Tuesday 25 June 2013

Re: [wanabidii] Polisi FFU sasa hadi Bungeni?????????? Inatisha

Mtoi sasa uhuni huu jamani mpaka lini? tufanye nini kukomesha uhuni huu? jibu ni Nguvu ya umma pekee

2013/6/25 Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
Kuwazuia wabunge wa chadema kwa kisingizio cha mavazi ulikuwa uhuni tu ambao haupaswi kuvumiliwa, leo Simbachawene kavaa mavazi kama waliyo vaa kina Mbowe na Lissu jana lakini yupo bungeni, tofauti ya vazi la Mbowe na Lissu na hili la Simbachawene leo ni kwamba la Simbachawene halina vile vishikizo vya mabegani lakini ni suti nyeusi yenye mafuko makubwa manne, miwili juu kifuani na miwili chini tumboni, sawa na zile za kina Mbowe na Lissu.

La msingi kukumbuka ni kwamba sio kuwa mavazi hayo ndio yamevaliwa kwa mara ya kwanza bungeni jana na Mbowe au Lissu, yamekuwa yana valiwa tangu mwaka 2011 na wala hayako kinyume na kanuni za bunge.

Hujuma hizi wanazo fanyiwa wabunge wa Chadema ni muendelezo wa hizi hujma tunazo ziona huku mitaani.

Soma kwa undani hapa...

Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la safari suti yenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, kwa mara ya kwanza Kiongozi wa Upinzani, Freeman Mbowe na wenzake watatu jana walizuiwa kuingia bungeni.

Mbowe na Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sera za chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni katika viwanja vya Bunge, Lissu alisema walishangazwa na uamuzi huo wakati mavazi hayo wamekuwa wakiyavaa na kuingia nayo bungeni kwa miaka mingi sasa.

Lissu alisema kuzuiwa kwao wanakuchukulia kuwa ni mkakati maalumu wa serikali ya CCM kutaka kuwazima na kuhakikisha hawapati nafasi ya kuingia bungeni ili wasijibu mashambulizi ya tuhuma wazosingiziwa kuhusiana na mlipuko wa bomu jijini Arusha.

"Sisi hali hiyo tulianza kuishtukia tangu asubuhi tulipoingia kwenye eneo la Bunge, kama mligundua kulikuwa na askari wengi sana kila kona kuliko kawaida kana kwamba nchi imepinduliwa. Kinyume cha utaratibu na kanuni, askari wa kawaida wameingiza hadi bungeni.

"Tulipofika wakati wa kuingia ukumbini mimi, Mbowe, Lema na Wenje tuliambiwa haturuhusiwi kwa kuwa tumevaa sare za chama. Tulipouliza nani kawapa maagizo hayo walidai ni uongozi wa juu, yaani Spika wa Bunge," alisema Lissu.

Aliongeza kuwa kitendo hicho ni kichekesho kwani wakati wote tangu mwaka 2010 Mbowe amekuwa akivalia vazi hilo, achalia mbali wabunge wenzake baadhi ambao mara moja moja nao walikuwa wakivaa suti hizo lakini hawajawahi kuzuiwa.

Hata hivyo, pamoja na uamuzi huo, kanuni za Bunge hakuna mahali zinazuia mbunge kuvaa sare ya chama chake isipokuwa kanuni limeainisha aina za mavazi ya kuvaliwa na wabunge wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3)(a) Kwa wanawake na (b) Kwa wanaume inasema: (a) Kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti.

(ii) Gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) Kilemba cha kadiri au mtandio (iv) Suti ya kike; au (v) Vazi linalovaliwa wakati wa eda.

(b) Kwa wabunge wanaume;-(i) Suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia; (ii) Vazi la kimwambao yaani ka nzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubadhi au viatu; (iii) Suti kamili ya Kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) Koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) Tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.

Chanzo: Tanzaniadaima 25 Juni, 2013.
...
"All those that fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the
oppressor." Come the day.
...Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

From: Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
Date: Tue, 25 Jun 2013 10:04:21 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Polisi FFU sasa hadi Bungeni?????????? Inatisha

Kitigwa kama ni kuwazuia wabunge wa Chadema wasiingie na magwanda nadhani spika angetoa amri kwa askari wa pale Bungeni ya kuwazuia hao wabunge kama wamevunja kanuni  hiyo ingetosha. Ndio waletwe FFU na kutanda nje hadi ndani ya uzio wa Bunge? Nguvu yote hiyo inatumika ya nini? Kwani wabunge wa Chadema waliovaa magwanda walikuwa wangapi?
Suleiman Swalehe
 
2013/6/25 F kitigwa <kitigwa@gmail.com>
Nia ilikuwa kuwazuia wabunge wa CHADEMA waliokuwa wamevaa magwanda
Mimi nashangaa sana kama watu hawatakiwi kuingia na nguo zinazoonyesha itikadi zao mbona inapofika siku ya Ijumaa huwa naona wabunge wenye imani fulani wakiingia bungeni na nguo ndeefu nyeupe ziko kama kanzu hivi tena wakiwa wamevaa na vijikofia vya rangi nyeupe vilivyodariziwa?
Hawa mbona huwa hawazuiliwi maana bungeni siyo sehemu ya kuvaa hayo mavazi yanayoonyesha itikadi na imani zao?
Huu ubaguzi ni mpaka lini?
Kwa nini macho yanaona makengeza tu upande mmoja? wanatumia nguvu nyiiiiiiingi kuwadhibiti CHADEMA.
wakati hilo si jambo la msingi lililowapeleka hapo mjengoni.

2013/6/25 Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
Hapa kwetu magazeti ni ya shida tunayapata kwenye kipindi cha tuongee magazetini cha Radio Free Afrika au kipindi cha kuperuzi na kudadisi cha  Radio Clouds. Leo asubuhi nimeshangaa sana baada ya kusikia eti askari wa FFU wametanda Bungeni Dodoma kwa ajili ya kupitisha bajeti ya serikali. Jamani hii inakuwaje? Kupitisha bajeti ya serikali sharti kulazimisha kwa nguvu ya dola? Au ndio yale ya mzee Pinda kwamba asiekubali bajeti  ni mkaidi apigwe? Kwanza huyu mzee inafaa apatiwe jina. Mzee mwinyi aliposema mtu yeyote kula kitu atakacho ruksa,akapewa jina la mzee ruksa. Sasa huyu mzee Pinda kasema atakae kaidi amri apigwe nae hafai kupewa  jina? Naona anafaa kuitwa Pinda Piga Piga, au ( Mzee Triple P). Kwangu mimi haileti picha nzuri.Ukifikiria kauli ya huyu mheshimiwa mzee triple P, na hili la FFU kutanda kwenye viwanja vya  Bunge, hii inaniambia kuwa tunatawaliwa kwa mabavu na hata ile mihimili mikuu yaani Serikali ,Bunge na Mahakama inatawaliwa kimabavu na kulazimishwa kufuata matakwa ya muhimili mmoja  ambao ni serikali. Bunge halina uwezo wa kuamua mambo ya msingi wanayohitaji wananchi na hata Mahakama pia haina uwezo wa kutoa haki stahiki kwa wananchi wake.Kwa maana hiyo  tulipofikia ili tuweze kupata ukombozi nguvu ya umma pekee ndio inayohitajika. Ifike hiyo  2015 au kabla au baada lakini all in all nguvu ya umma lazima itumike ndugu zangu.Tena umma ulio shupavu usio na woga kama ilivyotokea kule  Misri na kwingineko. Hebu tazama FFU kila mahali,kwenye maandamano ya amani ya wananchi wasio na silaha tena ya kikatiba FFU, kwenye mikutano ya hadhara  FFU, Mahakamani kesi zikiwa zinaendela za viongozi mbali mbali FFU, na sasa wameingia hadi Bungeni kwa wabunge wetu FFU. Ni kwa sababu gani kama sio kutumia mabavu??? Ni mawazo yangu tu napita.
Suleiman Swalehe

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment