Tunaisemea jamii inayounda Taifa na Serikali. Ina matendo na mitazamo inayohitaji pia kubadilika ili zifanikiwe. Kama dini ni away of Life, je ina maana mtu anasali kutwa hafanyi kazi? Watu watakupa mifano kuwa, kama mtu mfano yupo Chuo Kikuu na dini ni a way of life anasali in a routine way kutwa, kucha. Hii itamfanya kwa mfano akimaliza vipindi saa kumi na mbili jioni anakwenda kusali maombi kuanzia (mkristu huyo) saa 12 jioni hadi asubuhi (mikesha). Akirudi kesho darasani anasinzia, hajamaliza assignment na anajipa stress za zamisha. Huyu atafeli mitihani asipoangalia. Mwingine anarudi asubuhi kutoka mkesha (mke wa mtu) anakuta mtoto alizidiwa homa usiku akafariki. Housegirl hakuwa na uwezo wa huduma zaidi. Baba naye alilala nje kwa kimada kutokana kwamba mama daima yupo mikesha ya kusali na kuwajibika na familia na mumewe kudogo. Ndoa inavunjika hapo. Kama ni wa kusali sala 5- as a way of life, ni kusali kutwa na kufunga biashara au huduma ya kiofisi kila baada ya masaa fulani bila ya kuacha msaidizi. Kama ni mfanyakazi wa bank-madirisha yote yamefungwa kasoro labda moja na foleni ndefu sana-utakosa wateja watajiunga na bank ingine. Kama ni hotel-mwekezaji ataleta wahudumu wengine hata wa kutoka nchi jirani (malawi, Kenya, zambia) kuepuka misururu ya wageni reception mtu wa mapokezi yupo nyuma stoo ya hoteli anasali au kaenda kusali nje ya jengo. Mwekezaji au tajiri hatokubali kukosa wateja mtu anasubiri apokelewe au kupata chakula masaa kitu kidogo hakiji. Ni mifano ya kuonyesha-serikali haitotelemsha kama mvua. Budi kugangamala na kutafuta mibadala ili kujiajiri kiufanisi au kuajiriwa na kufanyakazi kwa ufanisi. Ni mifano hai na halisi bongoland kwa madhehebu ya wakristu na waislamu na tunayaona katika nchi yetu na za wenzetu. Sali sana lakini soma sana na pata ujuzi-zalisha sana. Tunza mila ya kabila lako lakini tendea haki wengine sio unasema amefariki au amehama lakini kumbe umemuoza na umemtorosha hapo katika umri mdogo hasomi au umemuozesha unamchanganya kimajukumu kijana shule haipambi. Ni mifano halisi tunayokumbana nayo katika kupanga mipango shirikishi, IEA, SEA ya kuangalia watafaidikaje na miradi. Baadhi ya desturi hizi hukatisha tamaa wenye nia nzuri na kusaidia maendeleo. --- On Mon, 3/6/13, Rashid Maalim <rashid.o.maalim@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment