Monday 3 June 2013

Re: [wanabidii] MRADI WA MJI MPYA WA KIGAMBONI , SERIKALI IFUATE SHERIA SIO UBABE

Wizara imevunja sheria ipi? Nijuavyo mimi ardhi ni mali ya serikali. Haki yangu mimi kama mwananchi ni kwenye fidia tu!


2013/6/2 Wanakijiji Kimbiji <wanakijijikimbiji@yahoo.com>


        Mradi wa Mji mpya wa Kigamboni ,Wizara ya Ardhi lazima ifuate Sheria 
        Sio Kutumia ubabe katika kuchukua ARDHI ya wananchi

        HAIWEZAKANI UWAONDOE WAZAWA ,ARDHI UMPE MGENI



Wizara ya Ardhi imejikuta kuwa mvunjivu wa sheria za nchi,na kutumia nguvu,
na kuwatisha wananchi wa wilaya Temeke  kwa kutaka kuwanyang'anya Ardhi
katika kutekeleza mradi wa mji mpya Kigamboni (KDA).

Malalamiko na vilio vya wananchi wa maeneo yanayokadiliwa kuanzia ekali
6,000 hadi 50,000 wilaya ya Temeke,vilio vya wananchi hao ambao wanatishiwa
kuondelewa katika makazi au ardhi zao ,vimekuwa vilio vya samaki machozi
yanakwenda na maji.

Sura mpya ya kutisha inayowaletea mashaka wakazi  Kigamboni na maeneo
mengine ambayo Waziri wa Ardhi Prof.Anna Tibaijuka ametangaza kuwa
yatachukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya Kigamboni,wananchi
wamekuwa wakijiuliza hivi serikali inaivunja sheria ya nchi kwa kupitia
wizara ya Ardhi? na kuwatosa wananchi wake katika wingu la giza !

Utata unakuja pale waziri Anna Tibaijuka anapozitaja kata za Pemba Mnazi,
Kisarwe II,Kimbiji, wilaya Temeke,kuwa kata hizo zitachukuliwa
ili kuongezea utanuzi wa mradi mji mpya Kigamboni,wakati maeneo ya awali
yaliotajwa jatika mradi,kata Kimbiji,pemba mnazi,kisarawe II haziku
wepo. Wananchi wa maeneo hayo wanajiuliza maswali mengi ambayo majibu
yake hakuna,
Hivi Serikali itachukua ardhi na kuwafukuza wananchi katika maeneo hayo
bila ridhaa ya wenye mali au makubaliano ?
Je ?kufanya hivyo Serikali itakuwa inavunja  "sheria za utwaaji Ardhi Na.47 ya mwaka 1967
na Sheria ya Mipango Mji Na.8 ya mwaka 2007."

Sheria za utwaaji Ardhi sura ya 118 inauhusu upangaji vizuri na ujenzi wa makazi tu na
siyo viwanda, maofisi,maghorofa ma tahasisi za Umma !
sasa kama sheria ndiyo hii ,Wananchi wa maeneo yaliyotajwa na Waziri Anna Tibaijuka
kwa nini waondelewe pale ? harafu wawekwe akina nani?

Sheria hii hairuhusu Serikali kuleta watu wengine ili kuwaendeleza kwa 
kisingizio chochote kile hata cha uwekezaji. Ardhi ikitwaliwa chini ya sheria
hii itagawanywa kwa wakazi walewale waliokuwapo baada ya kutenga maeneo ya
ardhi kwa ajili ya miundombinu.

Wizara ya Ardhi isijinye kichwa ngumu katika kuvunja sheria hizi na kuwa wasiri
wa kuwastukiza wanachi baadala ya kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo,
Sheria ya Mipango Miji Na.8 ya mwaka 2007 hisitumike kama mwanya wa
kuwanyang'anya Ardhi wananchi na kuigawa na itakayobaki kuwapa
marafiki au wawekezaji,kufanya hivyo ni kuwadhurumu wapiga kura na
wananchi wa maeneo usika. ni vema taratibu za kisheria zifuate kuliko
Wizara Ardhi kutumia Ubabe.kwa sababu kifungu namba 8 cha sheria hiyo
kinataka kabla ya kutangazwa eneo kuendelezwa lazima wananchi waitwe
na waelezwe na kukubali mpango au mradi huo. 
Kinyume cha ni kuvunja sheria

Tangazo la serikali la 24 Oktoba 2008 kwenye gazeti la Serikali Na. 43 Vol. 89 lilikuwa na taarifa ya
 amri ambayo ilianisha mipaka ya eneo litakalokumbwa na ujenzi wa mji mpya kuwa ni kata tano
 za Somangila, Kigamboni, Vijibweni, Kibada na Mji Mwema.  http://www.youtube.com/watch?v=Jh2jQcnWcQo
tumsikilize Rais Kuhusu Kigamboni http://www.youtube.com/watch?v=UaviGdsJJNI



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 



--
Wasalaam,
 
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment