Friday, 21 June 2013

Re: [wanabidii] Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Joseph Machali (NCCR MAGEUZI ) Ashambuliwa

Nilifika kumjulia hali Komredi Machali na hali yake ni nzuri, hakupata fracture yoyote ile zaidi maumivu ya mwili tu, na kunyang'anywa simu ya kiganjani. Kati ya vijana hao wanne, wawili wametiwa nguvuni na polisi. Jioni aliruhusiwa kurudi nyumbani.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: James Malima <james.malima@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 21 Jun 2013 18:40:59 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Joseph Machali (NCCR MAGEUZI ) Ashambuliwa

Imekuwa bahati mbaya sana, lkn Mheshimiwa angeepusha yote hayo kwa kudharau na kuendelea na shughuli zake. Sometimes we learn through hard ways.

Sent from my iPhone

On 21 Jun 2013, at 17:36, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime amethibitisha taarifa za kuvamiwa na kupigwa kwa mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Joseph Machali (NCCR-Mageuzi).

Kamanda Misime amesema jeshi la polisi mkoni humo linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo.

Amesema Machali alivamiwa na watu wanne jana usiku alipokuwa akirejea kutoka kwenye vikao vya Bunge.

Kwa sasa Machali amelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Dodoma (General) kwa matibabu zaidi.

Awali, taarifa zilipasha kuwa Machalli akiendesha gari lake meta kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi, aliwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita.

Kitendo hicho  kilionekana kuuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga kwa nguvu bodi ya gari la Machalli jambo ambalo lilimsababish Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni.

Baada ya kushuka,  vijana hao walimtolea  matusi kadhaa ya nguoni na pindi Machalli aliwajibu kwa hasira ndipo aliposhambuliwa na kupigwa

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia amesema amemkagua Mhe. Machali asubuhi ya leo akia hospitalini na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2WrTrfd3Q

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment