Monday 24 June 2013

Re: [wanabidii] Polisi FFU sasa hadi Bungeni?????????? Inatisha

Nia ilikuwa kuwazuia wabunge wa CHADEMA waliokuwa wamevaa magwanda
Mimi nashangaa sana kama watu hawatakiwi kuingia na nguo zinazoonyesha itikadi zao mbona inapofika siku ya Ijumaa huwa naona wabunge wenye imani fulani wakiingia bungeni na nguo ndeefu nyeupe ziko kama kanzu hivi tena wakiwa wamevaa na vijikofia vya rangi nyeupe vilivyodariziwa?
Hawa mbona huwa hawazuiliwi maana bungeni siyo sehemu ya kuvaa hayo mavazi yanayoonyesha itikadi na imani zao?
Huu ubaguzi ni mpaka lini?
Kwa nini macho yanaona makengeza tu upande mmoja? wanatumia nguvu nyiiiiiiingi kuwadhibiti CHADEMA.
wakati hilo si jambo la msingi lililowapeleka hapo mjengoni.

2013/6/25 Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
Hapa kwetu magazeti ni ya shida tunayapata kwenye kipindi cha tuongee magazetini cha Radio Free Afrika au kipindi cha kuperuzi na kudadisi cha  Radio Clouds. Leo asubuhi nimeshangaa sana baada ya kusikia eti askari wa FFU wametanda Bungeni Dodoma kwa ajili ya kupitisha bajeti ya serikali. Jamani hii inakuwaje? Kupitisha bajeti ya serikali sharti kulazimisha kwa nguvu ya dola? Au ndio yale ya mzee Pinda kwamba asiekubali bajeti  ni mkaidi apigwe? Kwanza huyu mzee inafaa apatiwe jina. Mzee mwinyi aliposema mtu yeyote kula kitu atakacho ruksa,akapewa jina la mzee ruksa. Sasa huyu mzee Pinda kasema atakae kaidi amri apigwe nae hafai kupewa  jina? Naona anafaa kuitwa Pinda Piga Piga, au ( Mzee Triple P). Kwangu mimi haileti picha nzuri.Ukifikiria kauli ya huyu mheshimiwa mzee triple P, na hili la FFU kutanda kwenye viwanja vya  Bunge, hii inaniambia kuwa tunatawaliwa kwa mabavu na hata ile mihimili mikuu yaani Serikali ,Bunge na Mahakama inatawaliwa kimabavu na kulazimishwa kufuata matakwa ya muhimili mmoja  ambao ni serikali. Bunge halina uwezo wa kuamua mambo ya msingi wanayohitaji wananchi na hata Mahakama pia haina uwezo wa kutoa haki stahiki kwa wananchi wake.Kwa maana hiyo  tulipofikia ili tuweze kupata ukombozi nguvu ya umma pekee ndio inayohitajika. Ifike hiyo  2015 au kabla au baada lakini all in all nguvu ya umma lazima itumike ndugu zangu.Tena umma ulio shupavu usio na woga kama ilivyotokea kule  Misri na kwingineko. Hebu tazama FFU kila mahali,kwenye maandamano ya amani ya wananchi wasio na silaha tena ya kikatiba FFU, kwenye mikutano ya hadhara  FFU, Mahakamani kesi zikiwa zinaendela za viongozi mbali mbali FFU, na sasa wameingia hadi Bungeni kwa wabunge wetu FFU. Ni kwa sababu gani kama sio kutumia mabavu??? Ni mawazo yangu tu napita.
Suleiman Swalehe

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment