Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
From: Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 22 Jun 2013 17:31:53 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mbowe kutoukabidhi ushaidi wa video ni kosa la jinai: Je kuukabidhi ni salama?
1. Mimi nadhani mwenye jukumu la kuchunguza na kupata ushahidi ni polisi.
2. Ushahidi maana yake ni kielelezo/vielelezo vinavyoonesha kuwa tukio fulani lilitokea kama lilivyotokea na siyo 'anything' au siyo zaidi au pungufu.2013/6/22 Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>
Ninachofahamu ni kwamba Mh Mbowe hawezi kutoa huo ushahidi kwa polisi na wala haogopi vitisho vya polisi kuhusu "kumshughulikia (kimabavu au kisheria)" endapo atakataa kutoa ushahidi wake. Anasubiri apelekwe mbele ya sheria kwa "kukataa kutoa ushahidi" ndipo akautoe ushahidi wake pale mbele ya jopo la mawakili, wanasheria na wananchi ili hata kama huo ushahidi ukaja ukachakachuliwa, kila mtu atakuwa ameuona. Kuna habari zimeendea mitandaoni kwamba CHADEMA ilitumia mitambo maalum ya DVR kurekodi mkutano wa tarehe 15/06/2013, na kwamba kwenye mkutano wake wa mwisho licha ya kutumia setlite kurekodi mikutano yake, imethibitika kuwa chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano kurekodi mkutano wake wa mwisho katika uwanja wa soweto Arusha. Mtambo huo ambao unauwezo wa kurekodi matukio kwa masaa 72 mfululizo bila kuhitaji chaji, ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano. Yawezekana ndiyo maana sasa hivi polisi wamenywea na kumtaka Mbowe apeleke ushahidi wakle kwa Rais.
Jambo lingine linalotia shaka, hasa kuhusu tuhuma kwamba polisi wanatumiwa vibaya na chama tawala ni kwamba Nape alitoa kauli mkwamba CHADEMA walijiripua wenyewe kwenye mkutano wao. Lakini mpaka sasa hivi, polisi hawajawahi kumtaka Nape awapelekee ushahidi kuhusu hayo matamshi yake.
Tuhuma kwamba polisi wanatumiwa na serikali na CCM, zinakolezwa na matamshi ya polisi wenyewe. Ukisikiliza utetezi wa polisi kwenye habari iliyopo hapo chini, lazima uutilie mashaka. Inawezekanaje polisi wafanye kazi ya kuwabeba majeruhi badala ya kudeal na muuaji aliyekuwa kifukuzwa na wananchi (wanaodai kwamba walipigwa risasi na polisi wakti wanajaribu kumfukuza mrusha bomu)?. Hebu msikilize huyu polisi anachosema kuhusu kurushwa kwa bomu na kutupwa kwa risasi zilizowaua raia wasiokuwa na hatia, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, ambao hawakuwwepo kwenye mkutano wa CHADEMA siku ya tukio:
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++Arusha: Mashuhuda wa tukio la mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini Arusha, wamedai kumwona na kumtambua mtu aliyehusika na tukio hilo lakini wanasema walishidwa kumkamata kutokana na "kushambuliwa kwa risasi na polisi".Mlipuko huo ulitokea katika Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani jijini humo na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 100.Mashuhuda hao ambao wote walijeruhiwa kwa risasi wanasema mlipuaji wa bomu alikuwa amevalia shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans yenye rangi ya blue na kwamba wajihi wake ni mtu wa kimo cha kati.Mmoja wa mashuhuda hao ni mlinzi katika Kikosi cha Ulinzi cha Chadema (Red Brigade) ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alidai kwamba alimwona mtu aliyerusha bomu mara tu baada ya tukio hilo.Mlinzi huyo ambaye alipigwa risasi za mguuni na kifuani wakati akimkimbiza mtu huyo, alisema bomu hilo lililipuka mara tu baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia na kushuka jukwaani."Baada ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kushuka jukwaani, nikawapanga walinzi kwa ajili ya kuwalinda viongozi waliokuwa wakichangisha fedha. Ghafla nikasikia mlipuko, sikujua ni nini, lakini kuna mama mmoja alikuwa karibu yangu akanionyesha mtu aliyelipua, akisema yuleee…" alisema na kuongeza:"Alikuwa amevaa shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans ya blue. Ni mtu wa kimo cha kati. Watu walianza kumkimbiza kuelekea upande wa Magharibi wa Uwanja kwenye nyumba za NHC. Tuliruka uzio alipopita yule mtu, mara nikasikia risasi imenipata mguuni.""Tulikuwa na uwezo wa kumkakata yule mtu, lakini nikaona risasi zimezidi upande wetu nikaona nigeuze na hapo hapo nikapigwa risasi ya kifuani, nikaishiwa nguvu, sikuweza kufahamu mtu huyo alikoishia. Nilijikongoja na kurudi uwanjani."Mlinzi huyo ambaye amelazwa katika moja ya hospitali za jijini Arusha anasema alilazimika kuhama hospitali ya Seliani alikokuwa amelazwa awali baada ya kuandamwa na polisi. "Nilikaa siku tatu hospitalini bila kupata huduma yoyote, lakini kila siku madaktari walikuwa wakinihoji maswali,"alisema na kuongeza:"Mwisho nikaambiwa kwamba nitahamishiwa ghorofa ya chini, nilipouliza sababu wakasema eti Waziri Mkuu atakuja kuniona… Niligoma mwisho daktari akaniambia kuwa kuna polisi waliovaa majoho ya udaktari ndiyo waliotaka nihamishwe".Maelezo yake yanafanana na yaliyotolewa na majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Alila ambaye alisema kuwa alimwona mtu aliyelipua bomu "akiingia kwenye gari la polisi"."Baada ya mlipuko, sikujua kama nimeshapigwa risasi, lakini niliona watu wakimkimbiza mtu baada ya mama mmoja kusema kuwa ndiye aliyerusha bomu.Watu waliokuwa wakimkimbiza walikuwa wakirushiwa risasi na polisi. Baadaye nilimwona mtu huyo akipanda gari la polisi. Nashangaa tena kusikia polisi wakimtafuta huyo mtu," alisema Alila.Polisi wodiniMbali na taarifa kwamba polisi walikuwa wakizunguka katika wodi za wagonjwa wakiwa wamevalia majoho ya madaktari, pia mgonjwa mwingine amedai kwamba askari wamekuwa wakimfuatilia kila kukicha.Peter Mshanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Selian hivi sasa kutokana na kujeruhiwa kwa risasi katika mguu wake wa kushoto alisema awali alipelekwa katika hospitali ya St. Elizabeth lakini alihama baada ya kuandamwa na askari kanzu."Mara baada ya bomu nilipelekwa Hospitali ya St. Elizabeth na huko nilishangaa kuwaona askari ninaowafahamu wakizingira kitanda changu. Hata nilipokwenda chooni askari mmoja alinifuata, nikamuuliza anataka nini, yeye akanijibu eti anataka kunisaidia, nikamkatalia akatoka nje," alisema Mshanga na kuongeza:"Waliendelea kuzingira kitanda changu kwa siku kadhaa, siku ya tatu daktari akasema nitakiwa nihamishiwa hospitali ya Mount Meru, nikapinga".Wakati huo walikuwa tayari wameandaa ambulance (gari la wagonjwa) na gari la polisi ili wanihamishe. Ndugu zangu walipinga ndipo nikahamishiwa hapa Seliani,"anasema.Kuhusu kujeruhiwa kwake, Mshanga alisema baada ya mlipuko alishtukia ameshajeruhiwa mguuni na akaanguka chini."Nilikuwa nimeshika Sh500 mkononi nikisubiri kutoa sadaka yangu. Mara nikaona watoto wanaanguka mbele yangu, nikasikia kishindo kikubwa, kisha nikakimbia kubeba mmoja wa watoto, na mimi nikaanguka, kumbe nilikuwa nimejeruhiwa," alisema.Jana gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas kuzungumzia suala la polisi kuwafuatilia majeruhi lakini alipopokea simu alisema hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwa kuwa yuko kwenye kikao. "Niko kwenye kikao," alisema Sabas na kukata simu yake.Mkanganyiko wa taarifaWakati Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi ikitoa kauli kuwa polisi walijihami kwa kuwapiga wananchi risasi na mabomu ya machozi, mmoja wa maofisa polisi aliyekuwa uwanjani wakati wa mlipuko ambaye pia hakutaka jina lake litajwe gazetini amekanusha kupiga watu risasi. "Mimi ndiyo nilikuwa pale uwanjani, baada ya bomu kulipuka wafuasi wa Chadema walianza kutushambulia tulipojitokeza kubeba majeruhi hadi wakavunja kioo cha gari yetu. Niliwaamuru askari warushe risasi hewani, hakuna hata mtu mmoja aliyepigwa risasi," alisema na kuongeza:"Unajua wafuasi wa Chadema wamelishwa chuki na viongozi wao, kama Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye alisema akivamiwa na majambazi heri afe kuliko kumpigia simu RPC. Ndiyo maana watu walijawa chuki wakaja kutushambulia."Aliendelea: "Baada ya kuona mashambulizi yamezidi tukaondoka, lakini baadaye tukarudi na kukuta majeruhi wote wameshaondolewa na wafuasi wa Chadema. Baadhi ya askari kanzu waliwafuatilia majeruhi ili kujua majina na idadi yao ili tutoe taarifa".Kama ni risasi basi wamepigwa na viongozi wa Chadema kwani maganda mengi ya risasi yameonekana kuwa ya bastola na viongozi wao wengi wanazo,"alisema.SOURCE: Mwananchi 22/6/2013
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, June 21, 2013 10:01 PM
Subject: [wanabidii] Mbowe kutoukabidhi ushaidi wa video ni kosa la jinai: Je kuukabidhi ni salama?
Ilipotoka hapa jamvini kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema anao ushaidi wa picha kuonyesha kuhusika kwa Polisi katika urushaji wa bomu katika mkutano wa chama chake huko Arusha mimi nilikuwa mmoja kati ya watu wa Mwanzo kumtaka atoe ushaidi huo mapema. Hadi sasa hajautoa. Nimesikia kupitia vyombo mbali mbali vya habari kuwa kutofanya hivyo ni kosa la jinai.Hata kabla ya sheria kusema hivyo kila mtu anaona kuwa kutoutoa ushaidi huo ni kuizuia sheria kumuandoa mhalifu katikati ya jamii na hivyo kuhatarisha usalama na amani. Mtu huyo anaweza kufanya jingine la hatari na lazima Mbowe atalaumiwa.Sasa nimesikia pia kupitia vyombo vya habari kuwa CHADEMA hawaiamini Polisi ndiyo maana hawataukabidhi ushaidi huo.Naomba kuuliza swali: Kama mtu ukiona huwaamini Polisi na kisheria unalazimika kuwakabidhi ushaidi; jema ni lipi kufanya. Kutoutoa ushaidi ukakabiliwa na kosa la jinai au kuutoa ushaidi huo ukachezewa? Jamii inasemaje na sheria zinasemaje.Si kusudi langu kumsaidia Mbowe kuhusu kutoaminika kwa jeshi letu la Polisi ila nasema tu matukio yanayojulikana kwetu wote ambayo jeshi letu la Polisi hata lenyewe haliwezi kujiamini:1 Dr Mwakyembe akiwa bado mzima wa Afya aligundua njama za kumdhuru. Akakusanya ushaidi wa kutosha akalikabidhi jeshi la polisi (kwa maneno yake na kama alifvyonukuliwa na vyombo vya habari). Jamii haijui kilichofanywa na Polisi hadi Dr Mwakyembe anaumwa ugonjwa wa ajabu na hakuna anayejua kama hakuna uhusiano wowote kati ya Polisi kutofanya lolote na kuumwa kwake.2 Dr Ulimboka alitekwa na kuteswa msituni. Alitoa maelezo ya kutosha. Gazeti la MwahaHalisi lilitoa ushaidi wa kutosha mpaka nikakumbuka habari moja kwenye Biblia ambapo mfalme alikwenda kupigana akamuomba Mungu wake kuwa ukiniongoza nikashinda kitakatojitokeza cha kwanza nikirudi nitakutolea sadaka. Aliporudi binti yake pekee alikuwa wa kwanza kumlaki na mfalme alimtoa kafara. Nilifikiri sasa Polisi watawachunguza waliotajwa kumdhuru Ulimboka bila kujali ni akina nani. Hadi sasa hakuna kilichofanyika na umma kuelezwa.3 Mwaka 2005 Polisi waliua wafanya biashara. Wakatangaza kuwa wameua majambazi waliomwibia mfanya biashara Fulani. Polisi hao wakaonyesha maiti za wafanyabiashara kuwa ndio majambazi. Ilipogundulika kuwa hawakuwa majambazi na kuwa waliuawa kikatili bila sababu na kuwa hela nyingi walizokuwa wameuza madini hazionekani Polisi wakikosa ushahidi wa kudhibitisha kuwa hao ndio wauaji. Ushaidi uko kwenye television wakikiri kuwa wameua hao. Polisi wakakosa ushaidi.4 Mwandishi David Mwangozi aliuawa. Kabla haijajulikana aliyemuua mtu mmoja mkubwa wa Polisi alisema Mwangozi ameuawa na wanachama wa CHADEMA. Tayari maandalizi ya kuwashughulikia yalianza. Mda huo CHADEMA wakatoa ushaidi kuonyesha muuaji wa Mwangosi. Mkubwa huyo aliyekuwa na ushaidi wa CHADEMA kuua alikuwa amesimama pembeni Mwangosi akiuawa. Polisi wamekosa ushaidi wa kufanya lolote na hakuna hatua hata za kinidhamu zinazochukuliwa dhidi ya wakubwa/Mkubwa huyo.5 Hivi karibuni Polisi wamepewa habari Fulani kuwa Chama Cha Siasa kinaandaa vijana kwa kusingizia kuwapa mazoezi ya 'ukakamavu' Wakadai mazoezi wanayofanya ni zaidi ya ukakamavu. Na kwanza kwa nini uwapeleke kambini. Kimya tunachoshuhudia huenda wanafanya uchunguzi au yameishia hapo.6 Hivi Karibuni Mr Lwakatare alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Ugaidi. Kwa kuichunguza kesi hiyo ilibidi wote aliokuwa akiwasiliana nao wakamatwe ili iweze kuwa kesi ya ugaidi sawasawa. CHADEMA ilitoa orodha hiyo. Tumeishia kusikia kuwa kuchukua habari hizo kwenye mtandao ni kosa la jinai. Wala sio kuwakamata magaidi wengine. Sasa mahakama imemuondolea mashtaka hayo. Lwakatare amekaa lupango siku 90 plus. Ubatizo na kipaimara alichopata, tusubiri kidogo tutajua. CHADEMA wajiandae.Ukiyachunguza hayo niliyoyataja utakubaliana na Mbowe na CHADEMA kuwa ushaidi walio nao hautakuwa salama kuukabidhi Polisi. Je waukabidhi potelea kote mhalifu asishughulikiwe au wakatae mpaka utakapokabidhiwa kwenye mikono salama.Jamii inasemaje?Sheria inasemaje?Haki inasemaje?Katiba inasemaje?Elisa Muhingo--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment