shikamoo Maggid, Kamwene mvina, heshima yako kaka na mwisho umenikuna mnyakaye!!

Sent from my iPad

On 24 Jun 2013, at 9:17 asubuhi, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

Ndugu zangu,

Leo jijini Dar wanakutana wanahabari na wadau wa habari zaidi ya 150. Watajadili maadili na wajibu wa wanahabari kwenye hali ya migogoro. Watachambua pia hatari ya lugha za chuki, udini na mengineyo. Wataangalia pia namna njema ya kukabiliana na hali hizo.

Ni hatua njema kabisa na imekuja wakati muafaka. Na hapa nawasifu MCT kwa kufanikiwa kuwakutanisha wanahabari katika hili. Kila la kheri.

Na kwenye hili la wanahabari na migogoro tunaweza kuona mfano wa moja ya habari kubwa jana Jumapili; Iliwahusu Wabunge Mwigulu Nchemba ( CCM) na Peter Msigwa ( CHADEMA)

Hakika niliamka nikisikia vichwa vya habari vya uhasama vikitamkwa redioni. Kisha nikajionea mwenyewe nilipoyanunua magazeti kadhaa ya jana.

Naam; " Mwigulu na Msigwa nusura wazichape!". Mengi ya magazeti yalibeba habari hiyo katika staili ya kufanana- Waheshimiwa nusura wachapane! Na picha kubwa ya waheshimiwa hao ikawekwa mbele kwenye magazeti hayo.

Kabla hata sijaisoma habari yenyewe, nilipoangalia picha tu, nikajiuliza; hivi walio kwenye nusura ya kuchapana makonde ndio hawa?!

Picha tu ilijieleza, kuwa Msigwa na Mwigulu ni watu wenye kufahamiana na pengine hukutana kunywa kahawa pamoja. Kwamba pale, na kwa mujibu wa habari yenyewe, walikuwa kwenye mabishano ya hoja. Ni kawaida. Maana, sikuona hata mahali wametukanana.

Masikini Msigwa na Mwigulu, hawa ni watu wazima na familia zao. Fikiri mtoto wa mheshimiwa anaambiwa na mwenzake shuleni; " Eeh, nimesikia baba yako anataka kuzichapa na mwenzake huko bungeni!" Ni mambo ya kudhalilisha kwa kweli, si kwa familia tu. Hata kwa Mheshimiwa kwa wapiga kura wake. Naam, Waheshimiwa wakianza kuchapana makonde hadharani badala ya kuzungumza wanaacha kuwa waheshimiwa. Wanabaki kuwa wahuni tu, kama wale wa mitaani.

Na hapa ndipo tunauona udhaifu wetu wanahabari, kuwa tunapenda sana kushabikia 'vurugu mechi'. Maana, utotoni tulipokuwa tukenda viwanjani, moja ya burudani tuliyoona ni ya kufurahisha ni pale ilipotokea ' vurugu mechi!' Kwamba hapo rafu mtindo mmoja na kinachofuatia refa kukimbia mwenyewe au kukimbizwa kwa fito.

Naziona dalili za media yetu kuanza hulka ya kushabikia ' vurugu mechi' badala ya mambo ya msingi. Ona jana, wabunge wale wapambanaji wa UKIMWI waliudhuria semina ya UKIMWI. Lakini, kilichoongewa na wabunge hao kuhusu UKIMWI hatukukisikia hata kimoja!

Hivyo, wakati wanahabari wakikusanyika hii leo pale Dar kujadili maadili ya kazi zao na wajibu wao kwenye migogoro waiangalie pia mifano kama ya jana kwenye media. Maana, badala ya media kuchangia kwenye kupunguza tension na migogoro, inaweza kuchangia kwenye kuichochea! Na hilo si jukumu la media yenye kuwajibika na kuzingatia uzalendo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment